3/08/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 10

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote, lazima uviachilie vitu vyote ulivyo navyo, na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, kulipa gharama zote kwa ajili Yangu. Huu ndio wakati Nitakujaribu, je, utatoa uaminifu wako Kwangu? Je utanifuata Mimi hadi mwisho wa barabara kwa uaminifu? Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka! Kila kitu ambacho hutokea ni kwa kusudi Langu njema na yote yako chini ya uangalifu Wangu. Je, kila neno na tendo lako linaweza kufuata neno Langu? Wakati majaribio ya moto yatakuja juu yako, utapiga magoti na kuomba msaada? Au wewe utajikunyata, bila uwezo wa kusonga mbele?
Lazima uwe na ushujaa Wangu ndani yako na lazima uwe na kanuni wakati unakabiliana na ndugu wasioamini. Lakini kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki. Weka juhudi zako zote katika kuweka moyo wako mbele Yangu na Mimi Nitakufariji na kukupa amani na furaha katika moyo wako. Hutatafuta kibali cha watu, je, si ni ya thamani zaidi na zito kuniridhisha? Katika kuniridhisha, wewe hautakuwa na maisha ya amani na furaha zaidi milele? Mateso yaliyo mbele yako yanaashiria ukubwa wa baraka zako za baadaye ziitakavyokuwa, ni za kushangaza. Haujui wingi wa baraka utakazokuwa nazo, huwezi hata ota ndoto zake. Leo zakuwa halisi, halisi kweli! Hii haiko mbali sana, unaweza kuiona? Kila chemba ya mwisho ya hii iko ndani Yangu na ni jinsi ngani kuna ung’avu mbele! Futa machozi yako, usihisi uchungu au huzuni, yote yamo mikononi Mwangu na lengo Langu ni kuwafanya washindi hivi karibuni na kuwaleta katika utukufu nami. Utashukuru na kusifu kwa yote yatakayokutokea, na hilo litaridhisha moyo Wangu.
Maisha ya kuzidi uwezo wa binadamu ya Kristo tayari imeonekana, hakuna kitu chochote unachopaswa kuhofia. Shetani yuko chini ya miguu yetu na muda wao ni mdogo. Amka! Tupilia mbali ulimwengu wa uasherati, jinusuru mwenyewe kutoka dimbwi la kifo! Kuwa mwaminifu Kwangu zaidi ya yote, songa mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, Nitegemee Mimi!
 kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili 
 Soma Zaidi: neno la Mungu—Sura ya 11, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni