Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Unabii. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Unabii. Onyesha machapisho yote

7/25/2019

“Fichua Siri Kuhusu Biblia” | Swahili Gospel Movie Clip 3/6


“Fichua Siri Kuhusu Biblia” – Je, Inamaanisha Nini katika Ufunuo Inaposema Mtu Asiongeze kwa Unabii? | Swahili Gospel Movie Clip 3/6


Ufunuo sura ya 22, mstari wa 18 "Kwa kuwa namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Iwapo mtu yeyote ataongeza kwa mambo haya, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki." Je, ungependa kujua maana halisi ya maneno haya? Video hii itakuonyesha jibu.

Soma Zaidi: Matamshi ya Mwenyezi Mungu hutoa ushuhuda wa mamlaka Yake, tabia yenye haki, kiini kitakatifu, kupelekea binadamu kumwelewa Mungu Mwenyewe wa peke na kuanza kutembea kwenye njia ya kumjua!

2/25/2018

Sura ya 44. Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
Kuutoa Ukweli Ndiyo Njia ya Kweli ya Kuwaongoza Wengine 
Mwenyezi Mungu alisema,Ikiwa mnataka kufanya kazi nzuri katika kuwaongoza wengine na kuhudumu kama mashahidi wa Mungu, la muhimu zaidi, lazima uwe na ufahamu wa kina wa kusudi la Mungu katika kuwaokoa watu na kusudi la kazi Yake. Lazima uyaelewe mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake mbalimbali ya watu. Unapaswa kuwa mwenye utendaji katika juhudi zenu; upitie tu kiasi unachoelewa na kuwasiliana tu kile unachokijua. Usijisifu, usitie chumvi, na usiseme maneno yasiyopaswa. Ukitia chumvi, watu watakuchukia na utahisi mwenye kushutumiwa baadaye;

12/20/2017

Umeme wa Mashariki | Je, Umekuwa Hai Tena?

Umeme wa Mashariki | Je, Umekuwa Hai Tena? 
Umeme wa Mashariki | Je, Umekuwa Hai Tena?
Mwenyezi Mungu alisema, Baada ya kutimiza kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, na umefanywa mkamilifu, ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe maiti—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena. Neno "wafu" linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. Roho za watu zinapowekewa uhai, wanakuwa hai tena.

12/04/2017

56 Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Makusudi ya Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu

56  Je, Unauelewa Upendo wa Mungu kwa Binadamu?

Mwenyezi Mungu alisema, Upendo wa Mungu, ambaye alikuwa mwili, unajidhihirisha wapi kwa binadamu? Baada ya kupitia uzoefu wa kazi hatua kwa hatua, mnaweza kuona kwamba Mungu anapozungumza katika kila hatua ya kazi, anatumia ruwaza fulani, anazungumza unabii fulani, na anaonyesha ukweli fulani na tabia ya Mungu, na watu wote wana mijibizo. Mijibizo yao ni nini? Hawajinyenyekeshi kwa Mungu, hususan hawachukui hatua ya kutafuta ukweli, au hawapo radhi kukubali kazi ya Mungu. Wote wana mitazamo hasi na wabishi, na wanakanganyikiwa, wanakataa na hawakubali.

9/11/2017

Umeme wa Mashariki | Utangulizi

Umeme wa Mashariki | Utangulizi
Umeme wa Mashariki | Utangulizi
"Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima" ni kundi la pili la matamshi yanayoonyeshwa na Kristo. Ndani yake, Kristo Anatumia utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Yanajumlisha kipindi cha kuanzia Februari 20, 1992 hadi Juni 1, 1992, na yana jumla ya matamshi arobaini na saba. Namna, maudhui na mtazamo wa maneno ya Mungu katika matamshi haya hayafanani kabisa na "Maneno ya Roho kwa Makanisa." "Maneno ya Roho kwa makanisa" inafichua na kuongoza tabia ya watu ya nje na maisha yao rahisi ya roho.Hatimaye, inaisha kwa "majaribu ya watendaji huduma." Hata hivyo, "Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima," inaanza na hitimisho la utambulisho wa watu kama watendaji huduma na mwanzo wa maisha yao kama watu wa Mungu.