4/08/2018

Kifo: Awamu ya Sita | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Maisha

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kifo: Awamu ya Sita

    Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa. Kusikia kwa mtu kunaanza kufifia, meno yake kulegea na kuanza kujiangukia, mwitikio wa mtu unaanza kuchelewachelewa, kutembea kunakuwa ni kwa kujikokota.... Wakati huu mtu ameaga kwaheri kabisa miaka yake ya nguvu ya ujana wake na kuingia katika maisha yake ya kwaheri: umri wa uzee. Kisha, mtu atakabiliana na kifo, awamu ya mwisho ya maisha ya binadamu.

1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu

    Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa na maisha ya awali ya mtu, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu ya maisha, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba amepangilia mseto maalum wa hali mbalimbali za kuzaliwa kwa mtu, ni wazi na dhahiri shahiri kwamba amepangilia pia mseto wa hali zisizobadilika kwa minajili ya kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu ambacho hakitarajiwi, na si kuzaliwa, si kufa vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kama vile tu mengi yanaweza kuzungumzwa kuhusu kuzaliwa kwa mtu, hata kifo cha kila mtu kitafanyika katika mseto tofauti katika hali maalum, hivyo basi urefu wa maisha tofauti miongoni mwa watu na njia tofauti pamoja na nyakati tofauti zinaandama vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi wanafarakana na dunia kutokana na sababu zisizokuwa za kawaida, wengine kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia hewani, wengine wakafia chini ya nchi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. ...Kila mtu hutaka kuzaliwa kwa heshima, maisha mazuri, na kifo kitukufu, hakuna mtu anayeweza kuendeleza hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Binadamu anaweza kufanya aina zote za mipango ya siku zote za usoni, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawaje watu hufanya kila wawezalo kuepuka na kuzuia kuja kwa kifo chao, ilhali, bila wao kujua, kifo huwa kinakaribia polepole. Hakuna anayejua ni lini atakapofarakana na dunia au ni vipi atakavyofanya hivyo, isitoshe hata pale hayo yote yatakapofanyikia. Bila shaka, si ubinadamu unaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa kimaumbile, lakini ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa kimaumbile, lakini athari ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.

2. Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo

    Wakati mtu anapoingia kwenye umri wa uzee, changamoto anazokabiliana nazo si kutosheleza mahitaji ya familia au kuanzisha maono makubwa katika maisha yake, lakini namna ya kuyaaga maisha yake, namna ya kukutana na mwisho wa maisha yake, namna ya kuweka kikomo kwenye mwisho wa uwepo wake binafsi. Ingawaje juujuu inaonekana kwamba watu hutilia makini kidogo kwa kifo, hakuna anayeweza kuepuka kuchunguza suala hili, kwani hakuna anayejua ikiwa ulimwengu mwingine uko kule upande mwingine wa kifo, ulimwengu ambao binadamu hawawezi kung’amua au kuhisi, ulimwengu wasiojua chochote kuuhusu. Hali hii huwafanya watu kuwa na wasiwasi kukabiliana na kifo moja kwa moja, wasiwasi wa kukabiliana nacho kama inavyostahili, na badala yake wanafanya kadri ya uwezo wao kuepuka mada hii. Na kwa hivyo mada hii humfanya kila mmoja kutishika kuhusu kifo, huongezea uzito kwenye fumbo hili kuhusiana na hoja hii isiyokwepeka ya maisha, huweka kivuli kisichoisha juu ya moyo wa kila mmoja.
    Wakati mtu anapohisi mwili wake unaanza kudhoofika, wakati mtu anapohisi kwamba kifo chake chakaribia, mtu huhisi tishio, woga usioelezeka. Woga wa kifo humfanya mtu kuhisi kuwa mpweke zaidi na asiyejiweza, na kwa wakati huu mtu hujiuliza: Nilitoka wapi? Ninaenda wapi? Je, hivi ndivyo nitakavyokufa, huku maisha yangu yakinipita kwa haraka hivi? Je, huu ndio wakati unaoadhimisha mwisho wa maisha yangu? Ni nini, hatimaye, maana ya maisha? Maisha yana thamani gani, kwa kweli? Je, yanahusu umaarufu na utajiri? Je, yanahusu kulea familia? ... Haijalishi kama mtu amewahi kufikiria maswali haya mahususi, haijalishi ni vipi mtu ana woga wa kifo, katika kina cha moyo wa kila mmoja siku zote kuna tamanio la kutaka kuchunguza zaidi mafumbo, hisia zisizoeleweka kuhusu maisha, pamoja na haya yote, ni uhusiano wa karibu na ulimwengu wenyewe, na kutotaka kuuacha. Pengine hakuna anayeweza kufafanua zaidi ni nini ambacho binadamu huogopa, ni nini ambacho binadamu hutaka kuchunguza zaidi, na nini kile ambacho ana uhusiano wa karibu nacho na kinachomfanya kutotaka kuondoka au kukiacha nyuma. …
    Kwa sababu wanaogopa kifo, watu huwa na wasiwasi mno; kwa vile wanaogopa kifo, vipo vitu vingi ambavyo hawawezi kuachilia. Wakati wako karibu kufa, baadhi ya watu huhangaika kuhusu hiki au kile; wanakuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao, wapendwa wao, utajiri wao, ni kana kwamba kwa kuwa na wasiwasi hivyo wanaweza kuondoa mateso na hofu ambayo kifo huleta, ni kana kwamba kwa kuendeleza aina fulani ya urafiki wa karibu na wale wanaoishi wanaweza kukwepa ile hali ya kutoweza kujisaidia na upweke unaoandamana na kifo. Katika kina cha moyo wa binadamu kunao woga usiokamilika, woga wa kuachwa na wapendwa, woga wa kutowahi kutuliza macho yako kwenye mbingu za samawati, woga wa kutowahi tena kuangalia ulimwengu huu yakinifu. Nafsi pweke, iliyozoeana na wapendwa wake, husita kuachilia mshiko wa maisha na kuondoka, ikiwa pekee, kuelekea kwenye ulimwengu usiojulikana, usiozoeleka.

3. Maisha ya Kuishi Ukitafuta Umaarufu na Utajiri Yatamwacha Mtu Akiwa na Hasara Akikabiliana na Kifo

    Kwa sababu ya ukuu na kuamuliwa kabla kwa Muumba, nafsi pweke iliyoanza bila chochote kwa jina lake huweza kupata wazazi na familia, fursa ya kuwa mwanachama wa kizazi cha binadamu, fursa ya kupitia maisha ya binadamu na kuona ulimwengu; na pia inafaidi fursa ya kupitia ukuu wa Muumba, kujua uzuri wa uumbaji wa Muumba, na zaidi kuliko vyote, kujua na kutii mamlaka ya Muumba. Lakini watu wengi zaidi huwa hawatumii vizuri fursa hii nadra na ya kipekee. Mtu hutumia nguvu zake zote maishani akipigana dhidi ya hatima yake, akatumia muda wake wote akihangaika na akijaribu kulisha familia yake na akisafiri huku na kule kati ya kutafuta utajiri na hadhi katika jamii. Mambo ambayo watu huthamini ni familia, pesa, na umaarufu; wanaona mambo haya kuwa mambo yenye thamani zaidi katika maisha. Kila mtu hulalamikia hatima yake, ilhali bado wanazisukuma hatima hizi nyuma ya akili zao na wanabaki na maswali ambayo ni lazima zaidi kuchunguza na kuelewa: kwa nini binadamu yuko hai, namna ambavyo binadamu anafaa kuishi, ni nini maana na thamani ya maisha. Katika maisha yao yote, hata hivyo iwe miaka mingapi, wanakimbilia tu kuhusu kutafuta umaarufu na utajiri, mpaka ujana wao ukawaacha, mpaka wakawa na nywele za kijivu na makunyanzi kwenye uso wao; mpaka wakagundua utajiri na umaarufu ni vitu visivyoweza kusitisha mtu kuelekea katika udhaifu unaotokana na uzee, kwamba pesa haiwezi kujaza utupu wa moyo: mpaka wanapoelewa kwamba hakuna mtu ambaye anaachwa nje kutoka kwenye sheria ya kuzaliwa, kuwa mzee, magonjwa, na kifo, kwamba hakuna mtu anayeweza kutoroka hatima ile inayomsubiri. Mpaka tu pale ambapo anapolazimishwa kukabiliana na awamu ya mwisho maishani ndipo anapong’amua kwa kweli kwamba hata kama mtu anamiliki mamilioni ya mali, hata kama mtu anayo heshima na cheo kikubwa, hakuna anayeweza kutoroka kifo, kwamba kila mtu atarudi kwenye sehemu yake asilia: nafsi pweke, bila chochote kwa jina lake. Wakati mtu anapokuwa na wazazi, mtu husadiki kwamba wazazi wa mtu ni kila kitu; wakati mtu anapokuwa na mali, mtu hufikiri kwamba pesa ndio kitu cha muhimu, kwamba ni rasilimali za mtu maishani; wakati watu wanapokuwa na hadhi katika jamii, wanaishikilia na hata wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya hadhi hiyo. Ni pale tu ambapo watu wanakaribia kuondoka ulimwenguni ndipo wanapotambua kwamba mambo yale waliyoishi katika maisha yao wakifuatilia si chochote bali mawingu yanayopita, hakuna chochote kati ya vitu hivi ambacho wanaweza kushikilia, hakuna hata chochote wanachoweza kwenda nacho, hakuna hata chochote kinachoweza kuwaondolea kifo, hakuna kile kinachoweza kuwapa ushirika au tulizo wakati nafsi yao inapokuwa pweke ikielekea kufa; na hata, hakuna kati ya hivyo vyote vinavyoweza kumpa mtu wokovu, na kuwaruhusu kushinda kifo. Umaarufu na utajiri ambao mtu hupata kwenye ulimwengu yakinifu humpa mtu kutosheka kwa muda, anasa ya kupita, hisia ya uwongo ya utulivu, na kumfanya mtu kupoteza njia. Na kwa hivyo watu, wanapong’ang’ana kila pahali kwenye bahari pana ya ubinadamu, wakitafuta amani, tulizo na utulivu wa moyo, wanafunikwa zaidi na zaidi na mawimbi. Wakati ambapo watu hawajapata maswali ambayo ni muhimu zaidi kuelewa—ni wapi wametoka, ni kwa nini wako hai, ni wapi wanakoenda na kadhalika—wanashawishiwa na umaarufu na utajiri, wanapotoshwa, wanadhibitiwa na vitu hivyo, na wanaishia kupotea bila kujua njia. Muda huyoyoma; miaka hupita kama kupepeswa kwa jicho; kabla ya mtu kutambua, mtu huaga kwaheri miaka yake bora zaidi ya maisha yake. Wakati mtu anakaribia kuondoka ulimwenguni, mtu anafika katika utambuzi wa taratibu kwamba kila kitu ulimwenguni kinamwacha polepole, kwamba mtu hawezi kushikilia tena vitu alivyomiliki; kisha mtu anahisi kwa kweli kwamba hamiliki chochote kamwe, kama mtoto mchanga anayelia ambaye ndio mwanzo amezaliwa na kubisha mlango ulimwenguni. Wakati huu, mtu anashawishiwa kutafakari kile ambacho amefanya maishani, thamani ya kuwa hai, ni nini maana yake, kwa nini mtu alikuja ulimwenguni; na wakati huu, mtu anaendelea kutaka kujua kama kweli kunayo maisha baada ya kifo, kama Mbinguni kweli ipo, kama kweli kunayo adhabu... Kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo anavyotaka zaidi kuelewa maisha yanahusu nini haswa; kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo moyo wake unapoonekana kuwa mtupu; kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo anapohisi kuwa hawezi kusaidika; na kwa hivyo woga wa mtu kuhusu kifo unazidi kuwa mwingi siku baada ya siku. Kunazo sababu mbili zinazoelezea kwa nini watu huwa hivi wanapokaribia kifo: Kwanza, wako karibu kupoteza umaarufu na utajiri ambao maisha yao yalitegemea, wako karibu kuacha nyuma kila kitu kinachoonekana ulimwenguni; na pili, wako karibu kukabiliana, wakiwa peke yao, na ulimwengu usiojulikana, wenye mafumbo, himaya isiyojulikana ambapo wana woga wa kukanyaga guu lao kule, kule wasikokuwa na wapendwa na mbinu zozote za kupata msaada. Kwa hizo sababu mbili, kila mmoja anayekabiliana na kifo huhisi vibaya, hupitia hali ya wasiwasi na hujipata katika hali ya kutoweza kusaidika ambayo hawajawahi kupitia awali. Kwa hakika punde watu wanapofikia wakati huu ndipo wanapotambua kwamba kitu cha kwanza ambacho mtu lazima aelewe, anapokanyaga guu lake hapa duniani, ni wapi binadamu hutoka, kwa nini watu wako hai, nani anayeamuru hatima ya binadamu, ni nani anayekidhi mahitaji ya binadamu, na Aliye na ukuu juu ya uwepo wa binadamu. Hizi ndizo rasilimali za kweli za maisha, msingi muhimu kwa kuwepo kwa binadamu, kutojifunza namna ya kutosheleza familia ya mtu au namna ya kutimiza umaarufu na utajiri, kutojifunza namna ya kujitokeza katika umati au namna ya kuishi maisha mazuri zaidi, bila kutaja namna ya kutia fora na kushindana kwa ufanisi dhidi ya wengine. Ingawaje mbinu mbalimbali za kuishi ambazo watu huishi wakijaribu kumiliki zinaweza kumpa wingi wa tulizo la mali, hazijawahi kumpa mtu amani ya kweli moyoni na tulizo, lakini badala yake hufanya watu kila wakati kupoteza mwelekeo wao, kuwa na wakati mgumu kujidhibiti, kukosa kila fursa ya kujifunza maana ya maisha; na kuunda mawimbi fiche ya matatizo kuhusu namna ya kukabiliana kikamilifu na kifo. Kwa njia hii, maisha ya watu yanaharibika. Muumba hushugulikia kila mmoja bila mapendeleo, huku akipatia kila mmoja wetu fursa ya kutosha maisha yote ili kuweza kupitia na kujua ukuu Wake, ilhali ni mpaka tu kifo kinapokaribia, wakati kivuli cha kifo kinaponing’inia karibu na mtu, ndipo mtu huyu huanza kuona nuru—na kisha muda huwa umeyoyoma mno.
    Watu huishi maisha yao wakitafuta pesa na umaarufu; wanashikilia nyuzi hizi, wakifikiri kwamba ndizo mbinu zao pekee za msaada, ni kana kwamba wakiwa nazo wangendeelea kuishi, wangejitoa kwenye hesabu ya wale watakaokufa. Lakini pale tu wanapokuwa karibu kufa ndipo wanapotambua namna ambavyo vitu hivi vilivyo mbali na wao, namna walivyo wanyonge mbele ya kifo, namna wanavyosambaratika kwa urahisi, namna walivyo wapweke na wasivyoweza kusaidika, na hawana popote pa kugeukia. Wanatambua kwamba maisha hayawezi kununuliwa kwa pesa au umaarufu, kwamba haijalishi mtu ni tajiri vipi, haijalishi cheo chake kilivyo cha hadhi, watu wote ni maskini kwa njia sawa na wanaofanya mambo bila mpango mbele ya kifo. Wanatambua kwamba pesa haiwezi kununua maisha, kwamba umaarufu hauwezi kufuta kifo, kwamba si pesa wala umaarufu vinaweza kurefusha maisha ya mtu kwa hata dakika moja, hata sekunde moja. Watu wanapohisi hivi zaidi, ndipo wanapotamani zaidi kuishi; watu wanapohisi hivi zaidi, ndipo wanapohofia kukaribia kwa kifo. Ni katika wakati huu tu ndipo wanapotambua kwa kweli kwamba maisha yao si yao, si yao kudhibiti, na kwamba mtu hana usemi kuhusu iwapo ataishi au atakufa, kwamba haya mambo yote yanapatikana nje ya udhibiti wa mtu.

4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu

    Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya. Kwa hivyo inafaa kuwa rahisi sana kwa kila mtu kutambua, kupitia kwa yale ambayo yeye mwenyewe amepitia maishani kwa kipindi cha miongo mbalimbali, kwamba hatima zote za binadamu zimeamuliwa kabla, na kung’amua au kujumlisha ni nini maana ya kuishi. Wakati uo huo ambao mtu anakumbatia mafunzo haya ya maisha, mtu ataelewa kwa utaratibu ni wapi maisha yanatokea, kunga’mua hasa ni nini ambacho moyo unahitaji kwa kweli, nini kitaongoza mtu kwenye njia ya kweli ya maisha, kazi maalum na shabaha ya maisha ya binadamu inafaa kuwa nini; na mtu ataanza kutambua kwa utaratibu kwamba kama mtu hataabudu Muumba, kama mtu hataingia kwenye utawala Wake, basi mtu anakabiliana na kifo—wakati nafsi iko karibu kukabiliana na Muumba kwa mara nyingine—moyo wa mtu utajazwa hofu na ugumu usio na mipaka. Kama mtu amekuwepo ulimwenguni kwa miongo kadhaa ilhali hajajua ni wapi maisha ya binadamu hutoka, angali hajatambua ni kwenye viganja vya mikono ya nani hatima ya binadamu huwa, basi si ajabu hataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu. Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na shukrani sahihi ya maana na thamani ya maisha; mtu aliye na kina cha maarifa kuhusu kusudi la maisha, aliye na hali halisi aliyopitia na anaelewa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anafaa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarudi kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni; mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hiyo, wakati mtu anapong’amua mambo haya, mtu ataanza kuweza kukabiliana na kifo kwa utulivu na kwa kawaida, kuweka pembeni mali yake yote ya dunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kutishika vivyo hivyo tu na kung’ang’ana dhidi ya kifo. Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake. Ni wazi kwamba, mtu kama huyo atahitajika kupendwa na kukubaliwa na Muumba, na mtu kama huyo ndiye anaweza kushikilia mtazamo mtulivu mbele ya kifo, na anayeweza kukaribisha awamu hii ya mwisho kwa furaha. Bila shaka Ayubu alikuwa na mtazamo kama huu kwa kifo; alikuwa katika nafasi ya kukubali kwa furaha awamu ya mwisho ya maisha, na baada ya kuhitimisha safari yake ya maisha vizuri, baada ya kukamilisha kazi yake maalum alirudi upande wa Muumba.

5. Bidii na Faida za Ayubu katika Maisha Zamruhusu Kukabiliana na Kifo kwa Utulivu

    Katika Maandiko imeandikwa kuhusu Ayubu: “Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku.” (Ayubu 42:17). Hii inamaanisha kwamba wakati Ayubu alipoaga dunia, hakuwa na majuto na hakuhisi maumivu, lakini aliondoka kimaumbile ulimwenguni. Kama vile kila mmoja anavyojua, Ayubu alikuwa mwanamume aliyemcha Mungu na aliyeambaa maovu alipokuwa hai; Mungu alimpongeza kwa matendo yake ya haki, watu waliyakumbuka, na maisha yake, zaidi ya yeyote yule mwengine, yalikuwa na thamani na umuhimu. Ayubu alifurahia baraka za Mungu na aliitwa mtakatifu na Yeye hapa duniani, na aliweza pia kujaribiwa na Mungu na kujaribiwa na Shetani; alisimama kuwa shahidi wa Mungu na alistahili kuwa mtu mtakatifu. Kwenye miongo mbalimbali baada ya kujaribiwa na Mungu, aliishi maisha ambayo yalikuwa yenye thamani zaidi, yenye maana zaidi, yaliyokita mizizi, na yenye amani zaidi kuliko hata awali. Kutokana na matendo yake ya haki, Mungu alimjaribu; kwa sababu ya matendo yake ya haki, Mungu alionekana kwake na kuongea naye moja kwa moja. Kwa hiyo, kwenye miaka yake baada ya kujaribiwa, Ayubu alielewa na kushukuru thamani ya maisha kwa njia thabiti zaidi, aliweza kutimiza ufahamu wa kina zaidi wa ukuu wa Muumba, na akapata maarifa yenye hakika na usahihi zaidi kuhusu namna ambavyo Muumba anavyotoa na kuzichukua baraka zake. Biblia inarekodi kwamba Yehovah Mungu alimpa hata baraka nyingi zaidi Ayubu kuliko hapo awali, Akimweka Ayubu katika nafasi bora zaidi ya kujua ukuu wa Muumba na kujua kukabiliana na kifo akiwa mtulivu. Kwa hiyo, Ayubu alipozeeka na kukabiliana na kifo, bila shaka asingekuwa na wasiwasi na mali yake. Hakuwa na wasiwasi wowote, hakuwa na chochote cha kujutia, na bila shaka hakuogopa kifo; kwani aliishi maisha yake akitembea ile njia ya kumcha Mungu, kuepuka maovu, na hakuwa na sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi kuhusu mwisho wake mwenyewe. Ni watu wangapi leo wanaweza kuchukua hatua kwa njia zote hizo ambazo Ayubu alitumia alipokabiliwa na kifo chake mwenyewe? Kwa nini hakuna mtu anayeweza kuendeleza mwelekeo wa mtazamo rahisi kama huu? Kunayo sababu moja tu: Ayubu aliishi maisha kwenye harakati ya kutafuta kimsingi kusadiki, utambuzi, na unyenyekevu kwa ukuu wa Mungu, na ilikuwa katika kusadiki huku, utambuzi huu na unyenyekevu huu ambapo aliweza kupitia zile awamu muhimu za maisha, aliishi kwa kudhihirisha miaka yake ya mwisho na akajuliana hali na awamu yake ya mwisho ya maisha. Licha ya kile ambacho Ayubu alipitia, bidii zake na shabaha zake katika maisha zilikuwa za furaha na wala si zenye maumivu. Alikuwa na furaha si tu kwa sababu ya baraka au shukrani aliyopewa yeye na Muumba, lakini muhimu zaidi kwa sababu ya shughuli zake na shabaha za maisha, kwa sababu ya maarifa yaliyoongezeka kwa utaratibu na ufahamu wa kweli wa ukuu wa Muumba ambao alitimiza kupitia kwa kumcha Mungu na kwa kuepuka maovu, na zaidi, kwa sababu ya matendo Yake ya maajabu ambayo Ayubu alipitia kibinafsi wakati huu akiwa chini ya ukuu wa Muumba, na hali aliyopitia yenye uchangamfu na isiyosahaulika na kumbukumbu za kuwepo kwake, kuzoeana na wenzake, na kuzoeana kati yake yeye na Mungu; kwa sababu ya tulizo na furaha zilizotokana na kujua mapenzi ya Muumba; kwa sababu ya kustahi kulikotokea baada ya kuona kwamba Yeye ni mkubwa, ni wa ajabu, Anayependeka, na ni mwaminifu. Sababu ya Ayubu kuweza kukabiliana na kifo bila ya kuteseka ni kwamba alijua kwamba, kwa kufa, angerudi kwenye upande wa Muumba. Na zilikuwa shughuli zake katika maisha zilizomruhusu kukabiliana na kifo akiwa ametulia, kukabiliana na matarajio ya Muumba kuchukua tena maisha yake, kwa moyo mzuri, na zaidi ya yote, kusimama wima, kutotikisika na kuwa huru kutokana na mashaka mbele ya Muumba. Je, watu wanaweza siku hizi kutimiza aina ya furaha ambayo Ayubu alikuwa nayo? Je, nyinyi wenyewe mko katika hali ya kufanya hivyo? Kwa sababu watu siku hizi wako hivyo, kwa nini hawawezi kuishi kwa furaha, kama alivyofanya Ayubu? Kwa nini hawawezi kutoroka mateso yanayotokana na woga wa kifo? Wakati wanapokabiliwa na kifo, baadhi ya watu hujiendea haja ndogo; wengine hutetemeka, wakazirai, na wakalalamika dhidi ya Mbinguni na binadamu vilevile, wengine hata wakalia kwa huzuni na kutokwa machozi. Kwa vyovyote vile, hii ndiyo miitikio ya ghafla inayofanyika wakati kifo kinapokaribia. Watu huwa na tabia hii ya kuaibisha haswa kwa sababu, ndani ya mioyo yao, wanaogopa kifo, kwa sababu hawana maarifa yaliyo wazi na uwezo wa kushukuru ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hata kujinyenyekeza mbele ya vitu hivi; kwa sababu watu hawataki chochote ila kupangilia na kutawala kila kitu wenyewe, kudhibiti hatima zao binafsi, maisha yao binafsi na hata kifo. Si ajabu, hivyo basi, kwamba watu hawajawahi kuweza kuacha woga wa kifo.

6. Ni kwa Kukubali tu Ukuu wa Muumba Ndipo Mtu Anaweza Kurejea Upande Wake

    Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.

Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba

    Awamu sita zilizofafanuliwa hapo juu ni awamu muhimu zilizowekwa wazi na Muumba ambazo kila mtu wa kawaida lazima apitie katika maisha yake. Kila mojawapo ya awamu hizi ni za kweli; hakuna mojawapo kati yazo ambayo inaweza kuepukwa, na zote zinasheheni uhusiano na kuamuliwa kabla kwa Muumba na ukuu Wake. Hivyo basi kwa binadamu, kila mojawapo ya awamu hizi ni sehemu muhimu ya kujikagua, na namna ya kupitia kila mojawapo vizuri ni suala muhimu sana ambalo nyinyi nyote mnakabiliwa nalo.
    Mkusanyiko wa miongo ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka ishirini na-kitu iliyopo katikati ya kuzaliwa na kukomaa hupita kwa muda mfupi tu wa kupepesa jicho, na ingawaje wakati huu katika maisha mtu anachukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika kundi hili la umri wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Wanapozidi kupata uzoefu zaidi, ndipo wanapopiga hatua kwa utaratibu hadi kwenye umri wa miaka ya kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini huanza kuupata uzoefu unaoanza kuota wa maisha na hatima yake, lakini fikira zao kuhusu mambo haya zingali na ukungu mwingi sana akilini mwao. Si mpaka umri wa arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kumwelewa binadamu na ulimwengu, vilivyoumbwa na Mungu, na kung’amua kwamba maisha ya binadamu yanahusu tu, kile ambacho hatima ya binadamu inahusu. Baadhi ya watu, ingawaje wamekuwa wafuasi wa muda mrefu wa Mungu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sikwambii hata unyenyekevu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawaje wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo hoja ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kwenye kipindi cha matendo halisi cha kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wajinga kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao bure bilashi.
    Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa kwa sura tatu. Sura ya kwanza ni ujana, miaka ile ya kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kuanzia kuzaliwa hadi kugonga miaka thelathini. Sura ya pili ni ya ukomavu, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi sitini. Na sura ya tatu ni kile kipindi cha uzee wa mtu, kuanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini hivi, mpaka pale mtu anapoondoka ulimwenguni. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha ni finyu na ni yale ya kuiga tu kama kasuku, fikira za wengine yanayokosa hali halisi iliyo ya kweli na ya matendo. Kwenye kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na namna ambavyo mtu anapojipanga katika ulimwengu vyote ni vya juujuu na vinyonge sana. Hiki ndicho kipindi cha mtu cha utoto. Baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo anapofaidi na kupata ufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—kwa kufichika akilini, na ndani kabisa ya moyo wake—huanza kwa utaratibu kushukuru kutoweza kurudishwa nyuma kwa hatima, na kuanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha kuanza kukomaa kwa mtu. Baada ya mtu kusita kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, na kujumlisha mafanikio na makosa ya maisha ya mtu huyo, na anasubiria hukumu ya Muumba kwa maisha ya mtu—hiki ni kipindi cha ukomavu. Tukitilia maanani aina hizi tofauti za kile mtu amepitia na kufaidi ambako watu hupata kwenye vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au karibu na hapo kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na kanuni za sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawaje ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua hoja ya ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, watu wale wanaotaka kazi ya Mungu kuisha haraka, wanaopenda Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama hali Yake halisi na muda si muda kubarikiwa, wanayo hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na ujinga wa kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, kwenye muda wao finyu, kung’amua fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu werevu, wenye akili zao. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na shughuli za kufuatilia: Wale wanaotafuta baraka ni wachoyo na waovu; hawatilii maanani mapenzi yoyote ya Mungu, wala hawatafuti kujua ukuu wa Mungu, wasiwahi kutamani kujinyenyekeza katika utawala huo, wanataka kuishi tu wanavyopenda. Wao ni watovu wa wema; wao ndio wanaofaa kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kutimiza tamanio la Mungu. Watu kama hao huishi kwa nuru, huishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kupongezwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda gani ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka katika huruma ya Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka katika huruma Yake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka katika huruma Yake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kijinga, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatapata maana na kuepuka kuwa hapo tu, ndipo watakapopata wokovu.

Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu

    Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yako ya hatima imebadilika? Unaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Umeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama ubinadamu utayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!

Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu

    Mwanadamu anatakiwa kuwa na mtazamo gani sasa katika kujua na kujali mamlaka ya Mungu, hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo la kweli linalokabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima waendeleze, kuelewa kile ambacho lazima kitimizwe na njia ambazo lazima wahifadhi, waelewe ni matokeo gani ambayo Mungu analenga kutimiza kwa binadamu na ni utimilifu gani Analenga kutimiza ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima ufanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo unapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.

Kumkubali Mungu kama Bwana Wako wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu

    Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao mwelekeo katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni ya kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kawaida, kwa kila hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukua mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutafaidi hata chembe maarifa ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo mingi, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, maarifa yako ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu yatakuwa kwa hakika sufuri bin sufuri. Huoni kuwa jambo hili ni la huzuni mno? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama baadhi yenu mngependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninawaambia, hilo haliwezekani! Kama baadhi yenu mwataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya ubinadamu ulioumbwa, lakini juu ya hata viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Hii ni hoja isiyopingika, hoja ambayo kweli ipo, ambayo hakuna binadamu au kiumbe chochote kinaweza kubadilisha. Kama baadhi yenu mngali hamjatosheka na mambo kama yalivyo, mnaamini kwamba mna ujuzi fulani maalum au uwezo, na bado mnafikiria mnaweza kubahatika na kubadilisha hali zenu za sasa au vinginevyo kuzitoroka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako kupitia kwa jitihada za binadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako binafsi wa kupita kiasi, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawaje sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kushukuru zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana wa hatima ya maisha, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Haijalishi kama kwa kweli unao moyo na, haijalishi kama wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea tu ni mtazamo aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na ule ukweli. Na, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakosa thamani kabisa, bila shaka utakuwa athari ya chukizo na zao la kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli. Kwa sababu wameujua ukuu wa Mungu, kwa sababu wameukubali, shukrani yao ya na kujinyenyekeza kwao katika hoja ya Mungu juu ya hatima ya binadamu ni ya halisi na sahihi. Wanapokabiliana na kifo wataweza, kama Ayubu, kuwa na akili isiyotishika na kifo, kujinyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Mungu katika mambo yote, bila chaguo lolote la kibinafsi, bila tamanio lolote la kibinafsi. Mtu kama huyo tu ndiye atakayeweza kurudi katika upande wa Muumba kama kiumbe cha kweli cha binadamu kilichoumbwa.
Machi 26, 2015
     Tanbihi:
     a. Maandishi asilia yameacha kauli “zile hali za.”
     b. Maandishi asilia yanasoma “hii.”
     c. Maandishi asilia yameacha “Katika wakati huu.”
     d. Maandishi asilia yameacha “Bila kujua.”
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Masomo yanayohusiana: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni