12/12/2019

Kristo wa uongo ni nini? Kristo wa uongo anaweza kutambuliwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ikiwa mwanadamu atajiita Mungu lakini hawezi kuonyesha uungu na kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, au amwakilishe Mungu, bila shaka si Mungu kwani hana sifa za Mungu, na kile ambacho Mungu Anaweza kukitimiza hakimo ndani yake.
kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia. Mwili usio na dutu ya Mungu kwa kweli sio Mungu mwenye mwili; kwa hili hakuna tashwishi. Kupeleleza kama kweli ni mwili wa Mungu mwenye Mwili, mwanadamu lazima aamue haya kutoka kwa tabia Yeye huonyesha na maneno Yeye hunena. Ambayo ni kusema, kama ni mwili wa Mungu mwenye mwili au la, na kama ni njia ya kweli au la, lazima iamuliwe kutokana na dutu Yake. Hivyo, katika kudadisi[a] iwapo ni mwili wa Mungu mwenye mwili, cha msingi ni kuwa makini kuhusu dutu Yake (Kazi Yake, maneno Yake, tabia Yake, na mengine mengi), bali sio hali ya sura Yake ya nje.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliyepata mwili Anaitwa Kristo, na hivyo Kristo ambaye Anaweza kuwapa binadamu ukweli anaitwa Mungu. Hakuna kitu kikuu kuliko hiki, kwa kuwa Anayo hali ya Mungu, na ana tabia za Mungu, na hekima katika kazi Yake, ambayo haiwezi kupatikana kwa binadamu. Wale wanaojiita Kristo, walakini hawawezi kufanya kazi ya Mungu, ni matapeli. Kristo wa kweli sio tu udhihirisho wa Mungu duniani, bali pia, mwili hasa ulioigwa na Mungu kufanya na kutimiza kazi Yake kati ya wanadamu. Mwili huu si ule unaoweza kubadilishwa na mtu yeyote tu, lakini ambao unaweza kutosha kufanya kazi ya Mungu duniani, na kueleza tabia ya Mungu, na pia kumwakilisha Mungu, na kumpa binadamu maisha. Hivi karibuni au baadaye, wale Kristo bandia wataanguka wote, ingawa wanadai kuwa Kristo, hawana chochote cha hali ya Kristo. Na hivyo Mimi nasema kwamba hali halisi ya Kristo haiwezi kuelezwa na mwanadamu, bali inajibiwa na kuamuliwa na Mungu Mwenyewe.
kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili
Japokuwa Kristo Anamwakilisha Mungu Mwenyewe katika mwili na hufanya binafsi ambayo Mungu Mwenyewe Anapaswa kufanya, Yeye hakani kuwepo kwa Mungu mbinguni, wala kuyatangaza matendo Yake Mwenyewe kwa msisimko. Badala yake, Yeye kwa unyenyekevu Hubaki kwa siri ndani ya mwili Wake. Mbali na Kristo, wale ambao wanadai kwa udanganyifu kuwa Kristo hawana sifa Zake. Wakiwekwa sambamba dhidi ya tabia za kiburi na kujiinua za Kristo wa uongo, inakuwa dhahiri aina gani ya mwili ndiye Kristo wa kweli. Walivyo waongo zaidi, ndivyo Kristo wa uongo wanavyojionyesha wenyewe, na ndivyo wanavyoweza zaidi kufanya kazi za ishara na maajabu ya kuwahadaa binadamu. Kristo wa uongo hawana sifa za Mungu; Kristo hajachafuliwa na kipengele chochote cha dutu ya Kristo wa uongo.
kutoka katika “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. Mimi sipigi mayowe Nikisema, “Mimi ni Mungu, Mimi ni Mwana Mpendwa wa Mungu!” Lakini kazi Nifanyayo ni ya Mungu. Kuna haja Nipige mayowe? Hakuna haja ya kujiinua. Mungu hufanya kazi Yake Mwenyewe na hahitaji mwanadamu kumpa ruhusa ama cheo kubwa, na kazi Yake inatosha kuwakilisha utambulisho Wake na cheo. Kabla ya ubatizo Wake, si Yesu alikuwa Mungu Mwenyewe? Je, Yeye hakuwa mwili wa Mungu? Hakika haiwezi kusemekana kuwa Alikuwa Mwana wa pekee wa Mungu baada ya kushuhudiwa? Je, hakukuwa na mwanadamu jina lake Yesu kitambo kabla Aanze kazi Yake? Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu. Mungu Mwenyewe Amekuja, lakini hakuna anayemtambua, ilhali Anaendelea na kazi Yake na Anafanya hivyo kwa uwakilishi wa Roho. Haijalishi unamwita mwanadamu ama Mungu, Bwana ama Kristo, ama umwite dada, yote ni sawa. Lakini kazi Afanyayo ni ile ya Roho na Anawakilisha kazi ya Mungu Mwenyewe. Hajali ni jina gani mwanadamu anamwita. Je, jina hilo linaweza kuamua kazi Yake? Bila kujali unachomwita, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, Yeye ni kupata mwili kwa Roho wa Mungu; Anawakilisha Roho na amekubaliwa na Yeye. Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. Kazi ya Mungu haipatani na dhana za mwanadamu; kwa mfano, Agano la Kale lilitabiri juu ya ujio wa Masihi, lakini ilikuwa dhahiri kwamba Yesu Alikuja, hivyo itakuwa makosa kwa Masihi mwingine kuja tena. Yesu tayari Amekwishakuja mara moja, na yatakuwa ni makosa ikiwa Yesu Atakuja tena wakati huu. Kuna jina moja kwa kila enzi, na kila jina linaeleza sifa ya enzi. Katika dhana za mwanadamu, Mungu ni lazima siku zote Aonyeshe ishara na maajabu, ni lazima siku zote Aponye wagonjwa na kutoa mapepo, na siku zote ni lazima Awe tu kama Yesu, lakini Mungu wakati huu Hayupo kama hivyo kabisa. Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Yeyote amwigaye Kristo kunena ili kuwadanganya watu ni Kristo wa uongo. Makristo wote wa uongo wana pepo waovu, nao ni wadanganyifu. Unawezaje kutambua Kristo wa uongo ambaye kila mara huzungumza ili kuwadanganya watu? Ukitazama tu baadhi ya maneno ya Kristo wa uongo, utakuna kichwa chako na hutaweza kubaini nia za pepo huyo mwovu kweli ni zipi. Ukiendelea kufuata pepo huyu mwovu na kufikiria kwa makini kila kitu ambacho amesema, ni rahisi sana kuona ni kitu cha aina gani kwa kweli, kile anachofanya, anachosema hasa, anachokula njama kuwafanyia watu na njia ambayo anawatolea watu—basi, utambuzi huwa rahisi. Tunaweza kuona kwamba kimsingi sifa hizo bainifu zipo katika maneno mengi ya pepo waovu. Yanaweza tu kuiga maneno ya Mungu, lakini kwa hakika hayawezi kuwa na kiini cha maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yana muktadha na madhumuni. Madhumuni na matokeo ya msingi ya maneno ya Mungu yako wazi sana na unaweza kuona kwamba maneno Yake yana mamlaka na nguvu, kwamba yanaweza kugusa moyo wa mtu na kusisimua nafsi yake. Lakini maneno ya pepo waovu na ya Shetani hayana muktadha wala matokeo—ni kama dimbwi la maji yaliyotuama, na watu huhisi wenye giza ndani ya mioyo yao baada ya kuyasoma. Hawapati chochote kutoka kwayo. Kwa hivyo, pepo waovu wa kila aina hawana ukweli na hakika wana giza na utusitusi ndani yao. Maneno yao hayawezi kuwaletea watu mwanga na hayawezi kuwaonyesha njia wanayopaswa kufuata. Pepo waovu hawasemi waziwazi lengo lao wala kile wanachojaribu kufanikisha; hakuna kutajwa kwa chochote kuhusu kiini cha ukweli au asili. Hata kidogo. Hakuna kitu ambacho watu wanapaswa kuelewa au kupata ambacho kinaweza kupatikana katika maneno ya pepo waovu. Kwa hivyo, maneno ya pepo waovu yanaweza tu kuwakanganya watu na kuwaletea utusitusi na giza ya ndani. Hayawezi kuwapa watu riziki yoyote hata kidogo. Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba hali na kiini cha asili cha pepo waovu ni kile cha uovu na giza. Hawana uzima, badala yake wana rihi mbaya ya kifo. Kwa kweli ni vitu vibaya ambavyo vinapaswa kulaaniwa. Hakuna ukweli katika hotuba yao hata kidogo; ni upuuzi mtupu ambao husababisha kichefuchefu, maudhi, na kutapika kama kwamba mtu alikuwa tu amekula nzi aliyekufa.
kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Hotuba ya Kishetani na Uongo wa Roho Wabaya, Makristo wa Uongo na Wapinga Kristo” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Mtu fulani akiwachanganya watu wa Mung u wateule na kusema kwamba yeye ni Kristo, mwili wa Mungu mwenye mwili, basi tunahitaji kuangalia kiini na maonyesho yake, kazi yake na maneno yake, na tabia yake iliyofichuliwa, ili kuyakinisha kama yeye ni Kristo. Kwa kuona kiini chake kutoka kwa vipengele hivi vikuu, tunaweza kuhakikisha kama yeye ni Mungu mwenye mwili. Kwanza, kutoka kwa kipengele cha kazi, tunafaa kuona kwamba kama kazi Yake ni kazi ya Mungu, Ataweza kuonyesha neno la Mungu, kile Mungu anacho na alicho, na tabia ya Mungu ya haki. Kama ni kazi ya mwanadamu, anaweza kusema tu juu ya chote mwanadamu anacho na alicho, uzoefu na ufahamu wa mwanadamu. Hawezi kuzungumza juu ya chote ambacho Mungu anacho na alicho, kazi ya Mungu, mahitaji na tabia, sembuse mpango wa usimamizi wa Mungu na siri ya Mungu. Pili, kutoka kwa kipengele cha neno, kuna tofauti kubwa kati ya neno la Mungu na neno la binadamu. Neno la Mungu huwakilisha chote ambacho Mungu anacho na alicho, na neno la mwanadamu huwakilisha chote ambacho mwanadamu anacho na alicho. Neno la Mungu huwakilisha tabia ya Mungu. Neno la mwanadamu huwakilisha ubinadamu wa mwanadamu. Neno la Mungu ni ukweli. Neno la mwanadamu sio ukweli. Si la ukweli. Tatu, kutoka kwa kipengele cha tabia, kazi ya Mungu inaweza kuonyesha tabia ya Mungu. Kazi ya mwanadamu haiwezi kuonyesha tabia ya Mungu; inaweza tu kuonyesha nafsi ya mwanadamu. Nafsi ya mwanadamu ina nini? Je, ina haki yoyote, uadhama, ghadhabu au ukweli? Nafsi ya mwanadamu haina chochote cha kile Mungu anacho na alicho. Hivyo kazi ya mwanadamu haihusishi dokezo la tabia ya Mungu. Ni rahisi sana kukisia kutoka kwa vipengele hivi kama ni neno la Mungu au neno la mwanadamu, kazi ya Mungu au kazi ya mwanadamu. Ikiwa mwanadamu hawezi kujua tofauti kutoka kwa vipengele hivi, ni rahisi kwake kuchanganywa na Makristo wa uongo na wapinga Kristo. Kama unaweza kujua tofauti kutoka kwa vipengele hivi vitatu, utaweza kubainisha nani ni Mungu mwenye mwili na nani siye. Kazi, maneno na tabia—ni sahihi zaidi kujua tofauti kutoka kwa vipengele hivi vitatu, na sio kukisia kwa sura za nje.
kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Udanganyifu wa Kristo wa Uongo na Mpinga Kristo” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni