2/17/2018

Sura ya 91. Kupitia Aina Tofauti Za Mazingira Kuna Manufaa Kwa ukuaji Wa Maisha Ya Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wakristo

    Ni vyema kupitia mazingira ya aina tofauti. Mungu hakupangii mazingira haya bila sababu. Yeye hakuongozi popote pale bila makusudi, bali Yeye huandaa mazingira fulani spesheli kwa kila mmoja—mazingira ya kifamilia, mazingira ya kimaisha, mazingira uliyokulia, na mazingira unatekeleza majukumu yako punde utakapo mwamini. Yeye hutayarisha hali au mazingira fulani spesheli kwako wewe kuzipitia. Iwapo umetambua jinsi ya kupata uzoefu katika hali zote, muktadha na mazingira, bila kushindwa hata kwenye mazingira ya kuchukiza zaidi, na iwapo katika mazingira mazuri kabisa na ya kustarehesha kabisa na katika hali za majaribu makubwa kabisa, haupotoshwi au kudanganyika na katu hauanguki, basi utakuwa umepiga hatua na kuzidisha kimo. Je, yote haya yaweza kuchukuliwa kama wokovu? Kwa hakika, bado haujaokolewa. Lakini angalau, mazingira yako hayawezi kushawishi imani yako kwa Mungu au kusadiki kwako kwa Mungu, na unao msingi. Msingi huu unajitokeza vipi? Unajitokeza kwa kuelewa ukweli fulani. Unaupokea ukweli fulani katika miaka hii yote, unapata kufahamu ukweli halisi wa maneno haya yaliyonenwa na Mungu, na unapata kufahamu mapenzi mema ya Mungu katika kutawala Kwake hatima ya mtu na katika tendo Lake la kumpangia mtu nyakati mwaka kwa mwaka—unaweza kufahamu mambo haya kwa kiasi fulani. Katika kina cha moyo wako unahisi kwamba mambo yote afanyayo Mungu ni makuu. Waweza kukosa kuelewa kwa wakati huo na waweza kuuliza, "Kwa nini Mungu kanipa mazingira kama yale?" au "Kwa nini Mungu kanipa majaribu kama haya?" Lakini unapoendelea kwa kutojua, roho yako itakuja kuelewa kwa nini Mungu hasa amefanya hivi, na kwa wakati huo utajihisi kwamba umekomaa. Haukuwa tena kuwa ulivyokuwa awali pale Mungu alipokupa jaribu au mazingira magumu, ulipohisi dhiki ndani ya moyo wako, na ulihisi daima kuasi dhidi ya ama kukataa mazingira haya. Siku utakapokomaa ikija, utahisi hisia hizi zikidhoofika na kudhoofika, utaweza kubadilika, na utakuwa mtiifu ndani ya roho yako. Fauka ya hayo, utamshukuru Mungu na utahisi chembe kidogo ya shukrani ukiwaza kwamba, "Mungu ni mwema sana kwangu. Hapo awali kimo changu kilikuwa hakijakomaa kabisa, sikuelewa mapenzi ya Mungu, sikumtii Mungu na nilimlalamikia Mungu, lakini Mungu hakukumbuka. Kupitia njia hii hadi wakati huu nahisi utunzaji wa Mungu na pia nahisi uongozo Wake.” Kwa wakati huo, utahisi kwamba upendo wa Mungu kwa binadamu ni wa ukweli na ni kitu unachoweza kugusa. Wakati haya yatatendeka, utakuwa umekomaa na utaweza kukabili mambo na kuchukua majukumu fulani.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

    Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni