4/18/2018

Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Ayubu

Neno la Mwenyezi Mungu  | 1. Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia

(Ayubu 1:1) Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu .
(Ayubu 1:5) Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.
(Ayubu 1:8) Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?
Ni nini hoja kuu unayoiona kwenye vifungu hivi? Vifungu hivi vitatu vifupi vya maandiko vyote vinahusu Ayubu. Ingawaje ni vifupi, vinaelezea waziwazi alikuwa mtu wa aina gani. Kupitia kwa ufafanuzi wake kuhusu tabia ya kila siku ya Ayubu na mwenendo wake, vinaelezea kila mmoja kwamba, badala ya kukosa msingi, ukadiriaji wa Mungu ya Ayubu ulikuwa na msingi wake na ulikuwa umekita mizizi. Vinatuambia kwamba iwapo ni utathmini wa binadamu kuhusu Ayubu (Ayubu 1:1), au utathmini wa Mungu kuhusu yeye (Ayubu 1:8), tathmini zote zinatokana na matendo ya Ayubu mbele ya Mungu na binadamu (Ayubu 1:5)
Kwanza, hebu tukisome kifungu nambari moja: “Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Ukadiriaji wa kwanza wa Ayubu kwenye Biblia, sentensi hii ndiyo utathmini wa mwandishi kuhusu Ayubu Kiasili, unawakilisha pia ukadiriaji wa binadamu kuhusu Ayubu, ambayo ni “mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu” Kisha, hebu tuusome utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu: “kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu” (Ayubu 1:8). Kati ya tathmini hizi mbili, moja ilitoka kwa binadamu, na nyingine ikatoka kwa Mungu; ni ukadiriaji aina mbili ulio na maudhui moja. Inaweza kuonekana, basi, kwamba tabia na mwenendo wa Ayubu ulijulikana kwa binadamu, na pia ulisifiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, mwenendo wa Ayubu mbele ya binadamu na mwenendo wake mbele ya Mungu ulikuwa sawa; aliweka tabia yake na motisha yake mbele ya Mungu siku zote, ili hivi viwili viweze kuangaliwa na Mungu, na yeye alikuwa mmoja aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo, katika macho ya Mungu, kati ya watu duniani, ni Ayubu tu ambaye alikuwa mtimilifu na mnyofu, ndiye aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Maonyesho Mahususi ya Kumcha Mungu kwa Ayubu na Kujiepusha na Maovu katika Maisha Yake ya Kila siku

Kisha, hebu tuangalie maonyesho mahususi ya kumcha Mungu kujiepusha na maovu kwa Ayubu. Juu ya vifungu hivi vinavyotangulia na kufuata, hebu pia tusome Ayubu 1:5, ambayo ni mojawapo ya maonyesho mahususi ya kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu. Inahusu namna ambavyo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu katika maisha yake ya kila siku; muhimu zaidi, hakufanya tu kile alichostahili kufanya kwa minajili ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, lakini pia mara kwa mara alitoa sadaka iliyoteketezwa mbele ya Mungu kwa niaba ya wana wake. Alikuwa na hofu kwamba walikuwa mara nyingi “wametenda dhambi, na kumlaani Mungu katika mioyo yao” wakati wakiwa na karamu. Na uoga huu ulijionyesha vipi ndani ya Ayubu? Maandishi asilia yanatupa simulizi ifuatayo: “Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa.” Mwenendo wa Ayubu unatuonyesha kwamba, badala ya kuonyeshwa katika tabia yake ya nje, kumcha Mungu kwake kulitokea ndani ya moyo wake, na kwamba kumcha Mungu kwake kungepatikana katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku, wakati wote, kwani hakujiepusha na maovu tu yeye mwenyewe, lakini pia alitoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume. Kwa maneno mengine, Ayubu hakuwa tu mwenye hofu ya kutenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Mungu katika moyo wake, lakini pia alikuwa na wasiwasi kwamba watoto wake wa kiume walitenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Yeye katika mioyo yao. Kutokana na haya ukweli unaweza kuonekana kwamba ukweli wa kumcha Mungu kwa Ayubu unapita uchunguzi, na ni zaidi ya shaka ya binadamu yeyote. Je, alifanya hivi mara kwa mara, au mara nyingi? Sentensi ya mwisho ya maandishi ni “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.” Maana ya maneno haya ni kwamba Ayubu hakuenda na kuangalia watoto wake mara kwa mara au wakati alipenda kufanya hivyo, wala hakutubu kwa Mungu kupitia kwa maombi. Badala yake, aliwatuma mara kwa mara na kuwatakasa watoto wake wa kiume kutoa sadaka iliyoteketezwa kwa niaba yao. Hiyo kauli “bila kusita” hapa haimaanishi alifanya hivyo kwa siku moja au mbili, au kwa muda mfupi tu. Inasema kwamba maonyesho ya kumcha Mungu kwa Ayubu hayakuwa ya muda, na hayakusita kwa maarifa aliyokuwa nayo au kwa maneno aliyotamka; badala yake, njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu iliongoza moyo wake, iliamuru tabia yake, na ilikuwa, ndani ya moyo wake mzizi wa uwepo wake. Kwamba alifanya hivyo bila kusita yaonyesha kwamba, katika moyo wake, mara nyingi alikuwa na hofu kwamba yeye mwenyewe angetenda dhambi dhidi ya Mungu na alikuwa na wasiwasi pia kwamba watoto wake wa kiume na binti zake walitenda dhambi dhidi ya Mungu. Inawakilisha namna tu ambavyo uzito wa njia ambayo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu ulibebwa ndani ya moyo wake. Alifanya hivyo bila kusita kwa sababu, ndani ya moyo wake, alikuwa na hofu na wasiwasi—wasiwasi kwamba alikuwa ametenda maovu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu, na kwamba alikuwa amepotoka kutoka kwenye njia ya Mungu, na basi alikuwa hawezi kutosheleza Mungu. Wakati huohuo, alikuwa pia na wasiwasi kuhusu watoto wake wa kiume na binti zake, akiogopa kwamba walikuwa wamemkosea Mungu. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa kawaida wa Ayubu katika maisha yake ya kila siku. Kwa hakika ni mwenendo wa kawaida ambao unathibitisha kwamba kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu si maneno matupu tu, kwamba Ayubu aliishi kwa kudhihirisha kwa kweli ukweli kama huo. “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote”: Maneno haya yanatuambia kuhusu matendo ya kila siku ya Ayubu mbele ya Mungu. Alipofanya hivi bila kusita, tabia yake na moyo wake vilifika mbele ya Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu mara nyingi alipendezwa na moyo wake na tabia yake? Basi, ni katika hali gani na katika muktadha gani Ayubu alifanya hivi bila kusita? Baadhi ya watu wanasema kwamba ilikuwa ni kwa sababu Mungu alijitokeza kwa Ayubu mara kwa mara na ndiyo maana akatenda hivi; baadhi wanasema kwamba alifanya hivi bila kusita kwa sababu angejiepusha na maovu; na baadhi wanasema kwamba alifikiria kwamba utajiri wake ulikuwa haujaja kwa urahisi, na alijua kwamba alikuwa amepewa na Mungu, na hivyo alikuwa na uoga mwingi wa kupoteza mali yake kutokana na kutenda dhambi dhidi ya au kumkosea Mungu. Je, yapo madai yoyote kati ya haya yaliyo kweli? Bila shaka la. Kwani, kwa macho ya Mungu, kile Mungu amekubali na kupenda sana kuhusu Ayubu si tu kwamba alifanya hivi bila kusita; zaidi ya hapo, ilikuwa ni mwenendo wake mbele ya Mungu, binadamu, na Shetani alipokabidhiwa Shetani na kujaribiwa. Sehemu zilizo hapa chini zinatupa ithibati yenye ushawishi mkubwa zaidi, ithibati ambayo inatuonyesha ukweli wa ukadiriaji wa Mungu kwa Ayubu. Kinachofuata, hebu tusome maandiko kwenye vifungu vifuatavyo.
2. Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 1:8) Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?
(Ayubu 1:12) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.
b. Jibu la Shetani
(Ayubu 1:9-11) Kisha Shetani akamjibu BWANA, akasema, Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure? Wewe hujamzingira kwa ukigo pande zote, na kwa nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo kwa kila upande? Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, na yeye atakukufuru mbele ya uso wako.

Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Timilifu

Ayubu 1:8 ndiyo rekodi ya kwanza tunayoiona kwenye Biblia kuhusu mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Na ni nini alichosema Mungu? Maandishi asilia yanatupatia simulizi ifuatayo: “Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?” Huu ulikuwa ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu kwa Shetani; Mungu alisema kwamba alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kabla ya maneno haya kati ya Mungu na Shetani, Mungu alikuwa ameamua kwamba Angemtumia Shetani kujaribu Ayubu—kwamba Angemkabidhi Ayubu kwa Shetani. Kwa mkondo mmoja, hali hii ingethibitisha kwamba uangalizi na utathmini wa Mungu kwa Ayubu ulikuwa sahihi na bila kosa, na ungesababisha Shetani kuaibishwa kupitia kwa ushuhuda wa Ayubu, kwa mkondo mwingine, ingefanya imani ya Ayubu kwa Mungu na kumcha Mungu kuwa timilifu. Hivyo, wakati Shetani alipokuja mbele ya Mungu, Mungu hakutatiza maneno. Alienda moja kwa moja kwenye hoja na kumuuliza Shetani: “Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?” Katika swali la Mungu kunayo maana yafuatayo: Mungu alijua kwamba Shetani alizunguka kila pahali, na mara nyingi alikuwa amemnyemelea Ayubu, aliyekuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mara nyingi amemjaribu na kumshambulia, akijaribu kupata njia ya kumwangamiza Ayubu ili kuthibitisha kwamba imani ya Ayubu katika Mungu na kumcha Mungu kwake kusingeweza kubadilika. Shetani pia alitafuta kwa haraka sana fursa za kumhangaisha Ayubu, ili Ayubu aweze kumkataa Mungu na kumruhusu Shetani kumpokonya kutoka kwenye mikono ya Mungu. Lakini Mungu aliuangalia moyo wa Ayubu na kuona kwamba alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alitumia swali moja kumwambia Shetani kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwamba Ayubu asingeweza kumwacha Mungu na kufuata Shetani. Baada ya kusikia utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu, ndani ya Shetani kukatokea hasira kali iliyotokana na udhalilishaji, na akawa mwenye hasira zaidi, na aliyekosa subira ya kumpokonya Ayubu kutoka kwa Mungu, kwani Shetani alikuwa hajawahi kusadiki kwamba mtu angeweza kuwa mtimilifu na mnyofu, au kwamba angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Wakati huohuo, Shetani pia alichukizwa na utimilifu na unyofu kwa binadamu, na aliwachukia watu ambao wangeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Na hivyo imeandikwa katika Ayubu 1:9-11 kwamba “Kisha Shetani akamjibu BWANA, akasema, Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure? Wewe hujamzingira kwa ukigo pande zote, na kwa nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo kwa kila upande? Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, na yeye atakukufuru mbele ya uso wako.” Mungu alikuwa amezoea kwa undani asili ya kijicho ya Shetani, na Alijua vizuri kabisa kwamba Shetani alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumwangamiza Ayubu, na hivyo kwa haya Mungu alitaka, kwa kumwambia Shetani kwa mara nyingine kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimwogopa Mungu na kujiepusha na maovu, kumrudisha Shetani pale anapofaa, kumfanya Shetani kufichua uso wake wa kweli na kumshambulia na kumjaribu Ayubu. Kwa maneno mengine, Mungu alitilia mkazo makusudi kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kwa njia hii alimfanya Shetani kumshambulia Ayubu kwa sababu ya chuki na hasira za Shetani kutokana na vile ambavyo Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kutokana na haya, Mungu angemletea Shetani aibu kupitia kwa ukweli kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, na Shetani angeachwa akiwa amedhalilishwa kabisa na kushindwa. Baada ya hapo, Shetani asingekuwa tena na shaka au asingetoa mashtaka kuhusu utimilifu, unyofu, ucha Mungu au hali ya kujiepusha na maovu ya Ayubu. Kwa njia hii, majaribio ya Mungu na yale ya Shetani yalikuwa karibu yasiyoepukika. Yule tu aliye na uwezo wa kustahimili majaribio ya Mungu na yale ya Shetani alikuwa ni Ayubu. Kufuatia mabadilishano haya, Shetani alipewa ruhusa kumjaribu Ayubu. Na hivyo raundi ya kwanza ya mashambulizi ya Shetani ikaanza. Kilengwa cha mashambulizi haya kilikuwa mali ya Ayubu, kwani Shetani alikuwa ametoa mashtaka yafuatayo dhidi ya Ayubu: “Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure?… Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi.” Kutokana na haya, Mungu alimruhusu Shetani kuchukua kila kitu ambacho Ayubu alikuwa nacho— ambalo ndilo lilikuwa kusudio lenyewe la Mungu kuzungumza na Shetani. Hata hivyo, Mungu alitoa sharti moja kwa Shetani: “yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe” (Ayubu 1:12). Hili ndilo sharti ambalo Mungu alitoa baada ya kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu na akamweka Ayubu kwenye mikono ya Shetani, na hiyo ndiyo mipaka aliyomwekea Shetani: Alimwamuru Shetani kutodhuru Ayubu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba Alikuwa na imani kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu kwake Yeye ulikuwa zaidi ya kutiliwa shaka, na kwamba angeweza kustahimili majaribio; hivyo, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, lakini akaweka hapo kizuizi kwa Shetani: Shetani aliruhusiwa kuchukua mali ya Ayubu yote, lakini asimguse hata kwa kidole. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba Mungu hakumkabidhi Ayubu kabisa kwa Shetani wakati huo. Shetani angeweza kumjaribu Ayubu kwa mbinu zozote zile ambazo alitaka, lakini hakuweza kumdhuru Ayubu mwenyewe, hata unywele mmoja wa kichwa chake, kwa sababu kila kitu cha binadamu kinathibitiwa na Mungu, iwapo binadamu anaishi ama anakufa inaamuliwa na Mungu na Shetani hana leseni yoyote ya kuthibiti haya. Baada ya Mungu kumwambia Shetani maneno haya, Shetani asingeweza kusubiri kuanza. Alitumia kila mbinu kumjaribu Ayubu, na baada ya muda usiyokuwa mrefu Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng'ombe na mali yote aliyokuwa amepewa na Mungu... Na hivyo majaribio ya Mungu yakamjia yeye.
Ingawa Biblia inatuambia asili ya jaribio la Ayubu, je Ayubu mwenyewe, ambaye alipatwa na majaribio haya, alijua kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea? Ayubu alikuwa tu binadamu wa kawaida; bila shaka hakujua chochote kuhusu hadithi ile iliyokuwa ikiendelea nyuma yake. Hata hivyo, kumcha Mungu kwake na utimilifu pamoja na unyofu wake, ulimfanya kutambua kwamba majaribio ya Mungu yalikuwa yamemjia. Hakujua ni nini kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme wa kiroho, wala nia alizokuwa nazo Mungu katika majaribio hayo. Lakini alijua kwamba haijalishi ni nini ambacho kingemfanyikia yeye, alifaa kuendelea kushikilia ukweli wa utimilifu na unyofu wake, na kwamba alifaa kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mwelekeo na mwitikio wa Ayubu katika masuala haya uliweza kutazamwa waziwazi na Mungu. Naye Mungu aliona nini? Aliuona moyo wa Ayubu uliyomcha Mungu, kwa sababu kutoka mwanzo hadi wakati ambapo Ayubu alijaribiwa, moyo wa Ayubu ulibakia wazi kwa Mungu, uliwekwa mbele ya Mungu, naye Ayubu hakuwacha utimilifu wala unyofu wake, wala hakutupilia mbali au kugeuka katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—na hakuna kingine chochote kilichokuwa cha kumtosheleza na kumfurahisha Mungu kama haya. Kisha, tutaangalia ni majaribio yapi aliyoyapitia Ayubu na ni vipi ambavyo aliyashughulikia majaribio haya. Hebu tuyasome maandiko.
c. Mwitikio wa Ayubu
(Ayubu 1:20-21) Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Na akasema, nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.

Kwamba Ayubu Anajiwajibikia Yeye Mwenyewe Kurudisha Kila Kitu Anachomiliki Kinatokana na Kumcha Kwake Mungu

Baada ya Mungu kumwambia Shetani, “yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe.” Shetani aliondoka, muda mfupi baadaye Ayubu alipata mashambulizi ya ghafla na makali: Kwanza, ng'ombe na punda wake waliibwa na watumishi wake kuuwawa; kisha, kondoo na watumishi wake waliteketezwa hadi kiwango cha kuangamia; baada ya hapo ngamia wake walichukuliwa na watumishi wake wakauliwa; hatimaye watoto wake wa kiume na wa kike waliaga dunia. Msururu huu wa mashambulizi ulikuwa ni mateso ambayo alipitia Ayubu kwenye jaribio hili la kwanza. Kama alivyoamrishwa na Mungu, kwenye kipindi hiki cha mashambulizi, Shetani alilenga tu mali ya Ayubu na watoto wake, na hakumdhuru Ayubu mwenyewe. Hata hivyo, Ayubu alibadilishwa papo hapo kutoka kuwa mtu tajiri aliyemiliki utajiri mwingi hadi kuwa mtu asiye na chochote wala lolote. Hakuna yeyote ambaye angestahimili mshangao huu mkubwa au ambaye angeitikia vizuri, ilhali Ayubu aliuonyesha upande wake usio wa kawaida. Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” Huu ndio uliokuwa mwitikio wa kwanza wa Ayubu baada ya kusikia kwamba watoto wake walikuwa wameaga dunia na alikuwa amepoteza mali yake yote. Zaidi ya yote, hakuonekana ni kana kwamba ameshangazwa, au amepigwa na butwaa chakari, isitoshe hakuonyesha hasira au chuki. Unaona, basi, kwamba moyoni mwake alikuwa tayari ametambua kuwa majanga haya hayakuwa ajali, au yalitokana na mkono wa binadamu, na wala hayakuwa kuwasili kwa kuadhibiwa au adhabu. Badala yake, majaribio ya Yehova yalikuwa yamemjia yeye; alikuwa ni Yehova ambaye alitaka kuchukua mali na watoto wake. Ayubu alikuwa mtulivu na mwenye akili-razini wakati huo. Ubinadamu wake wa utimilifu na unyofu ulimwezesha yeye kuweza kufanya uamuzi na uamuzi kwa usahihi kwa njia ya kiasili na kirazini hasa, kuhusu majanga yaliyokuwa yamemsibu, na matokeo yake ni kuwa, alijiendeleza kwa utulivu usio wa kawaida. “Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.”“Rarua joho lake” inamaanisha kwamba alikuwa hana nguo, na hakumiliki chochote; “alikinyoa kichwa chake” inamaanishwa kwamba alikuwa amerudi mbele ya Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa; “akaanguka ardhini, na kusujudu” inamaanisha alikuwa amekuja ulimwenguni akiwa uchi, na bado hakuwa na chochote leo, alirudishwa kwa Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa. Mwelekeo wa Ayubu kwa yote yaliyompata usingeweza kutimizwa na kiumbe yeyote wa Mungu. Imani yake kwa Yehova ilizidi ile ufalme wa imani; huku kulikuwa ni kumcha Mungu kwake, kuwa mtiifu kwa Mungu, na hakuweza tu kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa yeye lakini pia kuchukua kutoka kwake. Na zaidi ya hayo, aliweza kujiwajibikia yeye mwenyewe ili kurudisha yale yote aliyomiliki, pamoja na maisha yake.
Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa mwanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu— na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu hatamu bila malipo ili kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia. Ingawaje mwenendo wa Ayubu kwenye jaribio la kwanza ulikuwa wa moja kwa moja, vizazi vya baadaye havikuwa na uhakika wa kutimiza hali hiyo ya moja kwa moja hata baada ya kutia bidii maisha yao yote, wala hawangemiliki kwa vyovyote vile mwenendo wa Ayubu uliofafanuliwa hapo juu. Leo, wakikabiliwa na mwenendo wa moja kwa moja wa Ayubu, na katika kuulinganisha na kilio na bidii ya “utiifu wenye hakika na uaminifu hadi kifo” ulioonyeshwa kwa Mungu na wale wanaodai kusadiki Mungu na kufuata Mungu, je unahisi aibu kwa kina au la?
Wakati unaposoma maandiko kuhusu yale mateso yote aliyopitia Ayubu na familia yake, mwitikio wako ni upi? Unapotea kwenye fikira zako? Unashangazwa? Je, majaribio haya yaliyomsibu Ayubu yanaweza kufafanuliwa kama ya “kusikitisha” Kwa maneno mengine, inatisha vya kutosha kuyasoma majaribio ya Ayubu kama yalivyofafanuliwa kwenye maandiko, kutosema chochote kuhusu vile yangekuwa katika uhalisia. Unaona, basi, kwamba kile kilichomsibu Ayubu hakikuwa “mazoezi,” lakini “vita,” halisi vikiwa na “bunduki” na “risasi” za kweli. Lakini nani alisababisha yeye kuweza kupitia majaribio haya ? Yaliweza, bila shaka, kutekelezwa na Shetani, yalitekelezwa na Shetani mwenyewe—lakini yaliidhinishwa na Mungu. Je, Mungu alimwambia Shetani kumjaribu Ayubu kwa njia gani? Hakumwambia. Mungu alimpa Shetani sharti moja tu, na baadaye jaribio hilo likamjia Ayubu. Wakati jaribio lilipomjia Ayubu, liliwapatia watu hisia ya maovu na ubaya wa Shetani, ya uoneaji kijicho wake, na uchukivu wake kwa binadamu, na uadui wake kwa Mungu. Katika haya tunaona kwamba maneno yasingeweza kufafanua namna tu ambavyo jaribio hili lilikuwa la kikatili. Inaweza kusemekana kwamba asili ya kijicho ambayo Shetani alimnyanyasa binadamu na uso wake mbaya vyote vilichuliwa kabisa kwa wakati huu. Shetani alitumia fursa hii, fursa iliyotolewa kupitia kwa ruhusa ya Mungu, kumnyanyasa Ayubu kwa njia mbaya na ya kusikitisha, mbinu na kiwango cha ukatili ambao haufikiriki na hauvumiliki kabisa na watu wa leo. Badala ya kusema kwamba Ayubu alijaribiwa na Shetani, na kwamba alisimama imara katika ushuhuda wake wakati wa jaribio hili, ni bora zaidi kusema kwamba katika majaribio hayo yaliyokuwa mbele yake kutoka kwa Mungu Ayubu alianza kuwa katika mapambano na Shetani ili kuulinda utimilifu na unyofu wake, kutetea njia yake ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika shindano hili, Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng'ombe, alipoteza mali yake yote na watoto wake wa kike na kiume —lakini hakuacha utimilifu, unyofu, au hali yake ya kumcha Mungu. Kwa maneno mengine, katika pigano hili na Shetani alipendelea kunyang'anywa mali na watoto kuliko kupoteza utimilifu, unyofu na hali yake ya kumcha Mungu. Alipendelea kushikilia mzizi wa maana ya kuwa binadamu. Maandiko yanatoa simulizi halisi kuhusu mchakato wote ambao Ayubu alipoteza rasilimali zake, na pia ukasimulia mwenendo na mwelekeo wa Ayubu. Simulizi hizi za mkato, na wazi zinatoa hisia kwamba Ayubu alikuwa karibu anao utulivu wakati akipitia jaribio hili, lakini kama kile kilichofanyika kwa hakika kingeundwa upya, na kuongeza asili yale ya kijicho ya Shetani—basi mambo yasingekuwa rahisi au mepesi kama yalivyofafanuliwa kwenye sentensi hizi. Uhalisia ulikuwa wenye ukatili zaidi. Hicho ndicho kiwango cha uharibifu na chuki ambacho Shetani hushughulikia mwanadamu na wale wote wanaoidhinishwa na Mungu. Kama Mungu asingekuwa amemwomba Shetani kutodhuru Ayubu, Shetani bila shaka angekuwa amemwua bila ya shaka. Shetani hataki mtu yeyote kumwabudu Mungu, wala hataki wale wenye haki mbele ya macho ya Mungu na wale walio timilifu na wanyofu kuweza kuendelea kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa watu kumcha Mungu na kujiepusha maovu kunamaanisha kwamba wanajiepusha na kumwacha Shetani, na hivyo Shetani alitumia ruhusa ya Mungu kumlimbikizia hasira yake na chuki kwake Ayubu bila huruma. Unaona, basi, mateso aliyoyapitia Ayubu yalikuwa mengi sana, haya yalikuwa mengi kiasi gani ambayo Ayubu alipitia, kuanzia kwenye akili hadi kwenye mwili, kutoka nje hadi ndani. Leo, hatuoni namna ambavyo kwa wakati huu na tunaweza tu kupata kutoka kwenye simulizi za Biblia, mtazamo mfupi wa hisia za Ayubu wakati alipokuwa akipitia yale mateso wakati huo.

Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi. Ilikuwa, zaidi ya hapo, fursa ya Ayubu kutolea ushuhuda utakatifu wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu ulikuwa sahihi na bila makosa? Je, Ayubu alimshinda kweli Shetani? Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile.”Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “…BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.”Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani kuogopa, yaliyoleta aibu kwake na kumsababisha kutoroka kwa wasiwasi, na, vilevile, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kuelewa haiba kubwa na isiyo ya kawaida ya yule ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi, yalionyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu Shetani hivyo basi alishindwa kwenye shindano la kwanza. Licha ya utambuzi wake “uliopatikana kwa hali ngumu,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake ya unafiki. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …
Kisha, hebu tuyasome maandiko kuhusu mara ya pili ambapo Ayubu alijaribiwa.
3. Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 2:3) BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.
(Ayubu 2:6) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake.
b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani
(Ayubu 2:4-5) Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako.
c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio
(Ayubu 2:9-10) Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
(Ayubu 3:3) ) Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.

Upendo wa Ayubu ya Njia ya Mungu Inazidi Yoyote Ile Nyingine

Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu” (Ayubu 2:3). Katika maneno haya Mungu Anarudia swali moja kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha ukadiriaji wa uthibitisho wa Yehova Mungu kuhusu kile kilichoonyeshwa na kuishi na kudhihirishwa na Ayubu kwenye jaribio lake la kwanza, na ule ambao si tofauti na ukadiriaji wa Mungu wa Ayubu kabla ya kupitia jaribio lile la Shetani. Hivi ni kusema, kabla jaribio halijamfika, katika macho ya Mungu Ayubu alikuwa mtimilifu, na hivyo basi Mungu Alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki, alistahili kubarikiwa kwa macho ya Mungu. Baada ya jaribio, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu kumpongeza, na kumpa alama zote. Kwani machoni mwa Ayubu, watoto wake au rasilimali zake hazikutosha kumfanya yeye kumkataa Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, isingeweza kusawazishwa na watoto wake au kipande chochote cha mali yake. Kwenye jaribio la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwa sababu tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea tuzo kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.
Kwa Ayubu, hali hii aliyoipitia ilikuwa ya kweli na ambayo ilisafisha nafsi yake ikawa safi, ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza uwepo wake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu ya kutosha iliyojaribu utiifu wake kwa, na yeye kumcha Mungu. Jaribio hili lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka ule wa bwana tajiri hadi kwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia likamruhusu kupitia dhuluma za shetani kwa mwanadamu. Ufukara wake haukumfanya kuchukia Shetani; badala yake, kwenye vitendo vibovu vya Shetani aliuona ubaya na hali ya kudharau ya Shetani pamoja na uadui wa Shetani na uasi wake kwa Mungu, na hali hii ilimhimiza vizuri zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kugeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au urithi, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa jaribio, Ayubu alikuwa pia amepata jambo jingine: Alikuwa amepata utajiri mkubwa katikati ya majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.
Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu , na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa: Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.
Mungu Anaziangalia fikira za ndani zaidi za binadamu na yale yote ambayo binadamu anasema na kufanya. Fikira za Ayubu zilifikia masikio ya Yehova Mungu, na Mungu alisikiliza maombi yake na kwa njia hii jaribio la Mungu kwa Ayubu lililofuata liliwasili kama lilivyotarajiwa.

Katikati ya mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli utunzaji wa Mungu kwa mwanadamu

Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mtimilifu katika macho ya Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra. Shetani alitaka kutumia fursa hii kudhalilisha kabisa kujitolea kwa Ayubu kumfanya kupoteza imani yake kwa Mungu na hivyo basi kutomcha Mungu tena au kubariki jina la Yehova. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unaashiriwa kupitia kwa majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa makuu na hali ya kuonea kijicho ya Shetani kutokana na mabadilishano haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa utwezo na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi wakiwa wametishika na kusinyika kutokana na uongo wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu ataweza kutimiza utimilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda milele majaribio ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotaka matendo ya haki ya Ayubu yaweze milele kuenea na kuhimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na Shetani. Ingawaje nia ya kijicho ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani — lakini alikuwa pia na sharti moja: “yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, wakati huu, Shetani aliomba kunyosha mbele mkono wake ili kudhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba alimpa Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza maisha yake. Shetani asingeweza kuyachukua maisha ya Ayubu, lakini isipokuwa haya angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.
Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kunyosha mbele mkono wake ili kuathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, naye Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya Shetani hata kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kwenye kichwa hadi miguu akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza balaa ile iliyofanyikia roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine alipiga magoti kwenye ardhi, na kusema: Unaangalia ndani ya binadamu, unauona umaskini wake; kwa nini unyonge wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha neno la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha haraka haraka mkono wake mbele ili kudhuru mifupa ya Ayubu, akiwa na tamaa ya kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Mara, Ayubu akahisi mateso asiyoyatarajia; ni kana kwamba mwili wake ulikuwa umepasuliwa katikati kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa ikipasuliwa kipande hadi kipande. Mateso haya ya kuumiza yalimfanya akafikiria afadhali basi afe. …uwezo wake wa kuvumilia ulikuwa umefikia kilele. … Alitaka kulia kwa sauti, alitaka kuirarua ngozi kwenye mwili wake ili kupunguza maumivu—lakini alishikilia mayowe yake, na hakuirarua ngozi yake kutoka kwenye mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine, lakini wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu alikuwa hajawahi kuyatazama; Aliufunika uso wake na Akawa Amefichwa, kwa maana uumbaji wake wa binadamu haukuwa wa kumletea mateso binadamu. Wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijaribu kwa njia bora zaidi kuvumilia maumivu yake ya kimwili, lakini asingeweza kujizuia tena dhidi ya kutoa shukrani kwa Mungu: Binadamu aanguka kwa mpigo wa kwanza, yeye ni myonge na asiye na nguvu, yeye ni mchanga na asiyejua—kwa nini ukataka kumtunza na kuwa mzuri kwake yeye? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na ya Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti. … Akiwa amejaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio, Shetani aliondoka kimyakimya, lakini haya hayakufikisha hadi tamati majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijajulikana kwa umma, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Huku wahusika wengine wakiingia katika tukio hilo, matukio mengine ya ajabu zaidi yalikuwa yaje.

Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake kwa Jina la Mungu Katika Mambo Yote

Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na maudhi ya Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujiondoa na kuendeleza wajibu wa Shetani unaoweza kuonekana kwa kumshambulia Ayubu. Maandishi asilia yanafafanua hali hii hivyo basi: “Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe.” (Ayubu2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani akisingizia kuwa binadamu. Yalikuwa ni shambulizi, na shtaka, pamoja na kichocheo, jaribio, na matusi. Baada ya kushindwa kushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu kutupilia mbali uadilifu wake, kumwacha Mungu, na kusita kuishi. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kutumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova, asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo, angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.
Wakati mke wake alimshauri kulaani Mungu na kufa, maana yake ilikuwa: Mungu wako anakushughulikia hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakufanyii haki, na ilhali ungali unabariki jina la Yehova. Angekuleteaje janga hili huku unabariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kwa njia hii matatizo yako yataisha. Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika mojawapo ya hadithi za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona mapema kabla hata Ayubu kuongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu hakutupilia tu mbali uadilifu wake au kumuacha Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Je, maneno haya yanao uzito mkuu? Hapa, kunayo ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kusikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuona; maneno haya ndiyo pia kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika haya, utimilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke na watu wake wa ukoo walipomshauri, bado aliyatamka maneno hayo. Ili niweze kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni kiasi kipi cha majaribio, au ni vipi ambavyo masaibu au mateso yalivyokuwa, hata kama kifo kingemjia, hangemuacha Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama: Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.

Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli. Kama Ayubu hangekuwa amejaribiwa, kama Mungu Asingekuwa Amemletea Ayubu majaribio, wakati Ayubu aliposema, “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” ungesema kwamba Ayubu alikuwa mnafiki; Mungu alikuwa amempa rasilimali nyingi, hivyo bila shaka alilibariki jina la Yehova. Kama, kabla ya kupitia majaribio, Ayubu angekuwa amesema, “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Ungesema kwamba Ayubu alikuwa akipiga chuku, na kwamba hangeliacha jina la Mungu kwa sababu mara nyingi alibarikiwa kwa mkono wa Mungu. Kama Mungu Angekuwa Amemletea janga, basi kwa kweli angeliacha jina la Mungu. Lakini wakati Ayubu alipojipata katika hali hizi ambazo hakuna yeyote angetaka kujipata ndani au kutaka kuona, au kutaka zimpate, ambazo watu wangeogopa kupata, hali ambazo hata Mungu mwenyewe Hakuweza kuvumilia kuzitazama, bado Ayubu aliweza kushikilia uadilifu wake: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe” na “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Kama wangekumbwa na mwenendo wa Ayubu wakati huu, wale wanaopenda kuzungumzia maneno ya kuonyesha umuhimu na kuvutia, na wale wanaopenda kuongea barua na mafundisho ya dini, wanaachwa wanyamavu. Wale wanaotukuza jina la Mungu kwa matamshi pekee, ilhali hawajawahi kukubali majaribio ya Mungu, wanashutumiwa na uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa dhati, na wale ambao hawajawahi kusadiki kwamba binadamu anaweza kushikilia kwa dhati njia ya Mungu wanahukumiwa na ushuhuda wa Ayubu. Wakiwa wamekabiliwa na mwenendo wa Ayubu wakati wa majaribio haya na maneno aliyoyaongea, baadhi ya watu watahisi wakiwa wamechanganyikiwa, baadhi watamwonea wivu, baadhi wahisi shaka, baadhi wataonekana hata wasio na haja ya kufuatilia mambo haya, huku wakiukataa ushuhuda wa Ayubu kwa sababu hawayaoni tu mateso yaliyompata Ayubu wakati wa majaribio, na kusoma maneno yaliyozungumzwa na Ayubu, lakini pia ule “unyonge” wa binadamu uliofichuliwa na Ayubu wakati majaribio yalipomsibu. “Unyonge” huu wanaoamini kuwa ile hali ya kudaiwa ya kutokuwa mtimilifu katika utimilifu wa Ayubu, doa katika binadamu ambaye katika macho ya Mungu alikuwa mtimilifu. Hivi ni kusema kwamba, inasadikiwa kwamba wale walio watimilifu hawana doa wala toa, hawana dosari wala hila, kwamba hawana unyonge wowote, hawana habari yoyote kuhusu maumivu, kwamba hawahisi katu wakiwa wamehuzunika au wamekataliwa, na hawana chuki au tabia yoyote ya nje isiyofaa; kutokana na haya, watu wengi hawasadiki kwamba Ayubu alikuwa kwa kweli mtimilifu. Watu hawaidhinishi mambo mengi kuhusu tabia yake wakati wa majaribio yake. Kwa mfano, wakati Ayubu alipopoteza mali yake na watoto wake, hakuweza, kama vile watu wanavyofikiria, kuanza kulia. “Utovu wake wa adabu” unawafanya watu kufikiria alikuwa jiwe, kwani hakuwa na machozi wala upendo kwa familia yake. Hii ndiyo picha mbaya ya kwanza ambayo Ayubu anawaonyesha watu. Wanafikiri tabia yake baada ya hapo kuwa ya kushangaza zaidi: “Kulirarua joho lake” ni kauli iliyotafsiriwa na watu kuonyesha utovu wake wa heshima kwa Mungu, na “kunyoa kichwa chake” kunasadikiwa visivyo kumaanisha kukufuru kwa Ayubu na upinzani wake kwa Mungu. Mbali na maneno ya Ayubu kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” watu hawatambui uhaki wowote ndani ya Ayubu uliosifiwa na Mungu, na hivyo ukadiriaji kuhusu Ayubu kwa wengi wao si chochote zaidi ya kutofahamu, kutoelewa, shaka, lawama, na idhinisho kwa nadharia tu. Hakuna kati yao anayeweza kuelewa na kushukuru kwa kweli maneno ya Yehova Mungu kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Kutokana na picha yao kuhusu Ayubu hapo juu, watu wana shaka zaidi kuhusiana na uhaki wake, kwani vitendo na mwenendo wa Ayubu uliorekodiwa kwenye maandiko haukuwa wenye mguso wa kina kama vile watu wangefikiria. Hakutekeleza tendo lolote kubwa tu, lakini pia alikichukua kigae ili ajikwaruze akiwa ameketi kwenye jivu. Kitendo hiki kinawashangaza pia watu na kuwafanya kutilia shaka—na hata kukataa—uhaki wa Ayubu, kwani wakati akijikwaruza Ayubu hakumwomba Mungu, au kutoa ahadi kwa Mungu; wala, zaidi ya hayo, hakuonekana akilia machozi ya maumivu. Wakati huu, watu wanauona tu unyonge wa Ayubu na wala sio chochote kingine, na hivyo hata wanapomsikia Ayubu akisema “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? hawaguswi kamwe, au vinginevyo hawaonekani kuamua chochote, na bado hawawezi kutambua uhaki wa Ayubu kutoka kwa maneno haya. Picha ya kimsingi ambayo Ayubu anapatia watu wakati wa mateso ya majaribio yake ni kwamba alikuwa si mnyenyekevu wala mwenye kiburi. Watu hawaioni hadithi inayotokana na tabia yake iliyojitokeza katika kina cha moyo wake, wala hawaioni ile hali yake ya kumcha Mungu ndani ya moyo wake au kutii kwa kanuni ya njia ya kujiepusha na maovu. Utulivu wake unawafanya watu kufikiria kuwa utimilifu na unyofu wake vyote vilikuwa ni maneno matupu tu, kwamba kumcha kwake Mungu kulikuwa tu uvumi; ule “unyonge” alioufichua kwa nje, wakati huo, unawaachia picha ya kina, ukiwapatia “mtazamo mpya” kuhusu, na hata “uelewa mpya” kuhusu binadamu yule ambaye Mungu anafafanua kuwa mtimilifu na mnyofu. “Mtazamo mpya” na “uelewa mpya” kama huo vyote vinathibitishwa wakati Ayubu alipokifungua kichwa chake na kulaani siku aliyozaliwa.
Ingawaje kiwango cha mateso aliyoyapitia hakifikiriki wala kufahamika kwa binadamu yeyote, hakuzungumza maneno yoyote ya uvumi, lakini alipunguza tu maumivu ya mwili wake kwa njia zake mwenyewe. Kama ilivyorekodiwa kwenye maandiko, alisema: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.” (Ayubu3:3). Pengine, hakuna yeyote aliyewahi kutilia maanani maneno haya na kuona kwamba ni muhimu, na pengine kunao watu ambao wameyatilia maanani. Kwa maoni yako, yanamaanisha kwamba Ayubu alimpinga Mungu? Je, ni malalamiko dhidi ya Mungu? Najua kwamba wengi wenu mnayo mawazo fulani kuhusu maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu na mnasadiki kwamba kama Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, hakufaa kuonyesha unyonge wowote au huzuni yoyote, na badala yake alifaa kukabiliana vilivyo na shambulizi lolote kutoka kwa Shetani kwa njia nzuri, na hata kutabasamu wakati alikumbwa na majaribio ya Shetani. Hakufaa kuwa na mwitikio hata mdogo kuhusiana na mateso aliyoyapata kwenye mwili wake kutokana na Shetani, wala hakufaa kuonyesha hisia zozote ndani ya moyo wake. Alifaa hata kuuliza kwamba Mungu Ayafanye majaribio haya kuwa mabaya zaidi. Haya ndiyo yanayofaa kuonyeshwa na kumilikiwa na mtu ambaye hatikisiki na ambaye anamcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na maovu. Katikati ya mateso haya makuu, Ayubu hakufanya chochote ila kulaani siku aliyozaliwa. Hakulalamika kuhusu Mungu, hakuwa na nia yoyote ya kumpinga Mungu. Hali hii ni rahisi zaidi ikisemwa kuliko kutendwa, kwani tangu enzi za zamani hadi wa leo, hakuna yeyote ambaye amewahi kupitia majaribio kama hayo au kuteseka kama vile Ayubu alivyoteseka. Na kwa nini hakuna yeyote ambaye amepitia aina hiyo ya majaribio ya Ayubu? Kwa sababu, kama vile Mungu Anavyoona, hakuna yeyote anayeweza kuvumilia wajibu au agizo kama hilo, hakuna anayeweza kufanya kama Ayubu alivyofanya, na, zaidi, hakuna yule ambaye bado, mbali na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, anaweza kutoliacha jina la Mungu na kuendelea kubariki jina la Yehova Mungu, kama vile Ayubu alivyofanya wakati mateso kama hayo yalimpata. Je, mtu yeyote angeweza kufanya hivi? Tunaposema haya kumhusu Ayubu, tunapongeza tabia yake? Alikuwa binadamu mwenye haki, na aliyeweza kuwa na ushuhuda kama huo kwa Mungu, aliyeweza kumfanya Shetani kutoroka kwa haraka sana, ili asiwahi kuja mbele ya Mungu tena na kumshtaki yeye—kwa hivyo nini mbaya na kumpongeza? Inaweza kuwa kwamba kunavyo viwango vya juu zaidi kuliko Mungu? Inaweza kuwa kwamba ungechukua hatua hata bora zaidi kuliko Ayubu wakati majaribio yatakapokusibu? Ayubu alisifiwa na Mungu—ni upinzani upi unaoweza kuwa nao?

Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hataki Mungu Kupata Maumivu Kwa Sababu Yake Yeye

Mara nyingi mimi husema kwamba Mungu huangalia ndani ya mioyo ya watu, na watu huangalia namna watu walivyo kwa nje. Kwa sababu Mungu anaangalia ndani ya mioyo ya watu, Anaelewa kiini chao, huku nao watu wanafafanua kiini cha watu wengine kutokana na wanavyoonekana kwa nje. Wakati Ayubu alipoufunua mdomo wake na kulaani siku ya kuzaliwa kwake, kitendo hiki kilishangaza wahusika wote wa kiroho, wakiwemo wale marafiki watatu wa Ayubu. Binadamu alitoka kwa Mungu, na anafaa kuwa mwenye shukrani kwa maisha na mwili, pamoja na siku yake ya kuzaliwa, aliopewa na Mwenyezi Mungu, na wala hafai kuilaani. Hali hii inaeleweka na kufahamika na watu wengi. Kwa yeyote yule anayemfuata Mungu, uelewa huu ni takatifu na wenye dhabiti, ni ukweli usioweza kubadilika. Ayubu, kwa mkono mwingine, alizivunja sheria: Aliilaani siku ya kuzaliwa kwake. Hiki ni kitendo ambacho watu wengi huchukulia kuwa ni kuvuka hadi kwenye eneo haramu. Yeye hastahili tu uelewa na huruma ya watu, lakini pia hastahili msamaha wa Mungu. Wakati huohuo, hata watu wengi zaidi wanatilia shaka uhaki wa Ayubu, kwani inaonekana kana kwamba kibali cha Mungu kwake yeye kilimfanya Ayubu kujifikiria yeye mwenyewe, kilimfanya kuwa jasiri sana na asiyejali kiasi cha kwamba hakuweza tu kutoshukuru Mungu kwa kumbariki yeye na kumtunza yeye wakati wa maisha yake, lakini pia aliilaani siku ya kuzaliwa kwake na kuomba ingeangamizwa. Hii ni nini, kama si kumpinga Mungu? Mambo ya juujuu kama hayo yanawapa watu ithibati ya kushutumu kitendo hiki cha Ayubu, lakini ni nani anayejua kile Ayubu alichokuwa akifikiria kwa kweli wakati huo? Na ni nani anayeweza kujua sababu ya Ayubu kufanya hivyo? Mungu pekee na Ayubu mwenyewe ndio wanaojua hadithi ya ndani na sababu husika hapa.
Wakati Shetani alipounyosha mbele mkono wake ili kudhuru mifupa ya Ayubu, Ayubu aliangukia mashiko yake, bila ya mbinu za kutoroka au nguvu za kumpinga. Mwili na nafsi yake iliteseka na kupata maumivu makali, na maumivu haya yalimfanya kufahamu kwa kina kuhusu kutokuwa na umuhimu, unyonge, na hali ya kutokuwa na mamlaka iliyokuwemo ndani ya mwili. Wakati huohuo, alipata uelewa mkubwa wa kwa nini Mungu Anatilia maanani kujali na kumtunza mwanadamu. Akiwa ameangukia mashiko ya shetani, Ayubu alitambua kwamba binadamu, aliye katika mwili na damu, kwa hakika hana nguvu kamwe. Wakati aliposujudu na kumwomba Mungu, alihisi ni kana kwamba Mungu Alikuwa akiufunika uso Wake, na kujificha, kwani Mungu Alikuwa Amemweka kabisa katika mikono ya Shetani. Wakati huohuo, Mungu Alimlilia yeye, na, zaidi, Alimsikitikia yeye; Mungu Aliumizwa na maumivu yake na Aliumia kwa maumivu yake. … Ayubu alihisi maumivu ya Mungu, pamoja na namna ambavyo haikuweza kuvumilika kwa Mungu. … Ayubu hakutaka kuleta huzuni wowote zaidi kwa Mungu, wala hakutaka Mungu kulia kwa ajili yake yeye, isitoshe hakutaka kumwona Mungu akiwa katika maumivu kwa sababu yake yeye. Wakati huu, Ayubu alitaka tu kujiondoa mwenyewe kwenye mwili wake, kuacha kuvumilia tena maumivu yaliyoletewa kwake kupitia kwa mwili wake, kwani kufanya hivi kungekomesha Mungu kuteseka kwa maumivu yake—lakini hakuweza kufanya hivyo, na alifaa kuvumilia tu maumivu ya mwili, na pia mateso ya kutotaka kumfanya Mungu kuwa na wasiwasi. Maumivu haya mawili—moja kutoka kwa mwili, na mengine kutoka kwa roho—yalileta maumivu makali ya moyoni, yakusokotesha tumbo kwake Ayubu, na kumfanya yeye kuhisi namna ambavyo mipaka ya binadamu aliye na mwili na damu inavyoweza kumfanya mtu kuhisi akiwa amedhalilishwa na asiye na njia ya kusaidika. Katika hali hizi, tamanio lake la Mungu lilizidi kukua, na chuki yake kwa Shetani ikazidi kuwa nyingi. Wakati huu, Ayubu angependelea kutowahi kuzaliwa kwenye ulimwengu huu wa binadamu, afadhali asingekuwepo badala ya kumuona Mungu Akilia au Akihisi maumivu kwa sababu yake. Alianza kuchukia kwa kina mwili wake, kuwa mgonjwa na mchovu ndani yake mwenyewe, siku yake ya kuzaliwa, na hata ya hayo yote ambayo yalikuwa yameunganishwa kwake. Hakutaka kuwepo na kutajwa kokote zaidi kuhusu siku yake ya kuzaliwa au chochote kilichohusu siku hiyo, na hivyo aliufunua mdomo wake na kuilaani siku yake ya kuzaliwa: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba. Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” (Ayubu3:3-4). Maneno ya Ayubu yanaonyesha kuchukia kwake kwa nafsi yake mwenyewe, “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba,” pamoja na yeye kujilaumu mwenyewe na kuwa katika hali ya kuhisi kwamba yuko katika hatia kwa kumsababishia Mungu maumivu, “Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna Ayubu alivyohisi wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu utimilifu wake na unyofu wake kwa wote. Wakati huohuo, kama vile tu Ayubu alivyokuwa ametaka, imani na utiifu wake kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, vyote viliinuliwa. Bila shaka, kuinuliwa huku kwa hakika ni athari ambayo Mungu Alikuwa Ametarajia.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni