1/30/2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku–yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ni mada nyingine ambayo tutaijadili leo, ambayo pia inahusiana na matendo ya Mungu. Vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja na ya kimafundisho ya "Mungu," ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na miti taratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kupitia uzoefu wa msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu pia wanaanza kuvuna aina zote za vitu kwa sababu ya msimu wa majani kupukutika kuzalisha viumbe vyote hivi, ili kuandaa chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka masimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi--mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anawaongoza viumbe na binadamu kwa kutumia sheria hizi na Ameanzisha maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, Akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Binadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Haijalishi ni mabadiliko makubwa kiasi gani yanatokea duniani, sheria hizi zinaendelea kuwepo na zipo kwa sababu Mungu yupo. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia viumbe na mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.

1. Mungu Anaweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote

Leo nitazungumza juu ya mada ya jinsi aina ya kanuni hizi ambazo Mungu anazileta kwa binadamu na viumbe vyote humlea binadamu. Kwa hiyo mada hii ni nini? Ni jinsi ambavyo aina hii ya sheria ambazo Mungu amezileta kwa viumbe vyote humlea binadamu. Hii ni mada kubwa, kwa hiyo tunaweza kuigawanya katika sehemu kadhaa na kuzijadili moja baada ya nyingine ili ziweze kufafanuliwa vizuri kwenu. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwenu kupata maana na taratibu mnaweza kuielewa.Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji–haya yote ni nini? Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, je, hiyo inamaanisha nini? Ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote pia Aliamua mawanda ya jangwa, vilevile mawanda ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo–pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba–vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema "mipaka"? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo utawala wa Mungu kwa vitu vyote unavyoanzisha sheria kwa viumbe vyote. Kwa mfano, mawanda na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hii haibadiliki: Hii "isiyobadilika" ni kanuni ya Mungu. Kwamaeneo ya tambarare, mawanda yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima–hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiogarafia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani–hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu, ndani ya kanuni Yake. Hiyo ni sawa na kusema, viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu katikati ya binadamu vina sehemu zao, maeneo yao, na mawanda yao yasiyobadilika. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. "Kiholela" inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na kimo au eneo lake halitabadilika kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake–haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiogorafia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya–yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu–yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Viumbe vyote hivi–vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinapumua kupitia pua zao na vile ambavyo havipumui—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.
Mmeona nini kutokana na kile ambacho nimekizungumzia? Ni kwamba sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana–muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo viumbe vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng'ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Kutiririka kwa mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji na kwa mahitaji ya viumbe vyote. Vyovyote vile yanavyotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali. Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hiki ndicho tutakachokwenda kuzungumzia baadaye.
Pili, ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Licha ya kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha nini? Maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Kwa hiyo, ndege na wanyama wana makazi yao yasiyobadilika na hawatazungukazunguka mahali popote tu. Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, mpangilio huu utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? (Binadamu.) Ni binadamu! Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakizungukazunguka tu jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana. Hii ni kwa sababu mazingira ambamo tembo wanaishi ni msitu, na msitu ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Ana mazingira yake kwa ajili ya kuendelea kuishi na ana makazi yake yasiyobadilika, sasa kwa nini atangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba na duma wakizungukazunguka baharini? Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa kutoka baharini wakitembea jangwani? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini na hawawezi kuishi kwenye nchi kavu. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna mtu yeyote aliyewahi kumwona ng'ombe au kondoo msituni? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? Kama mlishawahi kuona, basi haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Hii ndio sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo ni matukio ya pekee machoni mwenu. Ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu–haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au vina pumzi na vinaweza kutembea–vyote vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyosimamia viumbe vyote. Ni kumwandalia binadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya viumbe vyote kila kimoja kina chakula kinachokimu maisha ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi; vimejifunga katika mazingira hayo. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, viumbe vyote vinaingiliana na binadamu kwa upatanifu, na binadamu na viumbe vyote vinategemeana.
Mungu aliviumba viumbe vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao na miongoni mwao akalea aina zote za viumbe hai. Huku viumbe vyote vikiwa vinalea aina zote za viumbe hai, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Ni vyanzo gani vingine vya vyakula ambavyo binadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa:
Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua kuhusu hilo. Je, wowote kati yenu wanawinda kwa ajili ya kuishi? Nyinyi nyote ni watu wa kisasa—hamjui jinsi ya kuwinda, jinsi ya kushika bunduki. Vyanzo vyenu vya chakula vinatoka ardhini. Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. "Windo" ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangefurahi endapo wangepata paa. "Vizuri, paa huyu anatosha kwa chakula kwa ajili ya familia kwa siku kadhaa." Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. "Kwa sasa kuna kitu cha kula; hatuna haja ya kuogopa kuwa na njaa." Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Ni mazingira ya aina gani ambayo mara nyingi watu wanaoishi kwa kutegemea uwindaji wanaishi? Wanaishi katika misitu ya milima. Kwa kiasi kikubwa hawalimi au kupanda mazao; wanaishi katika misitu ya milima. Je, kuna ardhi inayolimika katika misitu ya milima? Sio rahisi kupata ardhi inayolimika, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.
Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi hawalimi, sasa wanafanya nini? Wanafuga tu? Ikiwa yeyote miongoni mwenu hapa ni mtu wa Mongolia, mnaweza kuzungumza kidogo kuhusu mtindo wenu wa maisha ya kuhamahama. (Kwa sehemu kubwa, tunafuga ng'ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, hatulimi, na msimu wa baridi tunawachinja na kuwala mifugo wetu. Chakula chetu kikuu kinatokana na nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, tunakunywa chai ya maziwa, tunakula mchele uliokaushwa, na mbogamboga chache sana. Sasa aina zote za usafiri hazina usumbufu na tuna aina zote za mbogamboga na nafaka. Wamongolia hunywa chai ya maziwa, na Watibeti hunywa chai ya siagi. Ingawa wafugaji wanatingwa misimu yote minne, lakini wanakula vizuri. Hawapungukiwi na maziwa, bidhaa za maziwa, au nyama. Walikuwa wanaishi katika viduku lakini sasa wote wanajenga nyumba.) Chakula cha msingi cha watu wa Mongolia ni kula nyama ya ng’ome na nyama ya kondoo, kunywa maziwa, na kuendesha farasi kuenda kulisha wanyama wao. Huu ni mtindo wa maisha wa mfugaji. Mtindo wa maisha wa mfugaji sio mbaya–wanaendesha madume ya ng'ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao, na hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wote wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!
Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Aina hii ya watu hufanya uvuvi kwa ajili ya kuishi. Watu hawa wanaofanya uvuvi kwa ajili ya kuishi hutegemea nini kwa ajili ya chakula? Chanzo cha chakula chao ni nini? Ni aina zote za samaki na vyakula vya baharini? Wakati Hong Kong ilikuwa ni kijiji kidogo tu cha uvuvi, watu ambao waliishi pale waliweza kuvua kwa ajili ya kuishi. Hawakulima–walikwenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kilikuwa ni aina mbalimbali za samaki, nyama, na vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kuuza kiasi cha samaki kwa kubadilishana na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Watu wanaoishi kwa kutegemea uvuvi wote wanaishi pembezoni mwa bahari, na baadhi wanaishi kwenye mashua. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi pembezoni mwa maji. Wale wanaoishi pembezoni mwa maji wanategemea uvuvi; ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.
Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wale ambao wanategemea kulima kwa ajili ya kupata riziki zao kimsingi wanapanda mazao kwa vizazi. Wanapata chakula chao kutoka ardhini. Ama wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wote wanapata mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.
Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao. Aina ya mbari hiyo ingeelekea upande gani; aina ya watu hao wangeelekea wapi? Uwezo wa kuendelea kuishi au la ni kiwango kisichojulikana na wangeweza tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao–wanategemea uwanda wa mbuga. Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo wao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi–uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng'ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama wangekuwa na riziki gani? Wasingekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Mara tu tatizo linapotokea na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi–zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, matokeo yake yangekuwa nini? Wasingeweza kupanda vitu, wasingeweza kupata vyakula vyao kutoka katika mimea. Matokeo yake yangekuwa ni nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali ya kiikolojia. Ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira–ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.
Ikiwa viumbe vyote vingepoteza sheria zao, visingeishi tena; ikiwa sheria za viumbe vyote zingekuwa zimepotea, basi viumbe hai miongoni mwa viumbe vyote visingeweza kuendelea. Binadamu pia wangepoteza mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo wanayategemea kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ikiwa binadamu wamepoteza hiyo yote, wasingewea kuendelea kuishi na kuongezeka kizazi baada ya kizazi. Sababu ya binadamu kuendelea kuishi mpaka sasa ni kwa sababu Mungu amewapatia binadamu viumbe vyote kuwalea, kuwalea binadamu kwa namna tofauti. Ni kwa sababu tu Mungu anawalea binadamu kwa namna tofauti ndio maana wameendelea kuishi mpaka sasa, kwamba wameendelea kuishi hadi siku ya leo. Kwa aina hiyo ya mazingira yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni ya kufaa na yapo katika mpangilio, aina zote za watu duniani, aina zote za jamii zinaweza kuishi ndani ya mawanda yao husika. Hakuna anayeweza kwenda zaidi ya mawanda haya au mipaka hii kwa sababu ni Mungu ambaye ameichora. Kwa nini Mungu aichore kwa namna hii? Hii ni muhimu sana kwa binadamu wote–ni muhimu sana! Mungu alichora mawanda ya kila aina ya kiumbe hai na aliweka mbinu ya kuendelea kuishi kwa kila aina ya binadamu. Pia aligawanya aina mbalimbali za watu na jamii mbalimbali duniani na akaweka mawanda yao. Hiki ndicho tunachotaka kujadili wakati ujao.
Nne, Mungu alichora mipaka kati ya jamii za rangi tofautitofauti. Duniani kuna watu weupe, watu weusi, watu wa kahawia na watu wa njano. Hawa ni aina tofuati za watu. Mungu pia aliweka mawanda kwa ajili ya maisha ya aina hizi tofauti za watu, na bila kutambua, watu wanaishi ndani ya mazingira yao stahiki kwa kuendelea kuishi chini ya usimamizi wa Mungu. Hakuna anayeweza kwenda nje ya hapa. Kwa mfano, jamii ya watu weupe–yaani, wazungu–ni maeneo gani ambayo wanaishi kwa kiasi kikubwa? Kwa kiasi kikubwa wanaishi Ulaya na nchi za Marekani. Watu weusi kimsingi wanaishi Afrika. Na watu wa rangi ya kahawia wanaishi ndani ya eneo gani? Kimsingi ni Asia ya Kusinimashariki kama vile Thailand, India, Myanmar, Vietnam na Laos. Yaani ukanda wa Asia ya Kusinimashariki. Watu wa njano kimsingi wanaishi Asia, yaani, China, Japan, Korea ya Kusini na nchi nyinginezo kama hizo. Mungu amegawanya aina hizi tofautitofauti za jamii kwa usawa kiasi kwamba jamii hizi tofautitofauti zimegawanywa katika sehemu tofautitofauti za dunia. Katika sehemu tofautitofauti hizi za dunia, Mungu aliandaa zamani sana mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yanayofaa kwa ajili ya kila jamii tofauti ya binadamu. Ndani ya aina hizi za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi, Mungu amewaandalia rangi na vijenzi vya udongo. Vijenzi katika miili ya watu weupe na miili ya watu weusi havifanani, na pia ni tofauti na vijenzi vya miili ya watu wa rangi nyinginezo. Mungu alipoumba viumbe vyote, tayari Alikuwa ameandaa mazingira ya namna hiyo kwa ajili ya kuendelea kuishi. Lengo Lake katika hili lilikuwa kwamba pale ambapo aina hiyo ya watu inaanza kuongezeka, watakapoanza kuongezeka kwa idadi, wangeweza kuwekwa ndani ya mawanda hayo. Kabla Mungu hajawaumba binadamu alikuwa amekwishatafakari yote–Angeweza kutoa eneo fulani kwa watu weupe na kuwaruhusu kuliendeleza na kuendelea kuishi. Kwa hiyo Mungu alipokuwa anatengeneza dunia tayari Alikuwa na mpango, alikuwa na nia na kusudi katika kile alichokuwa anakiweka katika kipande hicho cha ardhi, na kile ambacho kingelelewa katika kipande hicho cha ardhi. Kwa mfano, Mungu zamani sana aliandaa mlima upi, tambarare ngapi, vyanzo vya maji vingapi, ni aina gani ya ndege na wanyama, samaki gani, na mimea gani ingeweza kuwepo katika ardhi hiyo. Alipokuwa anaandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina ya binadamu, kwa ajili ya jamii, Mungu aliangalia vipengele vingi vya masuala: mazingira ya kijiografia, vijenzi vya udongo, aina ya ndege na wanyama, ukubwa wa aina tofautitofauti za samaki, vijenzi katika samaki, ubora tofauti wa maji, vilevile aina tofauti za mimea... Mungu alikuwa ameandaa yote hayo zamani sana. Aina hiyo ya mazingira ni mazingira ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaumba na kuyaandaa kwa ajili ya watu weupe.
Mnapaswa kuweza kuona kwamba Mungu alipoviumba viumbe vyote, Alitafakari sana. Alifanya vitu kwa mpango. Sasa mnaweza kuona hilo, sio? (Fikira za Mungu kwa aina mbalimbali za watu zilikuwa ni za uangalifu sana. Kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa ajili ya aina tofautitofauti za binadamu, aliandaa aina za ndege na wanyama na aina za samaki, milima mingapi na tambarare ngapi zitakuwepo. Yote haya yalifikiriwa kwa uangalifu sana na kwa usahihi.) Kwa mfano, chakula wanachokula wazungu hasa ni kipi? (Kwa kiasi kikubwa ni vyakula vyenye kiwango cha juu cha protini–aina tofautitofauti za nyama, bidhaa za maziwa, na vyakula vinavyotokana na ngano.) Vyakula ambavyo watu weupe wanakula ni tofauti sana na vyakula ambavyo watu wa Asia wanakula. Vyakula vikuu ambavyo watu weupe wanakula hasa ni nyama, mayai, maziwa, na kuku. Nafaka kama vile mkate na mchele kwa ujumla sio chakula kikuu ambacho kinawekwa pembeni mwa sahani. Hata pale wanapokula kachumbari, ambayo imetengenezwa na mbogamboga, wanaweka kiasi cha nyama ya kukaanga au kuku ndani yake. Hata kama wanakula vyakula vinavyotokana na ngano, wanaongeza siagi, mayai, au nyama kwenye chakula hicho. Hiyo ni kusema, vyakula vyao vikuu havijumuishi hasa vyakula vinavyotokana na ngano au mchele; wanakula sana nyama na siagi. Mara nyingi wanakunywa maji ya barafu kwa sababu wanakula vyakula vyenye kalori ya juu sana. Wanapokula chakula, kabla chakula hakijawekwa mezani kila mtu anakunywa maji ya barafu kwanza, kwa hiyo watu weupe ni wenye afya kweli. Hivi ndivyo vyanzo vya maisha yao, mazingira yao kwa ajili ya kuishi yaliandaliwa na Mungu kwa ajili yao, yanawafanya wawe na aina hiyo ya mtindo wa maisha. Mtindo huo wa maisha ni tofuti na mitindo ya maisha ya watu wa rangi nyingine. Hakuna baya au zuri katika mtindo huu wa maisha–ni wa kuzaliwa, uliamuliwa kabla na Mungu na kwa sababu ya kanuni ya Mungu na mipangilio Yake. Aina hii ya mbari ina mtindo fulani wa maisha na vyanzo fulani vya riziki zao kitu ambacho ni kwa sababu ya mbari yao, vilevile ni kwa sababu ya mazingira kwa ajili ya kuendealea kuishi yaliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yao. Mngeweza kusema kwamba mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili ya watu weupe na chakula cha kila siku wanachokipata kutoka katika mazingira hayo ni kingi na kimejaa tele.
Mungu pia aliandaa mazingira faafu kwa ajili ya mbari nyingine kuendelea kuishi. Pia kuna watu weusi–watu weusi wanapatikana wapi? Hasa wanapatikana katikati na kusini mwa Afrika. Mungu aliwaandalia nini kwa ajili ya kuishi katika aina hiyo ya mazingira? Misitu ya kitropiki, aina zote za ndege na wanyama, pia majangwa, na aina zote za mimea ambayo inaambatana nao. Wana vyanzo vya maji, riziki zao, na chakula. Mungu hakuwabagua. Bila kujali kile walichowahi kukifanya, kuendelea kuishi kwao hakujawahi kuwa tatizo. Pia wanachukua mahali fulani maalumu na eneo fulani katika sehemu ya dunia.
Sasa, hebu tuzungumze kidogo kuhusu watu wanjano. Watu wa njano hasa wanapatikana nchi za Mashariki. Kuna tofauti gani kati ya mazingira na sehemu za kijiografia za nchi za Mashariki na nchi za Magharibi? Katika nchi za Mashariki, eneo kubwa la ardhi ni la rutuba, na zina hazina kubwa ya vitu na madini. Yaani, aina zote za rasilimali za juu ya ardhi na za chini ya ardhi zimejaa tele. Na kwa kundi hili la watu, kwa mbari hii, Mungu pia aliandaa udongo, hali ya hewa inayofanana nao, na mazingira mbalimbali ya kijiografia ambayo yanawafaa. Ingwa kuna tofauti kubwa kati ya mazingira hayo ya kijiografia na mazingira ya nchi za Magharibi, chakula cha lazima cha watu, riziki, na vyanzo kwa ajili ya kuendelea kuishi viliandaliwa na Mungu. Ni mazingira tofauti tu kwa ajili ya kuishi kuliko yale ambayo watu weupe wanayo katika nchi za Magharibi. Lakini kitu kimoja ni kipi ambacho Ninahitaji kuvuta usikivu wenu, ambacho Ninahitaji kuwaambia? Idadi ya mbari ya Mashariki kiasi fulani ni kubwa, hivyo Mungu aliongeza vipengele vingi katika kipande hicho cha nchi ambavyo ni tofauti na vya Magharibi. Katika upande huo wa dunia, Aliongeza mandhari mengi mbalimbali na aina zote za vitu vingi. Huko rasilimali za asili ni tele; mandhari pia yanatofautiana na anuwai, yanatosha kwa ajili ya kulea idadi kubwa ya mbari ya Mashariki. Kitu fulani ambacho ni tofauti na Magharibi ni kwamba Mashariki–kutoka kusini kwenda kaskazini, kutoka mashariki kwenda magharibi–hali ya hewa ni nzuri kuliko ya Magharibi. Misimu minne imeoneshwa kinaganaga, hali ya joto ni nzuri, rasilimali za asili zipo tele, mazingira ya asili na aina za mandhari ni mazuri zaidi kuliko ya Magharibi. Kwa nini Mungu alifanya hivi? Mungu alitengeneza uwiano razini kabisa kati ya watu weupe na watu wa njano. Hii inamaanisha nini? Kila kipengele ambacho watu weupe wanaweza kukifurahia ni kizuri zaidi kuliko kile ambacho watu wa njano wanaweza kukifurahia. Chakula chao na vitu ambavyo wanatumia ni bora zaidi. Hata hivyo, Mungu habagui mbari yoyote. Mungu aliwapatia watu wa njano mazingira mazuri na bora zaidi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hii ni uwiano. Kwa hiyo sasa mnaelewa, sio?
Mungu ameamua kabla ni aina gani ya watu waishi katika sehemu ipi ya dunia na binadamu hawawezi kwenda nje ya mawanda haya. Hili ni jambo la ajabu! Hata kama kuna vita au uvamizi katika enzi mbalimbali au nyakati fulani, vita hivi, uvamizi huu, hakika hauwezi kuharibu mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyaamua kabla kwa ajili ya kila mbari. Yaani, Mungu amewaweka aina fulani ya watu katika eneo fulani la dunia na hawawezi kwenda nje ya mawanda hayo. Hata kama watu wana lengo la kubadilisha au kuongeza eneo lao, bila ruhusa ya Mungu, hii itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Itakuwa vigumu sana kufanikiwa. Kwa mfano, watu weupe walitaka kuongeza maeneo yao na wakazitawala kwa mabavu baadhi ya nchi. Wajerumani walivamia baadhi ya nchi, Uingerza waliitwaa India. Matokeo yalikuwa ni nini? Mwishowe walishindwa. Tunaona nini kutokana na kushindwa huku? Kile ambacho Mungu amekiamua kabla hakiwezi kuharibiwa. Kwa hiyo, haijalishi ni nguvu kubwa kiasi gani ambayo umeweza kuiona katika upanuzi wa Uingereza, mwishowe matokeo ni kwamba bado walitakiwa kuondoka na ardhi hiyo bado ni ya India. Wale ambao wanaishi katika ardhi hiyo bado ni Wahindi, na si Waingereza. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho Mungu haruhusu. Baadhi ya wale ambao wanatafiti historia au siasa wametoa tasnifu juu ya hili. Wanatoa sababu kwa nini Uingereza ilishindwa, wanasema kwamba pengine ilikuwa ni kwa sababu mbari fulani isingeweza kushindwa, au pengine ni kwa sababu ya sababu nyinginezo za kibinadamu... Hizi sio sababu za kweli. Sababu ya kweli ni kwa sababu ya Mungu–Haruhusu hilo. Mungu anaamua mbari waishi katika nchi fulani na Anawaweka hapo, na kama Mungu hawaruhusu kuhama hawataweza kuhama kamwe. Ikiwa Mungu ataamua mawanda kwa ajili yao, wataishi ndani ya mawanda hayo. Binadamu hawezi kuvunja bure au kwenda nje ya mawanda haya. Hii ni hakika. Haijalishi nguvu za wavamizi ni kubwa kiasi gani, au jinsi gani wale wanaovamiwa ni dhaifu, mafanikio yao mwishowe yanamtegemea Mungu. Ameshaliamua hili tayari na hakuna anayeweza kulibadilisha. Hivi ndivyo Mungu alivyogawanya mbari mbalimbali. Ni kazi gani ambayo Mungu amefanya kuzigawanya mbari? Kwanza, aliandaa mazingira makubwa ya kijiografia, mazingira makubwa, akatoa maeneo tofautitofauti kwa ajili ya watu, kisha kizazi baada ya kizazi kuendelea kuishi pale. Hii imeamuliwa–mawanda ya kuendelea kuishi kwao yameamuliwa. Na milo yao, maisha yao, kile wanachokula, kile wanachokunywa, riziki zao–Mungu aliamua hayo yote zamani sana. Na Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, Alifanya maandalizi tofautitofauti kwa ajili ya aina tofauti za watu: Kuna vijenzi tofautitofauti vya udongo, hali ya hewa tofauti, mimea tofauti, na mazingira tofauti ya kijiografia. Maeneo tofautitofauti yana hata ndege na wanyama tofauti, maji tofauti yana aina tofauti za samaki na bidhaa za majini, na hata aina ya wadudu inaamuliwa na Mungu. Kwa mfano, kuna magipai (ndege wa jamii ya kunguru) Asia lakini pengine hawapatikani Marekani. Hii ni maalumu sana. Na shorewanda wa Marekani ni tofauti na shorewanda wa China Bara. Vitu ambavyo vinakua katika bara la Marekani vyote ni vikubwa sana, virefu sana na vyenye nguvu sana. Mizizi ya miti msituni yote haina kina kirefu kabisa, lakini inakua mirefu sana. Inaweza kurefuka hadi kufikia zaidi ya futi mia moja, lakini miti katika misitu ya Asia kwa kiasi kikubwa si mirefu kiasi hicho. Nina uhakika wote mmekwishawahi kusikia juu ya mimea ya mshubiri. Japan ni midogo sana, miembamba sana, lakini mimea ya mshubiri Marekeni ni mikubwa sana. Hii ni tofauti. Ni aina ile ile ya mmea ikiwa na jina lile lile, lakini katika bara la Marekani ni mkubwa kiasi–kweli kuna tofauti. Tofauti katika vipengele hivi tofautitofauti zinaweza zisionekane au kufahamika kwa watu, lakini Mungu alipokuwa anaumba viumbe vyote, alivionyesha kinaganaga na aliandaa mazingira tofauti ya kijiografia, mandhari tofauti, na viumbe hai tofauti kwa ajili ya mbari mbalimbali. Kwa sababu Mungu aliumba aina tofautitofauti za watu, Anajua kile ambacho kila mmoja anahitaji na mitindo yao ya maisha ni nini. Kwa hiyo, kile ambacho Mungu aliumba ni chema sana. Sasa mnapaswa kuwa mmeelewa.
Baada ya kuzungumza juu ya baadhi ya vitu hivi, sasa mna uelewa fulani wa mada kuu ambayo tumeijadili hivi punde? Je, mmeielewa kwa kiasi fulani? Kuna sababu ambayo nimeongea kuhusu mambo haya ndani ya mada pana–sasa mnapaswa kuwa mmeelewa angalau kwa muhtasari. Mnaweza kuniambia mmeelewa kwa kiasi gani. (Binadamu wote wamelelewa kwa sheria tu ambazo ziliamuliwa na Mungu kwa ajili ya vitu vyote. Mungu alipokuwa anaamua sheria hizi, Aliandaa mbari tofautitofauti zikiwa na mazingira tofauti, mitindo tofauti ya maisha, vyakula tofauti, na hali ya hewa na halijoto tofauti. Hii ilikuwa hivyo ili binadamu wote waweze kuishi duniani na kuendelea kuishi. Kutokana na hili naweza kuuona mpango wa usimamizi wa Mungu na mipango yake angalifu na sahihi vilevile hekima na ukamilifu Wake.) (Ili kumlea binadamu, Mungu ameamua sheria hizi kwa ajili yetu na Ameandaa mazingira ya kijiografia na vilevile aina tofauti za vyakula. Na ili tuweze kuendelea kuishi ndani ya aina hii ya mazingira Aliandaa sehemu tofauti za kuishi. Kutokana na hili ninaweza kuona kwamba kazi ya Mungu na mipango ipo sahihi sana, na ninaweza kuona upendo Wake kwa sisi binadamu.) Je, kuna mtu yeyote aliye na cha kuongeza? (Sheria na mawanda yaliyoamuliwa na Mungu hayawezi kubadilishwa kabisa na mtu yeyote, tukio, au kitu. Yote ipo chini ya kanuni Yake.) Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu–je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, hawawezi kupata kitu chochote kwa ajili ya kula, pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja. Watu kuendelea kuishi lingekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo na kuongezeka ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Hakiwezi kutenganishwa na wao kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Kwa hiyo usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, na haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kuona waziwazi.
Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, "Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona," na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema "Unachokizungumzia hakinihusu." Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki–huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: "Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo naweza kusema kwamba siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote." Lakini hii si kweli. Na kwa nini sio? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama? Huli mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia–ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: "Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi." Kama nini? Nipatie mfano. Baadhi husema: "Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu." Lakini hii si sahihi. Kwa nini sio? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? (Vilitoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu.) Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu. Kwa hiyo mambo haya tuliyoyajadili leo yanahusiana na mada yetu ya "Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote"? Kwa hiyo, vitu tulivyovijadili leo, vinaangukia chini ya mada hii kubwa? Ni kwa sababu tu ya uhusiano huu ndio maana nimesema yote haya. Pengine baadhi ya ambayo nimeyazungumzia leo ni ya kidhahania kidogo na ni vigumu kidogo kuweza kuyajadili. Hata hivyo, Nadhani kwamba sasa mnaelewa vizuri kidogo.
Nyakati chache hizi katika ushirika, kiwango cha mada ambazo tumekuwa nazo katika ushirika ni kipana sana, na mawanda yao ni mapana, kwa hiyo unapaswa uwe na jitihada kiasi fulani ili uweze kuzielewa zote. Hii ni kwa sababu mada hizi ni vitu ambavyo watu hawajawahi kukabiliana navyo katika imani yao kwa Mungu. Baadhi ya watu wanaisikia kama muujiza na baadhi ya watu wanaisikia kama hadithi–mtazamo gani ni sahihi? Unasikia haya yote kutoka katika mtazamo gani? Umepata nini kutokana na haya yote? Hebu mtu aseme. (Nimetambua kipengele cha mamlaka ya Mungu na pia nimeona heshima Yake, na kutokana na hili pia ninaweza kuona upendo Wake kwa binadamu. Kila kitu Anachokifanya kinajumuisha mipangilio na mipango Yake angalifu na sahihi kwa ajili ya binadamu. Anatupenda sana na kutuhifadhi kwa upendo mkubwa sana kiasi kwamba hata Ametupatia chakula chetu kwa umakini.) (Tumeyaona matendo ya Mungu, vilevile kwa mbinu gani Amepangilia vitu vyote na kwamba vitu vyote vina sheria hizi na kupitia maneno haya tunaweza kuelewa zaidi juu ya matendo ya Mungu na mpangilio wake angalifu na sahihi kwa ajili ya kumwokoa binadamu.) Kupitia nyakati hizi katika ushirika, Mmeona mawanda ya usimamizi wa Mungu wa vitu vyote ni nini? (Binadamu wote, kila kitu.) Je, Mungu ni Mungu wa mbari moja? Je, ni Mungu wa aina moja ya watu? Je, ni Mungu wa eneo dogo la binadamu? (Hapana, hayupo hivyo.) Kwa kuwa Hayupo hivyo, katika maarifa ya watu juu ya Mungu, ikiwa angekuwa ni Mungu wa sehemu ndogo tu ya binadamu, au ikiwa unaamini kwamba Mungu ni Mungu wako tu, je, mtazamo huu upo sahihi? Kwa kuwa Mungu anasimamia na kutawala vitu vyote, watu wanapaswa kuona matendo Yake, hekima Yake, na ukuu Wake ambavyo vimefunuliwa katika utawala Wake wa vitu vyote. Hiki ni kitu ambacho watu wanapaswa kufahamu. Ikiwa unasema kwamba Mungu anasimamia viumbe vyote, na Anatawala binadamu wote, lakini kama huna uelewa wowote au umaizi katika utawala Wake kwa binadamu, je, unaweza kutambua kwamba Anatawala vitu vyote? Unaweza? Unaweza kufikiri moyoni mwako, "Ninaweza, kwa sababu ninaona kwamba maisha yangu haya yote yanatawaliwa na Mungu." Je, kweli Mungu ni mdogo kiasi hicho? Hayupo hivyo! Unaona tu wokovu wa Mungu kwa ajili yako na kazi yake kwako, na kutokana na vitu hivi unauona utawala Wake. Hayo ni mawanda finyu sana, na yana athari katika maarifa yako halisi juu ya Mungu. Pia yanaweka mipaka kwenye maarifa yako halisi juu ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Ikiwa unayawekea mipaka maarifa Yake kwenye mawanda ya kile ambacho Mungu anatoa kwa ajili yako na wokovu Wake kwa ajili yako, hutaweza kutambua kwamba anatawala kila kitu, kwamba anatawala vitu vyote, na anatawala binadamu wote. Unaposhindwa kutambua haya yote, je, kweli unaweza kutambua ukweli kwamba Mungu anatawala majaliwa yako? Huwezi. Moyoni mwako hutaweza kutambua kipengele hicho–hutoweza kutambua kiwango hicho. Unaelewa, siyo? (Ndiyo.) Kwa kweli, Ninajua ni kwa kiwango gani mnaweza kuelewa mada hizi, maudhui haya ninayoyazungumzia, sasa kwa nini Naendelea kuizungumzia? Ni kwa sababu mada hizi ni mambo ambayo yanapaswa kueleweka kwa kila mfuasi wa Mungu, kila mtu ambaye anataka kuokolewa na Mungu–anapaswa kuelewa mada hizi. Ingawa kwa kipindi hiki, kwa kipindi hiki ambacho huzielewi, siku moja, ambapo maisha yako na uzoefu wako wa ukweli utafikia kiwango fulani, pale ambapo mabadiliko yako ya tabia yako ya maisha yanafikia kiwango fulani na kimo chako kinaongezeka kwa kiwango fulani, maneno haya–mada hizi ambazo naziwasilisha kwako katika ushirika–baada ya hapo tu zitakimu na kuridhisha utafutaji wako wa maarifa ya Mungu. Kwa hiyo maneno haya yalikuwa ni kwa ajili ya kuweka msingi, kuwaandaa kwa ajili ya uelewa wenu wa baadaye kwamba Mungu anatawala vitu vyote na kwa ajili ya uelewa wenu wa Mungu Mwenyewe.
Vyovyote vile uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Vyovyote vile kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa hadhi Yake ilivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi Mungu wa kwenye moyo wako pia yupo tupu na ni yule asiye yakini. Ikiwa Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya mawanda yako, basi ni Mungu mdogo kweli–Mungu huyo hajaunganishwa na Mungu wa kweli na wala hahusiani na Yeye. Kwa hiyo, kuyajua matendo halisi ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote–haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya hayatenganishwi na maisha ya kila mtu, na maisha halisi ya kila mtu ya kuutafuta ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba Mungu wako kabisa si Mungu wa kweli. Kabisa si Mungu Mwenyewe wa kweli, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini si Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu ambaye Ninamzungumzia ni yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote. Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaongoza binadamu wote kwa njia ya utawala Wake wa vitu vyote, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Sasa unaelewa yote haya, sio? Lengo Langu ni nini kusema yote haya? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Utapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu. Kwa hiyo, sasa unaelewa?
Lengo Langu la kuzungumza juu ya mambo haya yote ni nini? Lengo langu ni kuwafanya watu wamjue Mungu, kuwafanya watu waelewe matendo halisi ya Mungu. Mara utakapomuelewa Mungu na ukaelewa matendo Yake, ni baada ya hapo tu ndipo utakuwa na fursa au uwezekano wa kumjua Mungu. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwelewa mtu, ni jinsi gani unaweza kumwelewa? Je, inaweza kuwa kupitia kuangalia umbo lao la nje? Je, inaweza kuwa kupitia kile wanachokivaa, jinsi wanavyovaa? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia jinsi wanavyotembea? Je, inaweza kuwa ni kupitia kuangalia mawanda ya maarifa yao? Hakika isingeweza kuwa hivyo. Kwa hiyo unamwelewaje mtu? Unafanya hukumu kupitia mawazo ya mtu, kupitia maneno na tabia zake, kupitia kile anachokionyesha na kile anachokifichua. Hivyo ndivyo unavyomjua mtu, unavyomwelewa mtu. Kwa njia ile ile, ikiwa mnahitaji kumjua Mungu, ikiwa mnataka kuelewa upande Wake wa vitendo, upande Wake wa kweli, mnapaswa kumjua Yeye kupitia matendo Yake na kupitika kila kitu halisi Anachofanya. Hii ndiyo njia bora zaidi na ndiyo njia pekee. Kwa hiyo mnaelewa sasa? Mungu anadhihirisha matendo Yake miongoni mwa vitu vyote na miongoni mwa vitu vyote Anavyovitawala na Anashikilia sheria za vitu vyote. Ni lazima kabisa kwa kumuelewa na kumjua Mungu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni