6/11/2018

Matamshi ya Mungu | Kile Ambacho Mchungaji wa Kutosha Anapaswa Kujiandaa Nacho

Mwenyezi Mungu alisema, Lazima uwe na ufahamu wa hali nyingi ambazo watu watakuwa ndani wakati Roho Mtakatifu anafanya kazi juu yao. Hasa, wale wanaofanya kazi kwa namna sawa kumtumikia Mungu lazima wawe na ufahamu bora zaidi wa hali nyingi zinazoletwa na kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekeleza kwa wanadamu. Ikiwa unasema tu kuhusu uzoefu mwingi na njia nyingi za kuingia ndani, inaonyesha kwamba uzoefu wa watu unaegemea upande mmoja sana. Bila kufahamu hali nyingi kwa kweli, huwezi kufikia mbadiliko katika tabia yako. Ikiwa umeelewa hali nyingi, basi utaweza kuelewa maonyesho mbalimbali ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuona wazi na kutambua mengi ya kazi ya pepo wabaya. Lazima ufunue mawazo mengi ya wanadamu na uende moja kwa moja kwenye kiini cha suala hili; lazima pia uonyeshe mikengeuko mingi katika utendaji wa watu au matatizo katika kumwamini Mungu ili waweze kuyatambua. Kwa kiwango cha kidogo sana, lazima usiwafanye kuhisi hasi au wasiojishughulisha. Hata hivyo, lazima uelewe shida nyingi ambazo zipo kwa watu bila upendeleo, hupaswi kuwa bila busara au "ujaribu kumfunza nguruwe kuimba"; hiyo ni tabia ya upumbavu. Ili kutatua matatizo mengi ya wanadamu, lazima uelewe elimumwendo ya kazi ya Roho Mtakatifu, lazima uelewe jinsi Roho Mtakatifu anavyotekeleza kazi kwa watu tofauti, lazima uelewe matatizo ya wanadamu, upungufu wa wanadamu, ubaini masuala muhimu ya shida, na kufikia chanzo cha tatizo, bila mkengeuko au makosa. Ni mtu wa aina hii tu ndiye aliyestahiki kuratibu kumhudumia Mungu.
Bila kujali kama unaweza kuelewa masuala muhimu na kubaini kwa dhahiri mambo mengi hutegemea uzoefu wako binafsi. Namna ambayo unapata uzoefu huathiri jinsi unavyowaongoza wengine. Ikiwa unaelewa barua na mafundisho, basi unawaongoza wengine kuelewa barua na mafundisho. Njia ambayo unapitia ukweli wa maneno ya Mungu ndiyo njia ambayo unawaongoza wengine kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa unaweza kuelewa ukweli mwingi na kubaini kwa dhahiri mambo mengi katika maneno ya Mungu, basi unaweza kuwaongoza wengine kuelewa ukweli mwingi, na wale unaowaongoza watakuwa na ufahamu wa wazi wa maono. Ukilenga kushika hisia zisizo za kawaida, basi wale unaowaongoza pia watalenga hisia zisizo za kawaida. Ikiwa unapuuza matendo na kusisitiza kuzungumza, basi wale unaowaongoza pia watazingatia kuzungumza, bila utekelezaji wowote, bila mbadiliko wowote katika tabia zao, na watakuwa tu na shauku kwa nje, bila kutenda ukweli wowote. Wanadamu wote huwatolea wengine kile walicho nacho wenyewe. Aina ya mtu huamua njia ambayo anawaongoza wengine kuingia, na aina ya mtu huamua aina ya watu anaowaongoza. Ili kuwa wa kufaa kwa matumizi ya Mungu, huhitaji tu kuwa na matarajio, lakini unahitaji pia kupata nuru kwingi kutoka kwa Mungu, mwongozo kutoka kwa maneno ya Mungu, kushughulikiwa na Mungu, na usafishaji wa maneno Yake. Ongeza kwenye msingi huu uchunguzi, mawazo, kutafakari, hitimisho, utekwaji katika fikira au uondolewaji ambao kwa kawaida ninyi huzingatia. Hizi zote ni njia za kuingia kwenu katika uhalisi na zote ni za msingi—hii ndiyo njia ambayo Mungu hufanya kazi. Ikiwa unapaswa kuingia katika njia hii ambayo Mungu hufanya kazi, basi utakuwa na fursa ya kukamilishwa na Mungu kila siku. Na wakati wowote, bila kujali kama ni mazingira magumu au mazingira mazuri, kama unajaribiwa au unashawishiwa, kama unafanya kazi au la, kama unaishi maisha kama mtu binafsi au kwa pamoja, utapata fursa za kukamilishwa na Mungu kila wakati, bila kukosa hata moja yao. Utakuwa na uwezo wa kugundua zote, na kwa njia hii utakuwa umepata siri ya kupitia maneno ya Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni