Kumwamini Mungu si jambo rahisi kufanya. Ninyi mnajiboronga, mkiteketeza kila kitu mbele yenu mkifikiri kuwa haya yote ni ya kuvutia sana, matamu mno! Kuna baadhi ambao bado wanashangilia—wao tu hawana utambuzi katika roho zao. Ni vyema kuchukua muda wa kuuweka katika muhtasari uzoefu huu. Katika siku za mwisho, kila aina za pepo huibuka kutekeleza majukumu yao, wakikaidi kwa uwazi hatua za mbele za wana wa Mungu na kushiriki katika kuuvunja ujenzi wa kanisa.
Mkikuchukulia hii bila kutilia maanani, mkimpa Shetani nafasi za kufanya kazi, italichafua kanisa, watu watakuwa na hofu na kuhisi kukata tamaa, na katika kadhia kubwa, watu kupoteza maono. Kwa njia hii, gharama yenye jitihada ambayo Nimelipa kwa takribani miaka mingi yote inakuwa kazi bure.
Wakati wa ujenzi wa kanisa pia ni wakati wa mhemuko zaidi wa Shetani. Kupitia kwa watu wachache, Shetani mara kwa mara husababisha usumbufu na kukatiza na ni wale ambao hawaijui roho au wale waumini wapya ambao wanatekeleza jukumu la Shetani kwa urahisi zaidi. Kwa sababu watu hawaelewi kazi ya Roho Mtakatifu, mara nyingi wananyoosha mikono yao na kufanya mambo kiholela, kulingana kabisa na wanavyopenda wao wenyewe, njia za kufanya mambo na dhana. Shika ulimi wako—hii inasemwa kwa ajili ya ulinzi wako mwenyewe. Sikiliza na utii vyema. Kanisa na jamii ni tofauti. Huwezi tu kusema kile unachopenda, au kusema chochote unachofikiri. Haitawezekana hapa kwa kuwa hii ni nyumba ya Mungu. Mungu hakubali namna watu wanavyofanya mambo. Lazima ufanye mambo kwa kuifuata roho, ishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu na kisha wengine watakutazama na kupendezwa nawe. Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwako kutojijua. Kwanza ponya ugonjwa wako mwenyewe, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. Uache mwili na uasili. Daima yaruhusu maneno ya Mungu yawe na mamlaka ndani mwako. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maisha yako hayabadiliki; utakuja polepole kuhisi kwamba tabia yako imebadilika kiasi kikubwa. Mbeleni ulikuwa na haraka ya kujionyesha mbele ya watu, hukutii yeyote au ulikuwa na nia ya makuu, mwenye kujidai au mwenye majivuno, na utayatupilia mambo haya mbali hatua kwa hatua. Ukitaka kuyatupilia mbali sasa hivi, basi hiyo haiwezekani! Hii ni kwa sababu binafsi yako ya zamani haitawaruhusu wengine kuigusa, imekita mizizi kabisa ndani yako. Hivyo ni lazima ufanye juhudi za kibinafsi, utii kazi ya Roho Mtakatifu vyema na kikamilifu, utumie hiari yako kushirikiana na Mungu na uwe na nia ya kuyaweka maneno yangu katika vitendo. Ukitenda dhambi, Mungu atakufundisha nidhamu. Unaporejelea na kuwa na ufahamu basi yote yatakuwa mema ndani yako kwa mara moja. Kama unazungumza kifisadi, basi utafundishwa nidhamu mara moja kwa ndani. Unaona kwamba Mungu hafurahii jambo la aina hiyo, hivyo ukiliacha mara moja utakuwa na uzoefu wa amani ya ndani. Kuna baadhi ya waumini wapya ambao hawaelewi hisia za maisha ni nini au jinsi ya kuishi ndani ya hisia za maisha. Wakati mwingine unashangaa, ingawa hujasema lolote, kwa nini unahisi kutotulia sana kwa ndani? Wakati kama huu ni wazo lako na akili ambavyo vina makosa. Wakati mwingine unayo maamuzi yako mwenyewe, dhana na maoni yako mwenyewe; wakati mwingine unawaona wengine kuwa wadogo zaidi kukuliko; wakati mwingine unafanya hesabu zako mwenyewe za ubinafsi nawe huombi au kujichunguza, ikikuacha ukihisi kutotulia ndani. Labda unajua tatizo ni nini, kwa hiyo mara moja unaliita jina la Mungu moyoni mwako, unasogea karibu na Mungu nawe utarejeshwa. Wakati moyo wako umevurugika sana, umechanganyikiwa na hautulii, lazima kabisa usifikiri kwamba Mungu anakuruhusu kuongea. Hasa wale ambao ni waumini wapya lazima wamtii Mungu vyema katika suala hili. Hisia ambazo Mungu huweka ndani ya mtu ni amani, furaha, uwazi na udhamini. Mara nyingi watu hawaelewi na watatia fujo mambo na kufanya mambo kiholela—haya yote ni makatizo, na kabisa lazima uizingatie. Kama wewe ni wa kuelekea katika hali hii, unapaswa kwanza kuchukua dawa za kuzuia, la sivyo utaleta makatizo na Mungu atakupiga. Usiwe mwenye haki wa kibinafsi; zichukue nguvu za wengine na kuzitumia kusawazisha na mapungufu yako mwenyewe, angalia jinsi wengine wanaishi kwa kutegemea maneno ya Mungu na uone kama maisha, vitendo na hotuba zao ni vya thamani ya kujifunza kutoka kwavyo au la. Ukiwaona wengine kuwa chini yako wewe basi ni mwenye haki binafsi, mwenye majivuno ya kibinafsi na huna manufaa kwa yeyote. La muhimu sasa ni kulenga kuhusu maisha, kula na kunywa zaidi maneno Yangu, upate uzoefu wa maneno Yangu, kuyajua maneno yangu, kuyafanya maneno yangu kwa dhati kuwa maisha yako—hili ni jambo kuu. Je, maisha ya mtu ambaye hawezi kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu yanaweza kukomaa? Hapana, hayawezi. Lazima uishi kwa kutegemea maneno Yangu kila wakati. Katika maisha, lazima maneno Yangu yawe kanuni yako ya vitendo. Yatakusababisha kuhisi kuwa kufanya mambo kwa njia fulani ni kile Mungu anafurahia, na kufanya mambo kwa njia nyingine ni kile Mungu anachochukia; polepole, utakuja kutembea katika njia sahihi. Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.
Huu sasa ni wakati muhimu. Lazima muendelee kufanya kazi kwa bidii mpaka dakika ya mwisho kabisa, myaweke wazi macho yenu ya roho ili muweze kutofautisha kati ya mema na mabaya, na mtumie juhudi nyingi muwezavyo kwa ujenzi wa kanisa. Epukeni vikaragosi wa Shetani, misukosuko ya kidini na kazi ya roho mbaya. Litakaseni kanisa, kufanya mapenzi Yangu itendeke bila kupingwa, na katika wakati huu mfupi sana unaotangulia majanga kweli Nitawafanya kuwa kamili haraka iwezekanavyo, na kuwaleta katika utukufu.
Chanzo: Sura ya 22
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni