12/05/2019

Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Maneno Husika ya Mungu:
Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tu kwamba ikiwa unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu akisema ni vizuri na kukupa hongera inahesabika kama kuelewa, neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza mapenzi ya Mungu ni yapi ndani ya maneno hayo na yatafanikisha nini hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure!
kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ninyi hufikiri kwamba kupata weledi wa maarifa ya ukweli ni muhimu hasa, na kwamba kukariri mafungu ya maneno ya Mungu, kuzungumza kuhusu mafundisho na kugundua virai ndani ya maneno ya Mungu yote ni muhimu sana, lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili watu wote washirikiane, wakisema mambo sawa, na kuzungumza kuhusu mafundisho, ili wawe na maarifa sawa na kutii kanuni sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi kufanya hili kunaonekana kuwa kwa ajili ya watu kupata ufahamu, wakati kinyume chake hamjui kwamba hili linawaleta watu katikati ya kanuni ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwaruhusu watu wawe na ufahamu halisi wa ukweli, ni lazima uuunganishe na uhalisi na kazi, na kutatua shida za utendaji kulingana na ukweli wa maneno ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu wanaweza kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi, na kufanikisha matokeo kama hayo tu ndiko kuwaleta watu mbele ya Mungu kwa kweli. Ikiwa yote unayozungumzia ni nadharia za kiroho, mafundisho, na kanuni, ikiwa unaweka juhudi katika maneno sisisi tu, yote unayoweza kufanikisha ni kuwafanya watu waseme mambo sawa na kufuata kanuni, lakini hutaweza kuwaongoza watu kuelewa ukweli. Hasa hutaweza kuwafanya watu wajielewe vizuri zaidi, na kufanikisha toba na mabadiliko.
kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kama mmesoma sana neno la Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandishi na hamna maarifa ya kwanza ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu wa vitendo, hamtajua neno la Mungu. Ili mradi unahusika, neno la Mungu si maisha, lakini barua bila uhai. Na kama unaamini tu barua bila uhai, huwezi kufahamu kiini cha neno la Mungu, wala kuelewa mapenzi Yake. Wakati tu unapitia neno Lake katika uzoefu wako halisi ndio maana ya kiroho ya neno la Mungu itafunguka yenyewe kwako, na ni katika uzoefu tu ambapo unaweza kufahamu maana ya kiroho ya ukweli mwingi, na ni kwa kupitia tu uzoefu ndio unaweza kufungua mafumbo ya neno la Mungu. Usipoliweka katika vitendo, basi haijalishi jinsi neno Lake lilivyo wazi, jambo pekee ambalo umefahamu ukashikilia ni barua tupu na mafundisho, ambayo yamekuwa kanuni za dini kwako. Si hili ndilo Mafarisayo walifanya? Kama mtatenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa vitendo kwenu; msipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwenu ni kidogo zaidi ya hadithi ya mbingu ya tatu. …
… Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unatenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema ya kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema ya kwamba unalielewa. Baadhi wanasema kuwa njia pekee ya kutenda ukweli ni kuelewa ukweli kwanza, lakini hii ni nusu tu ya haki na sio sahihi kabisa. Kabla uwe na maarifa ya ukweli, bado hujapitia ukweli huo. Kuhisi ya kwamba unaelewa unachosikia sio kitu kimoja kama kweli kuelewa. Kujiandaa mwenyewe na ukweli kama inavyoonekana katika maandishi si sawa na kuelewa maana halisi humo. Kwa sababu tu una ufahamu wa ukweli wa juu juu haina maana ya kwamba kweli unaelewa ukweli au kuutambua; maana halisi ya ukweli inatokana na kuwa na uzoefu wake. Ndio maana nasema ya kwamba wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kuuelewa, na wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kufahamu sehemu ya undani wake. Kuwa na uzoefu wa ukweli kwa kina ni njia pekee ya kufahamu kidokezo cha ukweli, na kuelewa kiini chake.
kutoka katika “Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa vitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Hawa ni watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na kwa hivyo hawaielewi roho. Bila kujali unazungumzia kipengele gani cha maarifa, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikira.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Huwezi kupata ukweli kwa kuhubiri mafundisho; ukishiriki tu kuhusu mambo haya halisi, kuna manufaa gani? Lazima uelewe maana ya neno la Mungu, uelewe kiini na matokeo yanayonuiwa kufanikishwa na neno hilo. Neno la Mungu lina ukweli, maana na mwanga. Kuna vitu vingi ndani ya neno Lake; huwezi tu kueleza maana yake halisi. Nitakupa mfano. Mungu asema, “Lazima muwe watu waaminifu; msiwe wadanganyifu.” Je, maneno haya yanamaanisha nini kwa kweli? Huenda mtu akasema, “Je, si tu kuwaambia watu wawe waaminifu na sio wadanganyifu?” Mtu mwingine akiuliza, “Je, yanamaanisha nini tena?” mtu huyo ataendelea, “Ni tu kuwa mtu mwaminifu na sio mdanganyifu. Ni vitu hivyo viwili tu” “Kuwa mtu mwaminifu ni nini hasa?” Mtu mwaminifu ni mtu wa aina gani? Je, dalili za mtu mwaminifu ni zipi na dalili za mtu mdanganyifu ni zipi?” “Mtu mdanganyifu ni mtu mwenye kutoa maneno yenye maana isiyo dhahiri. Mtu asiyesema maneno yenye maana isiyo dhahiri na ambaye hunena ukweli usio zimuliwa ni mtu mwaminifu.” Bila kujali jinsi unavyouliza kiasi gani, utapata kiasi hiki tu kutoka kwake; kufikiria kwa mwanadamu kwa urahisi sana. Je, neno la Mungu linasema nini kuwahusu watu waaminifu? Kwanza, mtu mwaminifu hana tashwishi kuhusu wengine. Pili, mtu mwaminifu anaweza kuukubali ukweli. Hasa anaridhisha masharti haya mawili. Mungu anamaanisha nini kwa kusema hivi? Kwa nini Mungu anasema hili? Unapaswa kuelewa maana halisi ya mtu mwaminifu katika neno la Mungu, linazungumzia nini hasa—pata ufahamu sahihi wa huu. ufafanuzi Ni mienendo gani mingine ambayo mtu mwaminifu huonyesha ndani ya maneno ya Mungu, mtu mdanganyifu ni nini, na ni mienendo gani ambayo mtu mdanganyifu huonyesha—ukipima haya yote kwa msingi wa dalili ambazo Mungu amezungumzia, utaelewa mtu mwaminifu ni nini na mtu mwaminifu ni nini, na pia jinsi watu wadanganyifu wanavyochukulia neno la Mungu, Mungu, na watu wengine. Kwa njia hii utafikia ufahamu wa kweli wa neno la Mungu na kujua jinsi tofauti ilivyo kubwa kati ya wale watu wanaamini kuwa watu waaminifu au wadanganyifu, na kile kilichosemwa kuhusu hilo katika neno la Mungu. Unaona katika neno la Mungu, “Lazima muwe watu waaminifu; msiwe wadanganyifu.” Kuna maelezo mengi ya hili. Unapoelewa maana ya neno la Mungu kwa kweli, basi unajua mtu mwaminifu ni nini, na mtu mdanganyifu ni nini. Unapoweka hili katika vitendo utajua kile cha kufanya ambacho hakika ni mwenendo wa mtu mwaminifu, na basi utakuwa na njia ya kutenda, jambo linalohakikisha kwamba unaweza kuridhisha viwango vya Mungu. Iwapo kweli unaelewa maneno haya na kuyaweka katika vitendo, basi unaweza kupata kibali cha Mungu. Iwapo huelewi maneno haya, basi huwezi kuwa mtu mwaminifu, na kabisa hutaweza kupata kibali cha Mungu.
kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kwa nini inasemekana kwamba maneno ya Mungu ni mwongozo kwa mwanadamu? Ni kwa sababu maneno ya Mungu hayazungumzwi bure, sio nadharia ya aina fulani na sio hoja ya aina fulani. Yapo kwa ajili yako kutekeleza, kuweka katika vitendo. Unapokumbana na masuala na hujui cha kufanya, unapokosa njia ya kutenda, unafikiria mahitaji yaliyomo ndani ya maneno ya Mungu. Unatafakari juu ya maneno ya Mungu, na utajua cha kufanya na kuelewa maana ya maneno ya Mungu. Kisha, unaweza kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu. Kwa kutenda kwa njia hii, unapata thibitisho la mtazamo wako, na unagundua kuwa una amani na furaha ndani ya roho yako baada ya kutenda kwa njia hii; hili ni la kuadilisha kwa wengine pia. Wakati wa mchakato wa kutenda maneno ya Mungu, unapata nuru kiasi na vile vile uzoefu na kujifunza kiasi; unagutushwa kwa mambo fulani. Unagutushwa kwa kile ambacho Mungu anamaanisha kwa kusema maneno haya na kuwafanya watu wafanye mambo kwa namna fulani. Unapata kanuni husika za utendaji, na unapata kujua asili na umuhimu wa Mungu kutamka maneno haya—huku ni kuelewa ukweli. Mara unapoelewa ukweli, hutachanganyikiwa tena au kuona ugumu katika vitendo vyako—utakuwa na njia ya kutenda. Je, kuwa na njia ya kutenda maneno ya Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha unaelewa maneno ya Mungu na unaelewa kanuni za kutenda za maneno ya Mungu; unaelewa hali ambazo Mungu anamaanisha, na unajua jinsi unavyopaswa kutenda. Maneno ya Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi kwako, lakini kwa kweli yanakuambia jinsi unavyopaswa kuishi, kile unachopaswa kufanya unapokabiliwa na suala, na jinsi unavyopaswa kutatua shida unazokumbana nazo. Yanaweza kuwa njia yako na kukuruhusu ushughulikie masuala kwa hekima, maadili na kwa njia ya kutenda. Hayo ni ukweli. Kama una njia ya kufuata katika kutimiza wajibu wowote au katika kila jambo, kama una maadili katika kushughulikia mambo na unajua mapenzi ya Mungu ni nini, basi hili linaonyesha kwamba wewe unaelewa ukweli, na unaelewa maneno ya Mungu.
kutoka katika “Ni Wakati tu Unapoweka Moyo Wako, Akili Yako na Roho Yako Katika Kutimiza Wajibu Wako Ndipo Utakapokuwa na Mfanano wa Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Chochote ambacho hakijatoka kwa uzoefu wako mwenyewe, iwe umejifunza kutoka kwa vitabu au kutoka kwa uzoefu wa watu wengine, kinakuwa mafundisho kwako. Unapokipitia, na unafikia matokeo kutoka kwa uzoefu wako, basi utapata ufahamu wa kweli, na maneno unayoyasema unapotoa ushirika yatakuwa halisi; ni hapo tu ndipo kinakuwa uhalisi wa kweli. Angalia jinsi wasioamini wanavyotafiti nadharia fulani: Wanatafiti kutoka kwa kile kilichoandikwa tu, wanatafiti mafundisho na kuyapima na kisha kufikia mahitimisho yao. Hasa wanateolojia na wachungaji, na vile vile wasomi na watafiti wa teolojia, baada ya kusoma fungu la maneno ya Mungu, hawatafuti ukweli au kutafuta ufahamu wa kweli wa Mungu kutoka kwa uzoefu wa utendaji. Badala yake, wanachunguza na kupima nadharia mbalimbali na hatimaye kufikia mahitimisho fulani. Kwa hiyo, mahitimisho ambayo wanafikia ni halisi au ya mafundisho ya dini? Yote ni mafundisho? Hii ni kwa sababu walifikia mahitimisho haya kwa msingi wa utafiti wa maandishi maalum na majadiliano, na sio kwa msingi wa uzoefu wao wenyewe. Mahitimisho yaliyofikiwa kutoka kwa utafiti wa maandishi halisi na kutoka kwa kutafiti vitu vilivyorekodiwa katika Biblia, yameunda nadharia ya aina moja, inayoitwa nadharia ya teolojia. Hakuna ufahamu kutoka kwa uzoefu katika hili, na hakuna nuru ya Roho Mtakatifu. Ufahamu wa kina kutoka kwa nuru ya Roho Mtakatifu unazidi ule unaotoka kwa maana ya juu juu ya maneno; hauwezi kuelezwa kwa lugha yoyote ya juu juu. Roho Mtakatifu atakupa nuru na mwangaza wakati tu utakapotafuta ukweli baada ya kuingia katika uzoefu. Vitu ambavyo Roho Mtakatifu huvipa nuru na kuviangaza kwa ajili yako ni vitu ambavyo ni halisi zaidi na vitu ambavyo ni vya ukweli zaidi kwako, na hivi ndivyo vitu ambavyo huwezi kuvipata kutoka katika Biblia bila kujali jinsi unavyoichunguza kwa bidii. Kwa hiyo leo, Mungu anatutaka tupitie neno la Mungu. Kama, katika uzoefu wetu wa neno la Mungu, Roho Mtakatifu anatupa nuru, basi tunaweza kufikia ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu. Ufahamu huu wa kweli hauwezi kufikiwa bila kujali jinsi unavyochunguza maana halisi ya maneno ya Mungu kwa bidii; hili ni jambo ambalo haliwezi kufikiwa na fikira za binadamu, na kitu ambacho huwezi kukiwazia, bila kujali unavyojaribu kwa bidii jinsi gani. Kwa hiyo, ni ukweli unaopokewa kutoka kwa uongozi, nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu pekee ndio ufahamu wa kweli wa Mungu.
kutoka katika “Maswali na majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I
Tofauti kati ya maneno ya mafundisho na ukweli ni ipi hasa? Ukweli ni vitu halisi vya neno la Mungu; unawakilisha mapenzi ya Mungu. Maneno ya mafundisho ni ya kikundi cha vitu vya juu juu, na yanawakilisha mawazo na fikira za binadamu. Hayalingani na ukweli. Vitu halisi vya ukweli ni vya utendaji sana; ni vyenye maadili na vya kuridhisha hasa. Punde mtu anapoelewa kitu halisi, moyo wake unachangamka na kuachiliwa huru—hakabiliwi tena na shutuma za kanuni. Kwa upande mwingine, maneno ya mafundisho ni matupu na yasiyo ya kweli. Ni kanuni na mambo ya desturi tu, na huwafanya watu hasa wenye kuweza kuzuiwa na kutohisi huru. Aidha, bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho ambayo mtu anajua, hayawezi kuleta mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Yana faida ndogo ya msingi kwa watu. Kwa hiyo, maneno ya mafundisho hayawezi kabisa kulingana na ukweli. Ukweli unaweza kuwa uzima wa mtu. Punde mtu anapokubali ukweli utaleta mabadiliko ya tabia ya maisha. Kuelewa kiwango kikubwa cha mafundisho kunaweza tu kumletea mtu majivuno, majigambo, kiburi na kumfanya akose busara. Ni wakati tu ambapo mtu ana ukweli kama uzima wake ndiyo utendaji wake unakuwa halisi. Bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho mtu anaelewa, hatakuwa na uhalisi. Anapokabiliwa na suala bado hatajua cha kutenda. Wale wote ambao wanakamilishwa na Mungu ni watu walio na ukweli, wakati wale wote ambao hawajapitia kukamilishwa na Mungu ni watu wa maneno ya mafundisho. Wale walio na ukweli wanafaa kwa matumizi na Mungu. Kazi yao huzaa matunda, na wanaweza kweli kuwaleta wengine mbele za Mungu. Wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawapati matokeo ya kweli kutoka kwa kazi yao. Hawawezi kuwapa watu riziki ya uzoefu na ufahamu wa kweli, sembuse kutumia ukweli kutatua masuala. Hii ndiyo maana hawawezi kuwaleta wengine mbele za Mungu. Mtu ambaye ana ukweli hawahepi watu wanaotafuta ukweli, na anaweza kutatua shida zote za utendaji ambazo watu wako nazo katika imani yao. Wale ambao wanasisitiza maneno ya mafundisho wanaogopa watu kutafuta ukweli kwa sababu hawana vitu vya kweli ndani yao, na mafundisho wanayozungumzia hayawezi kutatua shida za kweli. Kwa hiyo, hawathubutu kuwaagiza wengine waulize maswali, na bila shaka hawawezi hata zaidi kutatua taabu za utendaji. Wale walio na ukweli wanathubutu kukabili uhalisi; wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawathubutu kukabili uhalisi, badala yake, wanauepuka. Hizo ndizo kanuni za kutambua kati ya ukweli na maneno ya mafundisho.
kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni