11/10/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (2)

                                          Fumbo la Kupata Mwili (2)

Mwenyezi Mungu alisema, Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi. Ingawa kwa Mungu yote ni wazi, yote yanakuwa wazi na yote yanaachiliwa, haya tu ni ya ukweli kwa wale wanaomwamini, na hakuna kitu kinachofanywa kujulikana kwa wale wasioamini Kazi inayofanywa hapa imetengwa kwa ushurutisho ili kuwazuia wasijue. Wakipata kujua, kinachowangojea ni shutuma na mateso. Hawataamini. Kufanya kazi katika taifa la joka kuu jekundu, mahali palipo nyuma zaidi, sio kazi rahisi. Kama kazi hii ingewekwa wazi na kujulikana, basi ingekuwa vigumu kuendelea. Hatua hii ya kazi haiwezi kuendelea katika sehemu hii. Wangestahimili vipi kama kazi hii ingeendelezwa kwa uwazi? Hii haingeleta hata hatari kubwa zaidi? Kama kazi hii haingefichwa, na badala Yake kuendelea kama wakati wa Yesu Alivyowaponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa njia ya kustaajabisha, basi si ingekuwa tayari ïmeshanyakuliwa” na ibilisi? Je, wangestahimili uwepo wa Mungu? Kama sasa ningeingia kwenye kumbi kuwahadhiria wanadamu, je, si ningekuwa nimeshapasuliwa katika vipande kitambo? Na ikiwa hivyo, kazi Yangu itawezaje kuendelea kufanyika? Sababu ambayo ishara na miujiza haitendeki wazi wazi ni kwa ajili ya kujificha. Kwa hivyo kazi Yangu haiwezi kuonekana, kujulikana wala kugunduliwa na wasioamini. Iwapo hatua hii ya Kazi ingefanyika kwa njia sawa na kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, haingekuwa thabiti sana. Kwa hivyo, kazi hii kufichwa namna hii ni ya manufaa kwenu na kwa kazi yote. Wakati kazi ya Mungu duniani inafika kikomo, kumaanisha, wakati kazi hii katika siri inakamilika, hatua hii ya kazi italipuka na kuwa wazi. Watu wote watajua kwamba kuna kundi la washindi ndani ya taifa la Uchina; kila mwanadamu atafahamu kuwa Mungu katika mwili yuko Uchina na kwamba kazi Yake imefika kikomo. Hapo tu ndipo kutampambazukia mwanadamu: Ni kwa nini taifa la Uchina halijaonyesha kudhoofika wala kuporomoka? Inaonekana kuwa Mungu anaendeleza kazi Yake binafsi katika taifa la China na amefanya kuwa kamilifu kundi la watu na kuwafanya washindi.
Mungu mwenye mwili Anajidhihirisha mwenyewe kwa watu kadhaa wanaomfuata Anapofanya kazi Yeye binafsi, na sio kwa viumbe wote. Alijifanya mwili ili Akamilishe hatua ya kazi Yake, na sio ili amwonyeshe mwanadamu mfano Wake. Hata hivyo, kazi Yake lazima ifanywe na Yeye binafsi, kwa hivyo inalazimu Afanye kazi hiyo katika mwili. Kazi hii inapokamilika, Ataondoka duniani; Hawezi kusalia duniani kwa muda mrefu kwa hofu ya kuzuia kazi inayokuja. Anachokionyesha kwa halaiki ni tabia Yake ya haki na matendo Yake yote, na sio umbo la mwili Wake wakati Amejifanya mwili mara mbili, kwa maana mfano wa Mungu unaweza tu kuonyeshwa kupitia kwa tabia Yake, na si kubadilishwa na mfano wa mwili Wake wa nyama. Mfano wa mwili Wake wa nyama huonyeshwa kwa watu wachache tu, kwa wale wanaomfuata Anapofanya kazi katika mwili. Hiyo ndio maana kazi inayofanywa wakati huu inafanywa kwa siri. Ni kama tu vile Yesu alivyojionyeshwa kwa Wayahudi pekee yao Alipofanya kazi Yake, na hakujionyesha hadharani kwa mataifa mengine. Hivyo, pindi Alipomaliza kazi Yake, Aliondoka miongoni mwa wanadamu na hakukawia; kwa wakati uliofuata Hakujionyesha kwa nafsi Yake kwa mwanadamu, bali kazi iliendeshwa moja kwa moja na Roho Mtakatifu. Mara tu kazi ya Mungu katika mwili inapokamilika, Anaondoka katika dunia ya mwanadamu, na kamwe Hafanyi tena kazi sawa na ile Aliyofanya Akiwa katika mwili. Kazi inayofuata hufanywa na Roho Mtakatifu moja kwa moja. Wakati huu, mwanadamu hawezi kuona mfano Wa Mungu katika mwili; Yeye Hajionyeshi wazi kwa mwanadamu hata kidogo, na daima Anabaki mafichoni. Muda wa kazi ya Mungu mwenye mwili ni mchache, ambayo lazima ifanywe katika Enzi bayana, muda, taifa na kati ya watu bayana. Kazi kama hiyo inawakilisha tu kazi ya wakati wa Mungu katika mwili, na inalenga enzi fulani, ikiwakilisha kazi ya Roho wa Mungu katika enzi moja hasa, na sio ujumla wa kazi Yake. Kwa hivyo, umbo la Mungu mwenye mwili halitaonyeshwa kwa kila mwanadamu. Kinachoonyeshwa kwa halaiki ni uhaki wa Mungu na tabia Yake kwa ukamilifu, na wala sio mfano Wake Alipokuwa mwili mara mbili. Sio sura inayoonyeshwa kwa mwanadamu, wala mifano yote miwili ikijumlishwa. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba mwili wa Mungu uondoke duniani baada ya kukamilisha kazi Anayohitajika kufanya, kwa kuwa Anakuja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanaya, na sio kuwaonyesha wanadamu mfano wa umbo Lake. Ingawa umuhimu wa kuingia katika mwili umeshatimizwa na Mungu mara mbili Akijifanya mwili na nyama, bado hatajionyesha wazi kwa taifa ambalo halijawahi kumwona mbeleni. Yesu hatajionyesha Mwenyewe kamwe mara nyingine kwa Wayahudi kama Jua la haki, wala Hataupanda Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa watu wote: yote ambayo Wayahudi huona ni taswira Yake wakati wa kipindi Chake katika Uyahudi. Hili ni kwa sababu kazi ya Yesu aliyepata mwili iliisha kitambo sana miaka elfu mbili iliyopita; Hatarudi Uyahudi katika sura Yake ya awali, sembuse kuionyesha sura Yake ya wakati huo katika nchi yoyote ya Mataifa, kwani sura ya Yesu aliyepata mwili ni sura ya Myahudi tu, na siyo sura ya Mwana wa Adamu ambayo Yohana alikuwa ameiona. Ingawa Yesu aliwaahidi wafuasi Wake kwamba Angerudi tena, Hatajionyesha tu Mwenyewe katika sura ya Myahudi kwa wote walio katika nchi za Mataifa. Mnapaswa kujua kwamba kazi ya Mungu katika mwili inafaa kufungua enzi mpya. Kazi hii ni ya muda wa miaka michache tu, na Hawezi kukamilisha kazi yote ya Roho wa Mungu. Hii ni sawia na vile umbo la Yesu kama Myahudi linaweza tu kuwakilisha mfano wa Mungu alivyofanya kazi katika Yudea, na Angefanya tu kazi ya msalabani. Wakati ambao Yesu Alikuwa katika mwili, Hangefanya kazi ya kutamatisha enzi au kumwangamiza mwanadamu. Kwa hivyo, baada ya kusulubiwa na kukamilisha kazi Yake, Alipaa juu na daima Akajificha kutoka kwa mwanadamu. Kutoka wakati huo kuendelea, wale waumini wa mataifa waliweza tu kuiona picha Yake ambayo walibandika kwenye kuta zao, na sio udhihirisho wa Bwana Yesu. Picha hii imechorwa na mwanadamu tu, na si mfano ambao Mungu Mwenyewe Alimwonyesha mwanadamu. Mungu Hatajionyesha kwa halaiki wazi wazi katika mfano ambao Yeye Alikuwa nao mara mbili Akiwa katika mwili. Kazi Anayofanya miongoni mwa wanadamu ni kuwaruhusu kuelewa tabia Yake. Haya yote yanafanyika kwa kumpitisha mwanadamu katika kazi za enzi tofauti, na vile vile tabia ambazo Ameziweka wazi na kazi ambayo Amefanya, na bali si kupitia kwa udhihirisho wa Yesu. Hiyo ni kusema, umbo la Mungu halionyeshwi kwa mwanadamu kupitia katika mfano wa Mungu mwenye mwili, lakini ni kwa kupitia katika kazi iliyotekelezwa na Mungu mwenye mwili wa sura na umbo; na kupitia katika kazi Yake, mfano Wake unaonekana na tabia Yake inajulikana. Huu ndio umuhimu wa kazi Angependa kufanya katika mwili.
Wakati kazi ya Alipokuwa mwili mara mbili inakamilika, Anaanza kuonyesha tabia Yake ya haki katika mataifa, Akiruhusu halaiki ione mfano wa umbo Lake. Anapenda kudhihirisha tabia Yake, na kupitia katika hili Aweke wazi tamati za aina tofauti ya wanadamu, hapo kuifikisha mwishokabisa enzi nzee. Kazi Yake katika mwili haitendeki katika sehemu pana (kama vile Yesu Alivyofanya kazi katika sehemu ya Yuda peke Yake, na leo hii Ninafanya kazi miongoni mwenu pekee) kwa sababu kazi Yake katika mwili ina mipaka na kingo. Anafanya tu kazi ya muda mchache katika mfano wa kawaida na mwili wa kawaida, badala ya kufanya kazi ya milele kupitia kwa Mungu mwenye mwili, ama kufanya kazi ya kuwaonekania watu wote wa mataifa. Kazi hii katika mwili lazima izuiliwe katika mawanda (kama vile kufanya kazi katika Yuda ama kati Yenu), kisha kupanua kazi iliyofanyika katika mipaka hii. Bila shaka, kazi ya upanuzi huu huendeshwa na Roho Mtakatifu moja kwa moja na haiwezi kuwa kazi ya mwili Wake wa nyama. Kwa maana kazi katika mwili iko na mipaka na haiwezi kuenea katika pembe zote za ulimwengu. Hauwezi kuyatekeleza haya. Kupitia kwa kazi katika mwili, Roho Wake hutekeleza kazi inayofuatia. Kwa hivyo, kazi inayofanywa katika mwili ni ya utayarisho inayotekelezwa ndani ya mipaka; Roho Wake kisha Anaendeleza kazi hii, na kuipanua.
Mungu huja tu katika dunia hii kufanya kazi ya kuongoza enzi; kufungua enzi mpya na kutamatisha enzi ya zamani. Hajakuja kuishi kulingana na maisha ya mwanadamu wa kawaida kwa kikamilifu, kupitia Mwenyewe raha na machungu ya maisha kama mwanadamu, au kumfanya mtu fulani mkamilifu kwa mkono Wake au kumtazama binafsi mtu Fulani anavyokua. Hii sio kazi Yake; kazi Yake ni kufunua tu enzi mpya na kutamatisha enzi iliyotangulia. Hiyo ina maana, Atafungua enzi mpya, akamilishe iliyotangulia, amshinde shetani kwa kufanya kazi Yake Yeye binafsi. Kila mara Anapotekeleza kazi Yeye Mwenyewe, ni kana kwamba Anakanyaga mguu wake katika uwanja wa vita Katika mwili, kwanza Anaishinda dunia kisha Anatawala juu ya Shetani; Anachukua utukufu wote na kufungua pazia kwa kazi ya enzi yote elfu mbili, na kuwapa binadamu wote duniani njia ya kweli ya kufuata, na maisha ya amani na furaha. Hata hivyo, Mungu Hawezi kuishi na mwanadamu duniani kwa muda mrefu, kwa maana Mungu ni Mungu, ni si kama mwanadamu kamwe. Hawezi kuishi urefu wa maisha ya mwanadamu wa kawaida, hiyo ina maana, Hawezi kuishi duniani kama mwanadamu ambaye si wa kawaida, kwa maana Yuko na sehemu ndogo ya uanadamu wa kawaida wa wanadamu wa kawaida kumuwezesha kuishi vile. Kwa maneno mengine, Mungu Anawezaje kuanzisha familia na kukuza watoto duniani? Je, si hii itakuwa ni aibu? Yeye anao uanadamu wa kawaida tu kwa minajili ya kutekeleza kazi Yake kwa njia ya kawaida, na sio kumwezesha Yeye kuanzisha familia kama mwanadamu wa kawaida. Hisia Zake za kawaida, mawazo ya kawaida, na kula kwa kawaida na mavazi ya mwili Wake yanatosha kuthibitsha kuwa Yuko na uanadamu wa kawaida; Hakuna haja Yake kuanzisha familia ndio athibitishe kwamba Yeye kweli yuko na uanadamu wa kawaida. Hiyo haina maana hata kidogo! Mungu Anakuja duniani, kumaanisha Neno linageuka kuwa mwili; Kwa urahisi Anamruhusu mwanadamu kulielewa neno Lake na kuliona neno Lake, hiyo ni, kumruhusu mwanadamu kuona kazi inayotekelezwa na mwili. Nia Yake sio kwamba wanadamu wanadamu wauchukue mwili Wake kwa njia Fulani, bali kwamba mwanadamu awe mtiifu mpaka mwisho, kumaanisha, aweze kutii maneno yote yanayotoka katika kinywa Chake, na kunyenyekea na kukubali kazi yote Anayofanya. Yeye Anafanya kazi katika mwili tu, sio kumfanya mwanadamu kwa kujua aabudu ukuu na utukufu wa mwili Wake. Anamwonyesha tu mwanadamu hekima ya kazi Yake na mamlaka yote Aliyo nayo. Kwa hivyo, ingawa Anao uanadamu wa kipekee, Hafanyi matangazo yoyote, na Anatilia tu maanani kazi ambayo Anapaswa kufanya. Mnapaswa kujua ni kwa nini Mungu Alijifanya mwili ilhali hajigambi wala kushuhudia juu ya uanadamau Wake wa kawaida, na badala Yake Anatekeleza tu kazi ambayo Angependa kufanya. Hii ndio sababu mnaona tu uwepo wa uungu katika Mungu mwenye mwili, kwa sababu Hatangazi kuwa Kwake katika mwili ndio mwanadamu aige. Wakati tu mwanadamu anamwongoza mwanadamu ndipo anapozungumzia kuhusu kuwa wa uanadamu, ili apate uongozi wa watu wengine kupitia kuwafurahisha na kuwashawishi. Kinyume na hilo, Mungu huwashinda watu kupitia katika kazi Yake pekee (hiyo ni, kazi isiyoweza kufanywa na mwanadamu). Hamshawishi mwanadamu au kuwafanya wanadamu wote wamwabudu, bali Anaweka tu katika mwanadamu hisia za uchaji Kwake au kumfanya mwanadamu aweze kujua kuhusu kutowezekana kwa kumchunguza Yeye. Hakuna haja ya Mungu kumpendeza mwanadamu. Kile anachohitaji ni kuwa wewe umheshimu na kumwabudu mara tu unaposhuhudia tabia Yake. Kazi ambayo Mungu hufanya ni Yake mwenyewe; haiwezi kufanywa na mwanadamu badala Yake, wala kuweza kutimizwa na mwanadamu. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye Anaweza kufanya kazi Yake mwenyewe na kuanzisha enzi mpya ili kumwongoza mwanadamu katika maisha mapya. Kazi ambayo Yeye hufanya ni kumwezesha mwanadamu kupokea maisha mapya na kuingia katika enzi mpya. Kazi nyingine yote hupokezwa kwa wale wanadamu wa ubinadamu wa kawaida na ambao wanapendwa na wengine. Kwa hivyo, katika Enzi ya Neema, Alimaliza kazi ya miaka elfu mbili katika miaka mitatu na nusu pekee wakati wa miaka Yake thelathini na mitatu ndani ya mwili. Wakati ambapo Mungu aliyekuja duniani hutekeleza kazi Yake, Yeye kila mara hukamilisha kazi ya miaka elfu mbili au ya enzi nzima katika miaka michache tu mifupi. Yeye hapotezi wakati, na Hachelewi; Yeye hufupisha tu kazi ya miaka mingi ili ikamilishwe katika miaka michache tu mifupi. Hili ni kwa sababu kazi ambayo Yeye hufanya Mwenyewe ni kuifungua tu njia mpya na kuiongoza enzi mpya.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Kujua zaidi : Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni