VIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Bwana Yehova alisema hivi kwa wachungaji; Ole wao wachungaji wa Israeli wajilishao! Wachungaji hawapaswi kuwalisha kondoo? Mnawala kondoo walio wanono, na kuvalia sufu zao, mnawaua wale ambao wamenona: lakini hamwalishi kondoo. Hamjawapa nguvu wagonjwa, wala hamjawaponya waliougua, wala hamjawafunga waliovunjika, wala hamjawarudisha wale waliofukuzwa, wala hamjawatafuta wale waliopotea; lakini mmewatawala kwa nguvu na ukatili” (Ezekieli 34:2-4).
“Kuweni macho dhidi ya manabii wa uongo, ambao wanawajia wakiwa wamevalia nguo za kondoo, lakini kwa ndani wao ni mbwa mwitu wakali” (Mathayo 7:15).
“Wao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimwelekeza kipofu, wote wawili wataanguka ndani ya shimo” (Mathayo 15:14).
“Kwa kuwa walaghai wengi wameingia ulimwenguni, ambao hawakubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili. Huyu ni mlaghai na anayempinga Kristo” (2 Yohana 1:7).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho. Kwa wafuasi kutambua endapo viongozi wana sifa, jambo la muhimu ni kuangalia njia wanayoiongoza na matokeo ya kazi yao, na kuangalia iwapo wafuasi wanapokea kanuni kulingana na ukweli, na kama wanapokea namna ya kutenda kunakowafaa wao ili waweze kubadilishwa. Unapaswa kutofautisha kati ya kazi tofauti za aina tofauti za watu; haupaswi kuwa mfuasi mpumbavu. Hili linaathiri suala la kuingia kwako. Kama huwezi kutofautisha ni uongozi wa mtu yupi una njia na upi hauna, utadanganywa kwa urahisi. Haya yote yana athari ya moja kwa moja katika maisha yako.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno halisi ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno halisi ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi halisi ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana, na huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga. Huduma hiyo huenda kinyume na Mungu, na hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu.
kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, na kula chakula cha bure, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao hula chakula cha bure katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila na njama dhidi ya ndugu zao, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?
kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo watakaoonekana katika siku za mwisho, na watu kuwa wanaowadanganya wanadamu. Makristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na mtu wa aina hii. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na lengo la kusimanga na kuwadhibiti na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu.
kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, wewe si mtu wa maneno matupu bila vitendo? Kutenda kwa namna hii ni kwa madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii haileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu kwa namna hii kutaleta taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ni udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli hauvumiliki.
kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati watu wa kawaida hutoa maoni kuhusu wale wenu ambao ni viongozi, nyinyi husema: “Mmh, ni nini kinakufanya kuwa na sifa zinazostahili kutoa mawazo hunihusu? Je, ni mahubiri mangapi unaweza kutoa? Je, ni watu wangapi unaweza kuwaongoza? Je, unaweza kufanya nini?” Ni kama mna sifa zinazostahili. Mkiendelea kwa njia hii mtakuwa katika shida; mnaweza kuhudumu kwa muda fulani lakini kisha mtakosea. Kuhusu nyinyi nyote, kama mngepewa makanisa katika eneo fulani na hakungekuwa na mtu wa kuwasimamia kwa miezi sita, mngeanza kupotoka. Kama hakuna mtu angekusimamia kwa mwaka mmoja, ungewapotosha. Miaka miwili ingepita na bado hakuna anayekusimamia, ungewaongoza mbali na kuwaleta mbele yako. Kwa nini hivi? Je, mmewahi kufikiri swali hili awali? Mnaweza kuwa hivi? Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa kipindi fulani cha muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema vitu vile vile, watu wengine watatambua hilo; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuhubiri kuhusu mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa imani na wa uzoefu na kuweka maneno na mafundisho hayo katika vitendo. Hatimaye unapoendelea kuhubiri na kuhubiri, wote watakuja kukutumia kama mfano. Katika kuwaongoza wengine unazungumzia mafundisho, hivyo wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako watachukua njia yoyote utakayochukua; wote watajifunza kutoka kwako na hukufuata, hivyo utahisi; “mimi ni mwenye nguvu sasa; watu wengi sana hunisikiza, na kanisa liko chini ya amri yangu.” Asili hii ya usaliti ndani ya binadamu bila kujua hukufanya umbadili Mungu kuwa mkubwa wa jina tu, na kisha wewe mwenyewe basi unaunda aina fulani ya madhehebu. Hivi ndivyo jinsi madhehebu mbalimbali hutokea. Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli? Watu wa aina hii ni wa namna sawa na Paulo.
kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Dhihirisho la majivuno ni kumwasi na kumpinga Mungu. Watu wanapokuwa na majivuno, wa kujikweza, na wa kujidai, wao huelekea kuanzisha falme zao huru na kufanya mambo jinsi wanavyotaka. Wao pia huwavuta wengine katika mikono yao wenyewe na kuwavuta katika kumbatio lao. Watu wanapoweza kufanya mambo ya aina hii, kiini cha majivuno yao ni kile cha malaika mkuu. Majivuno yao na kujikweza kwao kunapofika kiwango fulani, basi hilo huamua kwamba wao ni malaika mkuu na watamweka Mungu kando. Ikiwa una tabia ya aina hii ya majivuno, basi Mungu hatakuwa na nafasi moyoni mwako.
Tumehubiri injili tena na tena kwa viongozi wengi katika jamii za dini, lakini bila kujali jinsi tunavyoshiriki ukweli na wao, wamekataa kuukubali. Kwa nini hivi? Ni kwa sababu majivuno yao yamekuwa tabia yao mbaya na Mungu hayuko tena mioyoni mwao! Watu wengine wanaweza kusema: “Watu walio chini ya uongozi wa baadhi ya wachungaji katika ulimwengu wa dini kweli wana msukumo mwingi. Inaonekana kwamba wana Mungu kati yao!” Haijalishi jinsi mahubiri ya wachungaji hao yanavyoweza kuwa makubwa, je, wanamjua Mungu? Kama kweli wangekuwa wanamcha Mungu mioyoni mwao, wangewafanya watu wawafuate na kuwatukuza? Je, wao wangewahodhi wengine? Je, wangethubutu kuwawekea vikwazo wengine wanaotafuta ukweli na kuchunguza njia ya kweli? Kama wanaamini kuwa kondoo wa Mungu kwa kweli ni wao na kwamba kondoo Wake wote wanapaswa wawasikilize, je, wao wenyewe hawatendi kama Mungu? Mtu wa aina hiyo ni mbaya hata zaidi kuliko Mafarisayo—yeye si mpinga Kristo? Kwa hiyo, asili yake ya majivuno inaweza kumdhibiti afanye mambo ambayo yanamsaliti Mungu.
kutoka katika “Asili yenye Majivuno ya Mwanadamu Ndiyo Chanzo cha Upinzani Wake kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo vya Mungu katika mwili. Wakati huo, dhana zote za mwanadamu zinafutwa na kubaki povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. … Wale wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndiyo wanadamu kama hao watahukumiwa.
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo.
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wote wanaoanguka wanajikuza na kujitolea ushuhuda wao wenyewe, wao huenda wakijisifu na kujitwalia zaidi, na hawajamweka Mungu moyoni hata kidogo. Je, mmepitia au kushuhudia chochote Ninachosema? Watu wengi hujitolea ushuhuda bila kukoma: Nimeteseka kwa njia hii na ile, nimefanya kazi hii na ile, Mungu amenitendea kwa njia hii na ile, hatimaye Akiniuliza nifanye hiki na kile; Ananifikiria kwa heshima hasa, na sasa niko namna hii na ile. Wanazungumza kwa sauti fulani, na kuchukua msimamo fulani. Hatimaye, watu wengine huishia kufikiri kwamba wao ni Mungu. Wanapofikia hatua hiyo, Roho Mtakatifu atakuwa amewaacha muda mrefu uliopita. Ingawa, kwa sasa, wanapuuzwa, na hawatimuliwi, hatima yao imewekwa, na kile wanachoweza kufanya ni kusubiri adhabu yao tu.
kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni