4/10/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | (III) Aina Tano za Watu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | (III) Aina Tano za Watu

    Kwa sasa, Nitaacha ushirika wetu kuhusu tabia ya haki ya Mungu umalizikie hapo. Kinachofuata Nitaainisha wafuasi wa Mungu katika kategoria mbalimbali, kulingana na ufahamu wao wa Mungu na ufahamu wao na kile wamepitia kuhusiana na tabia ya haki Yake, ili muweze kujua awamu ambayo kwa sasa mnapatikana ndani pamoja na kimo chenu cha sasa. Kuhusiana na maarifa yao ya Mungu na ufahamu wao wa tabia Yake ya haki, awamu na kimo tofauti ambavyo watu huwa navyo vinaweza kugawanywa katika aina tano. Mada hii imeelezewa kwa msingi wa kumjua Mungu wa kipekee na tabia Yake ya haki; kwa hivyo, unaposoma maudhui yafuatayo, unafaa kujaribu kwa makini kuchambua ni kiwango kipi haswa cha ufahamu na maarifa ulichonacho kuhusiana na upekee wa Mungu na tabia Yake ya haki, na kisha utumie hayo kujua ni awamu gani ambayo kwa kweli unapatikana ndani, kimo chako ni kikubwa vipi kwa kweli, na wewe ni aina gani ya mtu kwa kweli.
    Aina ya kwanza yajulikana kama awamu ya “mtoto mchanga aliye bado na vitambaa vya kufungwafungwa”.
    Mtoto mchanga aliye katika vitambaa vya kufungwafungwa ni nani? Mtoto mchanga aliye katika vitambaa vya kufungwafungwa ni mtoto mchanga ambaye ndio mwanzo ameingia kwenye ulimwengu huu, amezaliwa. Huu ndio wakati ambao watu wako katika awamu ndogo zaidi na isiyo na ukomavu.
    Watu katika awamu hii kimsingi hawamiliki utambuzi au ufahamu wowote wa masuala ya kuamini Mungu. Wamekanganywa na hawajui kila kitu. Watu hawa huenda wamemsadiki Mungu kwa muda mrefu au kwa muda usiokuwa mrefu, lakini hali yao ya kukanganywa na kutojua kimo chao halisi kinawaweka kwenye awamu ya mtoto mchanga katika vitambaa vya kufungwafungwa. Ufafanuzi wa hakika wa hali hii ya mtoto mchanga katika vitambaa vya kufungwafungwa ni kama vile: Haijalishi ni muda upi ambao aina hii ya mtu amesadiki Mungu, siku zote atakuwa mpumbavu, atachanganyikiwa na ataonyesha werevu au uamuzi wa kiwango kidogo sana; hajui ni kwa nini anasadiki Mungu, wala hajui Mungu ni nani au Mungu ni nini. Ingawaje anafuata Mungu, hakuna ufafanuzi halisi wa Mungu katika moyo wake, na hawezi kuamua kama yule anayemfuata ni Mungu, sikuambii hata kama kweli anafaa kumsadiki Mungu na kumfuata Yeye. Hizi ndizo hali za kweli za aina hii ya mtu. Fikira za watu hawa zimezingirwa na ukungu, na kama nitasema wazi, imani yao ni ile ya mkanganyo. Siku zote wanakuwa katika hali ya mkanganyiko na utupu; kuwa mpumbavu, kuchanganyikiwa na kuonyesha werevu au uamuzi wa kiwango kidogo sana ndivyo vitu vinavyofanya muhtasari wa hali zao. Hawajawahi kuona wala kuhisi uwepo wa Mungu, na hivyo basi, kuwazungumzia kuhusu kujua Mungu ni sawa tu na kuwafanya kusoma kitabu kilichoandikwa kwa maandiko ya hieroglifu (maandiko au ishara zisizofahamika); hawataelewa wala kuyakubali. Kwao, kujua Mungu ni sawa na kusikia kisa cha kifantasia. Huku fikira zao zikiwa zinaweza kuwa na ukungu, kwa hakika wanasadiki kwa dhati kwamba kujua Mungu ni kupoteza muda na jitihada. Huyu ndiye mtu wa aina ya kwanza: mtoto mchanga aliye katika vitambaa vya kufungwafungwa.
    Aina ya pili ni yule wa awamu ya “mtoto mchanga anayenyonya”.
    Akilinganishwa na mtoto mchanga aliye katika vitambaa vya kufungwafungwa, aina hii ya mtu amepiga hatua fulani. Kwa bahati mbaya, bado hawana ufahamu wa Mungu kamwe. Wangali wanakosa ufahamu wazi wa na utambuzi wa Mungu, na hawaelewi vizuri sana ni kwa nini wanafaa kumsadiki Mungu, lakini katika mioyo yao wanalo kusudi lao binafsi na mawazo wazi. Hawajihusishi na suala la kama ni sahihi kumsadiki Mungu. Lengo na kusudi wanalotafuta kupitia kwa imani ya Mungu ni kufurahia neema Yake, kuwa na furaha na amani, kuishi maisha yenye utulivu, kuwa na utunzaji na ulinzi wa Mungu na kuishi katika baraka za Mungu. Hawajali kiwango ambacho wanamjua Mungu; hawana msisimko wa kutafuta kuelewa Mungu, wala hawashughuliki na kile ambacho Mungu anafanya au kile ambacho Angependa kufanya. Wanatafuta tu bila mwelekeo kufurahia neema Yake na kupata baraka Zake nyingi; wanatafuta kupokea baraka mara mia moja kwenye umri wa sasa, na maisha ya baadaye kwenye miaka ijayo. Fikira zao, matumizi na kujitolea kwao, pamoja na kuteseka kwao, vyote vinalo lengo moja: kupokea neema na baraka za Mungu. Hawana shughuli na kitu kingine chochote. Aina hii ya mtu bila shaka ana hakika kwamba Mungu anaweza kuwalinda wakawa salama na kuwapa neema Yake. Mtu anaweza kusema kwamba hawana kivutio chochote katika na hawana mwelekeo sana kuhusiana na kwa nini Mungu angependa kumwokoa binadamu au matokeo ambayo Mungu angependa kupata kutokana na matamshi na kazi Yake. Hawajawahi kutia jitihada za kujua hali halisi ya Mungu na tabia ya haki, wala hawawezi kujipa moyo na kuwa na nia ya kufanya hivyo. Hawahisi kumakinikia katika mambo haya, wala hawapendi kuyajua. Hawapendi hata kuulizia kuhusu kazi ya Mungu, mahitaji ya Mungu kwa binadamu, mapenzi ya Mungu au kitu chochote kingine kinachohusiana na Mungu; wala hawawezi kuwa na msukumo wa kuulizia mambo haya. Hii ni kwa sababu wanasadiki masuala haya hayahusiani na kufurahia kwao kwa neema ya Mungu; wanajali tu Mungu anayeweza kuwapa neema na ambaye ana uhusiano na masilahi yao ya kibinafsi. Hawana haja kamwe na kitu kingine chochote, na kwa hivyo hawawezi kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, licha ya miaka mingapi ambayo wamemsadiki Mungu. Bila kuwepo yeyote wa kuwafunza neno la Bwana, mara nyingi ni vigumu kwao kuendelea kupiga hatua katika njia ya imani ya Mungu. Kama hawawezi kufurahia furaha yao na amani ya awali au kufurahia neema ya Mungu, basi wana uwezekano mkubwa wa kujiondoa. Huyu ndiye mtu wa aina ya pili: mtu anayekuwepo kwenye awamu ya mtoto mchanga wa kunyonya.
    Aina ya tatu ni awamu ile ya mtoto mchanga anayeachishwa ziwa—awamu ya mtoto mdogo.
    Kundi hili la watu humiliki ufahamu fulani wenye uwazi. Watu hawa wanao ufahamu kwamba kufurahia neema ya Mungu hakumaanishi kwamba wao wenyewe wanamiliki uzoefu wa kweli; wanao ufahamu kwamba wasipochoka katika kutafuta furaha na amani, katika kutafuta neema, au kama wanaweza kushuhudia kwa kujadiliana yale yote ambayo wamepitia katika kufurahikia kwao kwa neema ya Mungu au kwa kusifia baraka za Mungu ambazo amewapa, mambo haya hayamaanishi kwamba wanayo maisha, wala hayamaanishi kwamba wanao uhalisi wa ukweli. Tukianzia katika fahamu yao, wanasita kufurahia matumaini yasiyo na mipaka kwamba wataandamana tu na neema ya Mungu; badala yake, wakati wanapofurahia neema ya Mungu, wanapenda wakati uo huo kufanya kitu kwa ajili ya Mungu; wako radhi kutekeleza wajibu wao, kuvumilia ugumu kidogo na uchovu, kuwa na kiasi fulani cha ushirikiano na Mungu. Hata hivyo, kwa sababu kufuatilia kwao katika imani yao katika Mungu kumetiwa najisi sana, kwa sababu nia za kibinafsi na matamanio waliyo nayo ni makali mno, kwa sababu tabia yao ni yenye kiburi kisicho na mipaka, ni vigumu sana kwao kutosheleza tamanio la Mungu au kuwa watiifu kwa Mungu; hivyo basi, wao mara nyingi hawawezi kutambua matamanio yao ya kibinafsi au kuheshimu ahadi zao kwa Mungu. Mara nyingi wanajipata katika hali za kukinzana: Wanapenda sana kutosheleza Mungu hadi kwenye kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana, ilhali wanatumia uwezo wao wote kumpinga Yeye; mara nyingi wanaweka nadhiri kwa Mungu lakini kwa haraka sana wanaishia kukwepa nadhiri zao. Hata mara nyingi wanajipata katika hali nyingine kinzani: Wanasadiki kwa dhati katika Mungu ilhali wanamkataa Mungu na kila kitu kinachotokana na Yeye; wanatumai kwa hamu kwamba Mungu atawapa nuru, atawaongoza, atawaruzuku na kuwasaidia, ilhali bado wanatafuta njia yao wenyewe. Wanapenda kuelewa na kujua Mungu, ilhali hawako radhi kuwa na uhusiano wa karibu na Yeye. Badala yake, siku zote wanamwepuka Mungu; mioyo yao haiko wazi kumkaribisha. Huku wakiwa na ufahamu wa juujuu na uzoefu wa maana ya moja kwa moja ya matamshi ya Mungu na ya ukweli, na dhana ya juujuu ya Mungu na ukweli, katika akili iliyofichika bado hawawezi kuthibitisha au kuamua kama Mungu ni ukweli; hawawezi kuthibitisha kama Mungu ni wa haki kwa kweli; wala hawawezi kuamua ule uhalisi wa tabia ya Mungu na hali halisi, sikuambii hata uwepo Wake wa kweli. Imani yao katika Mungu siku zote ina shaka na kutoelewana kwingi, na pia kunazo fikira za maono na dhana mbalimbali. Wanapofurahia neema ya Mungu, wanapitia pia bila kutaka au wanatenda baadhi ya kile wanachosadiki kuwa ukweli unaowezekana, ili kunufaisha imani yao, kukuza kile ambacho wamepitia katika kusadiki Mungu, kuthibitisha ufahamu wao wa kusadiki Mungu, na kutosheleza majisifu yao ya kutembelea njia ya maisha ambayo wao wenyewe wameanzisha na kukamilisha mkondo wa haki wa mwanadamu. Wakati uo huo wanafanya pia mambo haya ili kutosheleza tamanio lao binafsi la kufaidi baraka, ili wawekeane dau ndio waweze kupata baraka kubwa zaidi za ubinadamu, ili kutimiza maazimio ya maono na matamanio ya kimaisha ya kutopumzika mpaka pale ambapo wamefaidi Mungu. Watu hawa kwa nadra sana wanaweza kupokea nuru ya Mungu, kwani tamanio lao na nia yao ya kufaidi baraka ni muhimu sana kwao. Hawana tamanio la na hawawezi kuvumilia kutupilia mbali hili. Wanaogopa kwamba bila ya tamanio la kufaidi baraka, bila ya maono waliyotamani kwa muda mrefu ya kutopumzika mpaka pale ambapo wamefaidi Mungu, wataweza kukosa motisha ya kusadiki Mungu. Kwa hivyo, hawapendi kukabiliana na uhalisi. Hawapendi kukabiliana na matamshi ya Mungu au kazi ya Mungu. Hawapendi kukabiliana na tabia au hali halisi ya Mungu, sikuambii hata kuzungumzia mada ya kumjua Mungu. Hii ni kwa sababu mara tu Mungu, hali Yake halisi na tabia Yake ya haki vinapobadilisha maono yao, ndoto zao zitatoweka hivyo bila kuonekana; imani yao inayodhaniwa kuwa safi na “sifa njema” zilizokusanywa baada ya miaka ya kazi ngumu zitatoweka zote na kutokuwa na manufaa yoyote; “eneo” lao ambalo wameshinda kupitia kwa jasho na damu yao kwa miaka na mikaka itakuwa karibu kusambaratika. Hii itamaanisha kwamba miaka yao mingi ya kazi ya sulubu na jitihada vyote vimekuwa bure bilashi, kwamba lazima waanze tena kutoka sehemu ya kutokuwa na chochote. Haya ndiyo maumivu magumu zaidi kwao kuvumilia katika mioyo yao, na ni matokeo ambayo wanatamani kwa kiasi cha chini zaidi kuona; hivyo basi siku zote wamefungwa katika aina hii ya kutosonga mbele, na kukataa kurudi nyuma. Huyu ndiye mtu wa aina ya tatu: mtu anayekuwa katika awamu hii ya mtoto mchanga wa kuachishwa ziwa.
    Aina tatu za watu waliofafanuliwa hapo juu—kwa maneno mengine, watu wanaopatikana katika awamu hizi tatu—hawamiliki imani yoyote ya kweli katika utambulisho na hadhi ya Mungu au katika tabia Yake halisi, wala hawana utambuzi wowote wazi, wa hakika au thibitisho la mambo haya. Kwa hivyo, ni vigumu sana kwa aina hizi tatu za watu kuingia kwenye uhalisi wa ukweli, na ni vigumu pia kwa wao kupokea huruma, nuru au mwangaza wa Mungu kwa sababu ya namna ambavyo wanasadiki Mungu na mtazamo wao wa kimakosa kwa Mungu unamfanya Yeye kutoweza kutekeleza kazi yoyote ndani ya mioyo yao. Shaka zao, kuelewa kwao vibaya na kufikiria kwao kuhusiana na Mungu kumezidi imani yao na maarifa ya Mungu. Hizi ni aina tatu hatari sana za watu pamoja na awamu tatu hatari sana. Wakati mtu anapoendeleza mtazamo wa shaka kwa Mungu, hali halisi ya Mungu, utambulisho wa Mungu, lile suala la kama Mungu ni ukweli na uhalisi wa uwepo Wake na kwamba hawezi kuwa na hakika katika mambo haya, ni vipi ambavyo mtu anaweza kukubali kila kitu kinachotoka kwa Mungu? Mtu anawezaje kukubali hoja kwamba Mungu ni ukweli, njia na uzima? Mtu anawezaje kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu? Mtu anawezaje kukubali wokovu wa Mungu? Ni vipi ambavyo aina hii ya mtu anaweza kupokea mwongozo na ruzuku ya kweli kutoka kwa Mungu? Wale ambao wanapatikana katika awamu hizi tatu wanaweza kumpinga Mungu, kupitisha hukumu kwa Mungu, kukufuru Mungu au kusaliti Mungu wakati wowote. Wanaweza kuacha njia ya kweli na kumtoroka Mungu wakati wowote. Mtu anaweza kusema kwamba watu katika awamu hizi tatu wapo katika kipindi hatari sana, kwani hawajaingia kwenye njia sahihi ya kumsadiki Mungu.
    Aina ya nne ni awamu ya mtoto anayekomaa; yaani, kipindi cha utoto.
    Baada ya mtu kuachishwa ziwa—yaani, baada ya wao kufurahia kiwango tosha cha neema, mtu anaanza kuchunguza ni nini maana ya kusadiki Mungu, kutaka kuelewa maswali tofauti, kama vile kwa nini binadamu anaishi, binadamu anafaa kuishi vipi na kwa nini Mungu hutekeleza kazi Yake kwa binadamu. Wakati ambapo mawazo haya yasiyo wazi na fikira hizi zilizokanganyika hujitokeza ndani yao, na kuwepo ndani yao, wanaendelea kupokea kunyunyizwa na wanaweza pia kutekeleza wajibu wao. Kwenye kipindi hiki, hawana tena shaka kuhusiana na ukweli wa uwepo wa Mungu, na wanao ung’amuzi sahihi wa ni nini maana ya kumwamini Mungu. Kwenye msingi huu wanayo maarifa ya utaratibu kuhusu Mungu, na wanapokea kwa utaratibu baadhi ya majibu ya mawazo yao yasiyo wazi na fikira zilizokanganyika kuhusiana na tabia ya Mungu na hali halisi. Kwa mujibu wa mabadiliko yao katika tabia yao pamoja na maarifa yao kuhusu Mungu, watu katika awamu hii huanza kushika njia sahihi na kuingia kwenye kipindi cha mpito. Ni katika awamu hii ambapo watu huanza kuwa na maisha. Vionyeshi wazi vya kumiliki maisha ni uamuzi wa taratibu wa maswali mbalimbali yanayohusiana na kumjua Mungu ambayo watu wanakuwa nayo katika mioyo yao—kutoelewana, dhana, ufahamu na ufafanuzi usio wazi wa Mungu—ambao si kwamba wanakosa kusadiki tu na kujua uhalisi wa uwepo wa Mungu lakini pia wanamiliki ufasili wazi na mpangilio wa Mungu katika mioyo yao, ambapo kule kumfuata Mungu kwa kweli kutabadilisha imani yao isiyo dhahiri. Kwenye awamu hii, watu kwa utaratibu wanaanza kujua kutoelewa kwao katika masuala ya Mungu na kutafuta kwao kimakosa na njia za imani. Wanaanza kutamani ukweli, kutamani kupitia hukumu ya Mungu, kurudiwa na nidhamu, kutamani mabadiliko katika tabia yao. Kwa utaratibu wanaaza kuacha aina zote za dhana na fikira kuhusu Mungu kwenye awamu hii; wakati uo huo wanabadilisha na kurekebisha maarifa yasiyo sahihi kuhusu Mungu na kupata baadhi ya maarifa muhimu na sahihi kuhusu Mungu. Ingawaje sehemu ya maarifa inayomilikiwa na watu katika awamu hii si mahususi au sahihi sana, kwa kiwango cha chini zaidi wanaanza kwa utaratibu kuacha dhana zao, maarifa ya kimakosa na kutoelewa mambo kuhusu Mungu; hawaendelezi tena dhana zao binafsi na fikira zao kuhusu Mungu. Wanaanza kujifunza namna ya kuacha—kuacha mambo yanayopatikana miongoni mwa dhana zao binafsi, kutoka kwa maarifa yao na kutoka kwa Shetani; wanaanza kuwa radhi kutii mambo sahihi na mazuri, hata kwa mambo yanayotoka kwenye matamshi ya Mungu na kutii ukweli. Wanaanza pia kujaribu kupitia matamshi ya Mungu, kujua kibinafsi na kutekeleza matamshi Yake, kukubali matamshi Yake kama kanuni za hatua zao na kama msingi wa kubadilisha tabia yao. Kwenye kipindi hiki, watu bila kufahamu wanaikubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanakubali bila fahamu matamshi ya Mungu kuwa maisha yao. Huku wakikubali hukumu, kuadibu kwa Mungu, na kukubali matamshi ya Mungu, wanaendelea kuwa na ongezeko la fahamisho na wanaweza kuhisi kwamba Mungu wanayemsadiki ndani ya mioyo yao kweli yupo. Kwa maneno ya Mungu, hali yao wanayopitia na maisha yao, wanazidi kuhisi kwamba Mungu siku zote amesimamia hatima ya binadamu, kumwongoza binadamu na kuruzuku binadamu. Kupitia kwa ushirikiano wao na Mungu, wanaanza kwa utaratibu kuthibitisha uwepo wa Mungu. Kwa hivyo, kabla ya wao kutambua, tayari wameuidhinisha bila kufahamu na kusadiki kwa dhati katika kazi ya Mungu, na wameidhinisha matamshi ya Mungu. Baada ya watu kuidhinisha matamshi ya Mungu, na kuidhinisha kazi ya Mungu, bila kusita wanajikataa, wanakataa dhana zao binafsi, wanakataa maarifa yao binafsi, wanakataa fikira zao binafsi, na wakati uo huo wanatafuta bila kusita ukweli ni nini na mapenzi ya Mungu ni nini. Maarifa ya watu kuhusu Mungu ni ya juujuu sana kwenye kipindi hiki cha maendeleo—hata hawawezi kufafanua wazi maarifa haya kwa kutumia matamshi, wala hawawezi hata kufafanua kimahususi—na wanao ufahamu unaohusu utambuzi; hata hivyo, wakati awamu hii inawekwa sambamba na zile awamu tatu zilizotangulia, maisha ya watu wasiokomaa katika kipindi hiki tayari yameanza kupokea kunyunyizia na ruzuku ya matamshi ya Mungu, na tayari yameanza kuota. Ni sawa na mbegu iliyozikwa ardhini; baada ya kupokea unyevunyevu na virutubisho, lazima itapenyeza kupitia kwenye mchanga; kuota kwake kunawakilisha kuzaliwa kwa maisha mapya. Kuzaliwa huku kwa maisha mapya kunaruhusu mtu kuona vionyeshi vya maisha. Kupitia kwa maisha, watu wataweza kukua. Kwa hivyo, juu ya misingi hii—kwa utaratibu wanaanza kurudi katika njia sahihi ya kusadiki katika Mungu, kuacha dhana zao binafsi, kupata mwongozo wa Mungu—maisha ya watu yataweza kukua bila shaka hatua kwa hatua. Ni katika msingi gani ndipo ukuaji huu unapimwa? Unapimwa kulingana na uzoefu wao na maneno ya Mungu na ufahamu wao wa kweli kuhusu tabia ya haki ya Mungu. Ingawaje wanaona jambo hili likiwa gumu sana katika kutumia maneno yao binafsi ili kufafanua kwa usahihi maarifa yao kuhusu Mungu na hali Yake halisi kwenye kipindi hiki cha ukuaji, kundi hili la watu haliko radhi tena kufuatilia kimsingi furaha kupitia kwa kufurahia neema ya Mungu, au kufuatilia kusudi lao la kusadiki Mungu, ambapo ni kupokea neema Yake. Badala yake, wako radhi kutafuta kuishi kwa neno la Mungu, ili kuwa walengwa wa wokovu wa Mungu. Vilevile, wanamiliki ujasiri na wako tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Hii ndiyo alama ya mtu aliye katika awamu ya kukua.
    Ingawaje watu katika awamu hii wanayo maarifa fulani kuhusu tabia ya haki ya Mungu, maarifa yao si dhahiri wala bainifu. Huku wakiwa hawawezi kufafanua wazi hali hii, wanahisi kwamba tayari wamefaidi kitu fulani ndani kwa ndani, kwani wamepata kipimo fulani cha maarifa na ufahamu wa tabia ya haki ya Mungu kupitia kwa kuadibu kwa Mungu na hukumu yake; hata hivyo yote haya ni kana kwamba ni ya juujuu, na bado yangali katika awamu ya kimsingi. Kundi hili la watu linao msimamo wa maoni thabiti kuhusiana na neema ya Mungu. Msimamo huu wa maoni unaelezewa kupitia kwenye mabadiliko ya malengo wanayoyatafuta na njia ambayo wanayatafutia. Tayari wameona—katika maneno na kazi ya Mungu, kwenye aina zote za mahitaji Yake ya binadamu na kwenye ufunuo Wake wa binadamu—kwamba kama bado hawatafuatilia ukweli, kama bado hawatafuti kuingia kwenye uhalisia, kama bado hawatafuti kutosheleza na kujua Mungu huku wakipitia maneno Yake, watapoteza umuhimu katika kusadiki Mungu. Wanaona haijalishi ni kiwango kipi ambacho wanafurahia neema ya Mungu, hawawezi kubadilisha tabia yao, kutosheleza Mungu au kumjua Mungu, na kwamba wakiendelea kuishi miongoni mwa neema ya Mungu, hawatawahi kutimiza ukuaji, kupata uzima au kuweza kupokea wokovu. Kwa muhtasari, kama mtu hawezi kupitia maneno ya Mungu kwa njia ya kweli na hawezi kumjua Mungu kupitia kwa maneno Yake, mtu huyo daima dawamu atabakia katika awamu ile ya mtoto mchanga na hatawahi kupiga hatua yoyote mbele kwenye ukuaji wa maisha yake. Kama daima dawamu utakuwepo kwenye awamu ya mtoto mchanga, kama hutawahi kuingia kwenye uhalisi wa neno la Mungu, kama hutawahi kuweza kuishi kwa neno la Mungu, kama hutawahi kuweza kumiliki imani na maarifa ya kweli kuhusu Mungu, je, kunao uwezekano wowote kwako wewe kufanywa kuwa kamili na Mungu? Hivyo basi, yeyote anayeingia katika uhalisi wa neno la Mungu, yeyote anayekubali neno la Mungu kuwa maisha yake, yeyote anayeanza kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu, yeyote ambaye tabia yake potoshi inaanza kubadilika, na yeyote aliye na moyo unaotamani ukweli, analo tamanio la kumjua Mungu, analo tamanio la kukubali wokovu wa Mungu—watu hawa ndio wale wanaomiliki uzima kwa kweli. Hii kwa kweli ndiyo aina ya nne ya mtu, ile ya mtoto anayekomaa, mtu aliye katika awamu ya utoto.
    Aina ya tano ni ile awamu ya maisha yaliyokomaa, au awamu ya mtu mzima.
    Baada ya kupitia awamu ya mtoto mchanga hadi ya utoto, awamu hii ya ukuaji uliojaa kupindua kunakojirudia, maisha ya watu tayari yamekuwa thabiti, hatua yao ya kusonga mbele haisiti tena, wala hakuna yeyote anayeweza kuwazuia. Ingawaje njia iliyo mbele ingali na mabonde na misukosuko, si wanyonge tena au wenye woga; hawayumbiyumbi tena huko mbele au kupoteza mwelekeo wao. Misingi yao imekita mizizi kwenye hali halisi ya neno la Mungu. Mioyo yao imevutwa na heshima na ukubwa wa Mungu. Wanatamani kufuata nyayo za Mungu, kujua hali halisi ya Mungu, kujua Mungu kwa uzima Wake.
    Watu katika awamu hii tayari wanajua waziwazi ni nani wanayemsadiki, na wanajua waziwazi kwa nini wanafaa kumsadiki Mungu na maana ya maisha yao husika; wanajua pia waziwazi kwamba kila kitu ambacho Mungu huelezea ndicho ukweli. Kwenye miaka yao mingi ya uzoefu, wametambua kwamba bila ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, mtu hatawahi kuweza kutosheleza au kumjua Mungu, wala mtu huyo hataweza kuja mbele ya Mungu. Ndani ya mioyo ya watu hawa husika kunalo tamanio thabiti la kujaribiwa na Mungu, ili kuona tabia ya haki ya Mungu huku wakiendelea kujaribiwa, kufikia upendo safi zaidi, na wakati uo huo kuweza kuelewa na kujua Mungu kwa njia ya kweli zaidi. Wale walio katika awamu hii tayari wameaga kwaheri awamu ya mtoto, awamu ya kufurahia neema ya Mungu na kula mkate na kushiba. Hawaweki tena matumaini mengi katika kumfanya Mungu kuvumilia na kuwaonyesha huruma; badala yake, wanao ujasiri wa kupokea na kutumai kupata kuadibu na hukumu isiyosita ya Mungu, ili kuweza kujitenga na tabia yao potoshi na hivyo basi kutosheleza Mungu. Maarifa yao kwa Mungu, kufuatilia kwao au shabaha za mwisho za kufuatilia kwao: mambo haya yote yako wazi kabisa katika mioyo yao. Hivyo basi, watu katika awamu ya mtu mzima tayari wameaga kwaheri kabisa awamu ya imani isiyo dhahiri, kwenye awamu ambayo wanategemea neema kupata wokovu, kwenye awamu ya maisha yasiyo komavu yasiyoweza kustahimili majaribio, hadi kwenye awamu ya kutokuwa bainifu, hadi kwenye awamu ya kuyumbayumba, hadi kwenye awamu ya mara kwa mara kutokuwa na njia ya kufuata, hadi kwenye kipindi kisichokuwa thabiti cha kubadilisha kati ya joto na baridi ya ghafla, na hadi kwenye awamu ambapo mtu anafuata Mungu huku ameyafumba macho yake. Aina hii ya mtu hupokea nuru na mwangaza wa Mungu mara kwa mara, na pia mara kwa mara hujihusisha katika ushirikiano na mawasiliano ya kweli na Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika awamu hii tayari wameng’amua sehemu ya mapenzi ya Mungu; wanaweza kupata kanuni za ukweli katika kila kitu wanachofanya; wanajua namna ya kutosheleza tamanio la Mungu. Isitoshe, wamepata pia njia ya kumjua Mungu na wameanza kuwa na ushuhuda wa maarifa yao kwa Mungu. Kwenye mchakato huu wa ukuaji wa utaratibu, wanao ufahamu wa taratibu na maarifa ya mapenzi ya Mungu, ya mapenzi ya Mungu katika kuumba ubinadamu, ya mapenzi ya Mungu katika kusimamia ubinadamu; vilevile, kwa utaratibu wanao ufahamu na maarifa ya tabia ya haki ya Mungu kwa mujibu wa hali halisi. Hakuna dhana ya binadamu au kufikiria kunaweza kubadilisha maarifa haya. Huku mtu hawezi kusema kwamba kwenye awamu ya tano maisha ya mtu yamekomaa kabisa au kumwita mtu huyu mwenye haki au mkamilifu, aina hii ya mtu tayari amechukua hatua ya kuelekea kwenye awamu ya ukomavu katika maisha; mtu huyu tayari anaweza kuja mbele ya Mungu, kusimama ana kwa ana na neno la Mungu na kuwa ana kwa ana na Mungu. Kwa sababu mtu wa aina hii tayari amepitia mengi sana yanayohusu neno la Mungu, amepitia majaribio yasiyokadirika na kupitia matukio yasiyokadirika ya nidhamu, hukumu na kuadibu kutoka kwa Mungu, unyenyekevu wake kwa Mungu si wa kutegemea chochote bali ni kamili. Maarifa yao kwa Mungu yamebadilika kutoka kwenye kufichika akilini hadi kwa maarifa wazi na hakika, kutoka kwenye hali ya juujuu hadi kina, kutoka kwenye hali ya kutoeleweka na kutokuwa bainifu hadi hali ya umakinifu na uyakinifu, na wamebadilika kutoka kwenye kuyumbayumba kwa matatizo na kutafutiza kwa njia isiyofaa hadi katika hali ya kuwa na maarifa kwa hakika na utoaji ushuhuda wenye mnato. Inaweza kusemekana kwamba watu katika awamu hii wamemiliki uhalisi wa ukweli wa neno la Mungu, kwamba wamepitia kwenye njia ya utimilifu kama vile Petro alivyopita. Huyu ndiye mtu wa aina ya tano, yule anayeishi katika hali ya kuwa mkomavu—awamu ya kuwa mtu mzima.
Oktoba 30, 2014
Tanbihi:
    a. Maandishi asilia yameacha “wao.”
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni