11/02/2017

Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu
Umeme wa Mashariki | Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku Ya Ghadhabu
Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kusalimika kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba "siku za mwisho" ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza dunia nzima. Iko hivyo ili Niweze kupata utukufu mkuu, ili viumbe vyote duniani viweze kupitisha utukufu Wangu kwa mataifa yote, milele katika vizazi vyote, na viumbe vyote mbinguni na duniani viweze kuuona utukufu wote ambao Nimepata duniani. Kazi inayofanyika katika siku za mwisho ni kazi ya ushindi. Sio uongozi wa maisha ya watu wote duniani, lakini hitimisho la maisha ya milenia ya mwanadamu yasiyoangamia, ya mateso katika dunia. Matokeo yake ni kwamba kazi ya siku za mwisho haiwezi kuwa kama miaka elfu kadhaa ya kazi katika Israeli, wala kama muongo mmoja wa kazi katika Yuda ambayo kisha iliendelea kwa miaka elfu kadhaa mpaka kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu katika mwili. Watu wa siku za mwisho hukutana tu na kuonekana kwa Mkombozi katika mwili, na kupokea kazi binafsi na maneno ya Mungu. Haitakuwa miaka elfu mbili kabla ya siku za mwisho hazijafika ukingoni; zi fupi, kama wakati ambao Yesu alifanya kazi ya Enzi ya Neema katika Yuda. Hii ni kwa sababu siku za mwisho ni hitimisho la nyakati nzima. Ni ukamilisho na tamatisho la mpango wa miaka elfu sita wa usimamizi wa Mungu, na kuhitimisha safari ya maisha ya mateso ya mwanadamu. Hazichukui uanadamu mzima katika enzi mpya au kuruhusu maisha ya mwanadamu kuendelea. Hiyo haitakuwa na umuhimu wowote kwa ajili ya mpango Wangu wa usimamizi au kuwepo kwa mwanadamu. Kama mwanadamu angeendelea kwa namna hii, basi hivi karibuni au hapo baadaye wao wangevamiwa kabisa na Shetani, na zile nafsi za wale walio Wangu hatimaye zingetwaliwa na mikono yake. Kazi Yangu huendelea kwa miaka elfu sita, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, Nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kuthibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nami nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii yenye matokeo mazuri na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na umepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao umeshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa Nami kutoka utawala wa Shetani, na ni dhibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wao huja kutoka kila taifa na dhehebu, na kila mahali na nchi ulimwenguni mwote. Ni wa jamii tofauti, na wana lugha mbalimbali, mila na rangi ya ngozi, na huenea katika kila taifa na dhehebu la duniani, na hata kila pembe ya dunia. Hatimaye, watakuja pamoja na kuunda ubinadamu kamili, mkusanyiko wa binadamu usiofikiwa na majeshi ya Shetani. Wale miongoni mwa wanadamu ambao hawajaokolewa na kushindwa na Mimi watazama kwa kimya mpaka chini ya bahari, na watachomwa kwa moto wa kuteketeza milele. Nitaangamiza mwanadamu huyu mzee aliye mchafu sana, kama tu vile Nilivyoangamiza wazaliwa wa kwanza na ng’ombe wa Misri, na kuacha tu Waisraeli, waliokula nyama ya mwanakondoo, kunywa damu ya mwanakondoo, na kutia alama vizingitini mwa milango yao kwa damu ya mwanakondoo. Si watu ambao wameshindwa nami na ni wa jamii Yangu ndio wale pia wanaokula nyama Yangu, Mwanakondoo na kunywa damu Yangu, Mwanakondoo, na kukombolewa Nami na kuniabudu Mimi? Si watu wa namna hiyo kila mara huandamwa na utukufu Wangu? Si hao wasio na nyama Yangu, Mwanakondoo tayari wamezama kimya kwa kina cha bahari? Leo wao wananipinga, na leo maneno Yangu ni kama tu yale yaliyosemwa na Yehova kwa wana na wajukuu wa Israeli. Lakini ugumu katika kina cha nyoyo zenu unahifadhi tu ghadhabu Yangu, na kuleta mateso zaidi juu ya miili yenu, hukumu zaidi juu ya dhambi zenu, na ghadhabu zaidi juu ya udhalimu wenu. Ni nani atakayeweza kusamehewa katika siku Yangu ya ghadhabu, mnaponishughulikia kwa namna hii wakati huu? Udhalimu wa nani utaweza kuepuka macho Yangu ya kuadibu? Dhambi za nani zinaweza kuepuka mikono Yangu, Mimi Mwenyezi? Uasi wa nani unaweza kupokea hukumu Yangu, Mimi Mwenyezi? Mimi, Yehova, Nasema hivyo kwenu, kizazi cha jamii ya Mataifa, na maneno Ninayosema nanyi yanashinda matamko yoyote yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, ilhali bado nyinyi ni wagumu kuliko watu wote wa Misri. Je, si mnahifadhi ghadhabu Yangu Ninapofanya kazi kwa utulivu? Jinsi gani mnaweza kuepuka salama bila ya madhara kutoka siku Yangu, Mwenyezi?
Nimefanya kazi na kusema kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi, ila ni wakati upi kamwe mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia wazi wazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanishughulikia namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kukifanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini, mioyo yenu imeshupaa? Je, Nimewahi kuwapiga kumbo kamwe? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenishughulikia hivyo, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Yangu, kuchukua sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kulisha watoto wa mbwa mwitu na vitukuu vyake katika tundu la mbwa mwitu; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiza unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlishaonekana machoni Mwangu, Mimi Yehova, wakati mliiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Ni jinsi gani mnavyoweza kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Jinsi gani ghadhabu Yangu kali ingeweza kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ni jinsi gani ghadhabu Yangu ingepita juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayafungui njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Jinsi gani matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangeweza kuepuka kuadibu Kwangu? Jinsi gani maombi yenu yangefikia masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Jinsi gani Ningeweza kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Jinsi gani basi kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu yangeondoka kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, ni jinsi gani basi Mimi Ningewawacha nyinyi kuhepa kutoka mikono Yangu na muiondokee siku ambayo Mimi, Yehova, hukuadibu na kukulaani wewe? Je, hamjui kwamba maneno yenu yote mabaya na kauli tayari yamefikia masikio Yangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umelilaghai vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba makosa yenu tayari yameichochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Mimi kutokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Mimi nimevumilia mpaka sasa, hadi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefikia Macho Yangu, na kwamba kilio changu tayari kimefikia masikio ya Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni afu, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Mimi Niko tayari kuvumilia yote ya mateso haya kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjafurahi mengi Yangu? Leo, Nimepeanwa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishana kwa maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kufanya vita na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka vishawishi vingi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani nyoyo zenu zingebaki ngumu leo, kama kwamba zimekuwa sugu? Jinsi gani maovu mnayoyatenda leo yangeepuka siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wenye mioyo migumu kuepuka hasira ya Yehova?
Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Wakati upi Nimewakaripia bila mantiki? Wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini kunitendea Mimi hivi? Je, nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini kunilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya kuyumbayumba Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mu wadanganyifu Kwangu na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningeweza kuruhusu buu dogo kunikufuru hivyo? Ningewezaje kupendekeza wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, wala Sikuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kusamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu takatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kufukuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Jinsi gani mngeweza kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kupingwa na kukaidiwa kwa njia hii na nyinyi, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Jinsi gani mnaweza kuepuka siku ya ghadhabu Yangu? Nawaambia kwa kweli: uvumilivu Wangu ulikuwa tayari kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale ambao mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu? Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si ni nyinyi maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa karaha? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Yeye Asiwe adui wako?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni