10/15/2017

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,Yesu,Injili
Umeme wa Mashariki | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”
Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. Na mwanadamu anatumaini kuwa Atatekeleza tena kazi ya ukombozi Aliyoifanya kati ya Wayahudi, Atakuwa na huruma na mwenye upendo kwa mwanadamu, Atasamehe dhambi za mwanadamu, kuchukua dhambi za mwanadamu, na hata kuchukua makosa yote ya mwanadamu na kumkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Wanatamani Yesu Mwokozi Awe Alivyokuwa hapo awali—Mwokozi Ambaye Anapendeka, wa kirafiki na heshima, Asiye na hasira kwa mwanadamu, na Asiyemrudi mwanadamu. Mwokozi huyu Anasamehe na kubeba dhambi zote za mwanadamu, na hata kufa msalabani tena kwa ajili ya mwanadamu. Tangu Yesu Aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa na neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi Anawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea ghafla kwa Yesu Kristo, kutimiza maneno ya Yesu Akiwa duniani: “Nitarejea tu jinsi Nilivyoondoka”. Mwanadamu anaamini kuwa, kufuatia kusulubishwa na kufufuka, Yesu Alirudi mbinguni juu ya wingu jeupe, na kuchukua mahali Pake katika mkono wa kulia wa Yule Aliye Juu. Vilevile, mwanadamu anatazamia kuwa Yesu Atashuka, tena juu ya wingu jeupe (wingu hili linarejelea lile wingu ambalo Yesu Alipaa juu yake Aliporudi mbinguni), miongoni mwa wale ambao wamemtamani mno kwa maelfu ya miaka, na kuwa Atachukua mwonekano na mavazi ya Wayahudi. Baada ya kumwonekania mwanadamu, Atafadhili chakula kwa sababu yao, na kufanya maji ya uzima kuwamwagika kwa ajili yao, na Ataishi miongoni mwa wanadamu, Akiwa amejawa na neema na upendo, Akiwa hai na wa hakika. Na mengine. Ilhali Yesu Mwokozi hakufanya haya; Alitenda kinyume cha yale ambayo mwanadamu alikuwa anatazamia. Hakurejea kati ya wale ambao walikuwa wametamani kurejea Kwake, na hakutokea kwa wanadamu wote Akitumia wingu jeupe. Amerejea tayari, lakini mwanadamu hamjui, na kubaki mjinga kuhusu kurejea Kwake. Mwanadamu anamngoja tu bila mwelekeo, bila kujua kuwa ameshuka tayari juu ya wingu jeupe (wingu ambalo ni Roho Yake, maneno Yake, na tabia Yake yote na yale yote ambayo Yeye ni), na sasa yuko kati ya kikundi cha washindi ambacho Atakitengeneza katika siku za mwisho. Mwanadamu hafahamu haya: Ingawa Mwokozi Mtakatifu Yesu Amejawa na upendo na mapenzi kwa mwanadamu, Atafanya kazi vipi katika “hekalu” ambalo limejaa uchafu na roho wasio safi? Ingawa mwanadamu amekuwa akingoja kufika Kwake, Atawaonekania vipi wale wanaokula mwili wa wale wasio na haki, kunywa damu ya wasio na haki, kuvaa mavazi ya wasio na haki, wanaomwamini lakini hawamfahamu, na wanaompokonya kila wakati? Mwanadamu anajua tu kuwa Yesu Mwokozi Amejawa na upendo na huruma, na ni sadaka ya dhambi iliyojawa na ukombozi. Lakini mwanadamu hana habari kwamba Yeye pia ni Mungu Mwenyewe, ambaye Amejawa na haki, utukufu, ghadhabu, na hukumu, na kuwa na mamlaka na kujawa na hadhi. Kwa hivyo ingawa mwanadamu anayo hamu na kutamani kurudi kwa Mkombozi, na hata Mbingu inaguswa na maombi ya mwanadamu, Yesu Mwokozi hawaonekanii wale wanaomwamini ilhali hawamfahamu.
“Yehova” ni jina ambalo Nilichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, na linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Lina maana Mungu Anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. “Yesu” ni Imanueli, na lina maana sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, na Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, na Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja tu ya mpango wa usimamizi. Hivyo ni kusema, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wa Uyahudi waliochaguliwa, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa na Mungu wa Wayahudi wote. Na sasa katika enzi hii, Wayahudi wote isipokuwa kabila la Uyahudi wanamwabudu Yehova. Wanatoa kafara Kwake kwa madhabahu, na kumtumikia wakivaa mavazi ya kikuhani hekaluni. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Ambayo ni kusema, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, na kuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu liliwepo ili kuwezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, na ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hivyo jina Yesu linawakilisha kazi ya wokovu, na kuashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliwi bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. “Yehova” Anawakilisha Enzi ya Sheria, na ni jina la heshima kwa Mungu Aliyeabudiwa na Wayahudi. “Yesu” Anawakilisha Enzi ya Neema, na ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kufika kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anatarajia Afike na picha Aliyokuwa nayo kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, na usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, na enzi isingefikishwa kikomo. Hii ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni wa ukombozi na wokovu wa mwanadamu peke yake. Nilichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, na silo jina ambalo nitatumia kuleta wanadamu wote kufika kikomo. Ingawa Yehova, Yesu, na Masiha yote yanawakilisha Roho Wangu, majina haya yanaashiria wakati tofauti katika mpango Wangu wa usimamizi, na hayauwakilishi ukamilifu Wangu. Majina wanayoniita watu duniani hayawezi kueleza tabia Yangu nzima na yote Niliyo. Ni majina tu ambayo Ninaitwa katika enzi tofauti. Kwa hivyo, enzi ya mwisho—enzi ya siku za mwisho—itakapofika, jina langu litabadilika tena. Sitaitwa Yehova, au Yesu, na wala sio Masiha, lakini nitaitwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe mwenye nguvu, na chini ya jina hili Nitaleta enzi nzima kufikia tamati. Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Niliitwa pia Masiha, na watu wakaniita Yesu Mwokozi pia wakati mmoja kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi sio Yehova au Yesu Ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu Ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu Ambaye ataleta enzi kufika mwisho. Mimi ni Mungu Mwenyewe Ambaye Anainuka katika kingo za dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na wamekosa ufahamu kuhusu tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hapana hata mtu mmoja ambaye Ameniona. Huyu ni Mungu Ambaye ametokea kwa mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya mwanadamu. Anaishi kati ya mwanadamu, wa kweli na halisi, kama jua iwakayo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna hata mtu mmoja au kitu ambacho hakitahukumiwa na maneno Yangu, wala mtu hata mmoja au kitu ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa sababu ya maneno Yangu, na pia kupasuliwa kwa vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi Aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi Ambaye Ninatamalaki juu ya binadamu wote, na Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua Linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili na Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waone uso Wangu wa kweli: Mimi sio tu Mungu wa Wayahudi, wala Mimi sio Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.
Mwokozi Atakapofika katika siku za mwisho, kama Angeitwa Yesu bado, na kuzaliwa mara nyingine Uyahudi, na kufanya kazi Yake Uyahudi, basi hii ingeonyesha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana Aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitokea Uyahudi kufanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi sio tu Mungu wa Wayahudi, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi sio tu Yehova, Mungu wa Wayahudi, lakini, zaidi, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wote Niliowachagua kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi pekee, Misri, na Lebanoni, bali Niliumba pia Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu ya hii, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia tu Uyahudi kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome ya kazi Yangu ya ukombozi, na kutumia Mataifa kama msingi ambao Nitaleta enzi nzima kufika mwisho. Nilifanya hatua mbili za kazi kule Uyahudi (hatua mbili za kazi za Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), na Nimekuwa Nikitekeleza zaidi hatua mbili za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine nje ya Uyahudi. Kati ya Mataifa Nitafanya kazi ya kutamalaki, na hivyo kukamilisha enzi. Mwanadamu Akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa nimeanza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa hamu kufika kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao watu wasioniamini. Ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni bandia. Watu hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja sio kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, badala yake, wanatamani kurudi kwa Yesu mara ya pili, ambapo watakombolewa; wanamtazamia Yesu kumkomboa binadamu mara nyingine kutoka kwa hii dunia iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu hao watakuwa vipi wale wanaokamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Tamaa ya mwanadamu haina uwezo wa kufikia matakwa Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani tu au kuenzi kazi ambayo Nimefanya hapo awali, na hawajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya kila siku na hawi mzee. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, na hana ufahamu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule Ambaye Ataleta binadamu kufika mwisho. Yale ambayo mwanadamu anatamani na kujua ni ya dhana yake mwenyewe, na ni yale tu ambayo anaweza kuyaona na macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayofanya, bali kwa mvurugano nayo. Kama kazi Yangu ingefanywa kulingana na mawazo ya mwanadamu, basi ingefika mwisho lini? Mwanadamu angeingia mapumziko lini? Na Ningewezaje kuingia katika siku ya saba, siku ya Sabato? Nafanya kazi kulingana na mpango Wangu, kulingana na lengo Langu, na sio kulingana na nia ya mwanadamu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi :Kanisa la Mwenyezi Mungu | Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni