Swahili Christian Movie "Maskani Yangu Yako Wapi" | Mungu ni Kimbilio la Nafsi Yangu
Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake. Alikuwa na chaguo dogo — alilazimika kumpeleka Wenya nyumbani kwa mama yake, lakini mama yake alilenga kikamilifu kuendesha biashara yake na hakuwa na muda wa kumtunza Wenya, hivyo mara nyingi alipelekwa nyumbani kwa jamaa na marafiki zake kupata ulezi.
Baada ya miaka mingi sana ya maisha ya kutunzwa na walezi, Wenya alihisi upweke na asiyejiweza, na alitamani ukunjufu wa nyumbani. Ni wakati tu ambapo baba yake na mama wa kambo walitangua ndoa ndipo alirudi upande wa baba yake, na kuanzia hapo na kuendelea alikuwa na nyumbani, wakati mzuri au mbaya. Mara Wenya alipokua, alikuwa mwangalifu na mtiifu sana, na alisoma kwa bidii. Lakini wakati ule ule alipokuwa akitia bidii ili kujiandaa kwa ajili ya mitihani yake ya kuingilia chuo, msiba ulimfika: mama yake alikuwa na hemoraji ya ubongo na akapooza na kuwa mgonjwa kitandani. Babake wa kambo alimtelekeza mama yake na hata kuchukua udhibiti juu ya mali yake yote, na kisha babake akapelekwa hospitalini kwa ajili ya saratani ya ini... Wenya hangeweza kabisa kujitwisha mzigo wa kaya, hivyo yote ambayo angeweza kufanya ni kuwasihi jamaa na marafiki, lakini alikataliwa. ...
Tazama Video: Swahili Gospel Movie "Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni