II. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Wokovu wa Mungu kwa Wanadamu
2. Kujua madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
(1) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ambayo Yehova Alifanya kwa Waisraeli ilianzishwa miongoni mwa binadamu mahali pa asili pa Mungu hapa ulimwenguni, pahali patakatifu ambapo Alikuwepo. Hii kazi Aliiwekea mipaka miongoni mwa watu wa Israeli tu. Kwanza, hakufanya kazi nje ya Israeli;
badala yake, Alichagua watu Alioona kwamba walifaa ili kuwawekea mipaka upana wa kazi Yake. Israeli ndipo mahali ambapo Mungu Aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka kwenye vumbi la mahali hapo, Yehova Alimwumba mwanadamu; ndio msingi wa kazi Yake ya hapo ulimwenguni. Waisraeli, ambao ni kizazi cha Nuhu na Adamu, ndio waliokuwa msingi wa kazi ya Yehova ulimwenguni.
Umuhimu, kusudio, na hatua ya kazi ya Yehova nchini Israeli vyote vilikuwa vya kuanzisha kazi Yake katika ulimwengu mzima, na taratibu kuieneza kwenye nchi za Mataifa kutoka kwenye kitovu chake cha Israeli. Hii ndiyo kanuni ambayo Alitumia katika kufanya kazi kotekote ulimwenguni—kuanzisha mfano, kisha kuupanua mpaka watu wote ulimwenguni waweze kukubali injili Yake. Waisraeli wa kwanza walikuwa kizazi cha Nuhu. Watu hao walikuwa tu na pumzi za Yehova, na waliweza kujitunza wakatilia maanani mahitaji ya kimsingi ya maisha, lakini hawakujua Yehova Alikuwa Mungu aina gani, wala hawakujua mapenzi Yake kwa binadamu, na hata namna ambavyo walitakikana kumstahi Bwana wa viumbe vyote. Vizazi vya Adamu havikujua ni taratibu na sheria gani ambazo lazima wangetii, au ni kazi gani ambayo viumbe lazima wafanyie Muumba. Kile walichojua tu kilikuwa kwamba mume lazima atoke jasho na atie bidii ili kutosheleza familia yake, na kwamba mke lazima amtii mume wake na kuendeleza kizazi cha binadamu ambacho Yehova Aliumba. Kwa maneno mengine, watu hawa walikuwa tu na pumzi za Yehova na maisha Yake, lakini hawakujua namna ya kufuata sheria za Mungu au namna ya kutosheleza Bwana wa viumbe vyote. Walielewa kidogo sana. Kwa hivyo ingawaje hakukuweko na chochote kisichostahili au chenye ujanja katika mioyo yao, na ingawaje ilikuwa nadra sana kwao kuwa na wivu au hata ugomvi, hawakujua wala kuelewa Yehova, Bwana wa viumbe vyote. Vizazi hivi vya binadamu vilijua tu kula kile ambacho Yehova Alikuwa Ameunda, kufurahia kile ambacho Yehova Alikuwa ameunda, lakini hawakujua kustahi Yehova; hawakujua kile ambacho kilistahili kufanywa ili kumwabudu Yeye huku wakiwa wamepiga magoti. Wangeitwaje viumbe Wake? Kama hali ingekuwa hivyo, je, maneno "Yehova ni Bwana wa viumbe vyote" na "Alimwumba binadamu ili mwanadamu aweze kumdhihirisha, kumtukuza na kumwakilisha"—je, hayangekuwa yamesemwa bure bilashi? Watu wasiomstahi Yehova wangewezaje kuwa ushuhuda kwa utukufu Wake? Wangewezaje kuwa dhihirisho la utukufu Wake? Je, maneno ya Yehova "Nilimwumba binadamu kwa mfano Wangu" yakawa silaha kwenye mikono ya Shetani—yule mwovu? Je, haya Maneno hayangekuwa basi alama ya udhalilishaji kwa uumbaji wa binadamu na Yehova? Ili kukamilisha awamu hiyo ya kazi, Yehova, baada ya kumwumba mwanadamu, hakumwelekeza wala kumwongoza kuanzia kwa Adamu hadi Nuhu. Haukuwa mpaka wakati wa mafuriko ndipo Alianza rasmi kuwaongoza Waisraeli waliokuwa vizazi vya Adamu na Nuhu. Kazi na maneno Yake nchini Israeli vyote viliongoza watu wote wa Israeli walipokuwa wakiishi maisha yao kotekote nchini Israeli, na kwa njia hii kuonyesha binadamu kwamba Yehova hakuweza tu kutia pumzi ndani ya binadamu, ili apate maisha kutoka Kwake, na ainuke kutoka kwenye vumbi na kuwa mwanadamu aliyeumbwa, lakini pia aliweza kumteketeza mwanadamu kwa moto, na kumlaani mwanadamu kwa kutumia kiboko Chake ili kutawala mwanadamu. Kwa hivyo, wao pia, waliweza kuona kwamba Yehova angeweza kuyaongoza maisha ya binadamu ulimwenguni na kuongea na kufanya kazi miongoni mwao kulingana na saa za mchana na za usiku. Alifanya tu kazi hiyo ili viumbe Vyake viweze kujua kwamba binadamu alitoka kwenye vumbi na akachukuliwa na Yeye, kwamba binadamu aliumbwa na Yeye. Aidha, kazi Aliyoianza Israeli ilikuwepo ili watu wengine na mataifa mengine (ambao kwa hakika hawakuwa kando na wale wa Israeli, lakini walikuwa wamejitenga na wana wa Israeli, ilhali bado walikuwa kizazi cha Adamu na Hawa) waweze kupokea injili ya Yehova kutoka Israeli, ili viumbe vyote ulimwenguni vingemstahi na kumchukulia kuwa mkuu. Kama Yehova Asingekuwa Ameanza kazi yake Israeli, lakini badala yake baada ya kumwumba mwanadamu, na kumwacha kuishi vivyo hivyo tu hapa ulimwenguni, basi kwa sababu ya asili ya kimaumbile ya binadamu (asili inamaanisha kwamba binadamu hawezi kujua yale mambo ambayo hayaoni, yaani, hajui kwamba Yehova Alimwumba mwanadamu, na vilevile hata hajui kwa nini Alifanya hivyo), asingewahi kujua kwamba Yehova Alimwumba mwanadamu na kwamba ndiye Bwana wa mambo yote. Kama Yehova Angemwumba mwanadamu na kumweka ulimwenguni kwa raha Zake, kisha kuikung’uta tu mikono Yake na kuondoka badala ya kumwongoza miongoni mwa wenzake kwa kipindi cha muda, basi kizazi chote cha binadamu kingerudi katika hali ya kutokuwa na maana; hata mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoumbwa na Yeye, wakiwemo binadamu wote, vingerudi na kuwa katika hali isiyokuwa na maana na kutupiliwa mbali na kukanyagwa na Shetani. Na kwa hivyo, mapenzi ya Yehova kwamba "Ulimwenguni, yaani, miongoni mwa viumbe Vyake, Anafaa kuwa na mahali pa kusimama, mahali patakatifu miongoni mwa viumbe Vyake" yasingetimia. Kwa hiyo badala yake, baada ya Mungu kuumba wanadamu Aliwaongoza katika maisha yao na kuwazungumzia, wote ili waweze kutambua matamanio yake, kufikia mpango Wake. Kazi ya Mungu nchini Israeli ilinuiwa kutekeleza kazi Aliyokuwa Ameiweka wazi mbele ya viumbe Vyake vyote, na kwa hivyo Yeye kufanya kazi kwanza miongoni mwa Waisraeli na viumbe Wake kati ya vitu vyote havikuwa katika mgongano, lakini vyote hivi vilikuwa kwa minajili ya usimamizi Wake, kazi Yake na utukufu Wake, na kuzidisha maana ya kuumba Kwake wanadamu. Aliyaongoza maisha ya wanadamu ulimwenguni kwa miaka elfu mbili baada ya Nuhu ambapo Aliwafunza namna ya kustahi Yehova Bwana wa vitu vyote, Akawafunza namna ya kujiendeleza na kuisha maisha yao, na muhimu kuliko vyote, namna ya kuwa shahidi wa Yehova, kumtii Yeye na kumstahi Yeye, na kumsifu Yeye kwa muziki kama Daudi na kuhani wake walivyofanya.
Kabla ya miaka hiyo elfu mbili ambayo Yehova Alifanya kazi Yake, binadamu hakujua chochote na karibu wanadamu wote walizoroteka na kugeuka kuwa uasherati na upotovu vyote ambavyo vilitangulia mafuriko; mioyo yao haikuwa na nafasi yoyote ya Yehova, wala hata njia Yake. Hawakuwahi kuelewa kazi ambayo Yehova Alikuwa Akienda kufanya; walikosa akili, na hata maarifa, kama vile mitambo inayoishi na kupumua, kutojua binadamu, Mungu, ulimwengu, na maisha vilevile. Ulimwenguni walijihusisha na kupotoka kwingi kama alivyofanya yule nyoka, na kusema mambo mengi ambayo yalimchukiza Yehova, lakini kwa sababu hawakujua lolote, Yehova hakuwaadibu wala kuwafundisha nidhamu. Baada ya mafuriko wakati Nuhu alikuwa na umri wa miaka 601, Yehova Alijionyesha rasmi kwa Nuhu na Akamwongoza yeye na familia yake, Akamwongoza yeye, ndege, na wanyama walionusurika mafuriko na vizazi vyake mpaka mwisho wa Enzi ya Sheria, jumla ya miaka 2,500. Alikuwa rasmi kazini nchini Israeli kwa miaka 2,000, na kipindi ambacho Alikuwa kazini nchini Israeli na nje ya Israeli kilikuwa miaka 500, kwa hivyo kwa pamoja ni miaka 2,500. Kwenye kipindi hiki Aliwaagiza Waisraeli kwamba ili kuweza kumhudumia Yehova, wanafaa kujenga hekalu na kuvalia majoho ya kikuhani, kutembea bila viatu kwenye hekalu wakati wa mapambazuko, na kama wasingefanya hivyo viatu vyao vingechafua hekalu na moto ungetumwa chini kwao kutoka paa la hekalu na kuwateketeza hadi kifo. Walitekeleza wajibu wao na kutii mipango ya Yehova. Walimwomba Yehova hekaluni, na baada ya huhamasishwa na Yehova, yaani baada ya Yehova kuongea, waliwaongoza watu na kuwafunza kwamba wanafaa kumstahi Yehova—Mungu wao. Na Yehova Aliwafunza kwamba wanafaa kulijenga hekalu na madhabahu, na kwa wakati uliotengwa na Yehova, yaani, kwenye msimu wa Pasaka, wanafaa kutayarisha ndama na wanakondoo wachanga kwenye madhabahu kama dhabihu ili kuhudumia Yehova ili kuwazuia wao na kuweza kumstahi Yehova katika mioyo yao. Kama wangetii sheria hii ndicho kingekuwa kipimo cha uaminifu wao kwa Yehova. Yehova pia Aliwatengea siku ya Sabato, siku ya saba ya kuumba Kwake. Siku moja baada ya hiyo, Alifanya siku ya kwanza, siku ya wao kusifu Yehova, kumpa Yehova dhabihu na kumchezea muziki Yehova. Kwenye siku hii, Yehova Aliwaita makuhani wote kugawanya dhabihu hizo kwenye madhabahu ili watu waweze kula na kufurahia kafara zilizotolewa kwa Yehova. Naye Yehova Akasema kwamba walikuwa wamebarikiwa na walikuwa na sehemu Yake, na kwamba walikuwa ndio watu Wake waliochaguliwa (ambalo ndilo lililokuwa agano la Yehova na wana wa Israeli) Na ndiyo maana, mpaka siku hii watu wa Israeli wangali wanasema kwamba Yehova ndiye Mungu wao pekee na wala si Mungu wa watu wengine.
Kwenye Enzi ya Sheria, Yehova Aliweza kuweka wazi sheria nyingi kwa Musa kupitisha kwa wana wa Israeli waliomfuata kutoka Misri. Yehova Aliwakabidhi sheria hizi wana wa Israeli ambazo hazikuwa na uhusiano wowote na Wamisri, na zilinuiwa kuwazuia wana wa Israeli, na ndiyo yaliyokuwa mahitaji Yake kwao. Kama mtu alitii sheria ya Sabato, kama mtu aliheshimu wazazi wake, kama mtu aliabudu miungu na kadhalika, hizi ndizo zilizokuwa kanuni ambazo mtu alihukumiwa na kujulikana kama mwenye dhambi au mwenye haki. Kama mtu alichomwa na moto wa Yehova, au kupigwa na mawe hadi kufa, au kupokea baraka za Yehova, vyote hivi viliamuliwa kulingana na kama mtu alitii sheria hizi. Wale ambao hawakutilia maanani Sabato wangepigwa mawe hadi kufa. Wale makuhani ambao hawakutilia maanani Sabato wangeteketezwa na moto wa Yehova. Wale ambao hawakuheshimu wazazi wao wangepigwa mawe pia hadi kufa. Haya yote yalishauriwa na Yehova. Yehova Alianzisha sheria Zake na taratibu ili huku Akiyaongoza maisha yao, watu wangeweza kumsikiliza na kuheshimu neno Lake na wala si kuasi neno Lake. Alitumia sheria hizi kuweza kudhibiti kizazi kipya cha binadamu kilichozaliwa, kuweka msingi wa kazi Yake ambayo ingefuata. Na kwa hivyo, sababu ya kazi ambayo Yehova Alifanya, enzi ya kwanza iliitwa Enzi ya Sheria. Ingawaje Yehova Aliongea sana na Alifanya kazi nyingi, Aliwaongoza tu kwa njia nzuri huku Akiwafunza watu hawa wasiojua namna ya kuwa na wema, namna ya kuishi, namna ya kuelewa njia ya Yehova. Katika sehemu kubwa ya kazi Yake kwa hakika Alinuia kuruhusu watu Wake kufuatilia njia Yake na kufuata sheria Yake. Kazi ilifanyiwa watu ambao walikuwa wamepotoka kidogo; haikujali sana mageuzi ya tabia au ukuzi wa maisha. Alijali tu matumizi ya sheria ya kuzuia na kudhibiti watu. Kwa wana wa Israeli wakati huo, Yehova Alikuwa tu Mungu kwenye hekalu, Mungu kwenye mbingu. Alikuwa mnara wa wingu, mnara wa moto. Kile ambacho Yehova Aliwahitaji kufanya kilikuwa ni kutii kile ambacho watu wanajua leo kama sheria na mafundisho Yake—mtu angeweza hata kusema taratibu—kwa sababu kazi ya Yehova haikunuiwa kuwabadilisha, lakini kuwapatia vitu vingi ambavyo binadamu anastahili kuwa navyo, kuwaambia kutoka kwenye kinywa Chake mwenyewe, kwa sababu baada ya binadamu kuumbwa, binadamu hakujua chochote kuhusu kile alichostahili kumiliki. Na kwa hivyo Yehova Aliwapatia vitu walivyostahili kumiliki katika maisha yao hapa ulimwenguni, Akawafanya watu Aliokuwa Amewaongoza kuzidi vizazi vyao, Adamu na Hawa, kwa sababu kile Yehova Alichowapatia kilizidi kile Alichokuwa Amepatia Adamu na Hawa hapo mwanzo. Licha ya hayo yote, kazi ambayo Yehova Alifanya Israeli ilikuwa tu kuongoza binadamu na kuwafanya kutambua Mungu wao. Hakuwashinda wala kuwabadilisha, Aliwaongoza tu. Hii ndiyo jumla ya kazi ya Yehova kwenye Enzi ya Sheria. Ndiyo maelezo ya ziada, hadithi ya kweli, kiini cha kazi Yake kwenye nchi nzima ya Israeli na mwanzo wa kazi Yake ya miaka elfu sita—katika kudhibiti mwanadamu kwa mkono wa Yehova. Kutokana na haya yote kazi nyingi zaidi ilijitokeza kwenye mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita.
kutoka katika "Kazi Katika Enzi ya Sheria" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hapo mwanzo, kumwongoza mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria ya Agano la Kale ilikuwa kama kuyaongoza maisha ya mtoto. Wanadamu wa mwanzoni sana walikuwa wazaliwa wapya wa Yehova, ambao walikuwa Waisraeli. Hawakuelewa jinsi ya kumcha Mungu au kuishi duniani. Ambayo ni kusema, Yehova aliwaumba wanadamu, yaani, Yeye aliwaumba Adamu na Hawa, lakini Hakuwapa uwezo wa kuelewa jinsi ya kumcha Yehova au kufuata sheria za Yehova duniani. Bila mwongozo wa moja kwa moja wa Yehova, hakuna ambaye angeweza kulijua hili moja kwa moja, kwani mwanzoni mwanadamu hakuwa na uwezo huo wa kuelewa. Mwanadamu alijua tu kwamba Yehova alikuwa Mungu, na hakuwa na habari ya namna ya kumcha Yeye, nini cha kufanya ili kumcha Yeye, kumcha Yeye na akili gani, na nini cha kutoa katika kumcha Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kufurahia kile ambacho kingeweza kufurahiwa kati ya vitu vyote vilivyoumbwa na Yehova. Mwanadamu hakuwa na fununu ya aina gani ya maisha duniani yalifaa yale ya kiumbe cha Mungu. Bila maelekezo, bila mtu wa kuwaongoza binafsi, wanadamu kama hao hawangeweza kamwe kuishi maisha ya kufaa wanadamu, na wangeweza tu kutekwa na Shetani kwa siri. Yehova aliwaumba wanadamu, ambayo ni kusema kwamba Yeye aliumba babu za wanadamu: Hawa na Adamu. Lakini hakuwapa akili zaidi au hekima. Ingawa walikuwa tayari wanaishi duniani, hawakuelewa takriban chochote. Na kwa hiyo, kazi ya Yehova ya kuwaumba wanadamu ilikuwa imekamilishwa nusu tu. Haikuwa imekamilika hata kidogo. Alikuwa ameumba tu mfano wa mwanadamu kutoka kwa udongo na kumpa pumzi Yake, lakini Hakuwa amempa mwanadamu radhi ya kutosha kumcha Yeye. Hapo mwanzo, mwanadamu hakuwa na akili ya kumcha Yeye, au kumwogopa Yeye. Mwanadamu alijua tu jinsi ya kuyasikiliza maneno Yake lakini hakujua ujuzi wa msingi wa maisha duniani na sheria za kufaa za maisha. Na kwa hiyo, ingawa Yehova aliumba mwanamume na mwanamke na kumaliza siku saba za shughuli, Hakukamilisha uumbaji wa mwanadamu hata kidogo, kwa maana mwanadamu alikuwa ganda tu, na hakuwa na uhalisi wa kuwa mwanadamu. Mwanadamu alijua tu kwamba ni Yehova aliyeumba wanadamu, lakini mwanadamu hakuwa na fununu ya jinsi ya kutii maneno na sheria za Yehova. Na kwa hiyo, baada ya kuumbwa kwa wanadamu, kazi ya Yehova ilikuwa mbali sana kumalizika. Pia alitakiwa kuwaongoza wanadamu kabisa mbele Yake ili wanadamu waweze kuishi pamoja duniani na kumcha Yeye, na ili wanadamu waweze kwa mwongozo Wake kuingia katika njia sahihi ya maisha ya kawaida ya binadamu duniani baada ya kuongozwa na Yeye. Wakati huo tu ndio kazi ambayo ilikuwa imeendeshwa kwa kiasi kikubwa kupitia jina la Yehova ilimalizika kabisa; yaani, hapo tu ndipo kazi ya Yehova ya kuumba ulimwengu ilihitimishwa kabisa. Na kwa hiyo, kwa vile Alimuumba mwanadamu, Alipaswa kuongoza maisha ya wanadamu duniani kwa miaka elfu kadhaa, ili wanadamu waweze kutii amri na sheria Zake, na kushiriki katika shughuli zote za maisha ya kufaa ya binadamu duniani. Wakati huo tu ndio kazi ya Yehova ilikamilika kabisa. Alianza kazi hii baada ya kuumba wanadamu, na kazi Yake iliendelea mpaka wakati wa Yakobo, wakati wana kumi na wawili wa Yakobo walipokuwa makabila kumi na mbili ya Israeli. Tangu wakati huo na kuendelea, kila mtu katika Israeli akawa watu walioongozwa rasmi na Yeye duniani, na Israeli ikawa mahali maalumu duniani ambapo Alifanya kazi Yake. Yehova aliwafanya watu hawa kundi la kwanza kati ya watu ambalo kwalo Alifanya kazi Yake rasmi duniani, na kuifanya nchi nzima ya Israeli kuwa kiwango cha kuanzia kazi Yake. Aliwatumia kama mwanzo wa hata kazi kubwa zaidi, ili watu wote waliozaliwa kutoka Kwake duniani wangejua jinsi ya kumcha Yeye na kuishi duniani. Na kwa hiyo, matendo ya Waisraeli yakawa mfano wa kufuatwa na Mataifa, na kile kilichosemwa kati ya watu wa Israeli kikawa maneno ya kusikizwa na Mataifa. Kwa kuwa walikuwa wa kwanza kupokea sheria na amri za Yehova, na vivyo hivyo pia walikuwa wa kwanza kujua jinsi ya kuzicha njia za Yehova. Wao walikuwa mababu wa binadamu ambao walijua njia za Yehova, na walikuwa wawakilishi wa wanadamu waliochaguliwa na Yehova.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hivyo, umezisoma taratibu na kanuni hizi za Enzi ya Sheria, kweli? Je, taratibu hizi zinajumuisha mseto mpana? Kwanza, zinajumuisha Amri Kumi, na baadaye kuna taratibu za namna ya kujenga madhabahu, na kadhalika. Hizi zinafuatwa na taratibu za kuitimiza Sabato na kuzidumisha zile karamu tatu, na baadaye kuna taratibu za kutoa sadaka. Je, unaona ni aina ngapi za sadaka ambazo zimo? Kunazo sadaka zilizoteketezwa, sadaka za unga, sadaka za amani, sadaka za dhambi, na kadhalika, ambazo zinafuatwa na taratibu za sadaka za kuhani, zikiwemo sadaka zilizoteketezwa na sadaka za unga zilizotolewa na Kuhani, na aina nyingine za sadaka. Taratibu za nane ni za ulaji wa sadaka na Kuhani, na kisha kunazo taratibu zinazofaa kudumishwa wakati wa maisha ya watu. Kunayo masharti ya vipengele vingi vya maisha ya watu, kama vile taratibu zinazotawala kile wanachoweza au wasichoweza kula, kwa utakasaji wa wanawake baada ya wao kujifungua, na kwa wale ambao wameponywa ugonjwa wa ukoma. Katika taratibu hizi, Mungu Anafikia hadi kiwango cha kuzungumzia kuhusu ugonjwa, na kunazo hata sheria za kuchinja kondoo na ng’ombe, na kadhalika. Kondoo na ng'ombe waliumbwa na Mungu, na unafaa kuwachinja hata hivyo Mungu anakuambia kufanya hivyo; kunayo, bila shaka, sababu ya maneno ya Mungu, na ni sahihi bila shaka kutenda kama inavyokaririwa na Mungu, na kwa hakika itakuwa ya manufaa kwa watu! Kunazo pia karamu na sheria za kufuatwa, kama vile siku ya Sabato, Pasaka, na zaidi—Mungu aliweza kuzungumzia yote haya. Hebu tuangalie zile za mwisho: taratibu nyingine—kuteketezwa kwa taa, mwaka wa Jubilii, ukombozi wa ardhi, ulaji wa viapo, utoaji wa zaka, na kadhalika. Je, hizi zinajumuisha mseto mpana? Kitu cha kwanza cha kuzungumziwa ni suala la sadaka la watu, kisha kunazo taratibu za wizi na fidia, na udumishaji wa siku ya Sabato...; kila mojawapo ya maelezo ya maisha yanahusishwa. Hivi ni kusema, wakati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilifaa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kuunda madhabahu, namna ya kuyaunda madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kuamuru namna ambavyo binadamu alifaa kuishi—kile alichofaa kutilia maanani katika maisha, kile alichofaa kutii, kile anachofaa na hafai kufanya. Kile Mungu alichoweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinakubalika chote, na pamoja na tamaduni, taratibu, na kanuni hizi Aliwastanisha tabia ya watu, kuongoza maisha yao, kuongoza uanzishaji wao wa sheria za Mungu, kuwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, kuwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa mambo mengine yote ambayo Mungu alikuwa amemuumbia binadamu na yaliyomilikiwa na mpangilio na marudio ya mara kwa mara na ya kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi kuweka vipimo kwa binadamu, ili hapa duniani binadamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Taratibu na sheria zinajumuisha maudhui mapana mno, yote ni maelezo ya mwongozo wa Mungu wa mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria, lazima yangekubaliwa na kuheshimiwa na watu waliokuwa wamekuja kabla ya Enzi ya Sheria, ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria, na ni ithibati ya kweli ya uongozi na mwongozo wa Mungu kwa wanadamu wote.
kutoka katika "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanadamu wa mapema zaidi hawakujua chochote, na hivyo Mungu alilazimika kuanza kumfunza binadamu kutoka kwenye kanuni za juujuu na za kimsingi zaidi kwa minajili ya uwepo na taratibu zinazohitajika za kuishi, kutia moyoni mambo haya yote kwenye moyo wa binadamu kidogo kidogo, na kumpa binadamu uelewa wa Mungu kwa utaratibu, kutambua na kuelewa uongozi wa Mungu kwa utaratibu, na dhana ya kimsingi ya uhusiano kati ya binadamu na Mungu, kupitia kwa taratibu hizi na kupitia kwa sheria hizi, ambazo zilikuwa za maneno. Baada ya kutimiza athari hii, ndipo tu Mungu aliweza, kidogo kidogo, kufanya kazi ambayo Angeweza kufanya baadaye, na hivyo taratibu hizi na kazi iliyofanywa na Mungu kwenye Enzi ya Sheria zikawa ndiyo msingi wa kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu na hatua ya kwanza ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu.
kutoka katika "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Yehova ilikuwa imwongoze mwanadamu moja kwa moja na kumchunga kwa kuweka wazi sheria ili kwamba mwanadamu aweze kuishi maisha ya kawaida na kumwabudu Yehova kwa njia ya kawaida duniani. Katika Enzi ya Sheria Mungu alikuwa Asiyeonekana wala kuguswa na mwanadamu. Alikuwa tu Anawaongoza wanadamu waliokuwa mwanzo wamepotoshwa na Shetani, na Alikuwepo kuwaagiza na kuwaongoza wanadamu, kwa hivyo maneno yote Aliyoyanena yalikuwa ya kisheria, amri na uelewa wa kawaida wa kuishi maisha kama mwanadamu, na wala sio kuhusu ukweli unaomruzuku mwanadamu. Waisraeli chini ya uongozi Wake hawakuwa wale waliopotoshwa zaidi na Shetani. Kazi yake ya kisheria ilikuwa tu hatua ya kwanza kabisa katika kazi ya ukombozi, mwanzo hasa wa kazi ya wokovu, na haikuwa inahusiana kamwe na mabadiliko katika tabia za kimaisha za mwanadamu.
kutoka katika "Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati wa Enzi ya Sheria, kazi ya kumwelekeza mwanadamu ilifanyika katika Jina la Yehova, na awamu ya kwanza ya kazi ilifanyika duniani. Kazi ya awamu hii ilikuwa ni kujenga hekalu na madhabahu, na kutumia sheria kuwaongoza watu wa Israeli na kufanya kazi miongoni mwao. Kwa kuongoza watu wa Israeli, Alizindua kituo cha kazi Yake hapa duniani. Kwa msingi huu, Yeye Alipanua kazi yake nje ya Israeli, ambayo ni kusema kwamba, kuanzia Israeli, Aliendeleza kazi yake nje, ili vizazi vya baadaye walikuja kujua polepole kwamba Yehova Alikuwa Mungu, na kuwa Yehova Alikuwa Ameumba mbingu na nchi na vitu vyote, Alitengeneza viumbe vyote. Yeye Alieneza kazi yake kupitia kwa watu wa Israeli. Nchi ya Israeli ilikuwa ya mahali takatifu pa kwanza pa kazi ya Yehova hapa duniani, na kazi ya Mungu ya hapo mwanzoni ilikuwa kote katika nchi ya Israeli. Hiyo ilikuwa kazi ya Enzi ya Sheria.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
(2) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema
Aya za Biblia za Kurejelea:
"Kwa kuwa Mungu hakumtuma Mwana wake duniani ili kuishutumu dunia; ila ili dunia iweze kuokolewa kupitia yeye" (Yohana 3:17).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alikuwa mwili na kusulubiwa, na Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa "Kamanda Mkuu", "Sadaka ya Dhambi," "Mkombozi." Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui kutokana na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akajenga msingi imara wa nyumbani, mahali pa kuzaliwa pa kazi Yake hapa duniani, na Alitoa amri; haya yalikuwa mafanikio Yake mawili, yanayowakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu haikuwa kutoa amri, bali kutimiza amri, na hivyo kutangaza Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, kuikaribisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake Yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake. Kisha Akaondoka. Katika hatua hiyo, Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na mwanadamu aliingia katika Enzi ya Neema.
Kazi ya Yesu ilifanyika kulingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, uvumilivu, huruma na fadhili. Alibariki binadamu maradufu na kuwaletea neema kwa wingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu wa Yesu na upendo, huruma Yake na fadhili. Katika siku hizo, alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, Roho yake ilifarijika, na alikuwa anaendelezwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji wingi wa neema, ustahimili usio na mwisho na uvumilivu, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya dhambi ya binadamu, Yesu. Na walijua kwamba ni Mungu tu ndiye Anaweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na waliona tu huruma wa Yesu na fadhili Zake. Hii ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Hivyo kabla ya kukombolewa, walilazimika kufurahia neema nyingi ambayo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia kwa ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu ndio walikuwa na uwezo wa kupokea msamaha na kufurahia wingi wa neema kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alisema, "Nimekuja si kuwakomboa watu watakatifu, ila wenye dhambi, ili dhambi zao zisamehewe." Kama Yesu angekuwa mwili na tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi; na hivyo mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeendelea zaidi ya Enzi ya Sheria. Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita, dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi katika idadi na ziwe mbaya zaidi, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya Sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyompenda mwanadamu zaidi, kusamehe dhambi zao na kuwapa huruma ya kutosha na fadhili, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, na kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa thamani kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anachunga watoto wachanga walio katika mikono yake. Yeye hakuwa na hasira kwao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na hasira miongoni mwao, lakini alistahimili makosa yao na akageuza jicho la kipofu kwa upumbavu wao na kutofahamu, hata Alisema, "Uwasamehe wengine mara sabini mara saba." Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine, na kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha kupitia uvumilivu Wake.
kutoka katika "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Licha ya Yesu, kwa kuwa Mungu mwenye mwili, na kuwa bila hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaendeleza. Bila kujali kiwango cha kazi Aliyofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema Alijulikana kwa upendo kama "Mpendwa Mwokozi Yesu." Kwa watu wa wakati huo—na kwa watu wote. Kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, ilikuwa huruma na fadhili. Yeye kamwe hakukumbuka makosa ya watu au kuruhusu makosa yao kuathiri jinsi Yeye Alivyowachukulia. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula wasiweze tena. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifanya mpaka kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya kati yao na Alifanya kazi Yake ya ukombozi. Hata kabla Asulubiwe msalabani, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu. Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kumkomboa mwanadamu kabla hajasulubiwa. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka yeye mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Aliweka huruma Yake yote, fadhili Zake, na utakatifu juu ya mwanadamu. Aliendelea kuvumilia wanadamu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini kuwasamehe hao dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo wake kwa ndugu na dada uilizidi upendo wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwachukua wote waliomfuata kwa wema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete wakatembea, vipofu wakaona, viziwi wakasikia; Yeye Aliwaalika mpaka watu wasiofaa machoni pa wanadamu na maskini zaidi, wenye dhambi, wakala pamoja Naye, Hakuepukana nao ila daima Alikuwa na subira, hata Akasema, "Wakati mchungaji anapoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye huondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye hufurahia kwa shangwe." Yeye Aliwapenda wafuasi wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Alikuwa na fadhila kwao, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo aliyetolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akawaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijiwasilisha kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mpendwa Mwokozi Yesu, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko vya mnara, Hakuwaonyesha huruma na wema, bali Yeye Aliwachukia na kuchukizwa nao. Hakufanya kazi sana miongoni mwa Mafarisayo, mara chache tu Aliwahubiria na kuwakemea; Yeye hakuwakomboa, au kufanya ishara na miujiza kati yao. Alihifadhi huruma Yake na upendo kwa wafuasi Wake, kuvumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho wakati Alipigwa misumari msalabani, kustahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndio ilikuwa jumla ya kazi Yake.
Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, Shetani angechukua makazi duniani, na dunia nzima ingekuwa makao yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji huruma na fadhili kwa wanadamu; kupitia kwa kazi hiyo tu ndio mwanadamu angeweza kupokea msamaha na mwishowe afuzu kufanywa kuwa mkamilifu na kupatwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alifanya kazi Yake hapa duniani ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa na mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaanzisha hatima ya mwanadamu. Baada ya Yesu kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo mwanadamu alikombolewa. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Alidhihakiwa, Akatukanwa, na Akaachwa pweke, Aliachwa hata bila mahali pa kulaza kichwa chake, Hakuwa hata na mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, nafsi Yake yote—mwili safi na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na kupitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na askari hata wakamtemea mate usoni; ila Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea na kujitoa bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ya Yesu inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria na si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo binadamu amepitia—Enzi ya Ukombozi.
kutoka katika "Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Neema, Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote walioanguka (sio Waisraeli pekee). Alionyesha rehema na wema kwa mwanadamu. Yesu ambaye mwanadamu alimwona katika Enzi ya Neema Alikuwa amejazwa na wema na siku zote Alikuwa mwenye upendo, maana Alikuja kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao hadi pale ambapo msalaba Wake ungeweza kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini. Wakati huo, Mungu alionekana kwa mwanadamu katika rehema na wema; yaani, Alijitoa sadaka kwa ajili ya mwanadamu na Alisulubiwa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu ili kwamba waweze kusamehewa milele. Alikuwa mwenye rehema, mwenye huruma, mwenye upendo na mstahimilivu. Na wale wote waliomfuata Yesu katika Enzi ya Neema nao pia walionekana kuwa wastahimilivu na wenye upendo katika mambo yote. Walistahimili mateso yote, na hawakuweza kulipiza kisasi hata walipopigwa, kulaaniwa au kupigwa mawe.
kutoka katika "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Yesu Alipokuja, Alifanya pia baadhi ya sehemu ya kazi ya Mungu, na kuongea baadhi ya maneno—lakini ni kazi gani kuu Aliyokamilisha? Alichokamilisha hasa ni kazi ya kusulubishwa. Akawa mfano wa mwili wenye dhambi ili kukamilisha kazi ya kusulubiwa na kuwakomboa wanadamu wote, na ilikuwa kwa ajili ya dhambi zote za binadamu, ndio Alitumika kama sadaka ya dhambi. Hii ndiyo kazi hasa Aliyokamilisha. Hatimaye, Alileta njia ya msalaba ili kuwaongoza wale waliokuja baadaye. Yesu Alipokuja, ilikuwa kimsingi kukamilisha kazi ya ukombozi. Aliwakomboa binadamu wote, na kuleta injili ya ufalme wa mbinguni kwa mwanadamu, na zaidi, kuleta ufalme wa mbinguni. Kwa sababu hii, waliokuja baada ya yote walisema, "Tunapaswa tutembee njia ya msalaba, na tujitoe kama kafara kwa ajili ya msalaba." Bila shaka, hapo mwanzo Yesu pia Alifanya kazi nyingine na kuongea baadhi ya maneno ili kumfanya mwanadamu atubu na kukiri dhambi zake. Lakini huduma Yake ilikuwa bado ni kusulubiwa, na miaka mitatu na nusu Aliyotumia kuhubiri njia ilikuwa katika matayarisho ya kusulubiwa kulikokuja baadaye. Mara kadhaa ambazo Yesu Alisali zilikuwa pia ni kwa ajili ya kusulubishwa. Maisha ya mwanadamu wa kawaida Aliyoishi na miaka thelathini na tatu na nusu aliyoishi duniani yalikuwa kimsingi kwa ajili ya kukamilisha kazi ya kusulubishwa, yalikuwa ya kumpa nguvu, na kumfanya aweze kutekeleza kazi hii, na kwa sababu hii Mungu Alimwaminia kazi ya kusulubiwa.
kutoka katika "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya Enzi ya Neema, Yesu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu. Alichokuwa nacho na Aliyekuwa ni neema, upendo, huruma, uvumilivu, subira, unyenyekevu, huduma, na stahamala, na nyingi ya kazi ambayo Alifanya ilikuwa kumwokoa mwanadamu. Na kuhusu tabia Yake, ilikuwa tabia ya huruma na upendo, na kwa sababu Yeye Alikuwa na huruma na upendo, ilikuwa sharti asulubishwe msalabani kwa ajili ya mwanadamu, ili kuonyesha kwamba Mungu Alimpenda mwanadamu jinsi anavyojipenda, kwa kiasi kwamba Yeye mwenyewe Alijitoa kama kafara na kwa ukamilifu Wake. Shetani akasema, "Kwa kuwa Unampenda mwanadamu, Lazima Umpende kwakwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Upigiliwe misumari msalabani, kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, kutoka kwa dhambi, na Wewe utajitolea Mwenyewe badala ya wanadamu wote." Shetani akatoa dau ifuatayo: "Kwa kuwa Wewe ni Mungu Mwenye upendo na Mwenye huruma, lazima Umpende mwanadamu kwa kiwango cha juu zaidi: Lazima Ujitoe Mwenyewe msalabani." Yesu akasema, "Maadamu ni kwa ajili ya wanadamu, basi Niko tayari kutoa Yangu yote." Baadaye, Alikwenda msalabani bila kujifikiria hata kidogo, na kuwakomboa wanadamu wote. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu, ambalo lina maana kuwa Mungu Alikuwa Mungu ambaye Alimwokoa mwanadamu, na ya kwamba Alikuwa Mungu wa rehema na wa upendo. Mungu Alikuwa na mwanadamu. Upendo wake, huruma yake, na wokovu wake uliandamana na kila mtu. Mwanadamu angeweza tu kupata amani na furaha, kupokea baraka zake, kupokea neema yake kubwa na nyingi, na kupokea wokovu wake iwapo mwanadamu angekubali jina lake na akubali uwepo wake. Kupitia kusulubiwa kwa Yesu, wale wote ambao walimfuata Yeye walipokea wokovu na walisamehewa dhambi zao. Wakati wa Enzi ya Neema, jina la Mungu lilikuwa ni Yesu. Kwa maneno mengine, kazi ya Enzi ya Neema ilifanywa hasa katika Jina la Yesu. Wakati wa Enzi ya Neema, Mungu Aliitwa Yesu. Yeye Alifanya kazi mpya zaidi ya Agano la Kale, na kazi yake ilimalizika kwa kusulubiwa, na ya kwamba huo ulikuwa ukamilifu wa kazi yake.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Matamshi na kazi ya Yesu wakati huo hayakushikilia mafundisho, na hakufanya kazi Yake kulingana na kazi ya sheria ya Agano la Kale. Yalilingana na kazi iliyopaswa kufanywa kwa Enzi ya Neema. Alitenda kulingana na kazi Aliyokuwa ameleta mbele, kulingana na mipango Yake, na kulingana na huduma Yake; Hakufanya kazi kulingana na sheria ya Agano la Kale. Hakuna Alichofanya kilicholingana na Agano la Kale, na Hakuja kufanya kazi ili kutimiza maneno ya manabii. Kila hatua ya kazi ya Mungu haikuwa wazi ili kutimiza utabiri wa manabii wa zamani, na Hakuja kuyafuata mafundisho au kutambua makusudi utabiri wa manabii wa kale. Bado vitendo Vyake havikuvuruga utabiri wa manabii wa kale, wala havikuvuruga kazi Aliyokuwa amefanya awali. Hatua muhimu ya kazi Yake haikuwa kufuata mafundisho yoyote, na kufanya kazi ambayo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya. Yeye hakuwa nabii wala mwaguzi, ila mtendaji, aliyekuja kufanya hiyo kazi Aliyopaswa kufanya, na aliyekuja kufungua enzi Yake mpya na kufanya kazi Yake mpya.
kutoka katika "Kuhusu Majina na Utambulisho" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kungekuwepo tu na enzi mpya wakati Yesu Alikuja kufanya kazi mpya, Alipozindua enzi mpya, na kupenya katika kazi iliyokuwa imefanyika hapo awali katika nchi ya Israeli, na hakufanya kazi yake kwa mujibu wa kazi iliyofanywa na Yehova huko Israeli, hakuzingatia sheria Yake ya zamani, na hakufuata kanuni zozote, na Alifanya kazi mpya ambayo Alitakiwa kufanya. Mungu mwenyewe huja kuanzisha enzi, na Mungu mwenyewe huja kuleta enzi kwenye kikomo. Mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha enzi na kuhitimisha enzi. Kama Yesu hakuleta kazi ya Yehova kwenye kikomo, basi hio inadhihirisha ya kwamba Yeye Alikuwa tu mwanadamu, na hakuwakilisha Mungu. Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akafuata kazi ya Yehova kwa kuanza kazi yake mwenyewe, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu Alikuwa Mungu mwenyewe.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndio maana Mungu Anasema, "Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu." Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani …
kutoka katika "Kazi na Kuingia (6)" katika Neno Laonekana katika Mwili
(3) Lengo na umuhimu wa kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani ilimlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi, lakini pia ilimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uhai.
kutoka katika "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.
kutoka katika "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Huafikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
kutoka katika "Dibaji" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kufaidi ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka katika "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuutupa nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa.
kutoka katika "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu makosa, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.
kutoka katika "Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, "Neno kuonekana katika mwili"; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. "Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili." Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili.
kutoka katika "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani chake. Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa. Kupitia neno, binadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Binadamu ameliona neno, amelisikia neno, na akapata habari ya uwepo wa neno. Kutokana na haya, binadamu anaamini katika uwepo wa Mungu; binadamu anaamini katika uwezo na hekima za Mungu, pamoja na moyo wa upendo wa Mungu kwa binadamu na tamanio Lake la kumwokoa binadamu. Ingawa neno "neno" ni rahisi na kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu kuwa mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Baadaye, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, akichungwa na kujazwa na neno; wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata zaidi kuishi chini ya na hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kutimiza mapenzi ya Mungu, kubadilisha sura asilia wa ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia neno kufanya kazi Yake na kutimiza matokeo ya kazi Yake; Hafanyi maajabu au kutenda miujiza; Anafanya tu kazi Yake kupitia kwa neno.
kutoka katika "Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo Mungu Amekuwa mwili kimsingi ili kukamilisha kazi ya "Neno kuonekana katika mwili," kutumia neno kumfanya mwanadamu kamili, na kumfanya mwanadamu kukubali ushughulikiaji wa neno na usafishaji wa neno. Katika maneno Yake, anakufanya kupata kupewa na kupata uzima; katika maneno Yake, unaona kazi Yake na matendo. Mungu Anatumia neno kukuadibu na kukutakasa, na hivyo ukipata ugumu wa maisha, ni pia kwa sababu ya neno la Mungu. Leo, Mungu hafanyi kazi kwa kutumia mambo ya hakika, ila ni kwa maneno. Baada tu ya neno Lake kuja juu yako ndipo Roho Mtakatifu Atafanya kazi ndani yako na kukufanya upate uchungu ama uhisi utamu. Ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukuleta katika hali halisi, na ni neno la Mungu pekee ndilo linaloweza kukufanya mkamilifu. Kwa hivyo, angalau lazima uelewe kuwa kazi inayofanywa na Mungu katika siku za mwisho kimsingi ni kutumia neno Lake kumfanya kila mwanadamu kamili na kumwongoza mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ni kupitia kwa neno; Hatumii ukweli kuadibu. … Kwa hivyo, katika siku za mwisho, Mungu anapokuwa mwili, kimsingi Anatumia neno kukamilisha yote na kufanya yote yawe wazi. Katika maneno Yake pekee ndipo unaweza kuona kile Alicho; ni katika maneno Yake pekee ndiyo unaweza kuona kwamba yeye ni Mungu Mwenyewe. Mungu katika mwili Anapokuja duniani, hafanyi kazi nyingine ila kuongea maneno—hivyo basi hakuna haja ya kutumia uhakika; maneno yanatosha. Hii ni kwa sababu Amekuja kimsingi kufanya kazi hii, kumruhusu mwanadamu aone nguvu Zake na ukuu ulio kwenye neno Lake, kumruhusu mwanadamu kuona kupitia kwa maneno Yake jinsi Alivyojificha kwa unyenyekevu, na kumruhusu mwanadamu kujua ukamilifu Wake kupitia kwa maneno Yake. Kila kitu Alicho nacho na kile Alicho kiko katika maneno Yake, hekima Yake na ajabu yako katika maneno Yake. Katika hii ndipo unapofanywa kuona mbinu nyingi ambazo Mungu anatumia kuongea maneno Yake. … Leo Mungu wa kweli Mwenyewe wa mwili Anaongea tu, na hatendi. Huu ni ukweli! Anatumia maneno kukufanya mkamilifu, na Anatumia maneno kukulisha na kukunyunyizia. Pia Anatumia maneno kufanya kazi, na Anatumia maneno badala ya uhakika kukufanya ujue ukweli Wake. Kama una uwezo wa kutazama ukweli huu wa kazi ya Mungu, basi itakuwa vigumu kuwa wa kutoonyesha hisia.
kutoka katika "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu.
kutoka katika "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumua kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na kujua dutu yao. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote. Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno?
kutoka katika "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao.
kutoka katika "Fumbo la Kupata Mwili (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Umuhimu mkubwa zaidi wa kazi ya maneno ni kuwaruhusu watu kuweza kutia katika matendo ukweli baada ya kuuelewa ukweli, kutimiza mabadiliko katika tabia yao, na kutimiza maarifa kuhusu wao wenyewe na kazi ya Mungu. Mbinu za kufanya kazi tu kupitia kwa kuongea ndizo zinazoweza kuleta mawasiliano kuhusu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu, maneno tu ndiyo yanayoweza kuelezea ukweli. Kufanya kazi kwa njia hii ndiyo mbinu bora zaidi ya kumshinda mwanadamu; mbali na matamko ya maneno, hakuna mbinu nyingine inayoweza kumpatia mwanadamu uelewa wa wazi zaidi wa ukweli na kazi ya Mungu, na hivyo basi katika awamu Yake ya mwisho ya kazi, Mungu anazungumza naye mwanadamu ili kuweza kuwa wazi kwa mwanadamu kuhusu ukweli na siri zote ambazo haelewi, na hivyo basi kumruhusu kufaidi njia ya kweli na uzima kutoka kwa Mungu na kisha kutosheleza mapenzi ya Mungu.
kutoka katika "Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu atakamilishwa kabisa katika Enzi ya Ufalme. Baada ya kazi ya ushindi, mwanadamu atapitishwa kwenye mambo magumu ya kusafishwa na taabu. Wale ambao wanaweza kushinda na kushuhudia katika taabu hii ndio hatimaye watakaofanywa wakamilifu; wao ndio washindi. Katika taabu hii, mwanadamu anahitajika kukubali kusafishwa huku, na kusafishwa huku ndio tukio la mwisho la kazi ya Mungu. Itakuwa mara ya mwisho ambapo mwanadamu atasafishwa kabla ya hitimisho la kazi zote za usimamizi wa Mungu, na wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakubali jaribio hili la mwisho, lazima wakubali kusafishwa huku kwa mwisho.
kutoka katika "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Hii hatua ya kazi itaunda kundi la washindi na baada ya kuliunda kundi hili la washindi, wataweza kushuhudia matendo Yake, wataweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisia, na kumtosheleza na kuwa waaminifu Kwake hadi kifo, na kwa njia hii Mungu Atatukuzwa.
kutoka katika "Mazungumzo Mafupi Kuhusu ‘Ufalme wa Milenia Umefika’" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji ya mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa hali hii, umbo la usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa juu kuliko tabia yake inavyoweza kufikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo ambapo wanadamu wataanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani, ndipo kazi ya Mungu itafikia kikomo, wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Wakati huo utakapowadia, kazi ya Mungu itakuwa imefika mwisho, na ushirikiano wa mwanadamu na Mungu ili abadilishe tabia zake hautakuwepo, na wanadamu wote wataishi kwenye nuru ya Mungu, na kuanzia hapo kuendelea, hapatakuwa na uasi au upinzani wowote kwa Mungu.
kutoka katika "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku?
kutoka katika "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wa mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mzuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi zote zinahitaji kuadibu kwa haki na hukumu kutimizwa. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu.
kutoka katika "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya kushinda. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?
kutoka katika "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri yeyote asiyeweza kwenda sambamba na Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.
kutoka katika "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikipitisha wazi amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayeyakiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa viwango tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Ubinadamu wote utafuata aina yake, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
kutoka katika "Tamko la Ishirini na Sita" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.
kutoka katika "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani.
kutoka katika "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kufuatia kukamilika kwa maneno Yangu, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanashuhudiwa mwaka mzima. Kamwe, watu hawakumbwi tena na ulimwengu wa mwanadamu wenye huzuni na wenye taabu, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; maeneo yote yamejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu.
kutoka katika "Tamko la Ishirini" la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni