1/05/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kwanza

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Tamko La Kwanza

Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli. Ni jinsi gani tena ambayo mtu yeyote angenielewa Mimi? Ni nani anaweza kuelewa uadhama Wangu, ghadhabu Yangu, na hekima Yangu kupitia kwa maneno Yangu? Nitakamilisha Nilichoanza, lakini bado ni Mimi nipimaye mioyo ya wanadamu. Kwa kweli, hakuna mwanadamu anayenielewa Mimi kwa ukamilifu, kwa hiyo Ninamwongoza kwa maneno, na kumwongoza katika mwongo mpya kwa njia hii.

1/03/2018

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha | Nitampenda Mungu Milele

Nyimbo, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki


Wimbo wa Uzoefu wa Maisha | Nitampenda Mungu Milele

  I
 Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.Lakini Hujawahi kuniacha.

1/02/2018

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Kwa nini Mungu Huchukua Jina la Mwenyezi Mungu Katika Enzi ya Ufalme?

Watu wengi hawaelewi ni kwa nini, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu katika siku za mwisho, Bwana Yesu anaitwa Mwenyezi Mungu wakati Anapokuja kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Kwa nini haendelei kuitwa Bwana Yesu? Kwa kweli, Mungu ana jina jipya kila wakati Anapofanya hatua moja ya kazi Yake. Jina hili jipya linachukuliwa na Mungu Mwenyewe kama inavyofaa kazi hii–siyo kitu ambacho watu humuita Yeye kama wanavyotaka.

1/01/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ulikuwa hata umeshaamuliwa kabla zaidi Nilipoiumba dunia. Watu hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho, na pia hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini Nilikuwa Nimeshamwambia adui Yangu lilipokuwa linapambana na Mimi kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kwa muda mrefu walikuwa watoto wa Shetani, na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

12/31/2017

Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (4)

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Biblia
maandiko ya Biblia,neno la mungu

                           Umeme wa Mashariki | Kuhusu Biblia (4)

Biblia inaandika masuala ya Israeli na matendo ya watu wake wateule wakati huo. Kwa maneno mengine, ni maelezo ya masuala ya Yehova, ambayo kwayo Roho Mtakatifu hatoi lawama. Ingawa kulikuwa na uteuzi wa sehemu za kujumuisha au kuondolewa, ingawa Roho Mtakatifu hathibitishi, bado Hatoi lawama. Biblia si kitu chochote zaidi ya historia ya Israeli na kazi ya Mungu. Watu, masuala, na mambo inayoyarekodi yote yalikuwa ya kweli, na hakuna kitu kuhusu hayo kilikuwa ni ishara ya maisha ya baadaye—mbali na unabii wa Isaya na Danieli, au kitabu cha Yohana cha maono. Watu wa awali wa Israeli walikuwa wenye maarifa na watu wenye utamaduni wa hali ya juu, na maarifa yao ya kale na utamaduni ulikuwa wa kiwango cha juu, na hivyo kile walichoandika kilikuwa cha kiwango cha juu kuliko watu wa leo.

12/30/2017

Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?

kumwamini Mungu,makusudi ya Mungu
Mwenyezi Mungu alisema, Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa.

12/29/2017

Wimbo wa Uzoefu wa Maisha | Nimeuona uzuri wa Mungu



Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wimbo wa Uzoefu wa Maisha Nimeuona uzuri wa Mungu

 I
Nasikia sauti ijulikanayo ikiniita mara kwa mara.
Nikaamka na kuangalia kuona,
ni nani aliye pale akizungumza.
Sauti yake ni nyororo lakini kali,
picha Yake nzuri!
Nateseka kupigwa na kuvumilia maumivu makubwa,
nikipapaswa na mkono Wake wenye upendo.
Halafu natambua ni Mwenyezi ambaye nilipigana naye.

12/28/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu,Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
maneno ya Mungu,Kazi ya Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu,Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

3. Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu
(Ayu 1:6-11) Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao. BWANA akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Ndipo Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha BWANA bure? Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.

12/27/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa
ukamilifu,kukamilishwa na Mungu,watu wa Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi.

12/26/2017

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Yesu,Umeme wa Mashariki
Kumjua Yesu,kumpenda Yesu

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Mwenyezi Mungu alisema, Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. Katika kipindi hiki cha muda, hakuwahi kupata kumjua Yesu, lakini alikuwa radhi kumfuata kutokana na kuvutiwa na Yeye tu.

12/25/2017

Mungu ni upendo | “Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu” | Best Swahili Worship Gospel Songs


Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu

Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote, 
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde; 
jua linaaangaza kotekote.
wakiishi katika mwanga wa Mungu, 
wakiwa na amani na kila mmoja.
Dunia ni ya mbingu, mbingu inaungana na dunia.

12/24/2017

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Kazi ya Mungu,kumjua Mungu

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu?

12/23/2017

33 Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Yesu
Tabia ya Mungu,Yesu
Mwenyezi Mungu alisema,Watu wanaweza kupangwa kwa makundi, ambayo hubainishwa kwa roho zao. Watu wengine wana roho za binadamu, na wao huchaguliwa kwa njia iliyoamuliwa kabla. Ndani ya roho ya binadamu kuna sehemu iliyoamuliwa kabla. Watu wengine hawana roho; wao ni pepo ambao wamepenyeza.Hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu. Ingawa wamekuja ndani, hawawezi kuokolewa, na hatimaye wataondolewa na pepo. Inaamuliwa na asili ya ndani ya mtu huyo iwapo ataikubali kazi ya Mungu, au njia ipi atakayochukua au iwapo ataweza kubadilika baada ya kuikubali. Watu wengine hawana la kufanya ila kupotea. Roho zao huamua kwamba wao ni aina hii ya kitu; hawawezi kubadilika. Kuna watu ambao Roho Mtakatifu hukoma kufanya kazi kwa sababu watu hawa hawajachagua njia sahihi. Wakirudi Roho Mtakatifu huenda bado akafanya kazi Yake, lakini wakishikilia kutorudi basi wamemalizika kabisa.