10/12/2017

Kutafuta Mapenzi ya Mungu na Kuuweka Ukweli Katika Vitendo Kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Iwezekanavyo

Punde tu watu wanapokuwa na haraka wakati wakiutumiza wajibu wao, hawajui jinsi ya kuuzoea; punde tu wanaposhughulika na mambo, hali yao ya kiroho inakuwa na matatizo; hawawezi kudumisha hali yao ya kawaida. Inawezekanaje kuwa hivi? Unapoombwa kufanya kazi kidogo, haufuati ukawaida, unakosa mipaka, husogei karibu na Mungu na unajitenga mbali na Mungu. Hili linadhibitisha kwamba watu hawajui jinsi ya kuwa na uzoefu. Haidhuru nini ufanyacho, unapaswa kwanza kuelewa halisi kwa nini unalifanya hili na asili ya jambo hili ni lipi. Ikiwa imepangwa kama kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe? Hili ni jambo ambalo kwalo unapaswa kusogea karibu na Mungu. Kusogea karibu na Mungu ni kutafuta ukweli katika jambo hili, ni kutafuta jinsi ya kutenda, ni kutafuta mapenzi ya Mungu, na ni kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Hizi ndizo njia za kusogea karibu na Mungu unapofanya vitu; sio kufanya sherehe za kidini au tendo lionekanalo kwa nje; inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kufauta mapenzi ya Mungu. Ikiwa daima unasema “Asante Mungu, asante Mungu” wakati hufanyi chochote, lakini unapofanya kitu, bado unafanya kulingana na mapenzi yako, aina hii ya asante ni tendo la kuonekana kwa nje. Unapotimiza wajibu wako au kushughulikia kitu, unapaswa daima kufikiri: Ninapaswaje kutimiza wajibu huu? Kusudi la Mungu ni lipi? Katika mambo, unasogea karibu na Mungu, na katika kusogea karibu na Mungu, unazitafuta kanuni na kweli za kufanya vitu, unatafuta mapenzi ya Mungu kutoka ndani na humwachi Mungu kwa yote uyatendayo. Huyu ni mtu anayemwamini Mungu kwa kweli. Sasa wakati mambo mengine yajapo kwa watu, bila kujali hali yao halisi ilvyo, wanafikiri kwamba wanaweza kufanya hili na ile, lakini Mungu hayupo mioyoni mwao, na wanafanya haya kulingana na nia zao. Bila kujali jinsi jambo linavyokwenda inafaa au la, au kwamba inalingana na ukweli au la, wanafanya shingo zao kuwa ngumu tu na kutenda kulingana na nia zao binafsi. Kwa kawaida inaonekana kwamba Mungu yupo mioyoni mwao, lakini wafanyapo vitu, Mungu hayupo mioyoni mwao. Watu wengine husema: “Siwezi kukua karibu na Mungu katika vitu nivitendavyo; zamani nilizoea kufanya sherehe za kidini, na nilijaribu kusogea karibu na Mungu, lakini ilikuwa bure; sikuweza kusogea karibu na Yeye.” Mtu wa aina hii hana Mungu ndani yake, ana yeye binafsi tu moyoni mwake na hawezi tu kuuweka ukweli katika matendo kwa vitu afanyavyo. Kutofanya vitu kulingana na ukweli ni kufanya vitu kulingana na mapenzi yako, na kufanya vitu chini ya mapenzi yako ni kumwacha Mungu; yaani Mungu hayupo ndani ya moyo wako. Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu na yanaonekana kama hayakiuki ukweli kwa kiasi kikubwa. Watu wanahisi kwamba kufanya kwa jinsi hii ni kuweka kweli katika matendo, wanahisi kwamba kufanya kwa jinsi hii ni kumtii Mungu. Kwa kweli, watu hawamtafuti Mungu hakika na kumwomba Mungu kuhusu hili. Hawajitahidi kufanya vizuri kuridhisha mapenzi ya Mungu wala hawajitahidi kufanya vizuri kulingana na mahitaji Yake. Hawana hali hii ya kweli, na hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika matendo yao, kwa sababu unamwamini Mungu, lakini Mungu hayupo moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Huku sio kujidanganya mwenyewe vipi? Ni athari gani kuamini jinsi hii kutakuwa nayo? Uko wapi umuhimu wa matendo ya kumwamini Mungu?
Mungu hakuridhishwa kabisa na kitu ulichokitenda hasa; ungetafakari kwa ndani ufanyapo kitu hiki: Jambo hili Mungu Atalitazamaje ikiwa litaletwa mbele Yake? Je Mungu atafurahi au atakerwa Akijua kuhusu jambo hili? Je Mungu atalichukia? Hukulitafuta, sivyo? Hata kama watu wangekukumbusha, bado ungefikiria kwamba jambo hili halina uzito mkubwa na kwamba halikukiuka kanuni na kwamba haiukuwa dhambi. Matokeo yake, uliharibu na kumfanya Mungu kuwa na hasira kuu kufikia hatua ya kukudharau. Waza juu ya mambo ili usije ukavijutia; hili ndio lazima uzingatie. Kama ungetafuta na kuchunguza mambo kikamilifu kabla ya kutenda, basi usingekuwa na utawala juu ya mambo? Ingawa wakati mwingine hali za watu si nzuri, wakikagua kwa makini na kutafuta kila kitu kinachohitajika kufanywa mbele ya Mungu, basi hakutakuwa na makosa yoyote makubwa. Ni vigumu kwa watu kuepuka makosa wanapouweka ukweli katika matendo. Ikiwa unajua jinsi ya kufanya vitu kulingana na ukweli unapovifanya, laikini hauvifanyi kulingana na ukweli, basi shida ni kwamba hauupendi kweli. Mtu amabye hapendi ukweli hatabadilika katika tabia. Ikiwa huwezi kufahamu mapenzi ya Mungu kwa usahihi na hujui jinsi ya kutenda, basi unapaswa kuwasiliana na wengine. Ikiwa hakuna anayehisi kwamba anaweza kuyaona mambo kwa uwazi, basi unapaswa kutoa suluhu la kuwajibika mno; lakini hatimaye unapogundua kwamba kuna kosa kufanya jinsi hii, basi unapaswa kuirekebisha haraka, na Mungu hatahesabu kosa hilo kama dhambi. Kwa sababu dhamira yako ilikuwa njema wakati wa kutenda mambo haya, na ulikuwa unatenda kulinga na kweli ila tu haukuiona kwa wazi, na kukawa na makosa kiasi katika vitendo vyako; hili ni jambo la kupunguziwa ukubwa wa kosa. Hata ivyo, kwa sasa watu wengi wanategemea mikono yao miwili tu kufanya kazi na kutegemea akili zao kufanya hili na lile na mara chache hutafakari: Je, kutenda jinsi hii kunalingana na mapenzi ya Mungu? Je, Mungu atafurahi nikifanya jinsi hii? Je, Mungu ataniamini nikifanya jinsi hii? Je nitakuwa nikiuweka ukweli katika matendo nikitenda jinsi hii? Ikiwa Mungu atasikia hili, je Atasema “Jambo hili limefanywa kwa usahihi na kwa kufaa! Hongera!”? Je, unaweza kuchunguza kila kitu kwa umakini kama hivi? Je, unaweza kuwa mwangalifu sana kwa kila kitu? Au unapaswa kutafakari ikiwa Mungu anadharau jinsi unavyo fanya, jinsi yeyote yule anavyo hisi kuhusu jinsi unavyo fanya, kama unafanya chini ya mapenzi yako, au kuridhisha hamu yako…. Itakubidi kufikiria zaidi kuhusu hilo, uliza maswali mengi na utafute zaidi, na makosa yatakuwa madogo zaidi na zaidi. Kufanya vitu kwa njia hii kunathibitisha kwamba wewe ni mtu anayetafuta ukweli kwa dhati na kwamba wewe ni mtu anayemheshimu Mungu sana, kwa sababu unafanya vitu kulingana na mwelekeo uhitajikao na ukweli.
Ikiwa matendo ya mtu yanaachana na ukweli, basi yeye ni sawa na asiyeamini. Huyu ni aina ya mtu ambaye hana Mungu ndani ya moyo wake, ambaye anamwacha Mungu, na aina ya mtu huyu ni kama mfanyikazi aliyeajiriwa katika familia ya Mungu anayemfanyia bwana wake kazi na kupokea fidia kidogo, na kisha anaenda. Huyu sio mtu anaye mwamini Mungu. Haikuwa imetajwa awali, “Utafanya nini kupata idhini kutoka kwa Mungu”? Hili limezungumziwa, sivyo? Idhini kutoka kwa Mungu ni jambo la kwanza unalopaswa kufikiria kuhusu na kulifanyia kazi; inapaswa kuwa kanuni na wigo katika matendo yako. Sababu ikupasayo kuamua ikiwa kile unachokitenda kinalingana na ukweli ni kwamba kikilingana na ukweli, basi ni hakika kinalingana na mapenzi ya Mungu. Si kwamba unapaswa kuamua kama jambo ni sahihi au kosa, au kama linalingana na kile watu wote wanachopenda, au ikiwa kinalingana na tamaa zako mwenyewe. Badala yake, ni ya kuamua ikiwa inalingana na ukweli, ikiwa inafaidi kazi na masalahi ya kanisa. Ukizingatia vipengele hivi, basi utakuwa zaidi na zaidi sawa na mapenzi ya Mungu unapofanya vitu. Kama huzingatii vipengele hivi na kutegemea mapenzi yako tu kufanya vitu, basi una uhakikisho kuvifanya kimakosa, kwa sababu mapenzi ya mwanadamu sio ukweli na bila shaka hayakubaliani na Mungu. Ukitaka kupewa idhini na Mungu, basi ni lazima utende kulingana na ukweli, badala ya kulingana na nia zako mwenyewe. Watu wengine hufanya vitu vya kijanja bila ya ufahamu wa watu au kufanya mambo ya faragha. Baada ya kumaliza, akina ndugu na dada wanasema kwamba vitu walivyovifanya vinaonekana havifai kwa kiasi fulani, lakini hawatavitambua kwa njia hii. Wanafikiri kwamba hili ni jambo la kibinafsi na halihusu kazi ya kanisa, halihusu fedha za kanisa, na halihusu watu kanisani, kwa hivyo halihesabiki kama kukiuka wigo la ukweli na Mungu hapaswi kuingilia kati jambo hili. Vitu vingine vinaonekana kwako kama ni mambo ya faragha na hayahusu kanuni yoyote ile wala kweli. Hata hivyo, kutokana na mtazamo wa akina ndugu na dada, unapofanya kitu hiki, unaonekana kwamba unakuwa na ubinafsi sana na kwamba hufikirii kuhusu kazi ya familia ya Mungu na jinsi itakavyoathiri familia ya Mungu na kwamba unafikiria tu faida yako mwenyewe. Hii tayari inahusisha utaratibu wa watakatifu na inahusisha maswala ya asili ya binadamu. Unachofanya hakihusu maslahi ya kanisa na hakihusu ukweli, lakini unachokifanya kinakiuka maadili ya asili ya binadamu na hatimaye, hakilingani na kweli. Haidhuru unachokifanya, haidhuru jambo ni kubwa kiasi gani, na bila kujali kama unatimiza wajibu wako katika familia ya Mungu, au kama ni jambo lako la kibinafsi, lazima ufikirie kama jambo hili linalingana na mapenzi ya Mungu, kama jambo hili ni kitu ambacho mtu ambaye ana ubinadamu anapaswa kufanya, na kama kile unachokifanya kitamfanya Mungu awe na furaha. Unahitaji kufikiria kuhusu vitu hivi. Utakapofanya hivi, basi wewe ni mtu anayetafuta ukweli na mtu ambaye anamwamini Mungu kwa kweli. Ukishughulikia kwa moyo wote kila jambo na kila kweli kwa jinsi hii, basi utaweza kubadilisha tabia yako. Watu wengine wanafikiri ya kwamba wanafanya kitu cha kibinafsi, kwa hivyo wanaupuuza ukweli, wakifikiria: Hili ni jambo la faragha, na nitalifanya nitakavyo. Wanalifanya kwa njia yoyote ile inayowafanya wawe na furaha, na kwa njia yoyote ile iliyo na faida kwao; hawafikirii hata kidogo zaidi jinsi itakavyoathiri familia ya Mungu na hawafikirii kama inalingana na mpango wa watakatifu. Hatimaye, wanapomaliza jambo hili, wana giza ndani yao na wana wasiwasi; wana wasiwasi lakini hawajui ilifanyikaje. Je hii sio adhabu iwafaayo? Ukifanya vitu ambavyo havijaidhinishwa na Mungu basi umemkosea Mungu. Ikiwa watu hawaupendi ukweli, na mara nyingi wanafanya vitu kulingana na mapenzi yao, basi watamkosea Mungu mara kwa mara. Aina hii ya mtu kwa kawaida hapewi idhini na Mungu kwa yale ayatendayo na ikiwa hatageuka, basi hatakuwa mbali na adhabu.
Kujua zaidi : Kanisa la Mwenyezi Mungu | Umeme wa Mashariki
Baadhi ya Makala : Yesu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni