3/31/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IπŸ“–πŸŽ‰


Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu

πŸŽ‰~~~~~~~~*~~~~~~~~🀲***************πŸ‘‚~~~~~~~~~*~~~~~~~~πŸ””    

^^^^^      ~~~~~~      ^^^^^       ~~~~~~       ^^^^^^      ~~~~~~    ^^^^^

    Mwenyezi Mungu alisema, Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule ni sura mbaya kweli, hakuna vile ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kijinga ulioje! Kile wanachofaa kusema ni, “ingawaje mdudu huyu ana sura mbaya sana, aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Kwenye fikira za Mungu, Alinuia kupatia kila mojawapo ya sura, na kazi na matumizi aina zote, katika viumbe mbalimbali vilivyo na uhai Alivyoumba, na hivyo basi hamna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia sura yao ya nje hadi mkusanyiko wao wa ndani, kuanzia katika mazoea yao ya kuishi hadi mahali pa kuishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana sura ya ng’ombe, punda wana sura ya punda, paa ana sura ya paa, na ndovu wana sura ya ndovu. Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi kinachovutia zaidi na ni kipi kinachotisha zaidi kwa sura? Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi chenye manufaa zaidi na uwepo wa kile ambacho hakihitajiki sana? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu hufanana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui mkubwa mwenye milia walivyo, kwani sura inavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na viumbe vyote, binadamu anafaa kurejelea mamlaka ya Muumba, hivi ni kusema kwamba, rejelea mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika viumbe vyote; huu ndio mtazamo wenye hekima zaidi. Mtazamo tu wa kutafutiza, na wa kuwa mtiifu, kwa nia ama makusudio ya mwanzo ya Muumba ndio ukubalifu wa kweli na hakika wa mamlaka ya Muumba. Ni vyema kwa Muumba, kwa hivyo ni sababu gani ambayo binadamu atakuwa nayo ya kusema kwamba si vyema?
     Hivyo basi, viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba....

Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba

    Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, ingawaje vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawaje wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!
    Kupitia ushirika uliotajwa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Kiongozi wa viumbe vyote tu, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung'amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu kutazama vitendo halisi vya dhana nyingi za mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kushukuru, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.
    2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu.
    
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Baada ya Kuumba Viumbe Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye “Agano la Upinde wa Mvua”

    Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye hatawali tu hatima ya viumbe vyote, lakini pia Anatawala mwanadamu, kiumbe maalum ambacho Aliumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa uhai. Baada ya kuumba viumbe vyote, Muumba hakusita kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya viumbe vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kusimamia mwanadamu, kutawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kufaidi mwanadamu kwa kweli, kufaidi mwanadamu ambaye angetawala viumbe vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kutambua matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mbele katika sehemu zote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.
    Kunao mfanano kati ya fungu kwenye Mwanzo 9:11-13 na Mafungu yaliyo hapo juu yanayohusu rekodi za Mungu kuumba ulimwengu, ilhali kunayo pia tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, fungu hili ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utiliaji mkazo huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na Mungu, hivi ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia himizo na onyo kwa binadamu, na zaidi, kulikuwa na amri zilizotolewa kwa viumbe vyote vilivyokuwa na mamlaka Yake.
    Ni hatua gani ya Mungu imerekodiwa katika fungu hili? Inarekodi agano ambalo Mungu alianzisha na binadamu baada ya Yeye kuangamiza ulimwengu kwa gharika, linamwambia binadamu kwamba Mungu asingesababisha maangamizo katika ulimwengu tena, na kwamba, hadi mwisho huu, Mungu aliumba ishara—na ishara hii ilikuwa nini? Kwenye Maandiko inasemekana kwamba “naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.” Haya ni matamshi ya asili yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu fulani Yake mwenyewe kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya kimbinguni yatakayobakia milele hivyo, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, lazima isemwe, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa viumbe vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba havina mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na kilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka hadi leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu ni mzuri tu kama matamshi Yake, na matamshi Yake yataweza kukamilishwa, na kile ambacho kimekamilishwa kinadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inapambanua utambulisho na hali halisi inayomilikiwa tu na Muumba kutoka ile ya viumbe. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.
     Uanzishaji wa agano Lake Mungu na binadamu kilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na hadi hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa vipi? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwengine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, uzima wa “agano la upinde wa mvua” ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kushukuru, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwani hamna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika kujitokeza kwingine kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, lakini ni mamlaka yenyewe yasiyobadilika ya Muumba. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya kipekee na ya kimiujiza ya Muumba yanayopatikana kwenye sehemu zilizofichwa, na, wakati uo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kufifia, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la dhana nyingine ya mamlaka ya kipekee ya Muumba?
    3. Baraka za Mungu
    Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.
    Mwa 18:18-19 Kuona kwamba Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye? Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.
    Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.
  Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Njia na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

    Wengi hupenda kutafuta, na kufaidi, baraka za Mungu, lakini si kila mmoja anayeweza kufaidi baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Na kwa hivyo ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Huwa zinatwambia nini? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, au kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa kusudio la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.
    Mafungu manne ya maandiko yaliyotajwa hapo juu yote ni rekodi kuhusu baraka za Mungu kwa binadamu. Yanatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile yanatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa kwenye baraka hizi. Ile sauti na njia ya matamshi ya Mungu, mtazamo na mahali ambapo Alitamka, huturuhusu kushukuru kwamba Yule anayetoa baraka na mpokeaji wa baraka kama hizo ni wenye utambulisho, hadhi, na hali halisi tofauti kabisa. Sauti na njia ambayo matamshi haya yanatolewa, na mahali ambapo yalitamkwa, vinaonyesha upekee wao kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na adhama isiyovumilia shaka kutoka kwa binadamu yeyote.
    Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6: “Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.” Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni dhana gani ya hali halisi ya mamlaka ya Mungu unayoona? Kutoka kwa usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi na maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe…,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati uliozoeleka. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwengine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatatokana na wao, na kuwa wafalme watatoka miongoni mwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, hawathubutu kusema “Mimi nitakufanya kuwa hivi na hivi, kufanya hivi na hivi…,” kwani wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia ufanisi mkubwa. Ni utajiri upi mkubwa utakaokuwepo kama mmoja wao angekuwa mfalme mkuu! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu! Haya yote ni matamanio ya watu wote, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao ni zaidi ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima ya wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema mambo kama haya ni kwa vile Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kutambua ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazomwombea binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na ili Mungu aweze kumuumba mtu atakayezidi kwa uzao ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hatawahi kufanya kazi Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujifunga mafunda mbalimbali; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.
    Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Unaweza kuhisi hali isiyokuwa ya kawaida ya Muumba? Unaweza kuhisi hali ya mamlaka ya juu ya Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au kwa kuwakilisha, ujasiri Wake katika ufanisi; hayo ni, badala yake, ithibati ya mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kunazo semi mbili ambazo unafaa kutilia maanani hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” kunayo dalili ya kutoeleweka kwenye maneno haya? Kunayo dalili yoyote ya wasiwasi? Kunayo dalili yoyote ya woga? Kwa sababu ya matamshi “ataweza kwa hakika” na “atakuwa” kwenye matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna yule angethubutu kubariki mwengine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Maneno ya Mungu yanapokuwa na uhakika zaidi, ndipo yanathibitisha kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba ufanisi wake ni lazima. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, uzima wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Licha ya kilichotendeka, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uzito wenyewe wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywa cha Mungu, na kunazo nguvu, adhama na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na hoja zimethibitisha kuwa ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo ya kupitisha wakati, lakini ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.
    Ni nini tofauti kati ya maneno yanayotamkwa na Mungu na yale yanayotamkwa na binadamu? Unaposoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, unahisi nguvu za maneno ya Mungu, na mamlaka ya Mungu. Je, unahisi vipi unaposikia watu wakitamka maneno kama hayo? Je, unafikiria kuwa wao wana kiburi kupindukia, na ni wenye kujigamba na kujionyesha? Kwani hawana nguvu hizi, hawamiliki mamlaka kama haya, na hivyo basi hawawezi kabisa kutimiza mambo kama hayo. Kwamba wao wana hakika kabisa kuhusu ahadi zao, yaonyesha tu kutojali kwa matamshi yao. Kama mtu anasema maneno kama hayo, basi bila shaka watakuwa wenye kiburi, na waliozidisha ujasiri wao, huku wakijifichua kama mfano wa pekee wa tabia ya malaika mkuu. Maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu; je, unahisi dalili yoyote ya kiburi hapa? Je, unahisi ya kwamba matamshi ya Mungu ni mzaha tu? Matamshi ya Mungu ni mamlaka, Maneno ya Mungu ni hoja za kweli, na kabla hajatamka maneno kutoka kinywani Mwake, hivi ni kusema, wakati Anapofanya uamuzi wa kufanya kitu, tayari kitu hicho kimefanyika. Yaweza kusemwa kwamba kila kitu alichosema Mungu kwa Ibrahimu kilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, na ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu. Ahadi hii ilikuwa hoja iliyoanzishwa, pamoja na hoja iliyokamilika, na hoja hizi zilitimizwa kwa utaratibu kwa fikira za Mungu kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu kusema maneno kama hayo haimaanishi kuwa Ana tabia ya kiburi, kwani Mungu anaweza kutimiza mambo kama hayo. Anazo nguvu na mamlaka, na ana uwezo wa kutimiza hoja hizi, na mafanikio yake kwa jumla yanapatikana ndani ya uwezo Wake. Wakati maneno kama haya yanapotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, yanakuwa ufunuo na maonyesho ya tabia ya kweli ya Mungu, ufunuo na maonyesho timilifu ya hali halisi na mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu ambacho kinafaa zaidi na kizuri kama ithibati ya utambulisho wa Mungu. Namna, sauti, na mpangilio wa maneno ya matamshi kama hayo ndiyo alama haswa ya utambulisho wa Muumba, na vyote hivi vinalingana kwa njia timilifu na maonyesho na utambulisho wa Mungu, na ndani yao hakuna kusingizia, au kasoro; vyote hivi ni, onyesho timilifu na lililo kamili kabisa, la hali halisi na mamlaka ya Muumba. Lakini Kuhusu viumbe, havimiliki mamlaka haya, wala hali hii halisi, vilevile havimiliki nguvu inayotolewa na Mungu. Kama binadamu atasaliti tabia kama hiyo, basi hali hiyo itakuwa bila shaka mlipuko wa tabia yake iliyopotoka, na itaishia kwa athari ya kujihusisha visivyofaa na kiburi cha binadamu na maono yasiyo na mipaka, na kufichuliwa kwa nia haribifu za yuleyule ibilisi, Shetani, anayependa kudanganya watu na kuwashawishi kuweza kusaliti Mungu. Naye Mungu anachukuliaje kile ambacho kimefichuliwa kwa lugha kama hii? Mungu angesema kwamba ungependa kunyakua nafasi Yake na kwamba unapenda kumwiga Yeye na kumbadili Yeye. Wakati unaiga sauti ya matamshi ya Mungu, nia yako ni ya kubadilisha mahali pa Mungu katika mioyo ya watu, kujitwalia mwanadamu ambaye anamilikiwa kwa haki na Mungu. Huyu ni Shetani, wazi na bila kukuficha; haya ni matendo ya vizazi vya malaika mkuu visivyovumilika Mbinguni! Miongoni mwenu, kunao wowote waliowahi kuiga Mungu kwa njia fulani kwa kuongea maneno machache, kwa nia ya kupotosha na kudanganya watu na kuwafanya watu kuhisi kuwa maneno na matendo ya mtu huyu yana mamlaka na nguvu za Mungu, kama kwamba hali halisi na utambulisho wa mtu huyo ni vya upekee, na hata ni kana kwamba sauti ya mtu huyu ni sawa na ile ya Mungu? Umewahi kufanya jambo kama hili? Umewahi kuiga sauti ya Mungu kwenye matamshi yako, kwa miondoko iliyodai kuwakilisha tabia za Mungu, ikiwa pamoja na uwezo na mamlaka ya kudhaniwa? Je, wengi wenu huwa mara nyingi mnatenda, au kupanga kutenda kwa njia kama hiyo? Sasa, unapoona kwa kweli, kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, na kutazama kile ulichokuwa ukikifanya, na ulichokuwa ukifichua kujihusu, je, unahisi vibaya? Je, unatambua hali yako ya kutoheshimu na kuwa na utovu wa haya? Baada ya kuchambua tabia na hali halisi ya watu kama hawa, je, inaweza kusemekana kuwa wao ndio walaaniwa wa jahanamu? Yaweza kusemekana kuwa kila mtu anayefanya mambo kama haya anajiletea udhalilishaji? Je, unatambua uzito wa asili yake? Na uzito wake ni wa kiasi kipi? Nia ya watu wanaotenda mambo kwa njia hii ni kuiga Mungu. Wanataka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kuwaabudu kama Mungu. Wanataka kuondoa nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, na kutupilia mbali yule Mungu anayefanya kazi miongoni mwa binadamu, ili kutimiza nia ya kuwadhibiti watu, na kuwateketeza watu, na kuwamiliki watu hao. Kila mmoja anayo matamanio na maono kama hayo yaliyofichika akilini, na kila mmoja anaishi katika hali halisi potovu na ya kishetani kama hiyo na anaishi katika asili ya kishetani ambapo yumo katika uadui na Mungu, na anamsaliti Mungu, na anapenda kuwa Mungu. Kufuatia Ushirika Wangu katika mada hii ya Mungu, bado ungependa au ungetamani kujifanya wewe ni Mungu, au kuiga Mungu? Na bado unatamani kuwa Mungu? Ungali unapenda kuwa Mungu? Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawaje unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga hali halisi ya Mungu. Ingawaje unaweza kusimama mahali pa Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru viumbe vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, uzima wako wewe umetawaliwa na Muumba. Ingawaje unaweza kusema maneno fulani ya kijeuri, hilo haliwezi kuonyesha kuwa unayo hali halisi ya Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni hali halisi ya Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni hali ya asili ya Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe hauwezi katu kubadilishwa. Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia.

Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki

    Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.” Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao elfu moja, mbili, au hata elfu nyingi, lakini idadi isiyohesabika, iliyotosha kuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti uzao kiasi gani atakaokuwa nao? Je, inategemea yeye? Haitegemei binadamu kujua kama atakuwa na uzao mbalimbali au la, sikwambii uzao mwingi kama “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote yanategemea Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!
    Wakati Mungu alisema “nitazidisha mithili,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.
      Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawaje baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimefifia polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alisisitiza mamlaka Yake, namna ambavyo vitu vyote vilivyoundwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila kipande kizuri cha onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kutukuzwa miongoni mwa viumbe vyote, viumbe vyote vilijitokeza na kuongea kuhusu vitendo vya kimiujiza vya Muumba, na kila mojawapo ya hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote itaweza kutangazwa na viumbe vyote daima dawamu. Mamlaka ambayo Mungu anatawala viumbe vyote, na nguvu za Mungu, vinaonyesha viumbe vyote kwamba Mungu anapatikana kila pahali wakati wote. Wakati unashuhudia upekee wa mamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.
     Baadhi ya watu wanapenda kujijazia na kujifikiria, lakini, mawazo ya binadamu yanaweza kufikia wapi? Yanaweza kuzidi ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kujijazia na kufikiria uhalali na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, kule kujijazia na kujifikiria kwa binadamu kunaweza kuruhusu yeye kufikia maarifa ya mamlaka ya Mungu? Vinaweza kufanya binadamu kushukuru kwa kweli na kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Mungu? Hoja zinathibitisha kwamba uingiliaji kati na kufikiria kwa binadamu ni zao tu la akili za binadamu, na hakutoi hata msaada kidogo au manufaa kidogo kwa maarifa ya binadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala ya kidhahania ya kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni huku tu: kufikiria. Kuhusiana na hoja za mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kwa kurejelea muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung'amuzi wowote. Na je, ikiwa umeenda hadi mwezini? Je, hii inaonyesha kuwa unao ufahamu wa pande nyingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu huko kuingilia kati na kufikiria kwa mwanadamu hakuwezi kumruhusu kujua mamlaka ya Mungu, je, binadamu anafaa kufanya nini? Chaguo lenye hekima zaidi ni kutojijazia au kutojifikiria, ambapo ni kusema kwamba binadamu asiwahi kutegemea kufikiria na kutegemea uingiliaji kati inapohusu kujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho binafsi wa Mungu, na hali halisi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa kutegemea kufikiria kwako. Kwa vile huwezi kutegemea kufikiria ili kujua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kutimiza maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na hali halisi ya kujua kwa utaratibu na uthibitishaji wa mamlaka ya Mungu na hivyo basi utafaidi kuelewa kwa utaratibu na maarifa yaliyoongezeka. Hii ndiyo njia tu ya kutimiza maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuuliza kutofikiria si sawa na kukufanya uketi kimyakimya ukisubiri maangamizo, au kukusitisha dhidi ya kufanya kitu. Kutotumia akili zako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki ya kujijazia, kutotumia maarifa kuchambua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufurahia, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye Mungu Mwenyewe ni wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza nia hii, lakini unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Nakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua kwa uangalifu na bila kusita na kuhakikisha kile Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analolielezea na Analolifanya. Hii ndiyo njia pekee ya kujua Mungu. Kwani kile Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si cha wazi na tupu—lakini cha kweli.

    Hoja ya Udhibiti wa Muumba na Utawala Juu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Inazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba

     Vilevile, baraka za Yehova Mungu kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kutoka kwenye mtazamo wa binadamu, ni vitu gani alivyopewa Ayubu? Je, vilikuwa rasilimali ya binadamu? Akiwa na rasilimali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwenye kipindi hicho? Na aliwezaje kumiliki rasilimali kama hizo? Ni nini kilisababisha utajiri wake? Bila shaka ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu ambapo Ayubu alifanikiwa kumiliki. Namna ambavyo Ayubu alitazama rasilimali hizi, na vipi alivyochukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Tunapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na idadi ngapi ya rasilimali anaweza kufaidi katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—na hii ni hoja isiyopingika! Mungu anayo mamlaka, na nguvu za kumpatia mwanadamu rasilimali yoyote, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni ya baraka za Mungu. Ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki? Watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu walibarikiwa wote na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alibariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalitawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi za Mungu miongoni mwa viumbe vyote na viumbe vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huyu mwanadamu aliweza kupenyeza na kuwepo kwa kasi, na ndani ya upana, ulioamuliwa na Mungu. Haswa, uwezo wa taifa hili, kima cha upanuzi, na matarajio ya maisha vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitokana kwa ujumla kwa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea mbele bila kizuizi na kuweza kutambuliwa kulingana na uwepo wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, licha ya misukosuko ya ulimwengu, licha ya umri, licha ya majanga yanayovumiliwa na mwanadamu, vizazi vya Ibrahimu visingeweza kukabiliwa na hatari ya maangamizo, na taifa lao lisingefifia na kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya kuwa tajiri wa kupindukia. Kile Mungu alichompa kilikuwa mseto wa viumbe hai, vinavyopumua, maelezo yake yalikuwa—idadi yao, kasi yao ya kuzaa, kima cha kuishi, kiwango cha mafuta kwenye viumbe hivyo, na kadhalika—vilidhibitiwa pia na Mungu. Ingawaje viumbe hivi hai havikumiliki uwezo wa kuongea, navyo pia vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na Ayubu, ingawaje kile kilichokuwa kimeahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitumia kutawala viumbe vyote na viumbe vilivyo na uhai yalikuwa yale yale. Kila maelezo ya mamlaka na Nguvu za Mungu yameonyeshwa kwenye ahadi Zake tofauti na baraka zake kwa Ibrahimu na Ayubu, kwa mara nyingine zaonyesha binadamu kwamba mamlaka ya Mungu ni zaidi ya kufikiria kwa binadamu. Maelezo haya yanamwambia binadamu kwa mara nyingine kwamba kama angetaka kujua mamlaka ya Mungu, basi hii itawezekana tu kupitia kwa maneno ya Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu.
       Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya viumbe vyote huruhusu binadamu kuweza kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika matamshi “Mungu akasema, na Kuwepo na nuru, na kukawa na nuru, na, Kuwepo na anga, na kukawa na anga, na, Kuwepo na ardhi, na kukawa na ardhi,” lakini, vilevile namna Alivyofanya nuru ile kuendelea kuwepo, kulizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, pamoja na maelezo ya namna Alivyotawala na kusimamia viumbe: nuru, anga, na ardhi. Nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa mwanadamu? Ni wazi, kwamba baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikusita, kwani Alikuwa tu ameanza kuonyesha mamlaka Yake, na Alinuia kuhakikisha kwamba kila mojawapo ya matamshi Yake yangekuwa uhalisia, na kuhakikisha kuwa kila mojawapo ya maelezo ambayo Alizungumza yanatokea kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu anayo mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote yaweze kutimizwa. Kufikiria hivyo, ni, lazima Niseme, mzaha! Kama utachukua mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu na Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na hoja mbalimbali ambazo mamlaka ya Mungu yanatawala juu ya kila kitu, basi ufahamu wako kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni mdogo mno na wa mzaha! Kama binadamu anafikiria Mungu kuwa hivyo, basi, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anafikiria kuhusu ni mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande halisia wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, ingawaje Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawaje Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa kihalisia wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata ingawaje wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawaje binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawaje umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na ni Yasiyokosewa

    Ni nini umeona katika sehemu hizi tatu za maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, nalo agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka “Mimi nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni,” siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawaje Mungu anayamiliki mamlaka na nguvu, Anayo bidii sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Bidii Yake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na namna ambavyo mamlaka ya Muumba yalivyo magumu kushindwa. Ingawaje Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Sina haja ya kusema kwamba kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Kwenye macho ya Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi, kwenye utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatumiwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na ni yasiyokosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!
      Maneno yaliyo hapa chini ni lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
    Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni