6/16/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wivu, Ugonjwa Sugu Wa Kiroho

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, upendo wa Mungu


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wivu, Ugonjwa Sugu Wa Kiroho



He Jiejing    Jiji la Hezhou, Mkoa wa Guangxi
Dada mmoja na mimi tuliunganishwa ili tusahihishe makala pamoja. Tulipokuwa tukikutana, nilitambua kuwa haikujalisha kama ilikuwa ni kuimba, kucheza ngoma, kupokea neno la Mungu, au kuwasiliana ukweli, huyu dada alikuwa bora kuniliko katika kila kipengele. Ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji wote walimpenda na wangezungumza naye. Kwa sababu ya hili, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi sana na nilihisi kama nilikosa kuthaminiwa—hata kufikia kiasi kwamba nilifikiri kuwa mradi alikuwa huko, hakukuwa na nafasi yangu. Moyoni mwangu nilianza kuhisi kuchoshwa naye na kutotaka kuandamana naye katika kutimiza wajibu wetu. Nilitumaini kwamba angeondoka ili kwamba ndugu wa kiume na wa kike wangenipenda na kuniheshimu sana.
Siku moja, kiongozi alituzuru. Huyu dada aliomba kuhamishiwa kwa kazi tofauti kwa sababu ya usafishwaji wa jazba aliokuwa akiupitia ambao ulikuwa ukifanya hali yake kuwa hasi. Baada ya kusikia akisema hivi, nikawa na msisimko mno. Niliwaza: Nilikuwa nikitumaini daima ya kwamba ungeenda. Ukienda, basi nitayaondokea mashaka yangu. Kwa hiyo, nilikuwa na shauku ya kiongozi huyu kumpa kazi nyingine mara moja. Hata hivyo, mambo yaliniendea kinyume na matarajio na kiongozi hakukosa tu kumpa kazi mpya, lakini kwa uvumilivu aliwasiliana naye ukweli na kumsaidia kubadilisha hali yake. Nilipoona hayo, nilihisi kuwa na wasiwasi hasa, na nikatumaini hata zaidi kuwa huyu dada angeondoka. Nikafikiri: Ni lini nitaweza kuyaondokea mashaka haya kama haendi wakati huu? Hapana, ni lazima nifikirie njia ya kumfanya aondoke haraka. Kwa hiyo, nilitumia fursa wakati huyu dada hakuwepo ili kumpa kiongozi maelezo zaidi, nikisema: "Mara nyingi yeye huwa na usafishwaji wa jazba ambao humzuia kulenga kusahihisha makala. Sasa amepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na hawezi kusahihisha makala. Tayari imeathiri kazi ya kanisa ya kuhariri na kukusanya makala. Ni heri umpe kazi mpya. Dada X ni bora kwa kuandika makala, unaweza kumchagua kusahihiisha makala hayo. Anaweza kuwa na thamani bora ya kukuza kuliko dada niliyewekwa naye." Mara tu nilipomaliza kusema hili, neno la Mungu liliingia ndani yangu likinishutumu: “Wanadamu dhalimu, wakatili! Kufumba macho na kula njama, kusukumana, kung’ang’ania sifa na mali, kuuana—haya yote yataisha lini? Mungu Amezungumza maelfu na mamia ya maneno, ilhali hakuna hata mmoja ambaye amejifahamu. … Ni wangapi wasiobagua na kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hali yao?” (“Waovu Lazima Waadhibiwe” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kukabiliana na maneno ya hukumu ya Mungu, nilihisi kama Mungu alikuwa akinikaripia kwa ukali uso kwa uso. Kwa ghafla nilianza kutetemeka kwa hofu na sikuweza kujizuia kuhisi woga kwa maneno ambayo nilikuwa tu nimeyasema. Si mimi ni kama watu wanaofichuliwa na neno la Mungu ambao “kuonea wengine wakiwa na nia ya kudumisha hali yao”? Nilipoona kwamba dada niliyekuwa nikifanya kazi naye alikuwa bora zaidi kuniliko katika kila kipengele na kwamba ndugu wa kiume na wa kike wote walimpenda, nilikuwa na wivu moyoni mwangu. Nilikuwa nimechoshwa naye, nikambagua, na kutarajia kuwa angeondoka hivi karibuni ili kwamba ningeyaondokea mashaka yangu. Ili kuwafanya ndugu wa kiume na wa kike kunisikiliza ili kwamba ningejisikia kama nilikuwa na hadhi nikiwa nao, nilitumia hali mbaya ya dada huyu kwa manufaa yangu na kumsengenya kwa kiongozi kwa kisingizio cha kulinda maslahi ya kanisa. Lilikuwa jaribio langu la bure la kutumia kiongozi kumwondoa yule dada kabisa. Mwenendo wangu ulifunua kabisa sura yangu ya kweli na kufichua kwamba nilikuwa nyoka muovu na mwenye nia mbaya, kwamba kweli nilikuwa mtoto wa joka kubwa jekundu! Ili kubuni udikteta, joka kubwa jekundu hutumia njia yoyote muhimu ili kuwaondoa wapinzani kabisa. Ili kuwa kiini cha ndugu zangu wa kiume na wa kike na kuwafanya watake kuwa karibu nami, kwa hila niliwaondoa kabisa wale ambao hawakuwa na faida kwangu. Joka kubwa jekundu lina wivu kwa wale walio wakubwa kuliliko na huwaangamiza wale wenye malengo mema. Mimi pia nilikuwa na wivu kwa dada huyu kwa sababu alikuwa bora zaidi kuniliko katika kila kipengele na nilitumia mbinu za kusikitisha kumwondoa kabisa. Joka kubwa jekundu huwahukumu na kuwaua watu kwa matilaba yake mwenyewe. Ili kupata matilaba yangu mwenyewe, kwa makusudi nilitia chumvi mambo kumhusu dada huyu. Mwenendo wangu ulikuwa sawa na ule wa joka kubwa jekundu; nilikuwa tu mwenye kiburi, mwovu, na mbaya mno. Kanisa lilikuwa limetupangia kufanya kazi pamoja ili tuweze kusaidia na kuauniana, ili tuweze kufanya kazi nzuri kwa moyo na akili moja ili kumpendeza Mungu. Ilikuwa pia ili tuweze kutumia nguvu zetu ili kufidia udhaifu wa mwingine ili tuweze kuelewa na kupata ukweli zaidi na kubadilisha tabia yetu. Lakini sikuwa na ufahamu wa mapenzi ya Mungu hata kwa kiwango kidogo. Nilipoona huyu dada alikuwa katika hali mbaya, sio tu kuwa sikutegemea upendo kumsaidia, lakini pia nilitarajia abadilishwe kwa haraka ili kuilinda nafasi yangu. Mimi kwa kweli ni mbaya sana. Tabia yangu imeharibiwa sana. Sikuwa na upendo ambao mtu wa kawaida anapaswa kuwa nao. Nilikuwa nimepoteza ubinadamu wangu kabisa kiasi kwamba ningetumia njia yoyote ili kufanikisha malengo yangu mwenyewe. Kama sitaharakisha na kutubu, ni lazima hatimaye niangamizwe pamoja na joka kubwa jekundu.
Asante Mungu! Hukumu Yako na kuadibu vimeniamsha wakati ufaao kunifanya nione kwamba mwenendo wangu ulikuwa sawa na ule wa joka kubwa jekundu na kwamba mimi kwa kweli ni mtoto wa joka kubwa jekundu kwa jina na kwa vitendo. Hili limenisababisha niidharau asili ya Shetani ambayo iko ndani yangu. Kuanzia wakati huu kwendelea, nitageuka kutoka kwa asili ya Shetani iliyo ndani yangu. Sitajipignia mwenyewe tena. Natumaini kufanya kazi vyema na dada huyu ili kutimiza wajibu wetu na kumridhisha Mungu. Nitakuwa tayari zaidi kutafuta ukweli na kutupa sumu ya joka kubwa jekundu, na hivyo kuishi kama mtu halisi ili kumfariji Mungu! kuishi kama mtu halisi ili kumfariji Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1 
Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? | Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni