Maneno Husika ya Mungu:
Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetani haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu. Kwa sababu Nimesema awali kwamba asili ya mwanadamu haibadiliki, ngano siku zote itakuwa ngano.
kutoka katika “Sura ya 113” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Bila kujali jinsi wanavyojaribiwa, utii wa wale wenye Mungu ndani ya mioyo yao hubaki vile vile; lakini kwa wale wasiokuwa na Mungu ndani ya mioyo yao, wakati kazi ya Mungu hainufaishi miili yao, wanabadilisha mtazamo wao kwa Mungu, na hata kumkimbia Mungu. Hawa ndio wale hawatasimama imara mwishoni, wanaotafuta baraka za Mungu na hawana tamaa ya kujitolea wenyewe kwa Mungu na kujikabidhi wenyewe Kwake. Aina hii ya watu wa msingi watafukuzwa wakati kazi ya Mungu itakapofikia kikomo, na hawafai kuonewa huruma yoyote. Wale wasiokuwa na ubinadamu, hawawezi kumpenda Mungu kwa kweli. Wakati mazingira ni mema na salama, au kama watapata faida, wao ni watiifu kabisa kwa Mungu, lakini wakati walilokuwa wanataka limepatikana au hatimaye kukataliwa, wanageuka mara moja. Hata kama ni kwa muda wa usiku mmoja tu, wao watatoka katika hali ya tabasamu, watu wenye “mioyo mikunjufu” hadi wenye sura mbovu na wauaji wakatili, ghafla wakiwatendea wafadhili wao wa jana kana kwamba ni adui wa milele, bila chanzo wala sababu. Ikiwa mapepo haya hayatarushwa nje, mapepo ambayo yanaweza kuua kwa kufumba na kufumbua jicho, je, hayatakuwa chanzo cha mateso zaidi? … Wale wanaomfuata Mungu kiukweli wana uwezo wa kuhimili majaribu ya kazi yao, ilhali wale wasiomfuata hawawezi kuhimili majaribu yoyote ya Mungu. Karibuni au baadaye watatimuliwa, huku washindi wakisalia kwenye ufalme. Mwanadamu amtafute au asimtafute Mungu kwa ukweli itapimwa kulingana na kazi yake, yaani, kupitia kwa majaribu ya Mungu na hayahusiani na uamuzi wa mwanadamu mwenyewe. Mungu hamkatai mtu yeyote kwa wazo la ghafla; yote ambayo Yeye hufanya ni ili mwanadamu aweze kushawishika mwenyewe. Hafanyi lolote ambalo halionekani kwa mwanadamu ama kazi yoyote ambayo haiwezi kumthibitishia mwanadamu. Iwapo imani ya mwanadamu ni ya ukweli au sio huthibitishwa na ushahidi, na haiwezi kuamuliwa na mwanadamu. Kwamba “ngano haiwezi kufanywa magugu, na magugu hayawezi kufanywa ngano” ni jambo lililo wazi. Wale wote wanaompenda Mungu kwa dhati hatimaye watasalia katika ufalme, na Mungu hatamtesa yeyote ambaye Yeye anampenda kwa kweli.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa. Iwapo una ukweli na iwapo unampinga Mungu hayo yanaamuliwa kulingana na asili yako, si kulingana na sura yako ama hotuba na mwenendo wako wa mara kwa mara. Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakutakuwa na ajali yoyote, na hakika hakutakuwa na kosa hata kidogo. Mtu anapofanya kazi tu ndipo hisia za binadamu ama maana itachanganywa ndani. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote. Sasa kuna watu wengi wasioweza kutambua hatima ya baadaye ya binadamu na ambao pia hawaamini maneno Nisemayo; wote wasioamini, pamoja na wasiotenda ukweli, ni mapepo!
Wanaotafuta na wasiotafuta sasa ni aina mbili tofauti ya watu, na wao ni aina mbili ya watu na hatima mbili tofauti. Wanaotafuta maarifa ya ukweli na kutenda ukweli ni watu ambao Mungu ataokoa. Wale wasiojua njia ya ukweli ni mapepo na adui; ni vizazi vya malaika mkuu na wataangamizwa.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Sasa unajua kweli ni kwa nini unaniamini Mimi? Kweli unajua kusudi na umuhimu wa kazi Yangu? Kweli unajua wajibu wako? Kweli unaujua ushuhuda Wangu? Kama unaniamini Mimi tu, ilhali si utukufu Wangu wala ushuhuda Wangu vinaweza kuonekana ndani yako, basi Nimekutupa nje kitambo kirefu. Kwa wale wanaoona wanajua kila kitu, wao ni miiba zaidi katika macho Yangu, na katika nyumba Yangu, wao ni vizuizi tu Kwangu. Wao ndio magugu yanayopaswa kupepetwa kabisa na kuondolewa kwenye kazi Yangu, bila ya jitihada hata kidogo na bila ya uzito wowote; Nimevichukia kitambo kirefu. Na kwa wale bila ya ushuhuda, hasira Yangu siku zote iko juu yao, na kiboko Changu hakijawahi kutoka kwao. Kitambo kirefu Nimewakabidhi kwenye mikono ya yule mwovu, na hawana tena baraka Zangu zozote. Na siku hiyo ikifika, adhabu yao itakuwa mbaya zaidi kuliko ile ya wanawake wajinga. Sasa hivi Ninafanya kazi ile ambayo ndiyo wajibu Wangu kufanya; Nitakusanya pamoja ngano yote, pamoja na magugu. Hii ndiyo kazi Yangu sasa. Magugu haya yataweza kupepetwa na kuondolewa wakati wa kupepeta Kwangu, kisha nafaka za ngano zitakusanywa kwenye ghala, na magugu ambayo yatakuwa yamepepetwa yatawekwa motoni na kuchomwa hadi kugeuka jivu. Kazi Yangu sasa ni kuwaweka tu binadamu wote kwa pamoja, yaani, kuweza kuwashinda wote kabisa. Kisha Nitaanza upepetaji wa kufichua mwisho wa binadamu wote. Kwa hiyo unastahili kujua namna ya kunitosheleza Mimi sasa na namna unavyostahili kuwa kwenye njia iliyo sawa katika imani yako Kwangu. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho.
kutoka katika “Unajua Nini Kuhusu Imani?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Udhihirisho mkuu unaofichuliwa katika wale wanaofikia wokovu ni ufuatao: Wana uwezo wa kuitii kazi ya Mungu bila kujali mapendeleo ya kibinafsi; wanamfuata Mungu bila kujali Anakowaongoza, iwe ni kati ya majaribio ya watendaji huduma, kifo, nyakati za kuadibu, au dhiki kuu—katika haya yote hawamalizi mambo kwa kubahatisha au kupita kwa kujifanya. Katika uzoefu wao wa shida na kuvunjika moyo, hawajaiacha njia ya kweli, na hadi siku ya leo wanaendelea kutii mipango ya Mungu na kutekeleza wajibu wanaopaswa kutekeleza—huyu ni mtu mtiifu ambaye anatii na hakika ataokolewa na Mungu mwishowe. Hivi ndivyo mtu anayemtaka Mungu kwa kweli alivyo—atamfuata mpaka mwisho hata ikimlazimu kuhatarisha maisha yake. “Chochote kitokeacho, sitamwacha Mungu. Naweza kuiacha furaha ya familia yangu, naweza kumtupa mke, watoto, au mume wangu. Hiyo ni sawa alimradi naweza kujitumia kwa ajili ya Mungu.” Hii ndiyo tofauti ya wazi kati ya wale ambao wataokolewa na wale ambao wataondolewa. Katika uzoefu wao wa kazi ya Mungu, wale ambao watakaookolewa wanafuatilia ukweli na kulenga maisha, na ni wao ndio kwa kweli wapatao matokeo ya kuridhisha na kufikia mabadiliko katika tabia yao ya maisha kwa viwango tofauti. Wao wana fikira na kutotii kwa kiwango kidogo zaidi, na hatua kwa hatua wamekuja kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu. Ushirikiano wao na wengine umeongezeka kuwa wa kawaida zaidi na wao huonyesha upotovu mdogo zaidi. Wamefanya maendeleo katika ukweli, nao wanatafuta daima kufikia uwazi zaidi kuhusu ukweli. Wanathamini na wanalionea kiu neno la Mungu. Wanasoma neno la Mungu na kufanya ushirika juu ya kweli vizuri, wanasisitiza kujijua wenyewe, na wanasisitiza kubadilisha tabia yao kwa kina zaidi. Bila kujali ni wajibu gani wanaotekeleza, hawazembei kamwe katika kuingia kwao katika maisha. Inaweza kusemwa kuwa wako kwenye njia sahihi ya imani na Mungu hahitaji kuwa na wasiwasi sana kuwahusu. Wao ni watu ambao Mungu ametosheka nao kiasi. Hii ni tofauti nyingine kati ya wale ambao wataokolewa na wale ambao wataondolewa. Wale ambao wataokolewa wote hujitumia kwa ajili ya Mungu kwa uwezo wao wote na kufanya chochote wanachostahili. Wao huchukua hatua kwa shauku, sio wazembe wala wakwepaji, na hakuna kati ya kazi yao ambayo imekuwa ya uzembe ama hobelahobela. Wao huweka moyo na nguvu zao zote katika kazi yoyote iliyo mbele yao, wakiichukua kwa uzito, na katika kufanya kazi na wengine wanaweza kuzingatia manufaa kwa nyumba ya Mungu. Wao huzingatia athari ya kazi hiyo, wanafikiria kuhusu mapenzi ya Mungu, na wanajaribu kutimiza matakwa ya Mungu. Hawana nia za ubinafsi katika kutekeleza wajibu wao, hawafanyi njama kwa ajili yao wenyewe au kuhangaika kuhusu faida au hasara ya mtu binafsi, wanaweza kuweka kando raha za mwili na faida yoyote kwa familia yao wenyewe, na wako tayari kuvumilia shida ya kimwili ikiwa inahitajika. Kwao, kutimiza wajibu wao vizuri kuna kipaumbele, na vile vile kueneza injili kuokoa watu na kupanua kazi ya injili ya Mungu. Huu ni mwito wao. Kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wao kwa uaminifu ni thibitisho la dhamiri na mantiki ya mtu. Jambo la kusifiwa zaidi ni uwezo wao wa kufikiria mapenzi ya Mungu na kuwa kwao tayari kuvumilia shida ili kuufariji moyo wa Mungu. Kwa sababu watu hawa wanapenda ukweli na hutafuta maisha, wao daima huwa na Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani yao. Wana nuru na mwanga wa Roho Mtakatifu wanaposhiriki kuhusu neno la Mungu na wanaweza kukubali kweli. Kwa hiyo, nyoyo zao daima zimechangamshwa zaidi, wanatimiza wajibu wao kwa nguvu zaidi na zaidi, hali yao inazidi kuwa bora, na uhusiano wao na ndugu wengine huwa ya kawaida zaidi. Wanaweza kupendana, lakini pia wanaweza kuweka mipaka ya wazi kati yao wenyewe na wale ambao wanafichuliwa kama hawampendi Mungu na hawatekelezi wajibu wao, na wanajua jinsi ya kuwashughulikia watu hao kwa busara. Hasa, wanaona ulimwengu na wasioamini kwa uwazi kamili; wanawachukia kwa uchungu na wanachoshwa kabisa wakati wanakutana nao. Wanatamani tu kuingiliana na ndugu wengine. Machoni pao, ni ndugu zao tu ndio familia zao, na wanahisi wasingeweza kuendelea kuishi ikiwa wangejitenga na familia ya Mungu, kwamba ingekuwa bora kufa kuliko kutoishi kwa ajili Mungu. Watu hawa ni waaminifu na wenye haki moyoni, hivyo kama Mungu anachukia kitu watakiacha na kufanya kama Mungu anavyohitaji, alimradi Yeye ameridhika. Wao wanajiheshimu, na mioyoni mwao wana shauku kufaulu na wana uamuzi. Wao wako tayari kumfanyia Mungu huduma na huona kuwa mtendaji huduma mwaminifu kama utukufu wao wenyewe. Wanajitahidi kumridhisha Mungu, na hata kama ni kutenda huduma tu watatoa huduma hadi mwisho, mpaka pumzi yao ya mwisho. Wao wanaamini kuwa kufuata baraka ni jambo la kudharauliwa sana, kuwa na tamaa za kibinafsi ni jambo la chini, na kwamba wana wajibu wa kuwa sahihi na watendaji huduma waaminifu. Mungu anatukuzwa kupitia kwa watu hawa. Ingawa kuna uasi na upotovu kiasi ndani yao, wanapenda ukweli na kutafuta haki. Hawaogopi taabu, daima wanastahimili katika kutimiza wajibu wao, na hatimaye hupata baraka za Mungu. Tunaona matokeo ya kazi ya Mungu ndani yao ni dhahiri hasa—tabia zao za maisha zimebadilika kwa viwango tofauti, mitazamo yao maishani, kufikiria kwao, maisha yao, na mitazamo juu ya mambo vyote vinapitia mabadiliko makubwa, na kwa kiwango fulani wanakuwa watu wapya. Watu hawa ambao wataokolewa wamevuka bonde la kivuli cha mauti na wameona mwanga wa kwanza wa alfajiri, kama kwamba wamefufuliwa kutoka wafu. Mwisho unavyokaribia nguvu zao huzidi kua, nao huangaza uzuri wa vijana. Kumfuata Mungu, wanasimama imara katika ushuhuda wao. Hili hasa ndilo kundi la watu ambao Mungu amewapangia kupokea wokovu Wake mkuu leo.
Sasa, hebu tuangalie tabia za wale watu waovu ambao wamewekwa wazi. Wao huwaangusha watu kwa uchungu na kuwafanya wahisi uoga, na wanaudhihirisha msemo, “Ni rahisi zaidi kubadilisha milima na mito kuliko kubadilisha asili ya mtu.” Ingawa katika siku za nyuma, wamefanya kazi au kutoa huduma katika familia ya Mungu, hatimaye Mungu alipowafunua, walirudi nyuma na kuonyesha hali zao halisi. Walipenyeza kimya kimya wakitumaini kupata baraka, lakini hatimaye walikutana na hatima yao kwa kushindwa kukuu na kwa aibu. Hawapendi ukweli kabisa na hawana haja na kazi ya Mungu. Hajawahi kuchukulia kwa makini usomaji wa neno la Mungu. Ni vigumu zaidi kwao kusoma neno la Mungu kuliko wao kutumia dawa, na hata zaidi hawataki kushiriki juu ya ukweli. Hii ndiyo hulka yao kuu. Kwao, kuelewa ukweli na kutafuta ukweli hayawezekani, sembuse kujijua wenyewe. Wao si waumini; wao ni magugu yaliyopandwa na Shetani. Wao kimsingi hawana maisha ya kuzungumza kuhusu. Walipoingia kanisani, hawakuwa na nia njema. Maonyesho makuu ya watu hawa ni: Hawataki kamwe kujitolea chochote, na daima wanataka kupata faida na fadhila. Wanatumia fursa mbalimbali kufaidika. Isingekuwa kwa ajili ya kuwa na manufaa hawangeamka mapema. Wao ni watu wanaotafuta faida tu, na hawatekelezi wajibu wao kwa furaha au kwa hiari. Tabia zao ni za kishetani, na hawana moyo wa huruma au rehema kwa wengine hata kidogo. Wao ni wenye tamaa kwa kiasi cha kuchukiza na wasioridhika. Wanamshikilia mtu yeyote atakayewafaidi na kuwapa faida na wao humfanya mtu huyo awatolee huduma. Wao husema uongo daima. Chochote wanachosema kina uongo au uchafu. Hakuna wanachosema ambacho ni sahihi, kwa hivyo hujui kamwe ni maneno yapi wanayosema ni ya kweli na ni yapi ya uongo. Wanafanya kila kitu kwa siri, na hawafanyi chochote kilicho cha haki na cha heshima. Hawawezi kufungua mioyo yao kamwe na kusema kitu cha uaminifu kwa wengine, isipokuwa wanapokaribia kufa na kutoa machozi kiasi wanapoona jeneza. Kinachotoka vinywani mwao mara nyingi huwa majadiliano maovu kuhusu watu wengine, kupiga domo na ukosoaji, maneno ambayo yanaleta mgawanyiko na maneno ya lawama, pamoja na maneno ambayo huwatukana wengine. Wanachopenda zaidi ni kusifiwa na wengine na kuabudiwa nao, na wanapendezwa wakati watu wengine wanawazingatia. Wao wanatamani kwa shauku kuwa malkia au mamlaka kubwa zaidi ambaye kila mtu anamtegemea. Wanapokuwa wakifanya vizuri na kuwa na bahati nzuri, wanaweza kunyenyekea na kujifanya kuwa watu wema kwa muda mfupi. Wakati wanakabiliwa na kushindwa na wanaachwa na Mungu, hata hivyo, mara moja wao huonyesha hali zao halisi, na kupiga kelele ya matusi mara moja, kutangaza malalamiko makubwa, na kuwa pepo. Kisha wana uwezo wa kufanya chochote. Kama pigo ambalo linaloenea mbali na kwa upana, wao hueneza sumu kila mahali na kueneza uvumi ili kuwadanganya watu. Watu wote waovu kama hao ambao wanafanya kila aina ya uovu ni sawa katika asili yao, ingawa tabia zao zinaweza kutofautiana. Wote wana hali sawa ya kisaikolojia; wao hutofautiana tu katika ukali wa uovu unaoonekana. Mtu wa aina hii anaweza kupatikana kila mahali, na ni rahisi kumtambua. Inaweza kuelezwa hivi: Watu wote wanaotafuta faida ya kibinafsi badala ya kuweka vitendo vyao katika ukweli ni watu waovu; wote ambao hawafuatilii uzima na hawana hawajijui wenyewe hata kidogo wao ni watu waovu; wote ambao hawatoi mchango ingawa wana pesa na ambao hawako tayari kufanya wajibu wao ni watu waovu; wote ambao ni hobelahobela katika kufanya kazi yao, kufika kiwango ambacho wanatenda kwa ukaidi, ni watu waovu; wote wanashindania nafasi, kuvuruga maisha ya kanisa, na kutomtii yeyote ni watu waovu; wote wanaotenda kulingana na mapenzi yao wenyewe, wanaotenda kwa uasi, ambao hawamsikilizi mtu yeyote mwingine ni watu waovu; wote wanaoisikia sauti ya Mungu na hawana uoga, na ambao hata hawatubu, ni watu waovu; wale wote wenye tabia katili na kali, ambao huwatendea watu kwa ukatili, wanaowashambulia watu kila mahali kwa lugha ya matusi, wasiobadili maoni yao hata kidogo, wana hatia hata zaidi ya dhambi mbaya zaidi. Wale wote wanaorudi nyuma, ambao wanarudi katika hali zao za asili wenyewe ni kama wasioamini, na wao wote ni pepo wanaoonyesha hali zao halisi. Kazi ya Roho Mtakatifu imeshaondoka kwa watu hawa kitambo. Mungu tayari ameshawakabidhi kwa Shetani, na wao si wa familia ya Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni