Wimbo wa Maneno ya Mungu | Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki
I
Mungu aliipa Israeli utukufu Wake
kisha Akauhamisha mbali na pale,
na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.
Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga
ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,
Mungu atawaacha wote wanaotafuta kuuona mwanga tena
na utukufu Aliokuwa nao katika Israeli,
kuona kwamba Mungu tayari ameshuka chini juu ya wingu jeupe
miongoni mwa watu,
na kuona mawingu mengi meupe,
na kuona vishada vya matunda,
kumwona Yehova Mungu wa Israeli,
Mungu wa Israeli,
kumwona Mkuu wa Wayahudi,
kumwona Masihi Aliyengojewa,
na kuonekana kamili kwa Yeye aliyeteswa na wafalme
katika enzi zote.
II
Mungu atafanya kazi ya ulimwengu mzima na kufanya kazi kubwa,
akifichua utukufu Wake wote na matendo Yake yote kwa mwanadamu
katika siku za mwisho.
Mungu ataonyesha uso Wake uliojaa utukufu
kwa wale ambao wamemngoja Yeye kwa miaka mingi,
kwa wale ambao wametamani kumuona Yeye akija juu ya wingu jeupe,
kwa Israeli ambayo imemngoja Aonekane kwa mara nyingine tena,
kwa watu wote wanaomtesa Mungu.
Ili wote wajue kwamba
Mungu kwa muda mrefu uliopita Ameuchukua utukufu Wake
na kuuleta katika Mashariki.
Hauko katika Uyahudi, kwa maana siku za mwisho tayari zimewadia!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni