11/15/2018

Swahili Christian Movie "Kutamani Sana" (3) - Nani Atanyakuliwa Kwanza Wakati Bwana Atakaporudi?

Wengi wa wale wanaomsadiki Bwana wanasadiki kwamba mradi tu wajitolee, wajitumie, na kutia bidii, bila shaka watakuwa miongoni mwa wale wa kwanza kunyakuliwa. Lakini je, kuna msingi wowote wa haya katika maneno ya Bwana? Bwana Yesu alisema, "But many that are first shall be last; and the last shall be first" (Mathayo 19:30). "Kondoo wangu huisikia sauti yangu" (Yohana 10:27). Ni wazi kwamba kama mtu anaweza kunyakuliwa au la kunaamuliwa na kama ataisikia sauti ya Bwana. Wale wanaoisikia kwanza sauti Yake na kukubali kuonekana Kwake na kazi ni wanawali wenye hekima, na watakuwa wa kwanza kunyakuliwa.

Mwenyezi Mungu alisema, Mwokozi Atakapofika katika siku za mwisho, kama Angeitwa Yesu bado, na kuzaliwa mara nyingine Uyahudi, na kufanya kazi Yake Uyahudi, basi hii ingeonyesha kuwa Niliumba Wayahudi peke yao na kuwakomboa Wayahudi peke yao, na kuwa sina uhusiano wowote na Mataifa. Je, hii haitakuwa kinyume cha maneno Yangu kwamba “Mimi ni Bwana Aliyeumba mbingu na nchi na vitu vyote”? Nilitokea Uyahudi kufanya kazi Yangu kati ya Mataifa kwa sababu Mimi sio tu Mungu wa Wayahudi, ila Mungu wa viumbe vyote. Ninaonekana kati ya Mataifa katika siku za mwisho kwa sababu Mimi sio tu Yehova, Mungu wa Wayahudi, lakini, zaidi, kwa sababu Mimi ni Muumba wa wote Niliowachagua kati ya Mataifa. Sikuumba Uyahudi pekee, Misri, na Lebanoni, bali Niliumba pia Mataifa yote mbali na Israeli. Na kwa sababu ya hii, Mimi ni Bwana wa viumbe vyote. Nilitumia tu Uyahudi kama hatua ya kwanza ya kazi Yangu, Nikatumia Uyahudi na Galilaya kama ngome ya kazi Yangu ya ukombozi, na kutumia Mataifa kama msingi ambao Nitaleta enzi nzima kufika mwisho. Nilifanya hatua mbili za kazi kule Uyahudi (hatua mbili za kazi za Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema), na Nimekuwa Nikitekeleza zaidi hatua mbili za kazi (Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme) katika nchi nyingine nje ya Uyahudi. Kati ya Mataifa Nitafanya kazi ya kutamalaki, na hivyo kukamilisha enzi. Mwanadamu Akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa nimeanza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa hamu kufika kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao watu wasioniamini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni