Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maneno. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Maneno. Onyesha machapisho yote

6/03/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Arubaini na Tano

Mwenyezi Mungu alisema, Wakati mmoja Nilichagua bidhaa nzuri kubaki ndani ya nyumba Yangu, ili ndani yake kungekuwa na utajiri usio na kifani, na ingepambwa hivyo, Nilipata raha kutokana na hilo. Lakini kwa sababu ya mtazamo wa mwanadamu Kwangu, na kwa sababu ya motisha za watu, Sikuwa na budi ila kuiweka kazi hii kando na kufanya kazi nyingine. Nitatumia motisha za mwanadamu kufanikisha kazi Yangu, Nitashawishi vitu vyote vinihudumie, na kusababisha nyumba Yangu kutokuwa ya kusononeka na ya ukiwa tena kama matokeo.

11/03/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maneno kwa Vijana na Wazee

Umeme wa Mashariki,Wakristo,Roho Mtakatifu
Umeme wa Mashariki | Maneno kwa Vijana na Wazee

Mwenyezi Mungu alisema , Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana. Hili ni kwa sababu watu wamekuja kwa wakati wa sasa bila kuelewa kazi Ninayofanya, na wao hasa hukanganywa na maneno ambayo Ninawaambia. Wao huyabeba maneno Yangu mikononi mwao, wasijue kama wanapaswa kujitahidi kuamini au kama wanapaswa kuyasahau kwa shaka. Hawajui kama wanapaswa kuyatia katika vitendo, au kama wanapaswa kungoja kuona. Hawajui kama wanapaswa kuachana na kila kitu na kisha kufuata kwa ujasiri, au kama wanapaswa kuendelea kuwa wa kirafiki na ulimwengu kama hapo awali. Ulimwengu wa ndani wa watu ni wenye utata sana, na wao ni wajanja sana.