Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumwabudu-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kumwabudu-Mungu. Onyesha machapisho yote

4/05/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 35

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani! Katika pembe za mbali za dunia, kama mvua inayonyesha ndani ya kila pembe na kila mwanya, hakuna doa hata moja linalobaki, na inavyoosha wote kutoka kichwa hadi kidole, hakuna kinachojificha kutoka kwake wala hakuna mtu yeyote awezeya kujikinga kutoka kwake.

4/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo.

5/20/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sisitiza Zaidi Kwa Uhalisia

Mwenyezi Mungu alisema, Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu itakayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui chochote kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi sana hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi sana bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi.

3/21/2018

Sura ya 27. Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu”

Mwenyezi Mungu alisema, Ukilibadilisha au kulikanganya neno la Mungu Mwenyewe, basi hiyo ni sawa na uasi wa Mungu, kukufuru dhidi Yake na usaliti. Hii ni sawa tu na malaika mkuu kusema:”Mungu, Unaweza kuumba mbingu na ardhi na vitu vyote na Unaweza kufanya miujiza, lakini pia mimi ninaweza. Unapanda juu kwenye kiti cha enzi, na hivyo hivyo mimi pia napanda. Unatawala mataifa yote, Ninatawala mataifa yote pia. Wewe ulimuumba mwanadamu ilhali mimi ninawatawala!” Je, hii si ya hali sawa? Wengine wana mtazamo fidhuli kuhusu mipangilio ya kazi kutoka juu. Wanafikiri: “Aliye juu hufanya mipangilio ya kazi na sisi tunafanya kazi kwenye viwango vya chini.