4/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo. Mimi ndimi mwenyezi Mungu! Mradi tu uko radhi kushirikiana na Mimi, Nitayatibu yote yanayokuuguza. Mimi ni Mungu anayeangalia ndani kabisa ya mioyo ya watu, Naujua magonjwa yako yote na kule ambako dosari zako ziko. Haya ndiyo mambo ambayo yanakuzuia wewe kuwa na maendeleo maishani, na ni lazima yatupiliwe mbali hivi karibuni. La sivyo, mapenzi Yangu hayawezi kutimilika juu yako. Kile ambacho mwanga Wangu unamulika juu yake, lazima unitegemee Mimi kukitupilia mbali, Nitegemee kila mara, kuwa karibu na Mimi, na matendo yako lazima yafichue sura Yangu. Utakuwa na ushirika na Mimi zaidi wakati huna uhakika kuhusu kile cha kufanya, na Nitakuongoza kuelekea kwa matendo sahihi ili kwamba uweze kusonga mbele. Kama huna uhakika, usifanye vitendo vya kiholela; ngoja tu wakati Wangu. Dumisha silika thabiti, usiruhusu hisia zako kali ziwe moto au baridi; lazima uwe na moyo ambao daima inanicha. Kile unachofanya mbele Yangu au nyuma Yangu lazima daima kiwe kulingana na mapenzi Yangu. Usiwe mwenye huruma kwa yeyote kwa niaba Yangu, awe ni mumeo au mmoja wa jamii yako; halikubaliki, haijalishi wao ni wazuri kiasi gani. Lazima uchukue hatua kwa msingi wa ukweli. Ukinipenda Mimi, Nitakuridhia baraka kubwa. Sitamstahimili yeyote anayepinga. Wapende wale Ninaowapenda, na uwachukie Ninaowachukia. Usitilie maanani mtu yeyote, kitu chochote au chombo chochote. Angalia na moyo wako na uone kwa udhahiri watu wanaotumiwa na Mimi, kuwa katika mawasiliano zaidi na wanadamu wa kiroho. Usiwe mpumbavu; lazima utofautishe. Ngano itakuwa ngano daima na vigugu mwitu havitawahi kua viwe ngano, na ni lazima utambue aina tofauti za watu. Lazima uwe hasa mwangalifu katika usemi wako na uweke miguu yako katika njia ambayo Nimekusudia. Maneno haya lazima yatafakariwe kwa uangalifu. Lazima utupilie mbali uasi wako na ujifanye anayefaa kwa matumizi Yangu upesi iwezekanavyo, ili kwamba moyo Wangu uridhishwe.  
Chanzo: Sura ya 29  
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni