 |
Umeme wa Mashariki | Dhambi Zitampeleka Mwanadamu Jahanamu |
Mwenyezi Mungu alisema, Nimewapa maonyo mengi na kutawaza juu yenu kweli nyingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyokuwa hapo zamani, kuelewa kanuni nyingi za jinsi mtu anapaswa awe, na kumiliki kiasi kikubwa cha maarifa ya kawaida ambayo watu waaminifu wanapaswa kuwa nayo. Hiki ndicho mmepata baada ya miaka mingi sasa. Mimi sikani mafanikio yenu, lakini lazima Niseme wazi kuwa Mimi pia sikani kutotii kwenu kwingi na uasi dhidi Yangu hii miaka mingi, kwa sababu hakuna hata mtakatifu mmoja kati yenu, bila yeyote kuachwa nyuma nyinyi ni watu mliopotoshwa na Shetani, na maadui wa
Kristo. Dhambi zenu na kutotii kwenu hadi sasa havihesabiki, hivyo si ajabu kwamba Mimi daima Hujirudia mbele yenu. Sitaki kuishi hivi na nyinyi, lakini kwa ajili ya siku zenu za baadaye, kwa ajili ya hatima zenu, Mimi hapa Nitarudia Niliyoyasema mara nyingine tena.