3/23/2018

Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IIπŸ“–πŸ“š

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Wokovu

  Umeme wa Mashariki | Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

  (II) Ubinadamu Hupata Kibali cha Huruma na Uvumilivu wa Mungu Kupitia kwa Toba ya dhati

🌼🌼🌼🌼🌼*************🌻🌻🌻🌻*************🌺🌺🌺🌺🌺
      Kinachofuata ni hadithi ya biblia ya “Wokovu wa Mungu kwa Ninawi.”

    (Yona 1:1-2) Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
    (Yona 3) Neno la BWANA likamjia Yona mara ya pili, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, uhubiri habari Ninayokuamuru.Basi Yona akainuka, akaenda Ninawi, kulingana na amri ya BWANA.  Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo. Hivyo habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akavaa nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake, ikisema, Mwanadamu au myanma asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji: Bali mwanadamu na mnyama pia afunikwe nguo za magunia, nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye iwapo Mungu atageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya; Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda;na hakuliteBasi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa. Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo. Hivyo habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akavaa nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake, ikisema, Mwanadamu au myanma asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji: Bali mwanadamu na mnyama pia afunikwe nguo za magunia, nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye iwapo Mungu atageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya; Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; na hakulitenda.
    (Yona 4) Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika sana. Akaomba kwa BWANA, akasema, Nakuomba, Ee BWANA, sivyo hivyo nilivyosema, nilipokuwa bado katika nchi yangu? Kwa hivyo nilikimbilia Tarshishi kabla: kwa maana nilijua kuwa wewe ni Mungu mwenye neema, na mwenye huruma, si mwepesi wa hasira, na mwingi wa rehema, nawe unaghairi mabaya. Basi sasa, Ee BWANA, chukua, nakuomba, uhai wangu kutoka kwangu; kwa maana ni afadhali mimi nife kuliko kuishi. Naye BWANA akasema, Je, unatenda vema kukasirika? Hivyo Yona akatoka nje ya mji, akaketi upande wa mashariki wa mji, na huko akajifanyia kibanda, akakaa chini yake kivulini, mpaka aone mji ule utakuwaje. Na BWANA Mungu akatayarisha mtango, akaufanya uje juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumwokoa kutoka katika huzuni wake. Basi Yona akaufurahia sana ule mtango. Lakini Mungu akatayarisha buu siku ya pili kulipopambazuka, nalo likautafuna ule mtango hadi ukanyauka. Na hivyo ikawa, jua lilipopanda juu, kwamba Mungu akautayarisha upepo mkali wa mashariki; na jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akatamani afe, na akasema, Ni heri mimi nife kuliko niishi. Mungu akamwambia Yona, Je, unatenda vema kukasirika kwa ajili ya mtango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika, hata mpaka kufa. Kisha Bwana akasema, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuukuza; uliomea kwa usiku mmoja, na kuangamia kwa usiku mmoja: Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi, mji ule mkubwa, ambao ndani yake wamo zaidi ya watu mia na ishirini elfu ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?

    Muhtasari wa Hadithi ya Ninawi

    Ingawaje hadithi ya “wokovu wa Mungu wa Ninawi” ni fupi kwa urefu, inaruhusu mtu kuweza kuona kidogo tu ule upande mwingine wa tabia ya haki ya Mungu. Ili kuweza kuelewa haswa upande huo unajumuisha nini, lazima turudi kwenye Maandiko na kuangalia nyuma katika mojawapo ya matendo ya Mungu.
    Hebu kwanza tuangalie mwanzo wa hadithi hii: “Basi neno la BWANA lilimjia Yona mwana wa Amitai, likisema, Inuka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, upige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu” (Yona 1:1-2). Katika fungu hili kutoka kwenye Maandiko, tunajua kwamba Yehova Mungu alimwamuru Yona kwenda katika mji wa Ninawi. Kwa nini alimwamuru Yona kwenda katika mji huo? Biblia iko wazi kabisa kuhusu suala hili: Maovu ya watu walio ndani ya mji huo yalikuwa yamefikia macho ya Yehova Mungu, na hivyo basi Alimtuma Yona ili kuwatangazia kile Alichonuia kufanya. Ingawa hakuna kitu kilichorekodiwa kinachotwambia Yona alikuwa nani, jambo hili, bila shaka, halina uhusiano wowote na kumjua Mungu. Hivyo basi, huhitaji kumwelewa mwanamume huyu. Unahitaji kujua tu kile ambacho Mungu alimwamuru Yona kufanya na kwa nini Alifanya kitu hicho.

    Onyo la Yehova Mungu Lawafikia Waninawi

    Hebu tuendelee hadi kwenye fungu la pili, sura ya tatu ya kitabu cha Yona: “Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti, akasema, Baada ya siku arobaini mji wa Ninawi utaangamizwa.” Haya ndiyo maneno ambayo Mungu alipitisha moja kwa moja kwake Yona ili aweze kuwaambia Waninawi. Ndiyo pia, kwa kawaida, maneno ambayo Yehova alipenda kusema kwa Waninawi. Maneno haya yanatwambia kwamba Mungu alianza kukerwa na kuchukia watu wa mji huu kwa sababu ya maovu yao yaliyokuwa yamefika machoni pa Mungu, na hivyo basi, Alipenda kuuangamiza mji huo. Hata hivyo, kabla ya Mungu kuangamiza mji, Aliwatangazia Waninawi, na hapo kwa hapo Akawapa fursa ya kutubu maovu yao na kuanza upya. Fursa hii ingedumu kwa siku arubaini. Kwa maneno mengine, kama watu waliokuwa ndani ya mji huu wasingetubu, na kukubali dhambi au maovu yao wao wenyewe mbele ya Yehova Mungu ndani ya siku arubaini, Mungu angeangamiza mji huu kama Alivyoangamiza Sodoma. Hivi ndivyo ambavyo Yehova Mungu alipenda kuwaambia watu wa Ninawi. Ni wazi kwamba, hili halikuwa tangazo rahisi. Halikuweza tu kuonyesha hasira ya Yehova Mungu, lakini pia lilionyesha mtazamo Wake kwa wale Waninawi; wakati uo huo tangazo hili rahisi lilitumika kama onyo kali kwa watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huo. Onyo hili liliwaambia kwamba matendo yao maovu yalikuwa yamewafanya kuchukiwa na Yehova Mungu na liliwaambia kwamba matendo yao maovu yangewaletea hivi karibuni fedheha kutokana na maangamizo yao wenyewe; kwa hivyo, maisha ya kila mmoja kule Ninawi yalikuwa karibu kuangamia.

    Utofautishaji Mkavu wa Ninawi na Mwitikio wa Sodoma kwa Onyo la Yehova Mungu

    Kupinduliwa kunamaanisha nini? Kwa muktadha wa mazungumzo, kunamaanisha kutoweka. Lakini kwa njia gani? Ni nani angefanya mji mzima kupinduliwa? Haiwezekani kwa binadamu kufanya kitendo kama hicho, bila shaka. Watu hawa hawakuwa wajinga; mara tu waliposikia matangazo haya, walipata wazo hilo. Walijua kwamba yalikuwa yametoka kwa Mungu; walijua kwamba Mungu angetekeleza kazi Yake; walijua kwamba maovu yao yalikuwa yamemkasirisha Yehova Mungu na kumfanya kuwa na hasira kali kwao, ili waweze kuangamizwa pamoja na mji wao. Je, watu wa mji huo walichukulia vipi suala hilo baada ya kusikiliza onyo la Yehova Mungu? Biblia inafafanua kwa maelezo fafanuzi namna ambavyo watu hawa walivyoitikia, kuanzia kwa mfalme wao hadi kwa binadamu wa kawaida. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Basi watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, wakavaa nguo za magunia, kutoka Yule aliye mkubwa hadi aliye mdogo. Hivyo habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akavaa nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake, ikisema, Mwanadamu au myanma asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji: Bali mwanadamu na mnyama pia afunikwe nguo za magunia, nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake. …”
    Baada ya kusikia tangazo la Yehova Mungu, watu wa Ninawi walionyesha mtazamo uliokuwa kinyume kabisa na ule wa watu wa Sodoma—watu wa Sodoma walimpinga Mungu waziwazi, huku wakiendelea kutoka kwa maovu hadi maovu, lakini baada ya kusikia maneno haya, Waninawi hawakupuuza suala hilo, wala hawakuweza kulipinga; badala yake walimsadiki Mungu na kutangaza kufunga. “Walisadiki” inarejelea nini hapa? Neno lenyewe linapendekeza imani na unyenyekevu. Kama tutatumia tabia halisi ya Waninawi kuelezea neno hili, inamaanisha kwamba walisadiki Mungu anaweza na angeweza kufanya vile Alivyosema, na kwamba walikuwa radhi kutubu. Je, watu wa Ninawi walihisi woga mbele ya janga lililokuwa karibu kutokea? Imani yao ndiyo iliyotia woga katika mioyo yao. Kwa kweli, ni nini tunachoweza kutumia kuthibitisha Imani na woga wa Waninawi? Ni sawa na vile Biblia inavyosema: “Na wao[a] wakatangaza kufunga, na wakavalia nguo ya gunia, kuanzia wale walio wakubwa zaidi na hata kwa wale walio wadogo zaidi.” Hivi ni kusema kwamba Waninawi walisadiki kweli, na kwamba kutoka kwenye imani hii woga uliibuka, ambao sasa ulisababisha kufunga na kuvaliwa kwa nguo ya gunia. Hivi ndivyo walivyoonyesha mwanzo wa toba yao. Tofauti kabisa na watu wa Sodoma, Waninawi hawakumpinga Mungu tu, bali walionyesha pia waziwazi toba yao kupitia kwa tabia na matendo yao. Bila shaka, hii haikutumika tu kwa watu wa kawaida wa Ninawi; hata mfalme wao hakubakizwa.

    Toba ya Mfalme wa Ninawi Inasababisha Pongezi ya Yehova Mungu

    Wakati mfalme wa Ninawi alipozisikia habari hizi, aliinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua nguo zake, akavalia nguo ya gunia na kukalia jivu. Kisha akatangaza kwamba hakuna mtu kwenye mji huo ambaye angeruhusiwa kuonja chochote, na kuwa hakuna mifugo, wanakondoo na ng’ombe ambao wangekunywa maji na kula nyasi. Binadamu na mifugo kwa pamoja walitakikana kujifunika nguo ya gunia; nao watu wangemsihi Mungu kwa uaminifu. Mfalme pia alitangaza kwamba watu wote wangetupilia mbali njia zao za maovu na kukataa udhalimu ulioko mikononi mwao. Tukifanya uamuzi kutoka kwenye misururu ya vitendo hivi, mfalme wa Ninawi alionyesha toba yake ya dhati. Misururu ya vitendo alivyofanya—kutoka kwenye kiti chake cha ufalme, kulitupa joho lake la kifalme, kuvalia nguo ya gunia na kukalia majivu—kulionyesha watu kwamba mfalme wa Ninawi aliweka kando hadhi yake ya kifalme na kuvalia nguo ya gunia pamoja na watu wa kawaida wa nchi. Hii ni kusema kwamba mfalme wa Ninawi hakuweza kushikilia wadhifa wake wa kifalme ili aendelee na njia zake za maovu au udhalimu katika mikono yake baada ya kikao cha tangazo kutoka kwa Yehova Mungu; badala yake, aliweka pembeni mamlaka aliyoyashikilia na kutubu mbele ya Yehova Mungu. Kwenye kipindi hiki cha muda, mfalme wa Ninawi hakuwa akitubu akiwa mfalme; alikuwa amekuja mbele ya Mungu kuungama na kutubu dhambi zake akiwa binadamu wa kawaida wa Mungu. Aidha, aliuambia mji mzima kuungama na kutubu dhambi zao mbele ya Yehova Mungu kwa njia sawa na yeye; vilevile, alikuwa na mpango mahususi wa namna ya kufanya hivyo kama inavyoonekana kwenye Maandiko: “Mwanadamu au mnyama asionje kitu, wala makundi ya ng’ombe wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji. … nao wamlilie Mungu kwa nguvu: naam, na wageuke, kila mmoja aache njia yake ya uovu, na udhalimu ulio mikononi mwake.” Kama kiongozi wa mji, mfalme wa Ninawi alimiliki hadhi na nguvu za kimamlaka na angefanya chochote alichopenda. Alipokabiliwa na tangazo la Yehova Mungu, angeweza kupuuza suala hilo au kutubu na kuungama tu dhambi zake pekee; kuhusiana na kama watu wa mji wangechagua kutubu au la, angepuuza suala hili kabisa. Hata hivyo, mfalme wa Ninawi hakufanya hivyo kamwe. Mbali na kuinuka kutoka kwenye kiti chake cha enzi, kuvalia nguo ya gunia na kujipaka jivu na kuungama na kutubu dhambi zake mbele ya Yehova Mungu, aliweza pia kuwaamuru watu na mifugo ndani ya mji huo kufanya hivyo. Aliweza hata kuamuru watu “kumlilia Mungu kwa nguvu.” Kupitia misururu hii ya vitendo, mfalme wa Ninawi aliweza kukamilisha kwa kweli kile ambacho kiongozi anafaa kufanya; misururu ya vitendo vyake ndiyo iliyokuwa migumu kwa mfalme yeyote katika historia ya binadamu kutimiza, hatua na pia hatua ambayo hakuna aliyewahi kutimiza. Matendo haya yanaweza kuitwa shughuli isiyo na kifani katika historia ya binadamu; yanastahili kukumbukwa na kuigwa na binadamu. Tangu enzi ya mwanadamu, kila mfalme alikuwa amewaongoza wafuasi wake kukinzana na kumpinga Mungu. Hakuna yule aliyewahi kuwaongoza wafuasi wake kusihi Mungu kutafuta ukombozi kwa ajili ya maovu yao, kupokea msamaha wa Yehova Mungu na kuepuka adhabu kali. Mfalme wa Ninawi, hata hivyo, aliweza kuwaongoza raia wake kumlilia Mungu, kuacha njia zao mbalimbali za maovu na kutupilia mbali udhalimu ulio mikono mwao. Aidha, aliweza pia kuweka kando kiti chake cha enzi, na badala yake, Yehova Mungu alibadilisha na kughairi na kugeuza hasira Yake, na kuruhusu watu wa mji huu kuishi na kuwalinda dhidi ya kuangamia. Matendo ya mfalme yanaweza kuitwa tu muujiza wa nadra katika historia ya binadamu; yanaweza hata kuitwa kielelezo cha ubinadamu uliopotoka unaoungama na kutubu dhambi zake mbele ya Mungu.

    Mungu Aona Kutubu kwa Dhati katika Kina cha Mioyo ya Waninawi

    Baada ya kusikiliza tangazo la Mungu, mfalme wa Ninawi na raia Wake walitekeleza misururu ya vitendo. Je, ni nini asili ya tabia na matendo yao? Kwa maneno mengine, ni nini kiini cha uzima wa mwenendo wao? Kwa nini walifanya kile walichofanya? Katika macho ya Mungu walikuwa wametubu kwa dhati, si tu kwa sababu walikuwa wamemsihi Mungu kwa dhati na kuungama dhambi zao mbele Yake, lakini pia kwa sababu walikuwa wameacha mwenendo wao wenye maovu. Walichukua hatua namna hii kwa sababu baada ya kusikia matamshi ya Mungu, walitishika pakubwa na kusadiki kwamba angefanya vile ambavyo alikuwa amesema. Kwa kufunga, kuvalia nguo ya gunia na kukalia jivu, walipenda kuonyesha namna walivyokuwa radhi kubadilisha njia zao na kujizuia na maovu, kumwomba Yehova Mungu kuzuia hasira Yake, kusihi Yehova Mungu kutupilia mbali uamuzi Wake, pamoja na msiba mkuu ambao ulikuwa karibu kuwasibu. Kupitia uchunguzi wa tabia yao yote, tunaona ya kwamba tayari walielewa kwamba vitendo vyao vya awali vilimchukiza Yehova Mungu na kwamba walielewa sababu iliyomfanya kutaka kuwangaamiza hivi karibuni. Kwa sababu hizi, wote walipenda kutubu kabisa, kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, pindi tu walipotambua tangazo la Yehova Mungu, kila mmoja wao alihisi woga katika mioyo yao; hawakuendelea tena na mwenendo wao wa maovu wala kuendelea kutenda vitendo ambavyo Yehova Mungu alichukia. Vilevile, walimsihi Yehova Mungu kusamehe dhambi zao za kale na kutowatendea kulingana na vitendo vyao vya kale. Walikuwa radhi kutowahi kujihusisha tena katika maovu na kutenda kulingana na maagizo ya Yehova Mungu, kama tu wasingewahi kumkasirisha Yehova Mungu. Toba yao ilikuwa ya dhati na ya kweli. Ilitoka kwenye kina cha mioyo yao na haikuwa ya kujidanganya, wala haikuwa ya muda.
    Baada ya watu wa Ninawi, kutoka kwa mfalme mwenye mamlaka hadi kwa raia wake, kujua kwamba Yehova Mungu alikuwa amewakasirikia, kila mojawapo ya vitendo vyao, tabia yao nzima, pamoja na kila mojawapo ya uamuzi na machaguo yao vilikuwa wazi na dhahiri mbele ya Mungu. Moyo wa Mungu ulibadilika kulingana na tabia yao. Akili Zake Mungu zilikuwa zinafikiria nini wakati huo? Biblia inaweza kukujibia swali hili. Kama ilivyorekodiwa kwenye Maandiko: “Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya; Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; na hakulitenda.” Ingawaje Mungu alibadilisha fikira Yake, hakukuwa na chochote kigumu kuhusu mtazamo wa fikira Yake. Aliweza kubadilika kutoka katika kuonyesha hasira Yake hadi kutuliza hasira Yake, na kisha kuamua kutouleta msiba mkuu katika mji wa Ninawi. Sababu ya uamuzi wa Mungu wa—kuwaokoa Waninawi dhidi ya msiba wao mkuu—ilikuwa ya haraka mno, ni kwa sababu Mungu aliangalia moyo wa kila mmoja wa wale Waninawi. Aliona kwamba katika kina cha mioyo yao waliweza: kuungama na kutubu kwa dhati dhambi zao, imani yao ya dhati kwake Yeye, mtazamo wao wa kina kuhusu vile vitendo vyao vya maovu vilikuwa vimeipa tabia Yake hasira kali, na woga uliotokana na adhabu ya Yehova Mungu iliyokuwa inakaribia. Wakati uo huo, Yehova Mungu aliweza kusikia maombi kutoka kwenye kina cha mioyo yao wakimsihi kusitisha hasira Yake dhidi yao ili waweze kuepuka msiba huu mkuu. Wakati Mungu alipoangalia hoja hizi zote, kwa utaratibu hasira yake ilitoweka. Licha ya vile hasira yake ilivyokuwa kuu hapo awali, alipoona kutubu kwao kwa dhati ndani ya kina cha mioyo ya watu hawa, moyo Wake uliguswa na hili, na kwa hivyo Hakuweza kuvumilia kuwaletea msiba mkuu, na Alisitisha hasira yake kwao. Badala yake Aliendelea kuwaonyesha huruma Yake na uvumilivu kwao na akaendelea kuwaongoza na kuwakimu.

    Kama Imani Yako kwa Mungu ni Kweli, Utapokea Utunzaji Wake Mara Nyingi

   Kubadilisha kwa nia zake Mungu kwa watu wa Ninawi hakukuhusisha kusitasita au kutoeleweka kokote. Badala yake kulikuwa ni mabadiliko kutoka kwa hasira tupu hadi uvumilivu mtupu. Huu ni ufunuo wa kweli kuhusu hali halisi ya Mungu. Mungu hajawahi kusitasita au kufikiria mara mbili kuhusu hatua Zake; kanuni na makusudio yaliyo katika matendo Yake ni wazi na dhahiri yasiyo na kasoro wala hatia, yasiyo na njama yoyote kamwe ama mifumo iliyoingiliana. Kwa maneno mengine, hali halisi ya Mungu haina giza wala maovu mengine. Mungu alikasirikia Waninawi kwa sababu ya vitendo vya maovu ambavyo vilikuwa vimefikia macho Yake; wakati ule hasira Yake ilitokana na hali Yake halisi. Hata hivyo, wakati hasira ya Mungu ilipotoweka na akatoa uvumilivu Wake kwa watu wa Ninawi kwa mara nyingine tena, kila kitu Alichofichua kilikuwa bado ni hali Yake halisi. Uzima wa badiliko hili ulitokana na badiliko katika mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu. Kwenye kipindi hiki chote cha muda, tabia ya Mungu isiyoweza kukosewa haikubadilika; hali halisi ya uvumilivu wa Mungu haikubadilika; hali halisi ya upendo na huruma ya Mungu haikubadilika. Wakati watu wanapotekeleza vitendo vya maovu na kumkosea Mungu atawashushia ghadhabu Yake. Wakati watu wanatubu kwa kweli, moyo wa Mungu utabadilika, na hasira Yake itasita. Wakati watu wanapoendelea kumpinga Mungu kwa usumbufu, hasira Yake kali haitasita; hasira Yake itaendelea kuwa kwao hatua kwa hatua mpaka watakapoangamizwa. Hii ndiyo hali halisi ya tabia ya Mungu. Haijalishi kama Mungu anaonyesha hasira au huruma na upole, mwenendo wa binadamu, tabia na mtazamo wake kwa Mungu ndani ya kina cha moyo wake vinatoa masharti ya kile ambacho kinaonyeshwa kupitia kwa ufunuo wa tabia ya Mungu. Kama Mungu anaendelea kuonyesha mtu hasira Yake, moyo wa mtu huyu bila shaka humpinga Mungu. Kwa sababu hajawahi kutubu kwa kweli, kuinamisha kichwa chake mbele ya Mungu au kumiliki imani ya kweli kwa Mungu, hajawahi kupata huruma na uvumilivu wa Mungu. Kama mtu anapokea utunzaji wa Mungu na mara nyingi hupokea huruma na uvumilivu wake, basi mtu huyo bila shaka anaamini Mungu kwa kweli ndani ya moyo wake, na moyo wake haumpingi Mungu. Yeye kwa mara nyingi anatubu kwa kweli mbele ya Mungu; kwa hivyo, hata kama nidhamu ya Mungu mara nyingi humshukia mtu huyu, hasira Yake haitamshukia.
   Ufafanuzi huu mfupi unaruhusu watu kuuona moyo wa Mungu, kuona uhalisia wa hali Yake halisi ili kuona kwamba ghadhabu ya Mungu na mabadiliko katika moyo Wake yana sababu. Licha ya Utofautishaji mkavu ambao Mungu alionyesha Alipoghadhabishwa na pale Alipobadilisha moyo Wake, jambo ambalo linafanya watu kusadiki kwamba utofautishaji mkavu au nafasi kubwa yaonekana kuwepo kati ya dhana hizi mbili za hali halisi ya Mungu—ghadhabu Yake na Uvumilivu Wake—Mtazamo wa Mungu kwa kule kutubu kwa Waninawi kwa mara nyingine kunaruhusu watu kuweza kuona ule upande mwingine wa tabia halisi ya Mungu. Mabadiliko katika moyo wa Mungu yanaruhusu kwa kweli ubinadamu kwa mara nyingine kuuona ukweli wa huruma na upole wenye upendo wa Mungu na kuona ufunuo wa kweli wa hali halisi ya Mungu. Ubinadamu hauna budi kutambua kwamba rehema ya Mungu na upole wenye upendo si hadithi za uwongo tu, wala si ughushi. Hii ni kwa sababu hisia za Mungu kwa wakati huo zilikuwa kweli; Mabadiliko ya Mungu yalikuwa kweli; Mungu kwa kweli aliupa ubinadamu kwa mara nyingine tena rehema na uvumilivu Wake.

    Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kwawapa Kibali cha Rehema ya Mungu na Kwabadilisha Hatima Zao

    Je, kulikuwa na kuhitilafiana kokote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu kwa wakati ule ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotajwa kwenye Biblia: “Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ya maovu” na “kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwake.”
    Hii “Njia ya maovu” hairejelei kusanyiko la vitendo vya maovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu. “Kugeuka kutoka njia yake ya maovu” kunamaanisha kwamba wale wanaozungumziwa hawatawahi kutekeleza vitendo hivi tena. Kwa maneno mengine, hawatawahi kuwa na tabia inayoonyesha njia hii ya maovu tena; mbinu, chanzo, kusudio, nia na kanuni za vitendo vyao vyote vimebadilika; hawatawahi tena kutumia mbinu na kanuni hizi kuleta nafuu na furaha mioyoni mwao. Kule “kuacha” katika “kuacha udhalimu ulio mikono mwao” kunamaanisha kuweka chini au kuweka pembeni, kujitenga kabisa na mambo ya kale na kutorudi nyuma tena. Wakati watu wa Ninawi walipoacha udhalimu uliokuwa mikono mwao, hii ilithibitisha na vilevile iliwakilisha kutubu kwao kwa kweli. Mungu huangalia kwa makini sehemu ya nje na vilevile ndani ya mioyo ya watu. Wakati Mungu alipoangalia kwa makini kutubu kwa kweli katika mioyo ya Waninawi bila kuuliza swali na pia kutambua kwamba walikuwa wameacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu uliokuwa mikono mwao, Alibadilisha moyo Wake. Hivi ni kusema kwamba mwenendo na tabia ya watu hawa na njia mbalimbali za kufanya mambo, pamoja na kuungama na kutubu kwa kweli kwa dhambi zilizokuwa mioyoni mwao, kulisababisha Mungu kubadilisha Moyo Wake, kubadilisha nia Zake, kufuta uamuzi wake na kutowaadhibu wala kuwaangamiza. Kwa hivyo, watu wa Ninawi waliweza kufikia hatima tofauti. Waliyakomboa maisha yao binafsi na wakati uo huo wakapata kibali cha huruma na uvumilivu wa Mungu, na wakati uo huo Mungu akawa pia amefuta hasira Yake.

   Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Kutubu kwa Kweli kwa Binadamu Ni Nadra

    Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia misururu ya vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikaanza kubadilika kwa utaratibu na Akaanza kuwaonea huruma na uvumilivu. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu katika dhana hizi mbili za tabia ya Mungu kwenye tukio lilo hilo. Ni vipi ambavyo mtu anafaa kuelewa na kujua ukosefu huu wa kuhitilafiana? Mungu aliweza kuonyesha kwa ufanisi na kufichua vipengele hivi viwili tofauti kabisa wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na hali halisi ya kutokosewa kwa Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu havumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli mara nadra sana kwa Mungu, na ni nadra sana kwa watu kuweza kugeuka kwa kweli na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ana ghadhabu kwa binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kwa haki kumpa binadamu huyo huruma na uvumilivu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo wa maovu ya mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu mbele yake, kwa wale wanaoweza kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio kwenye mikono yao. Mtazamo wa Mungu uliweza kufichuliwa waziwazi kuhusiana na vile Alivyowashughulikia Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu kwa kweli si vigumu kuvipokea; Anahitaji mtu kuwa na kutubu kwa kweli. Mradi tu watu waweze kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuuacha udhalimu ulio mikono mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

    Tabia ya Haki ya Muumba ni Kweli na Wazi

     Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko haya kati ya dhana hizi mbili za tabia ya Mungu kwenye suala lili hili yalikuruhusu kuweza kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili na wazi; haina ugawanyi wowote. Licha ya kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanaambia ubinadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au chombo kilichofinyangwa kwa udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe mwenye uhai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa sababu ya watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Aliweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi mkosi na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupendelea kutumia sheria bila kumakinika na wanapendelea kutumia sheria ili kuthibitisha na kufafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia fomula ili kujua tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kulingana na himaya ya fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika mara moja kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, dhana tofauti za hali halisi ya Mungu zitaweza kufichuliwa. Kwenye kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye hufichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, upole wa upendo Wake na uvumilivu Wake. Hali hii halisi Yake itafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia yake ya haki hairuhusiwi kushukiwa, kukiukwa, kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi dhana hizi katika kila elementi ya asili na kuzitekeleza kila wakati. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka ya muda au nafasi, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kama inavyoongozwa na mipaka ya muda au nafasi. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kusita kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inayo maneno matupu tu. Wakati Mungu anapoonyesha hasira Yake na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa ubinadamu? Mungu huonyesha hasira kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina kosa. Moyo wa Mungu unavutiwa na kutubu kwa watu, na ni kutubu huku ambako hubadilisha moyo Wake. Kuvutiwa kwake, mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote kwa kweli havina kosa kamwe; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu kwa kweli ni uvumilivu; Huruma Yake ni huruma bila kasoro. Tabia yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; hali Yake halisi ni tofauti na chochote kile katika uumbaji. Kanuni za matendo ambayo Mungu anaonyesha, fikira na mawazo Yake, au uamuzi wowote ule, pamoja na kitendo chochote kimoja, vyote havina dosari wala doa. Kama vile Mungu alivyoamua, ndivyo Atakavyotenda, na katika njia hii, Yeye hukamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe chochote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kujitokeza na kuendeleza utekelezaji na uzoefu.
     Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, unauona upande ule mwingine wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu? Je, unauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwenu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile wa Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha hasira nyingi na kuamua kuangamiza au kuleta maafa kwa mwanadamu? Na ni nani amefuzu kutoa huruma, na kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake dhidi ya kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za binafsi za kipekee; Hategemei kudhibitiwa au kuzuiliwa na watu, matukio au mambo yoyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi yeye na kubadilisha uamuzi wowote Wake. Uzima wa tabia na fikira za uumbaji upo katika hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama ataendeleza hasira au huruma; ni hali halisi tu ya Muumba—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hivi. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
    Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni dhana ya hali halisi ya tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua dhana mbili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa pamoja na kushukiwa; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyoweza kukosewa; wakati uo huo, dhana ile nyingine ya tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, vinavyoweza kubadilisha au kuwakilisha Mungu katika vitendo Vyake, wala hakuna yeyote anayeweza kubadilisha au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

   Hisia za Dhati za Muumba kwa Mwanadamu

    Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa ubinadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kuelewa na kumjua Yeye, ni kwamba hajui Mungu ni nani, wala asingependa kujua Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yao…. Mikono yake ni yenye joto na thabiti; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote; uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka. Kuanzia mapambazuko hadi magharibi, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu. Utunzaji wake wa kujitolea na huba maalum kwa ubinadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, vyote vilionyeshwa kwa utaratibu wakati Alipookoa mji wa Ninawi. Haswa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yaliweza kuweka msingi wa huruma ya Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Aliumba. Kupitia kwa maneno haya, unaweza kupata ufahamu wa kina wa hisia za dhati za Mungu kwa ubinadamu….
    Yafuatayo yamerokodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuukuza; uliomea kwa usiku mmoja, na kuangamia kwa usiku mmoja: Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi, mji ule mkubwa, ambao ndani yake wamo zaidi ya watu mia na ishirini elfu ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?” Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, mazungumzo kati Yake na Yona. Huku mabadilishano ya mazungumzo haya yakiwa mafupi, yamejaa utunzaji wa Muumba kwa mwanadamu na kutotaka Kwake kukata tamaa. Matamshi haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kuhusu uumbaji Wake, na kupitia kwa maneno haya yaliyowekwa wazi, ambayo yanasikizwa kwa nadra sana na binadamu, Mungu anakariri nia Zake za kweli kwa ubinadamu. Mabadilishano ya mazungumzo haya yanawakilisha mtazamo ambao Mungu alishikilia kwa watu wa Ninawi—lakini mtazamo aina hii ni upi? Ni mtazamo Alioshikilia kuhusu watu wa Ninawi kabla na baada ya kutubu kwao. Mungu huchukulia ubinadamu kwa njia sawa. Ndani ya maneno haya mtu anaweza kupata fikira Zake, pamoja na tabia Yake.
     Je, ni fikira zipi za Mungu zinafichuliwa katika maneno haya? Usomaji wa makini unafichua mara moja kwamba Anatumia neno “huruma”; matumizi ya neno hili yanaonyesha mtazamo wa kweli wa Mungu kwa binadamu.
    Kutokana na mtazamo wa kisemantiki, mtu anaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: kwanza, kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani; pili, kupenda kwa dhati; hatimaye, kutokuwa radhi kukiumiza na vilevile kutoweza kuvumilia kufanya hivyo. Kwa ufupi, unaashiria yale mahaba na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawaje Mungu alitumia neno linalotamkwa mara nyingi miongoni mwa binadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.
    Huku mji wa Ninawi ukiwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo uliokuwa na utofauti mkavu na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na dhati kwa hali zote, Mungu kwa mara nyingine alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Tuzo ya Mungu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kurudufu; hakuna mtu anayeweza kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanamume mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, akiongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kujua masharti ya kuishi ya ubinadamu kama viganja vya mkono wake? Ni nani anayeweza kuvumilia mzigo na jukumu la kuwepo kwa ubinadamu? Nani anaweza kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani anaweza kusamehe mji? Ni nani wanaoweza kusema wanafurahia uumbaji wao binafsi? Muumba Pekee! Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu. Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu na kufurahia viumbe vyake vyote. Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu: Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu; Ameshukuru, amefurahia, amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia kutokana na kutubu na kuamini kwa binadamu; kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote vipo juu ya na vinazungukia mwanadamu; kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu; uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu. Kwa minajili ya mwanadamu, Anasafiri na kuzungukazunguka; kwa utaratibu Anatoa kila sehemu ya maisha Yake; Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua namna ya kuyahurumia maisha Yake, ilhali siku zote Amehurumia na kufurahia mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe aliumba …. Anatoa kila kitu Alichonacho kwa ubinadamu huu…. Yeye anatoa huruma na uvumilivu Wake bila masharti na bila matarajio ya kufidiwa. Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake, kupokea toleo Lake la maisha; Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu na kuruzuku maisha ya viumbe vyote.

    Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Juu ya Ubinadamu

     Mazungumzo haya kati ya Yehova Mungu na Yona bila shaka ni onyesho la hisia za kweli za Muumba juu ya ubinadamu. Kwa upande mmoja yanafahamisha watu kuhusu ufahamu wa Muumba wa asili yote yaliyo katika amri Yake; kama vile Yehova Mungu alivyosema, “Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi, mji ule mkubwa, ambao ndani yake wamo zaidi ya watu mia na ishirini elfu ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?” Kwa maneno mengine, ufahamu wa Ninawi na Mungu haukuwa hata karibu na ule wa laana. Hakujua tu idadi ya viumbe vilivyo hai ndani ya mji (wakiwemo watu na mifugo), bali Alijua pia ni wangapi wasingeweza kutambua kati ya mikono yao ya kulia na kushoto—yaani, ni watoto na vijana wangapi walikuwepo. Hii ni ithibati thabiti ya ufahamu bora kuhusu mwanadamu. Kwa upande mwingine mazungumzo haya yanafahamisha watu kuhusu mtazamo wa Muumba kwa ubinadamu, ambako ni kusema kwamba uzito wa ubinadamu katika moyo wa Muumba. Ni vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuukuza; uliomea kwa usiku mmoja, na kuangamia kwa usiku mmoja: Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi, mji ule mkubwa…?” Haya ndiyo maneno ya Yehova Mungu kuhusu lawama kwa Yona lakini yote ni kweli.
    Ingawaje Yona alikuwa ameaminiwa kutangaza matamshi ya Yehova Mungu kwa watu wa Ninawi, hakuelewa nia za Yehova Mungu, wala hakuelewa wasiwasi na matarajio Yake kwa watu wa mji huu. Kupitia kwa kemeo hili Mungu alinuia kumwambia kwamba ubinadamu ulikuwa zao la mikono Yake mwenyewe, na kwamba Mungu alikuwa ametia jitihada za dhati kwa kila mtu; kila mtu alisheheni matumaini ya Mungu; kila mtu alifurahia ruzuku ya maisha ya Mungu; kwa kila mtu, Mungu alikuwa amelipia gharama ya dhati. Kemeo hili lilimfahamisha Yona kwamba Mungu aliufurahia ubinadamu, kazi ya mikono Yake mwenyewe, kama vile tu ambavyo Yona mwenyewe aliufurahia mtango. Mungu kwa vyovyote vile asingewaacha kwa urahisi kabla ya ule muda wa mwisho unaowezekana; vilevile, kulikuwa na watoto wengi na mifugo isiyo na hatia ndani ya mji. Wakati wa kushughulikia mazao haya machanga na yasiyojua uumbaji wa Mungu, ambayo yasingeweza hata kutofautisha mikono yao ya kulia na ile ya kushoto, Mungu hakuweza kamwe kukomesha maisha yao na kuamua matokeo yao kwa njia ya haraka hivyo. Mungu alitumai kuwaona wakikua; Alitumai kwamba wasingetembea njia ile ile kama wakubwa wao, kwamba wasingeweza kusikia tena onyo la Yehova Mungu, na kwamba wangeshuhudia mambo ya kale ya Ninawi. Na hata zaidi Mungu alitumai kuiona Ninawi baada ya kuweza kutubu, kuuona mustakabali wa Ninawi kufuatia kutubu kwake, na muhimu zaidi, kuiona Ninawi ikiishi katika huruma za Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa hivyo, kwa macho ya Mungu, yale mazao ya uumbaji wake ambayo hayangeweza kutofautisha mikono yao ya kulia na kushoto yalikuwa mustakabali wa Ninawi. Wangeweza kubeba na kusimulia hadithi ya kale iliyostahili dharau, kama vile tu ambavyo wangeweza kusimulia wajibu muhimu wa kushuhudia hadithi ya kale ya Ninawi na mustakabali wake kupitia kwa mwongozo wa Yehova Mungu. Katika tangazo hili la hisia Zake za kweli, Yehova Mungu aliwasilisha huruma ya Muumba kuhusu ubinadamu kwa uzima wake. Lilionyesha ubinadamu kwamba “ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na majukumu ya kimsingi. Yeye ni kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia ii hii huruma Yake inawekewa ubinadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa ubinadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa ubinadamu na hisia Zake za kweli kuhusu ubinadamu. Mazungumzo haya ya Yehova Mungu yenye uchache na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu ubinadamu; ni maonyesho ya ukweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa ubinadamu, na ni ushahidi thabiti wa kutoa Kwake kwingi kwa huruma juu ya ubinadamu. Huruma yake haipewi tu vizazi vya wazee wa ubinadamu; lakini pia imepewa wanachama wachanga zaidi wa ubinadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa, kuanzia kizazi kimoja hadi kingine. Ingawaje hasira ya Mungu hushushwa mara kwa mara kwenye pembe fulani na enzi fulani za ubinadamu, huruma ya Mungu haijawahi kusita. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukifaa kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa ubinadamu hazitawahi kubadilika. Vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Na mimi, je, Sipaswi kuuhurumia mji wa Ninawi…?” Siku zote amefurahia uumbaji Wake mwenyewe. Hii ndiyo huruma ya tabia ya haki ya Muumba, na ndio pia upekee usio na kasoro wa Muumba!
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
     Jifunze zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni