Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maneno-ya-Roho-Mtakatifu-kwa-Makanisa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maneno-ya-Roho-Mtakatifu-kwa-Makanisa. Onyesha machapisho yote

4/27/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 22

Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.

4/13/2019

Neno la Mungu | Sura ya 52

 Mwenyezi Mungu anasema, “Ninatokea kama Jua la haki, na nyinyi pamoja na Mimi tunashiriki utukufu na baraka, milele na milele! Huu ni ukweli thabiti, na tayari umeanza kutimizwa kwenu. Kwa yote ambayo Nimewaahidi, Nitawatimizia; yote Nisemayo ni ya kweli, na hayatarudi tupu. Baraka hizi za ajabu ziko juu yenu, hakuna yeyote mwingine anayeweza kuzidai; ni matunda ya utumishi wenu kwa kukubaliana na Mimi kwa maafikiano.

4/12/2019

Umeme wa Mashariki | Sauti ya Mungu—Sura ya 37

Umeme wa Mashariki | Sauti ya Mungu—Sura ya 37

      Kwa kweli hamna imani mbele Yangu na mara kwa mara mnajitegemea wenyewe kufanya mambo. "Hamuwezi kufanya chochote bila Mimi!" Lakini nyinyi watu wapotovu daima mnachukua maneno Yangu ndani ya sikio moja na linatokea nje ya lile nyingine. Maisha siku hizi ni maisha ya maneno; bila maneno hakuna maisha, hakuna uzoefu, wala hakuna imani. Imani iko katika maneno;

4/08/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 36

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, kila kitu chini ya mbingu hung’aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika miisho ya ulimwengu vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli wamefungua mapazia yao, kuhuishwa, kama kuamka kutoka kwa ndoto, kuchipuka kwa kuvunja uchafu! 

4/05/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani! Katika pembe za mbali za dunia, kama mvua inayonyesha ndani ya kila pembe na kila mwanya, hakuna doa hata moja linalobaki, na inavyoosha wote kutoka kichwa hadi kidole, hakuna kinachojificha kutoka kwake wala hakuna mtu yeyote awezeya kujikinga kutoka kwake.

4/04/2019

Neno la Mungu | Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote , mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli kabisa! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vikasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi.

4/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo.

3/23/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | Sura ya 20

Kazi ya Roho Mtakatifu hushina mbele, ikiwaleta nyinyi ndani ya eneo mpya kabisa, ambayo ni kwamba hali halisi ya maisha ya ufalme imejitokeza mbele yako. Maneno ambayo yamesemwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja yamefichua ukina ulio ndani ya mioyo yenu na kwa hiyo picha moja baada ya nyingine zinaonekana mbele yenu. Wale wote ambao wana njaa na kiu ya haki, ambao wana nia ya kutii kwa hakika watabaki Sayuni na watakaa Yerusalemu Mpya.

3/18/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 15

Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru;

3/16/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa Makanisa | Sura ya 14

 Mwenyezi Mungu anasema, "Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru.

3/14/2019

Umeme wa Mashariki | Sura ya 13

Umeme wa Mashariki | Sura ya 13

Katika hali yenu ya sasa nyinyi hushika dhana ya "kibinafsi"zaidi kupindukia, na madakizo ya dini ni mazito kiasi. Mmeshindwa kutenda katika roho, hamuwezi kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu, na mmekataa mwanga mpya. Huoni jua wakati wa mchana kwa sababu wewe ni kipofu. Huwaelewi watu, umeshindwa kuwaacha wazazi wako, umekosa utambuzi wa kiroho, huijui kazi ya Roho Mtakatifu, na huna wazo la jinsi ya kula na kunywa ya neno Langu[a].

3/11/2019

Matamko ya Kristo Mwanzoni—Sura ya 12

Mwenyezi Mungu anasema, “ Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga.

3/10/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

 Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 11

        Mungu anasema, "Je, Mimi ni Mungu wako? Je, Mimi ni Mfalme wako? Je, kweli umeniruhusu Mimi kutawala kama Mfalme ndani yako? Unapaswa kutafakari kujihusu kabisa. Je, hukuchunguza na kukataa mwanga mpya na hata kuthubutu kuacha kuufuata ulipokuwa ukija? Kwa sababu ya hii utastahimili hukumu na kuanguka hadi kifo chako, utahukumiwa na kutandikwa kiboko na kiboko cha chuma na hutahisi kazi ya Roho Mtakatifu.

3/08/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 10

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho.

3/05/2019

Matamko ya Kristo Mwanzoni | Sura ya 7

Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo.

3/03/2019

Matamshi ya Kriso—Sura ya 6

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.