5/02/2018

Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

     Mwenyezi Mungu alisema, Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, umri, na walichokifanya maishani mwao. Kila walichokifanya maishani mwao kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni. Hilo halitishi sana.
    Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa sehemu atakayopelekwa, sehemu ambayo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi walizotenda, na ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—ambalo ni tukio la kwanza kutokea katika hatua ya pili. Kwa sababu ya mambo waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, katika kupata mwili kwao kunakofuata hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la.
    Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo haliogopeshi? Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na mafikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi kwa hakika. Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri au vibaya kuliko nguruwe? (Vizuri.) Inaonekana mkipewa fursa, mnapenda ustaarabu. Je, ingekuwa faraja zaidi kama mtu angekuwa paka? Itakuwa faraja zaidi kuliko kuwa farasi au ng’ombe. Mngeweza kuchagua kati ya wanyama, mngechagua kuwa paka, na hiyo ni faraja zaidi kwa sababu mngeweza kuupitisha muda wenu mwingi usingizini. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito, na kwa hivyo watu wakipata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo inaonekana kama adhabu nzito. Kuwa mbwa ni afadhali kidogo kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Aidha, siku hizi watu wengi hufuga mbwa na baada ya miaka mitatu au mitano mbwa huyu huwa amejifunza kuelewa mengi ya yale wanasema! Kwa kuwa mbwa anaweza kuelewa maneno mengi ya bwana wake, ana uelewa mzuri wa bwana wake, na anaweza kutohoa tabia na mahitaji kutoka bwana wake, kwa hiyo bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi—je, hivi mbwa hapati maisha ya furaha? Hivyo, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu anapata mwili kuwa mnyama, na anapata mwili kuwa aina gani ya mnyama. Mnaelewa, ndio?
    Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa na mzunguko mmoja wa uhai na mauti uliokamilika, na ina mambo makubwa. Tangu siku mtu anawasili katika ulimwengu wa kiroho hadi wakati adhabu yao inakamilika, wanaweza kupata mwili kama wanyama mara nyingi, halafu wajitayarishe kupata mwili kama wanadamu; huu ni mchakato mzima.
    Na wale waliokamilisha adhabu yao, na kamwe hawatapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Ni kwa haraka gani hawa watu watakuwa wanadamu?[a] Kwa hili kuna mipaka ya kiwakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kiwakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za kiwakati, na vipimo vyake ni vipi? Kuwasili kwa roho katika ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu, kunategemea uhitaji: inalingana na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao ni lazima wawe na nafasi maalum katika ulimwengu huu. “Maalum” inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili.[b] Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Huenda nyinyi nyote mnamjua; kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za kiwakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kupata mwili, na hizi sheria na desturi hutoka kwa Mungu, zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho. Sasa mnaelewa, naam?
    Kwa roho yoyote, nafasi zinayochukua baada ya kupata mwili—nafasi yao ni ipi katika haya maisha—watazaliwa katika familia gani, na maisha yao yatakuwaje vinahusiana kwa karibu na maisha yao ya zamani. Kila aina ya watu huja katika dunia ya wanadamu, na nafasi zao ni tofauti, kama zilivyo kazi wazifanyazo. Na hizi ni kazi gani? Watu wengine wanakuja kulipa deni: Ikiwa walikuwa na pesa nyingi za watu katika maisha yao ya awali, wanalipa deni. Wakati uleule, watu wengine, wamekuja kuchukua madeni yao: Walitapeliwa vitu vingi sana, na pesa nyingi sana katika maisha yao yaliyopita, na kwa hiyo, baada ya kuwasili katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapa haki na kuwapa fursa ya kukusanya madeni yao katika maisha haya. Watu wengine wamekuja kulipa deni la shukrani: katika maisha yao yaliyopita—kabla hawajafa—mtu alikuwa mkarimu kwao, na katika maisha haya wamepatiwa fursa nzuri kupata mwili ili kwamba waweze kuzaliwa upya ili kulipa upya deni hili la shukrani. Wakati uleule, wengine wamezaliwa upya katika haya maisha ili kudai uhai. Na wanadai uhai wa nani? Uhai wa mtu aliyewaua katika maisha yao yaliyopita. Kwa ujumla, maisha ya sasa ya kila mtu yana uhusiano mkubwa na maisha yao yaliyopita, yameungana kwa njia isiyoachana. Yaani, maisha ya sasa ya kila mtu yanaathiriwa pakubwa na maisha yao yaliyopita. Kwa mfano, kabla ya kufariki, Zhang alimtapeli Li kiwango kikubwa cha pesa. Je, Zhang ana deni la Li? Kama analo, ni kawaida kwamba Li anapaswa kuchukua deni lake kutoka kwa Zhang? Hivyo basi baada ya wao kufa, kuna deni kati yao ambalo linatakiwa kulipwa, na wakati wanapata mwili na Zhang anakuwa mwanadamu, je, Li anapataje deni hili kutoka kwake? Mbinu moja ni kwamba Li anapata deni lake kwa kuzaliwa upya kama mwanake Zhang, Zhang akiwa babake. Hili ndilo litafanyika katika maisha haya, katika maisha ya sasa. Babake Li, Zhang, anapata pesa nyingi, na zinaliwa na mwanake, Li. Haijalishi Zhang anapata pesa nyingi kiasi gani, mwanake Li “anamsaidia” kwa kuzitumia. Haijalishi Zhang anapata kiasi gani cha pesa, katu hazitoshi, na mwanake, wakati uleule, kwa namna fulani daima anazitumia pesa za babake kupitia njia na mbinu mbalimbali. Zhang anachanganyikiwa: “Ni nini kinaendelea? Kwa nini mwanangu daima amekuwa kisirani? Mbona wana wa watu wengine ni wema sana? Ni kwa nini mwanangu hana lengo, ni kwa nini hana maana na hana uwezo wa kuchuma pesa zozote, kwa nini daima ninapaswa kumsaidia? Kwa kuwa ni lazima nimsaidie, nitamsaidia, ila kwa nini hata nimpe pesa kiasi gani, daima anataka zaidi? Ni kwa nini asifanye kazi halali? Kwa nini yeye ni lofa, anakula, anakunywa, anazini, anacheza kamari—akiyafanya yote? Nini kinaendelea?” Halafu Zhang anafikiria kidogo: “Je, inaweza kuwa ni kwa sababu ananidai kutoka maisha ya zamani? O, inaweza kuwa ni kwa sababu nilikuwa na deni lake katika maisha ya zamani. Sawa basi, nitalilipa! Haya hayataisha hadi nilipe kikamilifu!” Inaweza kufika siku ambayo Li anafidia deni lake, na akiwa na umri wa miaka arobaini au hamsini, itafika siku ambayo atajitambua: “Sijafanya kitu kizuri hata kimoja katika hii nusu ya kwanza ya maisha yangu! Nimefuja pesa zote alizozipata baba—ninapaswa kuwa mtu mwema! Nitajikakamua: nitakuwa mtu ambaye ni mwaminifu, na anayeishi ipasavyo, na sitamletea babangu huzuni tena!” Kwa nini anafikiria hivi? Mbona anageuka kuwa mwema ghafla? Kuna sababu ya hili? Ni sababu gani? Kwa hakika, ni kwa sababu amepokea deni lake; deni limelipwa. Katika hili, kuna chanzo na matokeo. Kisa kilianza zamani sana, kabla hawa wawili hawajazaliwa, na kwa hivyo hiki kisa cha maisha yao ya zamani kimeletwa katika maisha yao ya sasa, na hakuna anayeweza kumlaumu mwingine. Haijalishi Zhang alimfundisha nini mwanake, mwanake hakumsikiliza, na hakufanya kazi halali hata ya siku—lakini siku ambayo deni lilipwa, hapakuwa na haja ya kumfundisha; mwanake alielewa kiasilia. Huu ni mfano rahisi, na bila shaka kuna mifano mingine kama huu. Na unawafunza watu kitu gani? (Wanapaswa kuwa wema.) Kwamba hawapaswi kutenda maovu, na kutakuwa na adhabu kwa maovu yao! Wengi wa wasioamini, unaona, hutenda maovu hayo na utendaji maovu wao umekutwa na adhabu, sawa? Je, hii adhabu ni ya kinasibu? Kila linalokutwa na adhabu lina asili na sababu. Unadhani hakuna litakalotendeka baada ya kumlaghai mtu pesa? Unadhani baada ya kuwatapeli pesa zao hakutakuwa na matokeo kwako baada ya kuchukua pesa zao? Hilo halitawezekana: utavuna ulichopanda—hili ni kweli kabisa! Ambayo ni kusema kwamba haijalishi wao ni nani, au kama wanaamini ama hawaamini kuwa kuna Mungu, kila mtu ni lazima atawajibikia mienendo yake na kubeba matokeo ya matendo yake. Kwa kurejelea huu mfano rahisi—Zhang kuadhibiwa, na Li analipwa—je ni haki? Ni haki. Watu wakifanya vitu kama hivyo, kuna aina hiyo ya matokeo. Na je, imejitenga na utawala wa ulimwengu wa kiroho? Haitenganishwi na utawala wa ulimwengu wa kiroho. Licha ya kuwa wasioamini, wale wasiomwamini Mungu, uwepo wao uko chini ya amri za peponi na sheria ambazo haziwezi kuepukika na yeyote; haijalishi nyadhifa zao katika ulimwengu wa mwanadamu ni za juu kiasi gani, hakuna anayeweza kuuepuka ukweli huu.
     Wale ambao hawana imani huamini kuwa kila kitu ambacho kinaweza kuonekana kipo, ilhali kila kitu kisichoonekana, au ambacho kiko mbali sana na watu, hakipo. Wanapenda kuamini kuwa hakuna “mzunguko wa uhai na mauti,” na hakuna “adhabu,” na kwa hiyo wanatenda dhambi na kufanya maovu bila majuto—ambayo baadaye wataadhibiwa kwayo, au watapata miili kama mnyama. Wengi wa watu mbalimbali miongoni mwa Wasioamini wanapatikana katika mzunguko huu. Na kwa nini hivyo? Kwa sababu hawajui kuwa ulimwengu wa kiroho ni mkali katika kuviendesha viumbe hai wote. Ikiwa unaamini au la, huu ukweli upo, na hakuna mtu hata mmoja au chombo chochote kinaweza kuepuka mawanda ya ambacho kinaonwa na macho ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja au chombo kinachoweza kuepuka sheria na mipaka ya sheria za peponi na amri za Mungu. Na hivyo basi Namwambia kila mmoja wenu mfano huu rahisi; haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu, haikubaliwi kutenda dhambi na kufanya maovu, kuna matokeo, na hili halina mjadala. Wakati mtu aliyemlaghai mwingine pesa anaadhibiwa hivyo, hiyo adhabu inafaa na ni ya busara, na ya haki. Mienendo inayoonekana ya kawaida kama hii inaadhibiwa na ulimwengu wa kiroho, inaadhibiwa na amri na sheria za mbinguni za Mungu, na vivyo hivyo uhalifu mkubwa na matendo maovu—ubakaji na unyang’anyi, ulaghai na udanganyifu, wizi na ujambazi, mauaji na uchomaji, na kadhalika—yanapitia adhabu aina aina zenye ukali wa viwango mbalimbali. Na hizi adhabu zenye ukali wa viwango mbalimbali zinajumuisha nini? Baadhi yake zinatumia muda kufikisha kiwango cha ukali, na nyingine hufikiwa kwa mbinu mbalimbali, na nyingi hufikiwa kupitia mahali mtu aendapo akipata mwili. Kwa mfano, watu wengine wana maneno machafu. Kuwa na “maneno machafu” kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwaapiza wengine mara kwa mara, na kutumia lugha chafu, lugha inayowalaani watu wengine. Lugha yenye nia mbaya inaashiria nini? Inaashiria kuwa mtu ana roho mbaya. Lugha yenye nia mbaya inayowalaani watu wengine mara nyingi inatoka vinywani mwa watu kama hao, na lugha yenye nia mbaya kama hiyo mara nyingi inaandamana na matokeo makali. Baada ya hawa watu kufa na kupokea adhabu stahili, wanaweza kuzaliwa kama mabubu. Watu wengine ni wajanja sana wakiwa hai, mara kwa mara wanawatumia watu wengine kwa manufaa yao, njama zao huwa zimepangwa barabara, na wanafanya mengi yanayowadhuru wengine. Wakizaliwa upya, wanaweza kuwa mataahira au mapunguani. Watu wengine mara nyingi huwachungulia watu wengine wakiwa faraghani; macho yao huona mengi ambayo hawakutakiwa kuona, na hujua mengi ambayo hawakupaswa kujua, hivyo basi wazaliwapo upya, wanaweza kuwa vipofu. Watu wengine ni hodari sana wakiwa hai, wanapigana mara kwa mara, na kufanya mengi ambayo ni maovu, na kwa hiyo wanapozaliwa upya, wanaweza kuwa vilema au wakakosa mkono, vinginevyo wanaweza kuwa vibyongo, au wenye shingo iliyopinda, huenda wakatembea wakichechemea, au wakawa na mguu mmoja mfupi kuliko mwingine, na kadhalika. Katika hali hii, wanapewa adhabu mbalimbali kutegemea kiwango cha maovu waliyotenda walipokuwa hai. Mwasemaje, kuhusu ni kwa nini watu huwa na makengeza? Je, kuna watu wengi wa hivyo? Kuna wengi wao siku hizi. Watu wengine wana makengeza kwa sababu waliyatumia macho yao sana katika maisha yao yaliyopita, walifanya mambo mengi mabaya, na kwa hiyo wazaliwapo katika haya maisha macho yao hupata makengeza, na katika hali mbaya, hata huwa vipofu. Je, unadhani hawa watu ambao ni makengeza wanapendeza? Je, wana sura nzuri? Ona jinsi walivyo wa wajihi mzuri wa uso, ngozi yao ni nyeupe isiyokuwa na doa, wana macho makubwa na vigubiko viwili—ila kwa bahati mbaya jicho lao moja lina kengeza. Wanaonekanaje? Je, hii haiathiri kabisa sura nzima ya mtu? Wakiwa na hii athari, wanakuwa na maisha ya aina gani? Wakikutana na wengine, wanajiwazia: “Ahaa, mimi nina makengeza! Sifai kuwaangalia watu sana, sitaki wayaone macho yangu. Ninapaswa kuzungumza huku nikiwa nimeinamisha kichwa changu, siwezi kuwatazama uso kwa uso.” Makengeza yao yanaathiri jinsi wanavyovitazama vitu, na uwezo wao wa kuwaangalia watu uso kwa uso. Katika hali hii, je, hawajapoteza matumizi ya macho yao? Je, matumizi yao kupita kiasi katika maisha yao yaliyopita hayajasawazishwa? Kwa hiyo katika maisha yao yafuatayo hawatathubutu kufanya kitu kibaya kama hicho. Haya ni malipo!
     Watu wengine wanaelewana vizuri na wengine kabla hawajafa, wanafanya mambo mengi mazuri kwa waliowazunguka, kwa wapendwa wao, marafiki, wenza, au watu wanaohusiana nao. Wanasaidia wengine, wanatoa hisani na matunzo kwa wengine, au kuwasaidia kifedha, wengine wanawaheshimu sana, na watu kama hao warudipo katika ulimwengu wa kiroho hawaadhibiwi. Kwa asiyeamini kukosa kuadhibiwa kwa njia yoyote inamaanisha alikuwa mtu mzuri sana. Badala ya kuamini katika uwepo wa Mungu, wanaamini tu katika Mzee aliye Angani. Wanaamini tu kuwa kuna roho juu yao akitazama yote wafanyayo—hayo tu ndiyo wanaamini. Na matokeo ni yapi? Wanakuwa na mwenendo mzuri. Hawa watu ni wenye huruma na wakarimu, na mwishowe wakirudi katika ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa kiroho utawapokea vizuri sana na watapata mwili na kuzaliwa upya mapema. Na watafikia katika familia za aina gani? Japo haitakuwa ya kitajiri, maisha ya kifamilia yatakuwa matulivu, kutakuwa na maelewano miongoni mwa wanafamilia, watakuwa na siku mwanana, za kupendeza, kila mmoja atafurahia, na watakuwa na maisha mazuri. Naye atakapokuwa mtu mzima, atapata wana na mabinti wengi, na kuwa na familia kubwa na jamaa wengi, watoto wake watakuwa na vipawa na kufanikiwa, yeye pamoja na familia yake watakuwa na bahati nzuri—na matokeo kama hayo yanahusiana kwa kiasi kikubwa na maisha ya zamani ya mtu. Yaani, maisha yote ya mtu, mpaka baada ya kufa na pale waendapo baada ya kupata mwili, wawe wanaume au wanawake, wito wao ni upi, watapitia nini maishani, vikwazo vyao, watapata baraka gani, watakutana na nani, ni nini kitawatokea—hakuna awezaye kulitabiri hili, kuliepuka, au kujificha kutokana nalo. Yaani, baada ya maisha yako kupangwa, kitakachokutokea, hata ujaribu namna gani kukikwepa, hata ukitumia mbinu gani kukiepuka, huna njia ya kuvuruga mkondo wa maisha uliopangiwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho. Kwani upatapo mwili, majaaliwa yako tayari huwa yameishapangwa, ikiwa yatakuwa mazuri au mabaya, kila mtu anapaswa kuyakubali yalivyo, na anapaswa kusonga mbele; hili ni jambo ambalo hakuna mtu aishiye katika maisha haya anaweza kuliepuka, na huu ndio uhalisia. Sawa, umeyaelewa haya yote, naam?
    Baada ya kulielewa hili, mnaona kwamba Mungu ana uangalizi unaolipiza sana na mkali pamoja na utawala kwa mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini? Kwanza, Mungu ameweka sheria mbalimbali za mbinguni, amri, na mifumo katika milki ya kiroho, na baada ya kutangazwa kwa hizi sheria za mbinguni, amri na mifumo, ambazo zinatekelezwa kabisa, kama zilivyopangwa na Mungu, na viumbe wenye nyadhifa rasmi mbalimbali katika ulimwengu wa kiroho, na hakuna anayethubutu kuzikiuka. Na kwa hivyo, katika Mzunguko wa uhai na mauti wa wanadamu katika dunia ya mwanadamu, mtu awe amepata mwili kama mwanadamu au mnyama, kuna sheria kwa yote mawili. Kwa kuwa sheria hizi zinatoka kwa Mungu, hakuna anayethubutu kuzivunja, wala hakuna awezaye kuzivunja. Ni kwa sababu tu ya huo ukuu wa Mungu, na kwa sababu kuna sheria hizo, ndiyo ulimwengu yakinifu uonekanao kwa mwanadamu ni wa kawaida na wenye mpangilio; ni kwa sababu tu ya ukuu wa Mungu ndipo mwanadamu anaweza kuishi kwa amani pamoja na ulimwengu mwingine ambao hauonekani kabisa kwa mwanadamu, na kuweza kuishi nao kwa amani—vitu ambavyo vyote haviwezi kutenganishwa na mamlaka ya Mungu. Baada ya maisha ya roho ya kimwili kufa, roho bado huwa na uhai, basi ni nini kingetendeka ikiwa roho ingekosa utawala wa Mungu? Roho ingezurura kila mahali, ikiingia kila sehemu, na hata kudhuru viumbe hai katika ulimwengu wa wanadamu. Madhara hayo hayangekuwa tu kwa mwanadamu bali pia kwa mimea na wanyama—ila wa kwanza kudhuriwa wangekuwa watu. Kama hili lingetukia—roho kama hiyo ingekosa uendeshaji, na kuwadhuru watu kwa hakika, na kufanya mambo maovu kwa hakika—basi pia kungekuwa na ushughulikiaji ufaao wa roho hii katika ulimwengu wa kiroho: Ikiwa mambo yangekuwa mabaya, roho haingeendelea kuwepo, ingeangamizwa; ikiwezekana, ingewekwa mahali fulani halafu ipatiwe mwili. Yaani, utawala wa ulimwengu wa kiroho kwa roho mbalimbali umepangiliwa, na kutekelezwa kulingana na hatua na sheria. Ni kwa sababu tu ya utawala huo ndiyo ulimwengu yakinifu wa mwanadamu haujatumbukia kwenye machafuko, ndiyo mwanadamu wa ulimwengu wa kuonekana ana akili ya kawaida, urazini wa kawaida, na maisha ya kimwili yenye mpangilio. Ni baada tu ya mwanadamu kuwa na maisha ya kawaida ndiyo wale wanaoishi katika mwili wanaweza kuendelea kufanikiwa na kuzaana katika vizazi vyote.
     Mnafikiri nini kuhusu maneno ambayo mmesikia hivi punde? Je, ni mageni kwenu? Na mnahisi nini baada ya Mimi kusema maneno haya leo? Licha ya kwamba ni mapya, mnahisi kitu kingine chochote? Niambie. (Ni lazima watu wawe na tabia nzuri, na ninaona Mungu ni mkubwa na wa kuogopwa.) (Najisikia mwingi wa heshima kwa Mungu, katika siku za usoni nitakuwa makini sana kitu kikinitokea, nitakuwa na mwenendo mwema kwa kila nisemacho na kutenda.) (Baada ya kusikia kuwasiliana kwa karibu kwa Mungu kuhusu jinsi Mungu anazishughulikia hatima za aina mbalimbali za watu, kwa upande mmoja ninahisi kuwa tabia ya Mungu haikubali kosa lolote, na kwamba ninapaswa kumheshimu sana; na kwa upande mwingine, ninafahamu Mungu anapenda aina gani ya watu, na ni aina gani hapendi, kwa hivyo ninataka kuwa mmoja wa wale ambao Mungu anapenda.) Je, mnaona kwamba Mungu ni mwenye kanuni katika matendo Yake katika mambo haya? Anatenda kulingana na kanuni gani? (Anapanga hatima za watu kulingana na yote wanayoyafanya.) Hii inahusu hatima mbalimbali za wasioamini ambao tumezungumzia. Ikija kwa wasioamini, je, kanuni iongozayo matendo ya Mungu ni ile ya kutuza mazuri na kuadhibu mabaya? Je, mnaona kwamba kuna kanuni katika matendo ya Mungu? Mnapaswa kuona kwamba kunayo kanuni. Wasioamini kwa hakika hawamwamini Mungu, hawatii mipango ya Mungu, na hawafahamu ukuu wa Mungu, na hawamtambui Mungu hata kidogo. Zito zaidi, wanamkufuru Mungu, na kumlaani, na ni mahasimu wa wale wanaomwamini Mungu. Japo watu hawa wana mwelekeo huo kwa Mungu, bado uongozi wa Mungu kwao hauachani na kanuni Zake; Anawaongoza kwa njia ya utaratibu kulingana na kanuni Zake na tabia Yake. Je, Mungu anauchukuliaje uhasama wao? Kama ujinga! Na kwa hiyo Amewasababisha hawa watu—wengi wa wasioamini—wakati mmoja kuwahi kupata mwili kama wanyama. Basi unasema wasioamini ni nini machoni mwa Mungu? (Mifugo.) Machoni pa Mungu, ni wa hii sampuli, wao ni mifugo. Mungu anaongoza mifugo, na Anaongoza wanadamu, na Ana kanuni sawa kwa hii aina ya watu. Hata katika utawala wa Mungu kwa watu hawa na matendo Yake kwao, bado kunaweza kuonekana tabia ya Mungu na sheria za utawala Wake juu ya vitu vyote. Hivyo basi, unaona mamlaka ya Mungu katika kanuni ambazo kwazo Anawaongoza wasioamini ambao Nimezungumzia hivi punde? Je, mnaona tabia ya haki ya Mungu? (Tunaona). Mnaona ukuu wa Mungu, na mnaona tabia Yake. Yaani, haijalishi Anashughulikia kitu gani kati ya vitu vyote Anavyoshughulikia, Mungu anatenda kulingana na kanuni na tabia Yake. Hiki ndicho kiini cha Mungu. Hawezi kujitenga kiholela na amri au sheria za mbinguni Alizozipanga kwa sababu Anawaona watu hawa wa aina hii kama mifugo; Mungu anatenda kulingana na kanuni, bila kuzivuruga hata kidogo, matendo Yake hayaathiriwi na jambo lolote, na haijalishi Anafanya nini, yote ni kulingana na kanuni Zake mwenyewe. Hili linaamuliwa na ukweli kwamba Mungu ana kiini cha Mungu Mwenyewe, ambacho ni kiini cha kipekee ambacho hakimo kwenye kiumbe yeyote. Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili. Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu. Hili ndilo linapaswa kueleweka na kujulikana kwa wanadamu.
     Kifo cha kiumbe hai—kuondokewa na uhai wa kimwili—kinaashiria kwamba kiumbe hai huyu ametoka katika ulimwengu yakinifu hadi ulimwengu wa kiroho, ilhali kuzaliwa kimwili kunaashiria kwamba kiumbe hai ametoka ulimwengu wa kiroho na kuja ulimwengu yakinifu kuanza kufanya kazi yake, kuchukua nafasi yake. Iwe ni kuondoka au kuwasili kwa kiumbe, vyote havitenganishwi na kazi ya ulimwengu wa kiroho. Mtu akija katika ulimwengu yakinifu, mipango kabambe na fafanuzi huwa tayari imetengenezwa na Mungu katika ulimwengu wa kiroho kuhusu watakwenda katika familia gani, watafikia enzi gani, watawasili saa ngapi, na nafasi yao. Hivyo basi, maisha yote ya hawa watu—mambo wafanyayo, na njia wazichukuazo—yanasonga kulingana na mipango ya ulimwengu wa kiroho, bila hitilafu hata kidogo. Wakati ambapo maisha ya kiroho yanaisha, wakati huo, na namna na mahali ambapo yanaishia, ni wazi na yanaonekana katika ulimwengu wa kiroho. Mungu anatawala ulimwengu yakinifu, na Anatawala ulimwengu wa kiroho, na Hawezi kuchelewesha mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti wa roho, wala Hawezi kufanya makosa katika mpangilio wa mzunguko wa uhai na mauti wa roho. Kila msimamizi katika nyadhifa rasmi katika ulimwengu wa kiroho anafanya majukumu yake na kufanya ambacho anapaswa kufanya, kulingana na maelezo na sheria za Mungu. Na kwa hiyo, katika ulimwengu wa wanadamu, kila tukio la kuonekana lishuhudiwalo na binadamu lina utaratibu, na halina vurugu yoyote. Haya yote ni kwa sababu ya utawala uliopangiliwa wa Mungu juu ya vitu vyote, hali kadhalika kwa sababu mamlaka ya Mungu yanatawala kila kitu, na kila kitu Anachokitawala kinajumuisha ulimwengu yakinifu ambamo mwanadamu anaishi, aidha, ulimwengu wa kiroho usioonekana nyuma ya mwanadamu. Na kwa hiyo, ikiwa mwandamu anataka kuwa na maisha mazuri, na anataka kuishi katika mazingira mazuri, hali kadhalika kupewa ulimwengu yakinifu mzima, mwanadamu sharti pia apatiwe ulimwengu wa kiroho, ambao hauwezi kuonekana kwa yeyote, ambao unaongoza kila kiumbe hai kwa niaba ya mwanadamu, na ambao una utaratibu. Basi, inaposemwa kwamba Mungu ndiye chanzo cha uhai kwa vitu vyote, je, hatujakuza ufahamu na uelewa wetu wa “vitu vyote”?

2) Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

    Tumemaliza kujadili mzunguko wa uhai na mauti wa kundi la kwanza, wasioamini. Hebu sasa tujadili ule wa kundi la pili, watu mbalimbali wenye imani. “Mzunguko wa uhai na mauti wa watu mbalimbali wenye imani” vilevile ni mada muhimu sana, na inafaa kwamba muwe na kiasi fulani cha uelewa wake. Kwanza, hebu tuseme ni imani gani “imani” katika “watu wenye imani” inarejelea nini: Inamaanisha Uyahudi, Ukristo, Ukatoliki, Uisilamu, na Ubudha, dini hizi kuu tano. Pamoja na wasioamini, watu ambao ni waumini katika hizi dini tano wanajumuisha idadi kubwa ya watu duniani. Miongoni mwa dini hizi tano, wale ambao wametengeneza ajira kutokana na uumini wao—wafuasi ambao wanafanya kazi muda wote kwa imani yao—ni wachache, lakini hizi dini zina waumini wengi. Waumini wake huenda sehemu tofauti wanapokufa. “Tofauti” na nani? Na wasioamini, watu wasiokuwa na imani, ambao tumemaliza kuzungumzia. Baada ya kufa, waumini wa hizi dini tano huenda mahali pengine, mahali tofauti na wasioamini. Ulimwengu wa kiroho pia utafanya uamuzi juu yao kutegemea yale yote waliyoyafanya kabla wafe, baadaye watatayarishwa ipasavyo. Lakini mbona hawa watu wanawekwa sehemu tofauti kutayarishwa? Kuna sababu muhimu ya hili. Na hii sababu ni gani? Nitawaambia kutumia mfano.
     Chukua Ubudha: Hebu Niwaambie ukweli. Mfuasi wa Budha, kwanza kabisa, ni mtu aliyebadili dini kwenda Ubudha, na ni mtu ajuaye imani yake ni nini. Mfuasi wa Budha akinyoa nywele zake na kuwa mtawa wa kiume au mtawa wa kike, hii inamaanisha kuwa wamejitenga na mambo ya kidunia na kuacha nyuma ghasia ya dunia ya mwanadamu. Kila siku wanakariri maandiko ya Kibudha na kula chakula bila nyama, wanaishi maisha ya kujinyima anasa za kimwili, na kupitisha siku zao ndani ya mwangaza baridi, na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi. Wanaishi maisha yao yote kwa njia hii. Maisha yao ya kimwili yaishapo, wanatengeneza muhtasari wa maisha yao, ila mioyoni mwao hawajui watakapoenda baada ya kufa, watakutana na nani, na watakuwa na hatima ya aina gani—mioyoni mwao hawana uhakika na haya mambo. Hawajafanya chochote zaidi ya kuishi bila mwelekeo maisha yao yote wakiambatana na imani, baadaye wanaondoka duniani wakiambatana na matamanio na maadili wasiyoyafahamu. Hiyo ndiyo tamati ya maisha yao ya kimwili wanapoiaga dunia ya walio hai, na wakati maisha yao ya kimwili yanapoisha, wanarudi katika sehemu yao asilia katika ulimwengu wa kiroho. Kama hawa watu watapata mwili na kurudi duniani kuendelea na kujikuza kwao inategemea mienendo na kujikuza kwao kabla ya kifo chao. Ikiwa hawakufanya kitu kibaya wakati wa uhai wao, watapata mwili haraka na kurudishwa duniani, ambapo watanyoa vichwa vyao tena na kuwa watawa wa kiume au watawa wa kike. Wanakuwa watawa wa kiume au watawa wa kike mara tatu hadi mara saba: kulingana na utaratibu wa mara ya kwanza, mwili wao unajikuza wenyewe, baada ya hapo wanakufa na kurudi katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanatathminiwa, baada ya hapo—ikiwa hakuna shida—wanaweza kurudi tena katika ulimwengu wa wanadamu, na kuendelea na kujikuza kwao, yaani, wanaweza kubadili dini hadi Ubudha tena na kuendelea kujikuza. Baada ya kupata mwili mara tatu hadi mara saba, watarudi tena katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanakwenda kila mara ambapo maisha yao ya kimwili yanamalizika. Ikiwa viwango na mienendeo yao mbalimbali katika ulimwengu wa wanadamu inaambata na sheria za mbinguni za ulimwengu wa kiroho, basi watabaki huko kutoka wakati huu kuendelea; hawatapata mwili tena kama wanadamu; wala hakutakuwa na tishio la wao kuadhibiwa kwa kutenda maovu duniani. Hawatawahi kupitia tena mchakato huu. Badala yake, kulingana na hali zao, watachukua nyadhifa katika milki ya kiroho, ambako ndiko wafuasi wa Budha wanaita kupata uzima wa milele. Sasa mnaelewa, naam? Na “kupata uzima wa milele” katika Ubudha kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwa afisa wa ulimwengu wa kiroho, na kutokuwepo na nafasi zaidi ya kupata mwili au adhabu. Zaidi ya hayo, ina maana kwamba hakuna kupata taabu tena ya kuwa mwanadamu baada ya kupata mwili. Hivyo basi, bado kuna uwezekano wao kupata mwili tena kama wanyama? Hakuna kabisa! Na hii ina maana gani? Kwamba wanabaki kushika nafasi katika ulimwengu wa kiroho na kamwe hawatapata mwili kama mtu. Huu ni mfano mmoja wa kupata uzima wa milele.
     Inakuwaje kwa wale ambao hawapati uzima wa milele? Baada ya wao kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanatathminiwa na kuthibitishwa na msimamizi anayehusika, na kuonekana hawakujikuza kwa makini au kuwa makini katika kukariri maandiko ya Kibudha kama inavyotakiwa na Ubudha; badala yake, walitenda maovu mengi, na kutenda mengi yaliyo mabaya. Wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho, hukumu inatolewa juu ya uovu wao, baada ya hapo wanaadhibiwa. Hakuna vighairi katika hili. Basi, mtu wa aina hii atapata lini uzima wa milele? Katika maisha ambamo hawatatenda maovu—wakati, baada ya kurudi katika ulimwengu wa kiroho, inaonekana hawakufanya chochote kibaya kabla hawajafa. Sawa! Wanaendelea kupata mwili, wanaendelea kukariri maandiko ya Kibudha, wanapitisha siku zao ndani ya mwangaza baridi na hafifu wa taa ya mafuta ya siagi, bila kuua chochote chenye uhai, bila kula nyama, na hawaufurahii ulimwengu wa mwanadamu, kuachana na vurugu zake kabisa, na kuepuka migogoro na wengine. Katika mchakato huu, hawafanyi maovu, kufuatia hayo wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na baada ya matendo na mienendo yao yote kutathminiwa, wanatumwa tena katika ulimwengu wa wanadamu, kwa mzunguko unaojirudia mara tatu au saba. Ikiwa hakuna kikwazo wakati huu, basi kupata kwao uzima wa milele hakutaathiriwa, na watafanikiwa. Hii ni sifa ya mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani: wanaweza kupokea uzima wa milele na kushikilia wadhifa katika ulimwengu wa kiroho. Hili ndilo linawafanya kuwa tofauti na wasioamini. Kwanza kabisa, wanapokuwa hai duniani, matendo ya wale wanaoweza kushika wadhifa katika ulimwengu wa kiroho ni yapi? Ni sharti wasifanye kabisa ovu lolote: ni lazima wasifanye mauaji, uchomaji, ubakaji, au wizi; wakifanya hila, udanganyifu, au ujambazi, basi hawawezi kupata uzima wa milele. Ina maana kwamba, wakiwa na uhusiano au ushirikishaji wowote na uovu, hawataweza kuepukana na adhabu ya ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho unafanya mipango faafu kwa wafuasi wa Budha wapatao uzima wa milele: wanaweza kuteuliwa kusimamia wale ambao wanaonekana kuamini katika Ubudha, na yule Mzee aliye Angani, na wafuasi wa Budha watapewa mamlaka, wanaweza kuteuliwa kuwasimamia wasioamini, vinginevyo wanaweza kuwa wasimamizi wadogo sana. Ugavi huo unalingana na asili ya hizi roho. Huu ni mfano wa Ubudha.
     Miongoni mwa dini tano tulizozungumzia, Ukristo ni maalum kiasi fulani. Ni nini maalum kuhusu Ukristo? Hawa ni watu wanaomwamini Mungu wa kweli. Je, inawezekanaje wale wanaomwamini Mungu wa kweli waorodheshwe hapa? Kwa sababu Ukristo unakiri tu kwamba kuna Mungu, na wanampinga Mungu na kuwa maadui Wake. Kwa mara nyingine wamemuangika Kristo msalabani, na kuwa mahasimu wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na matokeo yake ni kwamba wamefichuliwa na kushushwa kuwa kundi la kiimani. Kwa sababu Ukristo ni aina ya imani, basi, bila shaka, unahusiana tu na imani—ni aina ya sherehe, aina ya dhehebu, aina ya dini, na kitu tofauti na imani ya wale wanaomfuata Mungu kweli. Kilichonifanya kuuorodhesha miongoni mwa hizi dini tano ni kwa sababu Ukristo umeshushwa hadi kiwango sawa na Uyahudi, Ubudha, Uislamu. Wakristo wengi hawaamini kuna Mungu, au kwamba Anatawala juu ya vitu vyote, seuze kuamini katika uwepo Wake. Badala yake, wanatumia tu Maandiko Matakatifu kuzungumza kuhusu elimu ya dini, wakitumia elimu ya dini kuwafundisha watu kuwa wema, kuvumilia mateso, na kufanya vitu vizuri. Ukristo ni wa aina hiyo ya dini: Unazingatia tu nadharia za mafundisho ya kidini, hauna kabisa uhusiano wowote na kazi ya Mungu ya kusimamia na kuokoa wanadamu, ni dini ya wale wanaomfuata Mungu ambayo haitambuliwi na Mungu. Lakini pia Mungu ana kanuni kuhusu mtazamo Wake kwao. Hawatendei na kuwashughulikia wapendavyo bila mpango, njia sawa na wasioamini. Mtazamo Wake kwao ni sawa na Alio nao kwa wafuasi wa Budha: Ikiwa, angali hai, Mkristo anajiheshimu, anaweza kuzifuata kabisa Amri Kumi za Mungu na sheria nyingine, na kuzingatia sheria na mahitaji yake katika tabia zao wenyewe—na ikiwa wanaweza kufanya hivi katika maisha yao yote—basi pia watalazimika kuchukua muda sawa kupitia mzunguko wa uhai na mauti kabla hawajaweza kweli kupata huko kuitwako kuchukuliwa kuenda mbinguni. Baada ya kupokea huku “kuchukuliwa kuenda mbinguni,” wanabaki katika ulimwengu wa kiroho, ambapo wanashika wadhifa na kuwa miongoni mwa wasimamizi. Vivyo hivyo, wakifanya maovu duniani, ikiwa ni watenda dhambi na kufanya dhambi nyingi, basi haiepukiki kwamba wataadhibiwa kwa ukali unaotofautiana. Katika Ubudha, kupata “uzima wa milele” kunamaanisha kuingia Nirvana (hali ya kujisahau binafsi kwa kuungana na Mungu), lakini hii inaitwaje katika Ukristo? Inaitwa “kuingia mbinguni” na “kuchukuliwa kuenda mbinguni.” Wale ambao kwa kweli “wamechukuliwa kuenda mbinguni” pia wanapitia mzunguko wa uhai na mauti mara tatu hadi saba, halafu, wakiwa wamekufa, wanaingia katika ulimwengu wa kiroho, kana kwamba walikuwa usingizini. Ikiwa walikuwa wanafaa wanaweza kusalia kushika wadhifa, na tofauti na watu walio duniani, hawatapata mwili kwa njia rahisi, au kulingana na mazoea.
     Miongoni mwa dini hizi zote, mwisho wanaouzungumzia na kuupigania ni sawa na kupata uzima wa milele katika Ubudha—tofauti ni kuwa unapatikana kwa njia tofauti. Wote ni wa aina moja. Kwa watu wa dini hizi ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini katika tabia zao, kwa hili kundi la watu, Mungu huwapa hatima nzuri, sehemu nzuri ya kwenda, na kuwatendea inavyofaa. Haya yote ni sawa, ila si jinsi ambavyo watu wanadhani. Sasa, baada ya kusikia yanayowatokea Wakristo, mnajihisi vipi? Je, mnawasikitikia? Mnawahurumia? (Kidogo.) Hakuna linaloweza kufanywa—watajilaumu wenyewe. Kwa nini Ninasema hivi? Kazi ya Mungu ni ya kweli, Mungu yu hai na kweli, na kazi Yake inawalenga wanadamu wote na kila mtu—basi mbona Wakristo wasikubali hili? Ni kwa nini wanampinga kwa nguvu na kumtesa Mungu? Wana bahati hata kuwa na mwisho kama huu, basi mbona mnawaonea huruma? Kwa wao kutendewa namna hii kunaonyesha uvumilivu mkubwa. Kulingana na kiasi ambacho wanampinga Mungu, wanapaswa kuangamizwa—bali Mungu hafanyi hili, anaushughulikia Ukristo sawa tu na dini ya kawaida. Sasa kuna haja ya kutoa maelezo ya kina kuhusu dini nyinginezo? Maadili ya dini zote hizi ni yapi? Kwa watu kuwa wema, na wasitende maovu. Wapate shida, wasifanye maovu, wasema mambo mazuri, watenda mambo mema, wasiwaapize watu wengine, msifanye mahitimisho ya ghafla juu ya wengine, mjitenge na ugomvi, fanya vitu vizuri, kuwa mtu mzuri—mafundisho ya kidini mengi ni ya aina hii. Na kwa hiyo, kama hawa watu wa imani—hawa watu wa dini na madhehebu mbalimbali—wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, basi hawatafanya makosa au dhambi nyingi wakati wangali duniani, na baada ya kupata mwili mara tatu hadi saba, basi kwa jumla watu hawa, watu ambao wanaweza kufuata kabisa maadili ya kidini, watabaki kushikilia wajibu katika ulimwengu wa kiroho. Na je, kuna watu wengi wa aina hii? Si rahisi kutenda mazuri, au kufuata amri na sheria. Ubudha haumruhusu mtu kula nyama—unaweza kufanya hilo? Ungepaswa kuvaa kanzu za kijivu na kukariri maandiko ya Kibudha katika hekalu la wafuasi wa Budha siku nzima, ungeweza kufanya hivyo? Haingekuwa rahisi. Ukristo una Amri Kumi za Mungu na amri nyingine, je, hizi amri na sheria nyingine ni rahisi kufuata? Si rahisi! Chukua mfano wa usiwaapie wengine: Watu wanashindwa kufuata hii amri, naam? Kwa kushindwa kujizuia wenyewe, wanaapa—na baada ya kuapa hawawezi kurudisha kiapo, basi wanafanya nini? Usiku wanakiri dhambi zao. Hawawezi kujizuia kuwaapia wengine, na baada ya kuapa bado huwa kuna chuki mioyoni mwao, na hata wanazidi zaidi na kupanga ni lini watawadhuru. Kwa jumla, kwa wale wanaoishi katika hii imani iliyokufa, si rahisi kukosa kufanya dhambi au kutenda maovu. Na kwa hiyo, katika kila dini, ni watu wachache tu ndio wanaweza kupata uzima wa milele. Unadhani kwamba kwa sababu watu wengi sana wanafuata hizi dini, wengi wataweza kubaki kuchukua nafasi katika milki ya kiroho! Lakini si wengi hivyo, ni wachache tu ndio wanaweza kulifikia hili. Kwa jumla ni hayo tu kwa mzunguko wa uhai na mauti wa watu wenye imani. Kinachowapambanua ni kwamba wanaweza kupata uzima wa milele, ambayo ni tofauti yao na wasioamini.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
    Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni