Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno halisi ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno halisi ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi halisi ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana, na huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga. Huduma hiyo huenda kinyume na Mungu, na hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu.
kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima. Kwa kweli, kiini cha kazi yao ni kulea talanta, kumlea mtu kuwa mhitimu mwenye talanta aliyemaliza mafunzo ya kidini ambaye baadaye anakwenda kufanya kazi na kuongoza.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya maisha ya binadamu. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hatimaye watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo watakaoonekana katika siku za mwisho, na watu kuwa wanaowadanganya wanadamu. Makristo wa uwongo na wadanganyifu waliozungumziwa watatokana na mtu wa aina hii.
kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa nini watu wengi zaidi wametumia jitihada nyingi kusoma maneno ya Mungu lakini wana na maarifa tu na hawawezi kusema kitu chochote kuhusu njia halisi baada ya hapo? Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Je, huo si mtazamo uliokanganywa? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Katika hili, je huwadanganyi watu? Je, unafanya maonyesho matupu yasiyo na maana? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kumwongoza mwanadamu katika njia nzuri, na watawapotosha tu watu. Je, hii haileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa na kuwaruhusu watu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuwaongoza watu kwa namna hii kutaleta taratibu nyingi, ambazo zitafanya watu wakuchukie. Huu ni udhaifu wa wanadamu, na kwa kweli unadhalilisha.
kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine hufanya kazi na kuhubiri na, ingawa kwa juu juu inaonekana kana kwamba wanashiriki kuhusu neno la Mungu, yote wanayozungumza kuhusu ni maana sisisi ya neno la Mungu, lakini hakuna kitu halisi kinachotajwa. Mahubiri yao ni kama mafundisho kutoka kwa kitabu cha kiada cha lugha; maneno ya Mungu yanapangwa kitu kimoja baada ya kingine, kipengele baada ya kipengele, na baada ya wao kumaliza kila mtu huwasifu, kwa kusema: “Mtu huyu ana uhalisi. Alihubiri vizuri sana na kwa maelezo ya kina sana.” Baada ya wao kumaliza kuhubiri, wanawaambia wengine wayaweke yote pamoja na kuyatuma kwa kila mtu. Matendo yao yanakuwa kuwadanganya wengine na yote wanayohubiri ni uongo. Kwa juu juu, inaonekana kana kwamba wanahubiri neno la Mungu tu na linaonekana kulingana na ukweli. Lakini kwa utambuzi ulio makini zaidi, utaona kwamba ni maandishi na mafundisho tu na fikira za uongo pamoja na mawazo na mawazo kiasi ya binadamu na vile vile sehemu fulani zinazomwekea Mungu mipaka. Je, kuhubiri kwa namna hii hakuingilii kazi ya Mungu? Ni huduma inayompinga Mungu.
kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Maarifa yenu yanaweza kuwakimu watu kwa kipindi fulani cha muda tu. Wakati unapoendelea, ukiendelea kusema vitu vile vile, watu wengine watatambua hilo; watasema wewe ni mtu wa juu juu sana, aliyekosa kina sana. Hutakuwa na budi ila kujaribu kuwadanganya watu kwa kuhubiri kuhusu mafundisho, na kama wewe daima huendelea hivi, wale walio chini yako watafuata namna yako, nyayo, na mfano wa imani na wa uzoefu na kuweka maneno na mafundisho hayo katika vitendo. Hatimaye unapoendelea kuhubiri na kuhubiri, wote watakuja kukutumia kama mfano. Katika kuwaongoza wengine unazungumzia mafundisho, hivyo wale walio chini yako watajifunza mafundisho kutoka kwako, na vitu vinapoendelea utakuwa umechukua njia ambayo si sawa. Wale walio chini yako watachukua njia yoyote utakayochukua; wote watajifunza kutoka kwako na hukufuata, hivyo utahisi; “mimi ni mwenye nguvu sasa; watu wengi sana hunisikiza, na kanisa liko chini ya amri yangu.” Asili hii ya usaliti ndani ya binadamu bila kujua hukufanya umbadili Mungu kuwa mkubwa wa jina tu, na kisha wewe mwenyewe basi unaunda aina fulani ya madhehebu. Hivi ndivyo jinsi madhehebu mbalimbali hutokea. Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?
kutoka katika “Ukimbizaji wa Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Kuhudumu kwa njia ya kidini kunamaanisha kuhudumu kabisa kulingana na njia za desturi za kidini na utendaji wa huduma, kuzingatia kwa uthabiti aina zote za kaida za kidini, na kuwaongoza watu kwa maarifa ya Biblia tu. Ni kwa nguvu na kumejaa ladha ya dini nje, kuna ulinganifu kabisa na dhana za binadamu, na watu hawana ukosoaji juu yake, lakini hakuna kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Watu ambao hutumika kwa njia hii hutoa mahubiri ambayo yote ni mafundisho ya dini na maarifa ya biblia, yaliyojaa dhana za kidini, bila nuru yoyote ya Roho Mtakatifu. Na mikutano wayafanyayo yanachusha. Katika miaka mingi ya huduma ya aina hii, wateule wa Mungu hawawezi kupokea ukweli, hawawezi kumjua au kumtii Mungu, wala kuingia katika njia sahihi ya kumwamini Mungu. Kwa sababu kile ambacho watu wanakifuatilia si wokovu, ila ni neema na baraka, kwa hivyo mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu hayawezi kuonekana, na wanaishia kuwa mikono mitupu. Haya ni matokeo ya njia ya kidini ya huduma. Ni dhahiri kwamba mtu wa aina hii anayemtumikia Mungu kwa kweli hafahamu kazi ya Mungu, wala hajui nia za Mungu. Hajui kushirikiana na kazi ya Roho Mtakatifu ni nini na hii bila shaka ni kipofu kumwongoza kipofu. Yeye huwapotosha watu wa Mungu walioteuliwa. Anamwamini Mungu lakini anampinga na hamjui Mungu. Kama Mafarisayo, hawezi kuokolewa.
kutoka katika “Ni kwa Kuingia Kwanza Kwenye Njia Sahihi ya Imani kwa Mungu Ndio Mtu Anaweza Kutembea Kwenye Njia Sahihi ya Kumtumikia Mungu” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa dini wote wamefundishwa ndani ya seminari, na wao huthibitishwa tu kuwa wachungaji. Hawana ushahidi wa kazi ya Roho Mtakatifu au idhini ya Mungu kabisa. Huu ni ukweli. Kuelewa kitu fulani kuhusu Biblia kunahitajika, lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba mtu lazima ajue kazi ya Mungu ili awe na sifa inayostahili kazi ya kulichunga kanisa. Biblia ni rekodi ya hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, hivyo bila kusoma Biblia, haiwezekani kuelewa ukweli wa kihistoria wa kuonekana kwa Mungu na kazi Yake. Pia kujua ukweli ambao Mungu alionyesha katika hatua Zake mbili zilizopita za kazi hakuwezekani, na kupata majibu ya wazi kuhusu siri nyingi za ukweli ambazo watu lazima waelewe hakuwezekani. Hii ndiyo sababu kusoma Biblia ni sharti kwa imani katika Mungu, lakini kutegemea maarifa ya Biblia pekee hakuwezi kutufanya tufikie maarifa ya Mungu. Mtu lazima apitie nuru, mwangaza, mwongozo, mafunzo, na kukamilishwa na kazi ya Roho Mtakatifu ili aweze kuelewa kabisa maneno ya Mungu na ukweli, na kufikia maarifa ya Mungu. Kufikia ufahamu wa ukweli kunategemea kupitia kazi ya Mungu na kunurishwa na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Hakupatikani tu kulingana na kutafiti na kuwa mjuzi wa maarifa ya kibiblia. Wachungaji wengi miongoni mwa watu wa dini wana ufahamu wa kina sana wa Biblia, lakini hawana ufahamu wa kazi ya Mungu kabisa. Hii hasa ni kwa sababu hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa nini watu wengine wanaposoma maneno ya Mungu, wao huishia kuwa na nuru ya Roho Mtakatifu, lakini watu wengine wanaposoma maneno ya Mungu, hawana kazi Yake yoyote? Hii inaonyesha kama imani ya watu ni ya kweli, na ikiwa wanaupenda ukweli au la. Watu wengi huhudhuria seminari ili kuwa wachungaji, na ikiwa wana lengo sahihi au la, jambo la muhimu zaidi ni kwamba lazima waupende na kuufuatilia ukweli. Hii ndiyo njia ya pekee ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa kupitia miaka kadhaa ya kazi ya Roho Mtakatifu tu ndiyo mtu anaweza kwa kweli kuelewa ukweli na kuweza kuingia katika uhalisi wa ukweli. Hii ndiyo njia ya pekee ya kuwa na sifa zinazostahili kuongoza na kuwachunga watu wa Mungu walioteuliwa. Kutegemea tu cheti ya ithibati kama mchungaji kuwaongoza watu wa Mungu walioteuliwa ni dhana kamili ya binadamu na ni tofauti sana na matakwa ya Mungu. Kwa mfano, Bwana Yesu alipokuja kwa nini hakuingia hekaluni na kuwaita makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo, lakini badala yake, Alikwenda nje miongoni mwa watu kuwatafuta wale waliopenda na kufuatilia ukweli kuwapata mitume? Mapenzi ya Mungu yanaweza kueleweka kutoka ndani ya hili. Wale ambao hawapendi ukweli hawawezi kabisa kupata ukweli, kwa hivyo hawawezi pia kuwachunga watu wa Mungu wateule. Hivi ndivyo jinsi ni watu gani ambao Mungu anawapenda kwa kweli, ambao Atawaokoa kwa kweli, ambao Yeye Atawatumia kwa kweli, na ambao Anawachukia kwa kweli itakavyokuwa wazi yote. Wachungaji wengi miongoni mwa watu wa dini hawana kazi ya Roho Mtakatifu, kitu ambacho kinaonyesha kwamba wao si wale wanaopenda au kufuatilia ukweli, na hawana njia ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hii pia ndiyo mojawapo ya sababu kuu ya ulimwengu wa dini kukosa kazi ya Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Kwa nini Ulimwengu wa Dini Umekataa Mungu Daima Huku Ukimtumikia” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha
Sasa nitatoa ushirika juu ya kanuni tano za jinsi ya kutambua kiongozi wa uongo: Kanuni ya kwanza ni kwamba viongozi wengi wa uongo hawapendi ukweli na hawafuatilii ukweli, na kwa hiyo hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Wachache wao, au baadhi ya watu, wenye ubinadamu mzuri huenda wakakosa kazi ya Roho Mtakatifu kwa sababu wamemwamini Mungu kwa muda mfupi tu, kwa sababu hawajui jinsi ya kufuatilia ukweli au hawawezi kufuatilia ukweli kwa kawaida kwa sababu wanazuiliwa na mambo fulani. Mtu yeyote ambaye amehudumu kama kiongozi kwa miaka mitatu hadi mitano na ambaye bado hana kazi ya Roho Mtakatifu bila shaka si mtu anayependa ukweli au anayefuatilia ukweli, na bila shaka ni kiongozi wa uongo. Kanuni ya pili ni kwamba viongozi wa uongo huhubiri tu maandiko na mafundisho, hawana uhalisi wa ukweli kabisa, hawawezi kabisa kutumia ukweli kutatua matatizo, na hawawezi kuwaridhisha watu moyoni na kwa neno. Kanuni ya tatu ni kwamba, kwa sababu hawana uhalisi wa ukweli, viongozi wa uongo hawawezi kufanya kazi yoyote halisi na hawawezi kuwaongoza watu wa Mungu wateule kuingia katika uhalisi wa ukweli. Wao kwa kawaida hufanya kazi yao kwa uzembe na, wakilazimishwa kufanya kitu, basi wao huwashurutisha wengine kufanya kile wasichoweza kufanya, na huwakemea na kuwashughulikia wengine bila kufikiria. Kwa sababu hawana ukweli, hawawezi kuwaridhisha wengine kwa kuwa na ukweli, na hivyo viongozi wa uongo hutumia mbinu za kupogoa na kushughulikia. Wao hulenga makosa ya wengine na kuwadhulumu siku zote, wakitaka kuwadhibiti kupitia makaripio na adhabu ili kuonyesha mamlaka yao kama viongozi—huyu ni kiongozi wa uongo. Kiongozi wa kweli hutumia ukweli kuwaridhisha watu, hutumia ukweli kutatua matatizo na husifiwa na wengine; kiongozi wa uongo huwakandamiza wengine, hulenga makosa ya wengine na huwakemea kila mara na kuwafanya wajipime usahihi kulingana na neno la Mungu, na kuwafanya wahisi kushurutishwa kufanya kile ambacho kiko nje ya uwezo wao. Mwishoni, huyo kiongozi wa uongo huwaleta chini ya udhibiti wake na kuwafanya wafikiri, “Mimi kweli sina uhalisi wa ukweli. Nimepungukiwa sana, na sifuatilii ukweli. Kile ambacho kiongozi wangu anasema ni sahihi.” Wanasadikishwa moyoni na kwa neno na kiongozi wa uongo, lakini hawajaridhika kwa kweli kwa sababu kiongozi wa uongo ana ukweli, lakini kwa sababu kiongozi wa uongo amewashughulikia na kuwatesa. Hii ni mbinu maalum inayotumiwa na viongozi wa uongo, kutumia unafiki na kuvisha uongo kama ukweli. Kwa sababu hawawezi kuwaaminisha watu kwa kuwa na ukweli, wanalazimika kutumia njia nyingine, wakifikiria, “Nitalenga matatizo yako bila taratibu maalum na kukushughulikia, kukusadikisha, na nitatumia kukushughulikia kwangu kuonyesha kwamba nina ukweli. Nitakushughulikia sana kiasi kwamba utashindwa, na nitakufanya uamini vibaya kuwa nina ukweli na kwamba huna ukweli, na utaweza kuridhika basi.” Wakati ambapo mtu hana ukweli, atadanganywa na viongozi wa uongo, na atafikiri, “Anaweza kunishughulikia kwa njia hii basi bila shaka lazima awe anaelewa ukweli kuniliko, na hakika lazima awe na uhalisi wa ukweli.” Na hivyo, anaishia kudanganywa na kudhibitiwa na kiongozi wa uongo. Kanuni ya nne ni kwamba viongozi wa uongo hawana moyo wa upendo kwa watu wa Mungu walioteuliwa na hawawezi kujijua kwa kweli, sembuse kutafuta ukweli ili kutatua matatizo au kuwaongoza watu kuingia katika uhalisi. Wao huwashughulikia tu watu na kuwadhulumu pasipo kufikiria, wao huwafanya wengine wawatii kwa kutumia njia za kuwapogoa na kuwashughulikia, na wao huonyesha hadhi yao wenyewe na kuonyesha kuwa wao ni viongozi—hii ni sura nafiki ya uwongo. Kanuni ya tano ni kwamba viongozi wote wa uongo hufuatilia hadhi na sifa, wao hutamani sana baraka za hadhi na hutamani sana majisifu. Hawatendi kazi yoyote halisi, hata hivyo wanaamini bado kuwa wana sifa ya kufurahia sadaka za Mungu, na hili linawafanya wasio na haya kabisa. Je, wanastahili kufurahia sadaka za Mungu wakati ambapo hawatendi kazi yoyote halisi? Watu wengine hutafuta familia za wenyeji wakwasi sana kukaa nao, na kila siku wao huitisha nyama ya kuku iliyookwa na samaki wa kukaangwa—wanastahili hili? Wametoa nini kwa ajili ya maisha ya watu wa Mungu walioteuliwa, na wametenda kazi gani? Wao bila shaka ni lazima wale nyama na samaki kila siku, lakini si basi wanakuwa vimelea? Je, si wale wanaotamani sana hadhi na anasa hawana haya? Je, watu kama hawa wana dhamiri na mantiki?
kutoka katika “Ili Kufikia Wokovu, Mtu Lazima Atatue Matatizo ya Kuwafuata na Kuwaabudu Watu wengine” kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha IX
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni