4/13/2019

Neno la Mungu | Sura ya 52

 Mwenyezi Mungu anasema, “Ninatokea kama Jua la haki, na nyinyi pamoja na Mimi tunashiriki utukufu na baraka, milele na milele! Huu ni ukweli thabiti, na tayari umeanza kutimizwa kwenu. Kwa yote ambayo Nimewaahidi, Nitawatimizia; yote Nisemayo ni ya kweli, na hayatarudi tupu. Baraka hizi za ajabu ziko juu yenu, hakuna yeyote mwingine anayeweza kuzidai; ni matunda ya utumishi wenu kwa kukubaliana na Mimi kwa maafikiano. Zitupilie mbali dhana zenu za kidini; yaamini maneno Yangu kuwa ya kweli na msiwe mwenye shaka! Mimi sifanyi utani na nyinyi, Namaanisha Ninayoyasema; wale ambao Nawakirimu baraka ndio wanaozipokea; wale ambao Siwatawazi baraka hawazipokei[a]; hili linaamuliwa na Mimi. Baraka nzuri ya kidunia ni nini? Kwa mtazamo Wangu si kitu ila kinyesi cha mnyama, yenye thamani chini ya senti. Kwa hivyo msizithamini sana starehe za kidunia; si kufurahia baraka za mbinguni na Mimi ni ya maana zaidi, kitu cha thawabu zaidi?
Awali ukweli haukuwa umefunuliwa, na Mimi Sikuwa Nimejijulisha; nyinyi mlinishuku Mimi na hamkuthubutu kuwa wenye bidii. Hata hivyo, sasa mambo yote yamefunuliwa, na Nimejitokeza kama Jua la haki; kama bado mko katika shaka, mnasema nini kuhusu hilo? Wakati giza lilipofunika dunia, ya kwamba hamkuweza kuuona mwanga iliweza kusamehewa, lakini sasa jua limeangaza pembe zote zenye giza; yalilofichwa hayajafichika tena, yaliyosetiriwa hayajasetiriwa tena; kama bado mko na shaka, basi Sitawasamehe kwa urahisi! Sasa ni wakati wa kuwa na uhakika kabisa kunihusu, wakati wa kuwa tayari kujitolea Kwangu na kugharimika kwa ajili Yangu. Yeyote anayenipinga kwa njia yoyote ndogo ile atashambuliwa mara moja kwa mioto ya hukumu bila kuwaza tena au kusita. Kwani sasa ni wakati ambao hukumu isiyo na huruma imefika; kwa kuwa wale ambao fikra na mioyo yao si minyofu, kutakuwa na hukumu ya papo hapo; hii ni maana ya kweli ya "Kazi Yangu ni kama mwako wa ghafla wa umeme" kama ilivyozungumziwa.
Inafanyika kwa haraka; haina budi ila kuwastaajabisha watu, itawatia watu hofu, haiwezi kucheleweshwa tena na haiwezi kuzuiliwa. Kadri kazi Yangu inavyofanywa, ndivyo inavyosonga mbele kwa haraka; yeyote ambaye si mwangalifu na tayari siku zote huwa katika hatari ya kutelekezwa; kamwe msijaribu tena kujaribu moyoni mwako. Kazi Yangu imeanza kikamilifu, ikienea kwa mataifa yasiyo Uyahudi na ulimwengu wa dunia. Mioto ya hukumu ni katili na bila huruma au upendo kwa mtu yeyote. Wale ambao ni waaminifu kwa Mungu lakini bado wako na fikra na mawazo yasiyo sahihi, au hata wanapinga kidogo, watahukumiwa bila shaka. Yeyote ambaye mwanga Wangu unamwangazia ataishi ndani ya mwanga, na kutenda katika mwanga, na kunitumikia hadi mwisho wa barabara. Wale ambao hawaishi katika mwanga wanaishi gizani. Nitafanya uamuzi baada ya kuwahukumu, kulingana na msimamo wao kuhusu hatia yao.
Siku Yangu imefika, “Siku Yangu” iliyotajwa awali sasa iko mbele ya macho yenu, kwa kuwa nyinyi mnashuka pamoja na Mimi. Mimi na nyinyi, nyinyi na Mimi, tumekutana angani, tukishiriki utukufu pamoja. Siku Yangu kwa kweli imefika kabisa!
Tanbihi:
a. Nakala asili inasema "wale ambao Nawakirimu ndio wanapokea; wale ambao Siwakirimu hawapokei."
Chanzo: Sura ya 52   

        Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni