11/24/2019

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kutenda kama mwanadamu wa kawaida ni kuzungumza kwa kueleweka. Ndiyo inamaanisha ndiyo, na la inamaanisha la. Kuwa mwenye ukweli kwa uhakika na uzungumze inavyofaa. Usilaghai, usidanganye.
kutoka katika “Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Nawathamini sana wale wasio na shaka kuhusu wengine na pia nawapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Pangu wao ni waaminifu.
kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mnastahili kujua kwamba Mungu hupenda binadamu mwaminifu. Mungu ana kiini cha uaminifu, na kwa hivyo neno Lake siku zote linaweza kuaminika. Aidha, matendo Yake hayana dosari wala hayajadiliwi. Hii ndiyo maana Mungu anawapenda wale walio waaminifu kabisa Kwake.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa.
kutoka katika “Sura ya 33” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni wale walio waaminifu ndio Ninaowatafuta; kama wewe ni mtu mwaminifu na unayetenda kwa maadili, basi unaweza kuwa msiri wa Mungu.
kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa.
kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Inamaanisha nini kwa kweli kuwa mwanadamu mwaminifu? Kwanza, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba mwanadamu mwaminifu ana dhamiri na ana akili, kwamba katika moyo wake anamtukuza Mungu, na kwamba anaweza kulipiza upendo wa Mungu. Pili, mwanadamu mwaminifu huongea kwa njia ya kimatendo na halisi. Hapotoshi ukweli, anazungumza kwa haki, na anawatendea watu kwa haki. Huyu ni mwanadamu mwaminifu. Tatu, mwanadamu mwaminifu humcha Mungu, hutenda ukweli na kumtii Mungu. Anamcha Mungu katika moyo wake na anaweza kutenda ukweli na kumtii Mungu. Mwanadamu wa aina hii ni mtu mwaminifu. Nne, mwanadamu mwaminifu hutekeleza wajibu wake kwa uaminifu. Ni mwaminifu kwa Mungu katika kila kitu anachofanya. Tano, mwanadamu mwaminifu humpenda Mungu katika moyo wake. Anaweza kufikiria mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Sita, mwanadamu mwaminifu huishi kwa neno la Mungu. Anaweza kumwabudu Mungu kwa kweli. Mtu fulani anayeweza kumiliki sifa hizi za juu ni mwanadamu mwaminifu. Mungu anaridhika na kumfanya mtu huyu kuishi katika uwepo Wake kwa sababu huyu hasa ni aina ya mtu ambaye Anataka. Huyu hasa ni aina ya mtu ambaye Mungu anataka kumfanya kuwa kamili. Huyu hasa ni aina ya mtu ambaye Mungu anataka kuona. Mtu wa aina hii ni mtu mwaminifu.
kutoka katika “Muhtasari wa Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha V
Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu? Kwanza, watu waaminifu wanaweza kuelewana na wengine kwa amani; wanaweza kuwa marafiki wa karibu wa wengine. Hawakudanganyi, lakini wao hunena ukweli; unapojihusisha na watu wa aina hii, akili yako iko wazi, iliyofunguliwa na yenye amani. Pili, cha muhimu zaidi ni kwamba watu waaminifu ni wa kutumainiwa na kutegemewa; unaweza kuwaamini unapowaaminia kitu fulani au wanapokusaidia. Hii ndiyo sababu unahisi kupumzika, mtulivu, asiye na wasiwasi, na mwenye amani unaposhughulika na watu waaminifu; unahisi hisia ya faraja na raha. Ni wale tu ambao ni watu waaminifu ndio wanaweza kuwa marafiki wa karibu kwa wengine na kuaminiwa na wengine, kwa hiyo mtu mwaminifu pekee ndiye mfano wa kweli wa mwanadamu.
kutoka katika “Kuelewa Ukweli Tu na Kutupa Ushawishi wa Shetani Ndiko Wokovu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VII

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni