2/15/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu,
3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea
(Mat 18:12-14) Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi wale tisini na tisa, aende milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? Na iwapo atapata kumwona, amini nawaambieni, anamfurahia huyo kondoo mmoja zaidi, kuliko wale tisini na tisa ambao hawakupotea. Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni, kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.

Hii ni sitiari—unapata hisia gani kutoka katika dondoo hii? Namna ambavyo sitiari hii inaelezwa inatumia mbinu za lugha katika lugha ya binadamu; ni kitu kilicho ndani ya mawanda ya maarifa ya binadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba hakikuambatana na Alichokuwa Mungu , lakini wakati Mwana wa Adamu alivyoonyesha ufahamu huu katika Enzi ya Neema, ilionekana ya kufariji, yenye uzuri, na iliyo karibu kwa watu. Wakati Mungu alipokuwa mwili, wakati Alipoonekana katika umbo la binadamu, Alitumia sitiari inayofaa sana kuonyeshakuonyesha sauti Yake katika binadamu. Sauti hii iliwakilisha sauti binafsi ya Mungu na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mwelekeo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya mwanadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliewalezea au “aliwatafsiria” binadamu lugha Yake ya maana sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuelewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Angeweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuongea na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu wangeweza kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili wangeweza kuuona moyo Wake. Unaona nini katika haya? Kwamba hakuna kuzuiliwa katika maneno na vitendo vya Mungu? Namna watu wanavyoona, hakuna njia ambayo Mungu angetumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia aina hii ya sitiari ili watu wangeweza kuhisi ule uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mwelekeo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha muda. Mfano huu uliwazindua watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhemsha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kuisoma dondoo ya mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kumwokoa mwanadamu na wanaelewa uzito wa mwanadamu katika moyo Wake.
Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika dondoo hii: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Haya yalikuwa maneno binafsi ya Bwana Yesu, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, yaonekana alikuwa Bwana Yesu akiongea, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndio maana Akasema: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Watu wakati huo walimtambua tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na mtu huyu waliyeona mbele ya macho yao alikuwa ametumwa tu na Yeye, na hakuweza kuwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kusema hivyo vilevile, ili waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi ule uhalali na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na ufiche wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika himaya ya kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu wAlichohitaji, Alijua ni nini watu walikuwa na wasiwasi kuhusu, na kile kilichowakanganya, hivyo Akaongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, wakati Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Vivyo hivyo sio mapenzi ya Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini usahihi wao na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba wakati Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano wa kufedhehesha sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu Akifanya kazi katika mwili Alikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili shaka na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na kutochangamka kwao. Yaweza kusemekana kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na mwanadamu, na mchakato wa kupitia mwanadamu akishindana dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kushinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile Alicho nacho na kile Alicho, kupitia kiini Chake binafsi halisi. Haikuwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile Alicho nacho na kile Alicho, na upendo na hekima Yake. Aliweza kupata watu Aliowataka, kushinda utambulisho na hadhi Aliyostahili, na kurudi kwa kiti Chake cha enzi.
Kifuatacho, hebu tuangalie dondoo mbili zifuatazo katika maandiko.
4. Samehe Sabini Mara Saba
(Mat 18:21-22) Kisha Petro akamwendea, na akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi na mimi nimsamehe? Mpaka mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii mpaka mara saba: bali, mpaka sabini mara saba.
5. Upendo wa Bwana
(Mat 22:37-39) Yesu akamwambia, Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri ya kwanza na iliyo kuu. Na ya pili inafanana nayo, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Kati ya dondoo hizi mbili, moja yazungumzia msamaha na nyingine inazungumzia upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.
Wakati Mungu alipokuwa mwili, Alileta pamoja naye hatua ya kazi Yake—Alileta pamoja naye kazi mahususi ya enzi hii na tabia Aliyotaka kuonyesha. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilizungukia kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza ilihusiana yote na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—shabaha Yake ilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuokoa mwanadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu mara kwa mara kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona Yeye kutoka katika mtazamo wa mwelekezi wa kawaida Akiongea na watu, Akiwaruzuku mahitaji yao, Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Aligeuka na kuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kimatendo katika umbo Lake na tabia Yake. Usemi kusamehe watu “sabini mara saba” unafafanua zaidi hoja hii. Kusudio lililotimizwa kupitia kwa nambari katika usemi huu ni kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wa kibinafsi, kitu ambacho lazima wajifunze, na njia ambayo lazima waendeleze. Hata ingawa huu ulikuwa usemi tu, ulikuwa hoja muhimu. Uliwasaidia watu kufahamu kwa kina kile Alichomaanisha na kugundua njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango katika utendaji. Usemi huu uliwasaidia watu kuelewa waziwazi na ukawapa dhana sahihi kwamba wanafaa kujifunza kusamehe—kusamehe bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na ufahamu kwa wengine. Wakati Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu sabini mara saba? Hakuwa akifiki kuhusu hilo. Ipo idadi fulani ambayo Mungu atasamehe binadamu? Kunao watu wengi walio na shauku katika “idadi” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kunauhusisho wa kina zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Uhusisho au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulielezewa kutoka katika himaya ya kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika himaya ya kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na mazungumzo haya yalitokana na, na yakazidi ule upana wa himaya ya kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu kile Alicho na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisia zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.
Hapa chini, hebu tuzungumzie kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka silo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alisema katika ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Kuwapenda wengine ni sawa na kuyatunza maisha yako binafsi,” na watu tu ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya imani, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufichuzi wa kiasili wa kile Alicho nacho na kile Alicho. Ni lini umewahi kumsikia Mungu akisema kitu kama “Nampenda mwanadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Alicho nacho na kile Alicho. Upendo wa Mungu kwa mwanadamu na jinsi Anavyowashughulikia watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani kimakusudi, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kimakusudi ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilielezwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile wAlichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu kwa mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa pingamizi au kizuizi cha mawasiliano na kuingiliana kwa binadamu na Mungu mbinguni tu, bali kwa hakika ilikuwa ndio njia ya pekee na daraja la pekee la mwanadamu kuungana na Bwana wa uumbaji. Wakati huu, huhisi kwamba kunayo mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Awamu ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kueleza tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi binafsi ya Mungu. Punde Mungu anapokuwa mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, wingi wa lugha na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, ndiyo fursa bora zaidi ya wewe kuweza kuona kudura ya ya Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati Alipokuwa Akikua, Alipata kuelewa, kujifunza, na kuelewa baadhi ya maarifa ya mwanadamu, maarifa ya kawaida, lugha, na mbinu za maonyesho katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili alimiliki mambo haya yaliyotokana na binadamu Aliyekuwa ameumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya mwanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Iliiwezesha kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, si jambo la busara zaidi kwa Mungu kufanya kazi kupitia kwa mwili kwa njia hii? Je, hili si hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake akiwa mashinani, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakukuwepo tena na ghuba kati ya Mungu na binadamu, kwamba Mungu angesitisha karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia kwa wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe binafsi angeweza kuonyesha maneno na kazi zote Alizotaka kufanya katika mwili. Hii ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu huokoa walikuwa karibu na Yeye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia eneo jipya, na kwamba ubinadamu mzima ulikuwa karibu kukumbwa na enzi mpya.
Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika wakati Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na Shetani, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, Alikuwa anahisi vipi? Watu wanafaa kuweza kuelewa hilokiasi, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Wakati Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake kukamilisha huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuona na kugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa binadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kulia meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa njia ambayo binadamu walifanya hivyo na hata kupitia kwa macho yao. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Yaweza pia kusemekana kwamba yalikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hii bila shaka ndiyo ambayo Mungu alifurahi zaidi kuihusu. Kuanzia hapo ndiyo mara ya kwanza ambayo Mungu alihisi tulizo fulani katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kimatendo sana na ya asili sana, na tulizo ambalo Mungu alihisi lilikuwa halisi. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusonga karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, aidha, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na mzuri sana; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni habari za maana sana. Wakati Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa wanadamu, ni wakati ambao matokeo ya awamu hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona athari yake ya mwisho na tunda. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu kuridhika, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari meona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amepata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumpa utoshelevu, Mungu anahisi Akiwa ameondolewa shaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anahisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yamefanikishwa, tayari Ameuona mwisho. Na kwa sababu ya mwisho huu Yeye ametosheka, na mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Unaweza kufikiria hayo? Je, Mungu Angeweza kulia? Mungu Anaweza kulia? Mungu Anaweza kupiga makofi? Mungu Anaweza kucheza? Mungu Anaweza kuimba? Na wimbo huo ungekuwa upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao ungeweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuuimbia wanadamu, Kujiimbia mwenyewe, na kuuimba kwa viumbe vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni kawaida kwa sababu Mungu anayo shangwe na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuelezewa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na ndilo jambo la kawaida zaidi. Hufai kufikiria chochote kingine kuhusu hili, na hufai kusingizia vizuizi vyako binafsi kwa Mungu, huku ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki wala kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka shangwe Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia yale tuliyowasiliana nanyi katika nyakati hizi mbili, Ninasadiki hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtaruhusu Mungu kuwa na uhuru na uwachiliaji fulani. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu wakati mnaposikia kwamba Yeye anayo huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli shangwe Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu anayo huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu anayo furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochote na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu na fikira dhana na maarifa ya binadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo imani kama hii? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?
Halafu hebu tusome fahamu zifuatazo.
6. Ibada Mlimani
1) Sifa na Heri (Mt 5:3-12)
2) Chumvi na Nuru (Mt 5:13-16)
3) Sheria (Mt 5:17-20)
4) Kuhusu Hasira (Mt 5:21-26)
5) Kuhusu Uzinzi (Mtt 5:27-30)
6) Kuhusu Talaka (Mt 5:31-32)
7) Kuhusu Viapo (Mt 5:33-37)
8)Kuhusu Kujilipiza Kisasi (Mt 5:38-42)
9) Upendo kwa Adui (Mt 5:43-48)
10) Kuhusu Utoaji Sadaka (Mt 6:1-4)
11) Kuhusu Maombi (Mt 6:5-8)
7. Mifano ya Bwana Yesu
1) Mfano wa Mpanzi (Mt 13:1-9)
2) Mfano wa Magugu katikati ya Ngano (Mt 13:24-30)
3) Mfano wa Punje ya Haradali (Mt 13:31-32)
4) Mfano wa Chachu (Mt 13:33)
5) Mfano wa Magugu Umeelezwa (Mt 13:36-43)
6) Mfano wa Hazina (Mt 13:44)
7) Mfano wa Lulu (Mt 13:45-46)
8) Mfano wa Wavu (Mt 13:47-50)
8. Amri
(Mat 22:37-39) Yesu akamwambia, Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri ya kwanza na iliyo kuu. Na ya pili inafanana nayo, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya matendo haya bado yanafaa leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katikaMungu. Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au akitumia lugha gani, asili yake, na sehemu yake ya kuanzia, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo Ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na upana uliotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndandi ya mawanada haya.
Halafu, hebu tuangalie ni nini kimo katika “Mifano ya Bwana Yesu.”
Mfano wa kwanza ni mfano wa mpanzi. Huu ni mfano wa kusisimua kweli; upanzi wa mbegu ni tukio maarufu sana katika maisha ya watu. Mfano wa pili ni mfano wa magugu. Kulingana na jinsi magugu yalivyo, yeyote aliyepanda mimea na ambaye na watu wazima watajua. Wa tatu ni mfano wa punje ya haradali. Nyinyi nyote mnajua haradali ni nini, sivyo? Kama hujui, unaweza kupekuapekua katika Biblia. Nao mfano wa nne ni mfano wa chachu, watu wengi wanajua kwamba chachu inatumiwa katika kutia chachu; ni kitu ambacho watu wanatumia katika maisha yao ya kila siku. Mifano yote iliyotajwa hapa chini ukiwemo mfano wa sita, mfano wa hazina, mfano wa saba, mfano wa lulu, na wa nane mfano wa wavu; ni mifano iliyotolewa katika maisha ya watu; inatoka katika maisha ya watu halisi. Ni picha aina gani inayoonyeshwa na mifano hii? Ni picha aina gani ambayo mifano hii inatuonyesha? Hii ni picha ya Mungu akigeuka mtu wa kawaida na kuishi pamoja na mwanadamu, Akitumia lugha ya maisha ya kila siku, Akitumia lugha ya mwanadamu ili kuwasiliana na binadamu na kuwapa kile wanachohitaji. Wakati Mungu alikuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa muda mrefu, baada ya kupitia na kushuhudia hali ya maisha mbalimbali ya watu, hali hii Aliyopitia kilikuwa kitabu Chake cha kiada cha kubadilisha lugha Yake ya kiungu kuwa lugha ya binadamu. Bila shaka, mambo haya Aliyoyaona na kuyasikia katika maisha yaliweza pia kumwimarisha Mwana wa Adamu kupitia yale Aliyopitia akiwa binadamu. Wakati Alipotaka watu kuelewa ukweli fulani, ili kuwaelewesha mapenzi ya Mungu, Angetumia mifano inayofanana na ile iliyotajwa hapo juu ili kuwaeleza watu kuhusu mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu. Mifano hii yote ilihusiana na maisha ya watu; hakukuwa na hata mmoja ambao haukuwa na mguso wa maisha ya binadamu. Wakati Bwana Yesu alipoishi na mwanadamu, Aliwaona wakulima wakilima mashamba yao; Alijua magugu yalikuwa nini na kutia chachu kulikuwa nini; Alielewa kwamba binadamu walipenda hazina na hivyo basi Alitumia sitiari za hazina na hata lulu; mara kwa mara Aliwaona wavuvi wakizirusha nyavu zao na kadhalika. Bwana Yesu aliziona shughuli hizi katika maisha ya mwanadamu na pia Alipitia aina hiyo ya maisha. Alikuwa sawa na kila mtu mwingine wa kawaida Akipitia milo mitatu kwa siku ya binadamu na mazoea yale mengine ya kila siku. Aliweza kupitia kibinafsi maisha ya mtu wa kawaida na akashuhudia maisha ya wengine. Aliposhuhudia na kupitia haya yote yeye binafsi, kile Alichofikiria kilikuwa si namna ya kuwa na maisha mazuri au namna ambavyo Angeishi kwa uhuru zaidi au kwa utulivu zaidi. Alipokuwa akipitia maisha halisi ya binadamu Bwana Yesu aliuona ugumu katika maisha ya watu, Aliuona ugumu, ule ufukara, huzuni ya watu waliopotoshwa na Shetani, wakiishi katika utawala wa Shetani na walioishi katika dhambi. Huku akiyapitia maisha ya binadamu Yeye binafsi aliweza pia kushuhudia namna ambavyo watu waliokuwa wakiishi ndani ya upotovu walivyokuwa wasioweza kujisaidia, na Akawaona kupitia ule umaskini wa wale walioishi katika dhambi, wale waliopotea katika mateso ya Shetani, ya mwovu. Wakati Bwana Yesu alipoyaona mambo haya, Aliyaona kwa macho Yake ya kiungu au macho Yake ya kibinadamu? Ubinadamu Wake ulikuwepo kwa kweli—ulikuwepo waziwazi—Angewezea kuyapitia na kuyaona haya yote na bila shaka kiini Chake halisi, uungu Wake uliona vilevile. Yaani, Kristo Mwenyewe, Bwana Yesu, binadamu Aliyaona haya na kila kitu Alichokiona kilimfanya kuhisi umuhimu na haja ya kazi Aliyokuwa Ameamua kuifanya wakati huu akiwa mwili. Hata ingawa Yeye Mweyewe Alijua kwamba jukumu Alilohitaji kushughulikia Akiwa mwili lilikuwa kubwa mno, na namna ambavyo Angepitia maumivu ya kikatili, Alipomwona mwanadamu asiyejiweza ndani ya dhambi, Alipoona umaskini wa maisha yao na mapambano hafifu chini ya sheria, Alihuzunika zaidi na zaidi, na Akawa na hamu kubwa zaidi na zaidi ya kumwokoa binadamu kutoka dhambini. Haijalishi ni aina gani ya ugumu ambao Angepitia au aina gani ya maumivu Angehisi, Alikuwa shupavu zaidi na zaidi katika kuwakomboa wanadamu wanaoishi katika dhambi. Wakati wa mchakato huu, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alianza kuelewa waziwazi kazi Aliyohitajika kufanya na kile Alichokuwa Ameaminiwa kutekeleza. Alikuwa pia mwenye hamu kubwa zaidi ya kukamilisha kazi ambayo Alikuwa Aichukue—kushugulikia dhambi zote za mwanadamu, upatanisho wa Mungu na binadamu ili wasiishi tena katika dhambi naye Mungu Angeweza kusahau dhambi za binadamu kwa sababu ya sadaka ya dhambi, na hivyo basi kumruhusu kuendeleza kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu. Yaweza kusemwa kwamba katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe sadaka. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja. Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake binafsi yangekuwa wala hakufikiria kwa muda wowote zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Mradi tu Alijitoa Mwenyewe, mradi tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetimia na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kutekeleza mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayoingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa kwa akili ya Bwana Yesu wakati huo.
Akiishi katika mwili, Mungu mwenye mwili Alimiliki ubinadamu wa kawaida; Alikuwa na hisia na kule kuwaza kwa mtu wa kawaida. Alijua furaha ilikuwa nini, maumivu yalikuwa nini na Alipowaona wanadamu katika hali hii ya maisha, Alihisi kwa kina kwamba kuwapatia watu kiasi cha mafunzo tu, kuwapatia kitu au kuwafunza kitu kusingewaongoza kutoka katika dhambi. Wala kuwafanya kutii amri pia kusingewakomboa kutoka katika dhambi—pale tu Alipozichukua dhambi za ubinadamu na kuwa mfano wa mwili wenye dhambi ndipo Alipoweza kuibadilisha na uhuru wa mwanadamu na kuibadilisha na msamaha wa Mungu kwa wanadamu. Kwa hivyo baada ya Bwana Yesu kupitia na kushuhudia maisha ya binadamu katika dhambi, kulikuwa na tamanio kuu liliojionyesha katika moyo Wake—kuwaruhusu wanadamu kujiondoa kutoka katika maisha yao ya kupambana na dhambi. Tamanio hili lilimfanya kuhisi zaidi na zaidi kwamba lazima Aende katika msalaba na kuzichukua dhambi za ubinadamu haraka iwezekanavyo, kwa dharura. Hizi ndizo zilizokuwa fikira za Bwana Yesu wakati huo, baada ya Yeye kuishi na watu na kuwaona, kuwasikia, na kuhisi umaskini wa maisha yao ndani ya dhambi. Kwamba Mungu mwenye mwili Angekuwa na nia ya aina hii kwa mwanadamu, kwamba Angeweza kueleza na kufichua tabia ya aina hii—je, hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida angekuwa nalo? Mtu wa kawaida angeona nini akiishi katika aina hii ya mazingira? Angefikiria nini? Kama mtu wa kawaida angekumbwa na haya yote, angeangalia matatizo haya kwa mtazamo wa juu? Bila shaka hapana! Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni toleo tu la ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadha ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu wanadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Wakati watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya mwanadamu na masharti na nadharia za wanadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Wakati Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo. Je, unaona udhirisho na ufichuzi wa Mungu Mwenyewe ndani ya Bwana Yesu? Unaweza kusema kwamba kile ambacho Bwana Yesu Alifanya na kusema kilihusiana na huduma Yake na kazi ya usimamizi ya Mungu binafsi, kwamba yote hayo yalikuwa ni udhihirisho na ufichuzi wa kiini cha Mungu. Ingawa Alikuwa na udhihirisho wa binadamu, kiini Chake cha kiungu na ufichuzi Wake wa kiungu hauwezi kukataliwa. Je, udhihirisho huu wa wanadamu ulikuwa udhihirisho wa kweli wa ubinadamu? Udhihirisho Wake wa ubinadamu ulikuwa, kwa kiini chake, tofauti kabisa na udhihirishaji wa ubinadamu wa watu waliopotoka. Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, na kama Angekuwa kweli mmojawapo wa wale wa kawaida, watu waliopotoka, Angeweza kuyaona maisha ya wanadamu ndani ya dhambi kutoka katika mtazamo wa kiungu? La hasha! Hii ndiyo tofauti kati ya Mwana wa Adamu na watu wa kawaida. Watu wote waliopotoka wanaishi ndani ya dhambi na wakati mtu yeyote anapoiona dhambi, hana hisia zozote kuihusu hiyo dhambi; wako sawa tu, kama vile nguruwe anayeishi kwenye matope na hahisi chochote kamwe kuhusu kutokuwa na utulivu, au uchafu—anakula vizuri na kulala vizuri. Kama mtu anasafisha nyumba ya nguruwe, nguruwe kwa hakika hatahisi utulivu, na hatabakia akiwa msafi. Baada ya muda mfupi tu atakuwa tena akijigaragaza katika matope akiwa mtulivu kabisa, kwa sababu yeye ni kiumbe mchafu. Wakati binadamu wanapomwona nguruwe wanahisi kwamba anao uchafu na ukimsafisha yule nguruwe hahisi vyema zaidi—ndio maana hakuna anayemfuga nguruwe ndani ya nyumba yake. Namna ambavyo wanadamu wanavyomwona nguruwe itakuwa tofauti siku zote na namna ambavyo nguruwe wenyewe wanavyojihisi, kwa sababu wanadamu na nguruwe si wa aina moja. Na kwa sababu Mwana wa Adamu kwa mwili si wa aina moja na wanadamu waliopotoka, Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kusimama kutoka kwa mtazamo wa kiungu, na kusimama kutoka katika kimo cha Mungu ili kuwaona wanadamu, ili kuona kila kitu.
Wakati Mungu anapokuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu, ni mateso yapi Anayopitia katika mwili? Yupo yeyote anayeelewa kwa kweli? Baadhi ya watu husema kwamba Mungu huteseka pakubwa, na ingawa Yeye ni Mungu Mwenyewe, watu hawaelewi kiini Chake na siku zote wanamchukulia Yeye kama mtu, hali ambayo humfanya Yeye kuhisi vibaya na kuona kwamba Amekosewa—wanasema kwamba mateso ya Mungu kwa kweli ni makubwa. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu hana hatia na hana dhambi, lakini Yeye huteseka sawa na wanavyoteseka wanadamu, na Yeye hupitia mateso, matusi, na kuvunjiwa heshima pamoja na wanadamu; wanasema Yeye pia huvumilia kutoelewana na kutotiiwa na wafuasi Wake—kuteseka kwa Mungu kwa kweli hakuwezi kupimwa. Yamkini humwelewi kwa kweli Mungu. Kwa hakika, mateso haya unayoyaongelea hayaonekani kuwa mateso ya kweli kwake Mungu, kwa sababu kunayo mateso makubwa zaidi ya haya. Basi mateso ya kweli kwa Mungu Mwenyewe ni yapi? Mateso ya kweli ya mwili wa Mungu ni yapi? Kwa Mungu, wanadamu kutomwelewa Yeye haihesabiki kuwa ni mateso, na kwa watu kuwa kutokuwa na uelewana fulani wa Mungu na kwa kutomwona Yeye kama Mungu hakuhesabiki kuwa mateso. Hata hivyo, mara nyingi watu huhisi kwamba Mungu lazima alipitia dhuluma kubwa sana, kwamba wakati Mungu yumo katika mwili Hawezi kuionyesha nafsi Yake kwa wanadamu na kuwaruhusu kuuona ukubwa Wake, na Mungu anajificha kwa unyenyekevu katika mwili duni nahivyo basi hali hili lazima lilikuwa la kumpa Yeye maumivu makali. Watu hushikilia moyoni kile wanachoweza kuelewa na kile wanachoweza kuona kuhusu mateso ya Mungu, na kuwekelea aina zote za huruma kwake Mungu na mara nyingi hata wataisifia kidogo hali hiyo. Kwa uhakika, kunayo tofauti, kuna pengo kati ya kile watu wanachoelewa, kile watu wanaelewa kuhusu mateso ya Mungu na kile Anachohisi kwa kweli. Ninakwambia ukweli, kwa Mungu haijalishi kama ni Roho wa Mungu au mwili wa Mungu, mateso hayo si mateso ya kweli. Basi ni nini hasa ambacho kwa kweli Mungu huteseka? Hebu tuzungumze kuhusu mateso ya Mungu kutoka katika mtazamo wa Mungu mwenye mwili pekee.
Wakati Mungu anapokuwa mwili, kuwa mtu wa wastani, mtu wa kawaida akiishi miongoni mwa wanadamu, pamoja na watu, hawezi kuona na kuhisi mbinu za watu, sheria na filosofia zao za kuishi? Ni vipi ambavyo mbinu na sheria hizi zinamfanya Yeye kuhisi? Je, Anahisi kuwa na chuki katika moyo Wake? Kwa nini Ahisi chuki? Mbinu na sheria za kuishi za wanadamu ni gani? Zimekita mizizi katika kanuni gani? Ziko katika misingi ipi? Mbinu, sheria, n.k za kuishi kwa wanadamu,—zote hizi zimeundwa kwa misingi ya mantiki, maarifa na filosofia ya Shetani. Wanadamu wanaoishi chini ya aina hizi za sheria hawana ubinadamu, hawana ukweli—wote wanaukataa ukweli, na ni wakatili kwa Mungu. Tunapoangalia kiini cha Mungu tunaona kwamba kiini Chake ni kinyume kabisa na mantiki, maarifa na filosofia ya Shetani. Kiini Chake kimejaa haki, ukweli, na utakatifu na uhalisia mwingine wa mambo yote mazuri. Mungu, akimiliki kiini hiki na Akiishi miongoni mwa wanadamu—Anahisi vipi katika moyo Wake? Je, haujajaa maumivu? Moyo Wake umo katika maumivu, na maumivu haya ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuelewa wala kutambua. Kwa sababu kila kitu Anachokumbana nacho, kukabiliana nacho, kusikia, kuona na kupitia vyote ni upotovuwa wanadamu, uovu, na uasi wao dhidi ya, na upinzani wa ukweli. Kila kitu kinachotoka kwa wanadamu ndicho chanzo cha mateso Yake. Hivi ni kusema kwa sababu kiini Chake halisi si sawa na wanadamu waliopotoka, kupotoka kwa wanadamu kunakuwa ndiko chanzo cha mateso Yake makuu. Wakati Mungu anapokuwa mwili, Anaweza kupata mtu anayetumia lugha moja na Yeye? Hili haliwezi kupatikana miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayeweza kupatikana anayeweza kuwasiliana, anayeweza kuwa na mabadilishano haya na Mungu—unaweza kusema Mungu anayo hisia aina gani? Yale mambo ambayo watu huzungumza ambayo wanapenda, ambayo wanafuatilia na kutamani yote yanahusu dhambi, na yana mielekeo ya uovu. Wakati Mungu anapokabiliana na haya, haya si kama kisu katika moyo Wake? Akiwa Amekabiliwa na mambo haya, Anaweza kuwa na furaha katika moyo Wake? Anaweza kupata kitulizo? Wale wanaoishi na Yeye ni wandamu waliojaa uasi na uovu, je, moyo Wake utakosaje kuteseka? Mateso haya kwa kweli ni makubwa vipi, na ni nani anayeyajali? Ni nani anayeyasikiliza? Na ni nani anayeweza kuyatambua? Watu hawana njia yoyote ya kuuelewa moyo wa Mungu. Mateso Yake ni kitu ambacho watu hawawezi hasa kutambua, na ubaridi, na kutojua kwa ubinadamu kunayafanya mateso ya Mungu kuwa yenye kina zaidi.
Kunao baadhi ya watu ambao huonea huruma hali ya Kristo kwa sababu kunao mstari katika Biblia unaosema: “Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pahali pa kupumzisha kichwa chake.” Wakati watu wanaposikia haya, wanayatia moyoni na kusadiki kwamba haya ndiyo mateso makubwa zaidi ambayo Mungu huvumilia, na mateso makubwa zaidi ambayo Kristo huvumilia. Sasa, tukiangalia katika mtazamo wa ukweli, hivyo ndivyo ilivyo? Mungu haamini kwamba ugumu huu ni mateso. Hajawahi kulia dhidi ya dhuluma hizi kwa ajili ya ugumu wa mwili, na hajawahi kuwalipizia kisasi wanadamu au Kujitoza na chochote. Hata hivyo, Anaposhuhudia kila kitu cha wanadamu, maisha yaliyopotoka na uovu wa wanadamu waliopotoka, Anaposhuhudia kwamba wanadamu wamo katika ung’amuzi wa Shetani na wamefungwa na Shetani na hawawezi kukwepa, kwamba wanaoishi ndani ya dhambi hawajui ukweli ni nini—Hawezi kuvumilia dhambi hizi zote. Chuki Yake kwa binadamu huongezeka siku baada ya siku, lakini lazima Avumilie yote haya. Haya ni mateso makuu ya Mungu. Mungu hawezi kujieleza kikamilifu hata sauti Yake au hisia Zake miongoni mwa wafuasi Wake, na hakuna yeyote miongoni mwa wafuasi Wake anayeweza kuelewa kwa kweli mateso Yake. Hakuna yule ambaye hujaribu kuyaelewa au kuutuliza moyo Wake—moyo Wake huvumilia mateso haya siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, mara kwa mara. Unaona nini katika yote haya? Mungu hahitaji chochote kutoka kwa wanadamu kama malipo kwa kile Alichokitoa, lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, Hawezi kuvumilia kamwe uovu, upotovu na dhambi ya wanadamu, lakini Anahisi chukizo na chuki kupindukia, hali ambayo husababisha moyo wa Mungu na mwili Wake kuvumilia mateso yasiyoisha. Je, ungeyaona yote haya? Kunao uwezekano, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeyaona kwa sababu hakuna yeyote kati yenu anayeweza kumwelewa Mungu kwa kweli. Baada ya muda mnaweza kuyapitia haya wenyewe kwa utaratibu.
Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.
...
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni