Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mti-Wa-Uzima. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mti-Wa-Uzima. Onyesha machapisho yote

9/06/2017

Umeme wa Mashariki | Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

 Umeme wa Mashariki |1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake


Kama wale mamia ya mamilioni ya wengine wanaomfuata Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo—na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa pia wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri kwamba sisi pia tunajiamini kuwa kwenye njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni.