Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-ni-ya-Kipekee. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-ni-ya-Kipekee. Onyesha machapisho yote

4/07/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Neno la Mwenyezi Mungu  | Mamlaka ya Mungu (II)

    Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, umepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamekusaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”

Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo

    Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum;