7/22/2018

Kupima kwa Sura Ni Upuuzi Tu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Ushuhuda
Yifan    Jiji la Shangqiu, Mkoa wa Henan
Katika siku za nyuma, mimi mara nyingi niliwapima watu kwa sura zao, nikiwachukua watu wachangamfu, wajuzi na wambuji hasa kwa heshima sana. Niliamini kwamba watu kama hao walikuwa wa busara, hodari kwa kuwaelewa wengine na kwa ujumla wema na wakarimu. Ni juzi juzi tu, kama ambavyo uhalisi umejifichua, nimekuja kurekebisha njia hii ya upuuzi ya kufikiri.
Usiku mmoja karibu na magharibi, nilirudi nyumbani kwa familia yangu mwenyeji na kumwona mwanamume mbichi aliyevalia suti na viatu vya ngozi ambaye alizungumza na kujichukua kwa utulivu wa madaha. Pia alikuwa amevaa jozi ya miwani iliyofuliwa kwa uzuri, ambayo ilitia mkazo tabia yake ya kustaarabika na ya kisomi. Mwenyeji wangu alitutambulisha sote wawili na akaniarifu kuwa huyo mwanamume mbichi alikuwa mwanawe na kwamba sasa alikuwa akifanya kazi kama afisa katika serikali ya manispaa ya jiji fulani kubwa. Nikiwa nimetoka kwa usuli wa umaskini na kuacha shule nilipokuwa na umri mdogo, nilihisi wivu mno kwa ajili ya mavazi yake sanifu, uzuri wenye elimu na adabu njema, bila kutaja shahada yake ya juu kutoka chuo maarufu na ajira stahiki. Kwa hakika ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu kumuona mtu mwenye uzuri kama huo na usomi. Nilifikiria mwenyewe, mtu aliyestaarabika na mwenye hadhi ya juu jinsi hiyo na mwenye elimu na adabu njema atakuwa maridhia kwa hakika, mwenye ubinadamu na razini. Nikiwa na fikra hiyo katika mawazo, nilianza kujaribu kujadili mambo ya imani na mwanamume huyo mbichi, lakini mijibizo yake ilikuwa kinyume kabisa na matarajio yangu. Alisimama kwa makelele na kubamiza ngumi yake juu ya meza akisema kwa sauti kubwa, "Ondoka hapa hivi sasa! Kama hutatoka mara moja nitawaita polisi!" Baada ya kumaliza kuzungumza, mara moja alitoa simu yake ya mkono na akaanza kupiga simu nambari 110. Nilijaribu kwa haraka kutengeneza mambo, nikisema, "Rafiki yangu, nina hakika kuwa kwa kweli hutawaita polisi, ni lazima una unacheza." Hata hivyo, aliendelea kuwa mkaidi na akasisitiza kuwa niondoke mara moja. Nilipigwa na bumbuazi kabisa na sikujua cha kufanya tena. Kuangalia saa yangu niliona kuwa ilikuwa karibu saa nne usiku, kama ningeondoka sasa ningelala wapi? Wakati huo huo, mwenyeji wangu akasema, "Kumechelewa tayari, unaweza kuondoka kesho." Mara tu mwana wa mwenyeji alipoona kwamba nilikuwa napanga kulala, aliongeza juhudi zake, akinisukuma hasa nje ya mlango, na wakati wa mchakato huo akisema kwa sauti kubwa, "Ningewezaje, ofisa wa serikali na mfadhiliwa wa fedha za umma, kumruhusu mmisionari nyumbani kwangu? Ondoka hapa sasa!" Kwa hayo, kwa ghadhabu akaiinua baiskeli yangu na kunitupia na kisha akanisukuma mimi na baiskeli yangu hadi nje ya mlango. Mwenyeji wangu alinifuata kwa nia ya kunipeleka kwa nyumba ya familia nyingine mwenyeji, lakini mwanawe hangemruhusu, akimvuruta kumrudisha nyuma ndani na kuufunga mlango. Nilipokuwa nikienda, nikasikia mwenyeji huyo akilia, "Unatarajia msichana kwenda wapi usiku mkuu akiwa peke yake?" "Mwache aende anakokwenda—akiwa na ulinzi wa Mungu hana kitu cha kuogopa sio?" Alisema kwa sauti kubwa kwa kujibu, akimrudisha mwenyeji nyuma hadi ndani.
Nikitumbulia macho nyota zilizopepesa za anga ya usiku bila kuonyesha hisia na taa za mbele za magari zilizomulika kwenye barabara kuu, nilihisi huzuni na kuwa na moyo mzito. Malalamiko yalidondoka kutoka moyoni mwangu: Kama hutaki niishi nyumbani kwako basi ni sawa, lakini hakuna sababu ya kumzuia mwenyeji wangu anipeleke kwa familia nyingine mwenyeji. Unawezaje kuwa mkatili jinsi hiyo, muovu mno! Hata mwombaji hastahili kutendewa kwa njia hii! Sijui ambapo familia nyingine mwenyeji ilipo na nimekwama bila mahali pa kwenda usiku wa manane. Napaswa kufanya nini? … Mawazo haya yakiwa yanagongagonga kichwani mwangu, machozi yalikuja machoni mwangu. Wakati huo, picha angavu niliyokuwa nayo ya uzuri wa mwana wa mwenyeji, maarifa, hadhi na elimu na adabu njema zilifutwa kabisa. Nilifikiria kifungu kinachofuata cha neno la Mungu: “Watu wazuri wako wapi siku hizi? Bila mfano wa kibinadamu, unawezaje kuitwa mtu? Watu wema hawapo. Watu wana magamba ya kibinadamu tu kwa nje na hawana kiini cha binadamu. Kusema kuwa watu ni wanyama kwa mavazi ya binadamu si kutia chumvi” (“Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilifikiria kuhusu ushirika wa mwanadamu ambamo mlisemwa, "Tunawezaje kuwaita wale wanaompinga au kumtesa Mungu watu wema kwa hakika? Tangu mwanadamu alipopotoshwa na Shetani, amekuwa mtaalam wa kujificha na kujifunika kwa falsafa ya maisha. Kwa nje, yeye huonekana kama mtu, lakini wakati mtu anapoanza kumshuhudia Mungu, asili yake ya pepo mbaya huwa inafichuliwa. Sio watu wengi huelewa jambo hili, kwa hivyo mara nyingi hupofushwa na kudanganywa na mambo ya kawaida mno na mambo madogo madogo ya wengine. Maneno na kazi za Mungu zinaweza kumfichua mwanadamu vizuri mno. Wale ambao hawana ukweli ni wanafiki tu. Wale ambao huelewa ukweli wataona kwa dhahiri kuhusu suala hili. Wale ambao hawauelewi ukweli hawawezi kuona chochote kwa dhahiri na matokeo yake ni kuwa mitazamo yao ni ya upuuzi" ("Mabadiliko ya Msingi Katika Mitazamo Ni Ishara ya Kuuelewa Ukweli Kwa Hakika" katika Kumbukumbu za Ushirika na Mipango ya Kazi (I)). Nikitafakari maneno haya, nilikuwa na ufahamu wa haraka. Kweli, Mungu alisema kwa hakika hakuna watu wazuri katika ulimwengu wa kidunia: Hili ni kweli kabisa. Kwa kuwa ni Mungu pekee anayeweza kubaini asilii ya kweli ya mwanadamu. Mungu hufichua asili halisi ya ubinadamu. Mimi, hata hivyo, sikuamini neno la Mungu, sikuwaona wengine kulingana na neno la Mungu, bali nilitumia mawazo yangu mwenyewe na maoni ya kidunia kuwapima wengine. Daima nilidhani kuwa wale walio na maarifa, hadhi na elimu na adabu njema walikuwa wema kila wakati, wenye razini na ufahamu wa wengine. Mtazamo wangu ulikuwa wa upuuzi zaidi. Sikujua hata kidogo, kwamba wale ambao hawamwamini Mungu ni mapepo ambao humpinga Mungu. Kwa nje wanaweza kuonekana wastaarabu na wa kuchangamsha, lakini kwa ndani wao ni waovu kwa kina na wakatili. Mtazamo wa ofisa huyu wa serikali kuhusu imani na waumini ulikuwa mfano kamili. Kwa juu, alikuwa na uzuri, umbuji, na hali ya maendeleo ya maarifa, lakini mara tu nilipoleta masuala ya imani, alishindwa kudhibiti mihemko yake kabisa. Kwa kunishutumu, kunifukuza na kunitisha, alifichua kabisa asili yake ya kishetani. Kama nimekabiliwa na ukweli huu, nilitambua kwamba hakuna watu wema miongoni mwa wanadamu waliopotoshwa. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu tu, kukubali kuadibiwa na hukumu za Mungu na hivyo kufanikisha mabadiliko katika tabia, kupata ubinadamu wa kawaida, busara, na kujifunza kumwabudu na kumtii Mungu kwa hakika mtu anapoweza kuwa mwanadamu wa kweli. Kama mtu anakosa ukweli, bila kujali ana maarifa kiasi gani, hadhi, uzuri au elimu na adabu njema aliyo nayo, yeye bado ni pepo moyoni.

Kupitia uzoefu huu, nilitambua kuwa sikuwa nikiwaona watu walikuwa ni akina nani kwa kweli, lakini badala yake nikitegemeza kupima kwangu kwa sura yao. Jinsi nilivyosikitisha, jinsi nilivyokuwa mjinga. Ilifunuliwa kuwa licha ya kumfuata Mungu kwa miaka mingi, bado sikuelewa ukweli na kwa hakika bado sikuwa nimemiliki ukweli. Kwa kuwa, ni wale walio na ukweli pekee wanaoweza kutofautisha watu na kuona asili halisi ya hali; wale ambao hawaelewi ukweli hawawezi kuona asili ya kweli ya chochote. Katika siku zijazo nimeapa kujitolea kutafuta kuuelewa ukweli na kuumiliki ukweli, kujifunza jinsi ya kutofautisha watu na hali kwa njia ya neno la Mungu, kurekebisha maoni yangu yote ya upuuzi na kufuatilia kuwa mtu ambaye analingana na Mungu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1 

Sikiliza zaidi:Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni