Mwenyezi Mungu alisema, Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu? Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe;
wengine wanayo maoni kwamba kitu muhimu zaidi ni kujua namna ya kupata wokovu kupitia kwa Mungu, namna ya kumfuata Mungu, na namna ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Tutayaweka masuala haya yote pembeni kwa leo. Hivyo basi ni nini tunachozungumzia basi? Tunazungumzia mada kuhusu Mungu. Je, haya ndiyo mada muhimu zaidi kwa kila mtu? Maudhui ya mada kuhusu Mungu ni yapi? Bila shaka, mada hii haiwezi kamwe kutenganishwa na tabia ya Mungu, kiini cha Mungu na kazi ya Mungu. Hivyo leo, hebu tuzungumzie “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.”
Tangu wakati binadamu walipoanza kumsadiki Mungu, wamekuwa wakikutana na mada kama vile kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Inapokuja kwa kazi ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Sisi ndisi tunaofanyiwa kazi ya Mungu; tunaipitia kila siku, na hivyo basi tumezoeana nayo.” Na kuhusiana na tabia ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Tabia ya Mungu ni mada tunayoyasoma, kuchunguza, na kuzingatia katika maisha yetu yote, hivyo basi tunafaa kuzoeana nayo” Na kama ni Mungu Mwenyewe, baadhi ya watu watasema: “Mungu Mwenyewe ndiye tunayemfuata,tuliye na imani Kwake, na ndiye tunayemfuata, hivyo tumejuzwa pia kuhusu Yeye.” Mungu hajawahi kukomesha kazi Yake tangu uumbaji, wakati wote huu Ameendelea kuonyesha tabia Yake na kutumia njia mbalimbali kuonyesha neno Lake. Wakati huohuo, hajawahi kusita kujionyesha Yeye Mwenyewe na kiini Chake kwa mwanadamu, akionyesha mapenzi Yake kwa binadamu na kile Anachohitaji kutoka kwa huyo binadamu. Hivyo kutoka katika mtazamo wa moja kwa moja, mada hizi hazifai kuwa ya kigeni kwa yeyote yule. Kwa watu wanaomfuata Mungu leo, hata hivyo, Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe kwa hakika ni mambo ambayo hayajulikani kwao. Kwa nini hali iko hivi? Kwa kadri binadamu anapopitia kazi ya Mungu, anawasiliana pia na Mungu, na kuwafanya kuhisi ni kana kwamba wanaelewa tabia ya Mungu au wanajua sehemu kidogo kuhusu vile inavyofanana. Hivyo basi, binadamu hafikiri kuwa yeye ni mgeni katika kazi ya Mungu au tabia ya Mungu. Badala yake, binadamu anafikiri ni mwenyeji kabisa na Mungu na anaelewa mengi kuhusu Mungu. Lakini kulingana na hali ya sasa, uelewa wa watu wengi kumhusu Mungu umezuiliwa katika kile walichosoma vitabuni, na upana mfinyu wa kile walichopitia wao binafsi, wakiwa wamezuiliwa na kufikiria kwao, na zaidi ya yote, ukiwa umewekewa mipaka ya ukweli wanaoweza kuona kwa macho yao binafsi. Haya yote yapo mbali sana na Mungu Mwenyewe wa kweli. Sasa huu umbali upo “mbali” vipi? Pengine binadamu mwenyewe hana hakika, au pengine binadamu anayo dhana, ana fununu kiasi —lakini kwake Mungu Mwenyewe, uelewa wa binadamu kumhusu Yeye u mbali sana na kiini cha Mungu Mwenyewe wa kweli. Hii ndiyo maana tunahitajika kutumia mada kama “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” ili kuwasilisha ujumbe huu hatua kwa hatua na kwa njia mahususi.
Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haifichwi, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu. Anapofanya kazi hii, Anafichua bila kusita tabia Yake, huku Akitumia bila kusita kiini Chake na kile Anacho na alicho kuongoza na kukimu kila mmoja. Katika kila enzi na kila awamu, licha ya kama hali ni nzuri au mbaya, tabia ya Mungu siku zote iko wazi kwa kila mtu binafsi, na vile vitu Anavyomiliki na uwepo wake siku zote viko wazi kwa kila mtu binafsi, kwa njia sawa kwamba maisha Yake yanamtoshelezea mwanadamu kila wakati na bila kusita na kumsaidia mwanadamu. Licha ya haya yote, tabia ya Mungu inabakia fiche kwa baadhi ya watu. Kwa nini iko hivyo? Ni kwa sababu ingawaje watu hawa wanaishi ndani ya kazi ya Mungu na wanamfuata Mungu, hawajawahi kutafuta kuelewa Mungu au kutaka kumjua Mungu, sikwambii hata kumkaribia Mungu. Kwa watu hawa, kuelewa tabia ya Mungu kunamaanisha mwisho wao wawadia; kwa maanisha karibu wanahukumiwa na kushtakiwa na tabia ya Mungu. Hivyo basi, watu hawa hawajawahi kutamani kuelewa Mungu au tabia Yake, na hawatamani uelewa au maarifa ya kina ya mapenzi ya Mungu. Hawanuii kufahamu mapenzi ya Mungu kupitia ushirikiano wa kimakusudi—wanafurahia tu milele na hawachoki kufanya mambo wanayotaka kuyafanya; kusadiki kwa Mungu wanayetaka kusadiki kwake; kusadiki kwa Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao, Mungu anayekuwepo tu katika dhana zao; na kusadiki kwa Mungu asiyeweza kutenganishwa na wao katika maisha yao ya kila siku. Na kwake Mungu Mwenyewe wa kweli, wanapuuza kabisa, hawataki kusikia mambo ya Mungu na hawana tamanio la kumwelewa Yeye, kumtilia maanani Yeye, na hata hawana nia kidogo ya kuwa karibu zaidi na Yeye. Wanayatumia tu maneno ambayo Mungu anayaonyesha ili kuweza kujipamba, kujiandaa upya. Kwa wao, hilo tayari linawafanya kuwa waumini wenye mafanikio na watu walio na imani kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Ndani ya mioyo yao, wanaongozwa na kufikiria kwao, dhana zao, na hata ufasili wao binafsi wa Mungu. Mungu Mwenyewe wa kweli, kwa mkono mwingine, hana chochote kuhusiana na wao. Kwa sababu pindi wanapomwelewa Mungu Mwenyewe wa kweli, kuelewa tabia ya Mungu ya kweli, na kuelewa kile Mungu anacho na alicho, hii inamaanisha kwamba vitendo vyao, imani yao, na yale yote wanayoyafuatilia yatashutumiwa. Na ndiyo maana hawako radhi kukielewa kiini cha Mungu, na ndiyo maana wanasitasita na hawako radhi kutafuta kwa bidii au kuomba kumwelewa zaidi Mungu, kupata kujua zaidi kuhusu mapenzi Yake Mungu, na kuelewa kwa njia bora zaidi tabia ya Mungu. Afadhali Mungu kwao awe kitu kilichotungwa, kisicho na chochote na kibaya. Afadhali kwao Mungu awe mtu ambaye yupo hasa vile ambavyo wamemfikiria Yeye, Anayeweza kunyenyekea mbele zao, Asiyeishiwa na ujazo na Anayepatikana siku zote. Wanapotaka kufurahia neema ya Mungu, wanamuomba Mungu kuwa hiyo neema. Wanapohitaji baraka za Mungu, wanamuomba Mungu kuwa baraka hizo. Wanapokabiliwa na dhiki, wanamwomba Mungu kuwatia wao moyo, na kuwa usalama wao. Maarifa ya watu hawa kumhusu Mungu imebakia palepale pa mipaka ya neema na baraka. Uelewa wao wa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu umezuiliwa pia na kufikiria kwao na vilevile barua na mafundisho ya kidini tu. Lakini wapo baadhi ya watu walio na hamu ya kuielewa tabia ya Mungu, wanaotaka kumwona Mungu Mwenyewe kwa kweli, na kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli na kile Anacho na alicho. Watu hawa wanautafuta uhalisia wa ukweli na wokovu wa Mungu na wanatafuta kupokea ushindi, wokovu, na utimilifu wa Mungu. Watu hawa wanaitumia mioyo yao kulisoma neno la Mungu, wanaitumia mioyo yao kuthamini hali na kila mtu, tukio, au kitu ambacho Mungu amewapangia, na kuomba na kutafuta kwa uaminifu. Kile wanachotaka zaidi ni kuyajua mapenzi ya Mungu na kuielewa tabia ya kweli na kiini cha Mungu. Hivi ndivyo ilivyo ili wasiweze tena kumkosea Mungu, na kupitia kwa mambo waliyoyapitia, waweze kuona upendo zaidi wa Mungu na upande Wake wa kweli. Iko hivyo pia ili Mungu halisi na wa kweli ataweza kuwepo ndani ya mioyo yao, na ili Mungu atakuwa na nafasi katika mioyo yao, kiasi cha kwamba hawatakuwa wakiishi tena miongoni mwa kufikiria, dhana, au hali ya kuyaepuka mambo. Kwa watu hawa, sababu inayowafanya kuwa na tamanio kuu la kuielewa tabia ya Mungu na kiini Chake ni kwa sababu tabia ya Mungu na kiini Chake ni mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyahitaji wakati wowote katika uzoefu wao, mambo yanayojaza uhai katika maisha yao yote walioishi. Pindi wanapoielewa tabia ya Mungu, wataweza kumheshimu sana kwa njia bora zaidi, kushirikiana kwa njia bora zaidi na kazi ya Mungu, na kuyaweka zaidi katika fikira mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora zaidi wakitumia uwezo wao. Hawa ndio watu wa aina mbili inapokuja katika mielekeo yao kwa tabia ya Mungu. Watu wa aina ya kwanza hawataki kuielewa tabia ya Mungu. Ingawaje wanasema wanataka kuielewa tabia ya Mungu, kupata kumjua Mungu Mwenyewe, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kushukuru kwa dhati mapenzi ya Mungu, ndani yao kabisa wanaona afadhali Mungu asikuwepo. Ni kwa sababu watu wa aina hii wanakosa kumtii Mungu kila wakati na wanampinga; wanapigana na Mungu kwa sababu ya vyeo vilivyo ndani ya mioyo yao na mara nyingi wanashuku na hata kukataa uwepo wa Mungu. Hawataki kuruhusu tabia ya Mungu au kuacha Mungu mwenyewe wa kweli kumiliki mioyo yao. Wanataka tu kutosheleza matamanio, kufikiria, na maono yao binafsi. Hivyo basi, watu hawa wanaweza kumsadiki Mungu, kumfuata Mungu, na hata wanaweza kutupilia mbali familia na kazi zao kwa sababu Yake Yeye, lakini hawasitishi njia zao za maovu. Baadhi yao hata huiba au kubadhiri sadaka au kumlaani Mungu kisirisiri, huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu, kwani hawajawahi kujaribu kumwelewa Mungu. Wanaweza kumjua Mungu kama hawamwelewi? Haiwezekani! Hivyo, ingawa maneno katika mada “kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu mwenyewe” yanaweza kuwa rahisi, maana yao ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa mtu anayekosa kumtii Mungu mara kwa mara, na anampinga Mungu na ni mkatili kwa Mungu, yanamaanisha shutuma; huku kwa mtu anayetafuta uhalisia wa kweli na mara nyingi anakuja mbele ya Mungu kutafuta mapenzi ya Mungu, maneno hayo bila shaka ni kama samaki na maji. Hivyo miongoni mwenu, wakati baadhi yenu mnaposikiza mazungumzo ya tabia ya Mungu na kazi ya Mungu, wanaanza kuumwa na kichwa, mioyo yao inajaa upinzani, na wanakuwa katika hali isiyo na utulivu kabisa. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wanaofikiria: Mada hii ndiyo hasa Ninayohitaji, kwa sababu mada hii ni yenye manufaa sana kwangu. Ni sehemu ambayo haiwezi kukosekana katika uzoefu wangu wa maisha; ni swali ambalo halijapata jibu bado, msingi wa imani kwa Mungu, na jambo ambalo mwanadamu hawezi kufikiria kuliacha. Kwenu nyote, mada hii inaweza kuonekana kuwa karibu na mbali, isiyojulikana ilhali inayozoeleka. Lakini haijalishi ni nini, hii ni mada ambayo kila mmoja aliyeketi hapa lazima aisikilize, aijue, na lazima aielewe. Haijalishi ni vipi utakavyoishughulikia, haijalishi ni vipi utakavyoiangalia au utakavyoipokea, lakini umuhimu wa mada hii huwezi kupuuzwa.
Mungu amekuwa akifanya kazi Yake tangu Alipomuumba mwanadamu. Mwanzoni, kazi ilikuwa rahisi sana, lakini hata hivyo, ingali ilikuwa na maonyesho ya kiini na tabia ya Mungu. Ingawa kazi ya Mungu sasa imepandishwa daraja, na Yeye akitia kiwango kikubwa mno cha kazi thabiti kwa kila mmoja anayemfuata Yeye, na kuonyesha kiwango kikubwa cha neno Lake, kuanzia mwanzo hadi sasa, ubinafsi wa Mungu umekuwa ukifichwa kutoka kwa mwandamu. Ingawaje amekuwa mwili mara mbili, kuanzia wakati wa simulizi za biblia hadi kwa siku za kisasa, nani amewahi kuuona ubinafsi halisi wa Mungu? Kutokana na uelewa wenu, yupo mtu amewahi kuuona ubinafsi halisi wa Mungu? La. Hakuna aliyewahi kuuona ubinafsi halisi wa Mungu, kumaanisha hakuna aliyewahi kuona nafsi ya kweli ya Mungu. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anakubaliana nalo. Hivi ni kusema, ubinafsi halisi wa Mungu, au Roho wa Mungu, amefichwa kutoka kwa ubinadamu wote, wakiwemo Adamu na hawa, ambao Aliwaumba, na akiwemo Ayubu mwenye haki, ambaye alikuwa Amemkubali. Hata wao hawakuuona ubinafsi halisi wa Mungu. Lakini kwa nini Mungu anauficha kimakusudi ubinafsi wake halisi? Baadhi ya watu husema: “Mungu anaogopa kuwaogofya watu.” Wengine husema: “Mungu huuficha ubinafsi Wake halisi kwa sababu binadamu ni mdogo sana na Mungu ni mkubwa sana; wanadamu hawaruhusiwi kumwona Yeye, la sivyo watakufa.” Wapo pia wale wanaosema: “Mungu ameshughulika sana akisimamia kazi Yake kila siku, huenda Asiwe na muda wa kuonekana na kuruhusu watu kumwona Yeye.” Haijalishi ni nini mnachosadiki, Ninayo hitimisho hapa. Hitimisho hilo ni nini? Ni kwamba Mungu hataki hata watu kuuona ubinafsi wake halisi. Akiwa amefichwa kutoka kwa ubinadamu ni kitu ambacho Mungu anafanya kimakusudi. Kwa maneno mengine, ni nia ya Mungu kwa watu kutoona ubinafsi Wake halisi. Hili linafaa kuwa wazi kwa wote sasa. Kama Mungu hajawahi kuuonyesha ubinafsi Wake kwa yeyote, basi mnafikiria ubinafsi wa Mungu upo? (Upo.) Bila shaka upo. Uwepo wa ubinafsi wa Mungu haupingiki. Lakini kuhusu ubinafsi wa Mungu ni mkubwa vipi au unafanana vipi, haya ni maswali ambayo mwanadamu anafaa kuchunguza? La. Jibu ni la. Kama ubinafsi wa Mungu si mada ambayo tunafaa kuchunguza, basi ni swali lipi ambalo tunafaa kuchunguza? (Tabia ya Mungu.) (Kazi ya Mungu.) Kabla hatujaanza kuwasiliana mada hii rasmi, hata hivyo, hebu turudi katika kile tulichokuwa tukikizungumzia muda mfupi uliopita: Kwa nini Mungu hajawahi kuuonyesha ubinafsi Wake kwa mwanadamu? Kwa nini Mungu anaficha kimakusudi ubinafsi wake kutoka kwa mwanadamu? Kunayo sababu moja tu, nayo ni: Ingawaje binadamu aliyeumbwa amepitia miaka elfu na elfu ya kazi ya Mungu, hakuna hata mtu mmoja anayejua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na kiini cha Mungu. Watu kama hao, mbele ya macho ya Mungu, ni upinzani kwake Yeye, na Mungu hatajionyesha kwa watu walio wakatili kwake Yeye. Hii ndiyo sababu ya pekee mbona Mungu hajawahi kumwonyesha binadamu ubinafsi Wake na ndio sababu anaukinga yeye kimakusudi ubinafsi Wake dhidi yao. Sasa mnaelewa kuhusu umuhimu wa kujua tabia ya Mungu?
Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha ubinafsi Wake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza ubinadamu wote na kiini Chake , na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huuficha ubinafsi Wake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minaajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho ubinadamu umekuwa ukitagusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawakaribisha siku zote watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake. Hivi ndivyo binadamu alivyoishi katika Enzi ya Sheria—enzi asilia ya ubinadamu—akiongozwa na Mungu asiyeonekana na asiyegusika.
Mungu alikuwa mwili kwa mara ya kwanza baada ya Enzi ya Sheria, hali ya kupata mwili iliyodumu kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Kwa mwanadamu, miaka thelathini na mitatu na nusu ni muda mrefu? (Si mrefu sana.) Kwa sababu urefu wa maisha ya mwandamu ni mirefu kuliko miaka thelathini-na kitu, huu si muda mrefu kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mwenye mwili, miaka hii thelathini na mitatu na nusu ilikuwa mirefu mno. Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Kiwango cha mateso aliyovumilia Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, kuanzia mwanzo wa kazi Yake hadi wakati Aliposulubishwa kwenye msalaba, huenda kisiwe ni kitu watu wa leo wangeweza kushuhudia wao binafsi, lakini mnaweza angaa kutambua kiasi kupitia hadithi zilizo kwenye Biblia? Licha ya ni maelezo mangapi yaliyopo kwenye ukweli huu uiliorekodiwa, kwa ujumla, kazi ya Mungu katika kipindi hiki kilijaa ugumu na mateso. Kwa mwanadamu aliyepotoka muda wa miaka thelathini na mitatu na nusu si mrefu; mateso kidogo si jambo la kutisha. Lakini kwa Mungu mtakatifu asiye na doa, ambaye lazima avumilie dhambi zote za binadamu, na kula, kulala na kuishi na watenda dhambi, maumivu haya ni mengi mno. Yeye ndiye Muumba, Bwana wa viumbe vyote na Mtawala wa vitu vyote, lakini Alipokuja duniani alilazimika kuvumilia unyanyasaji na ukatili wa wanadamu waliopotoka. Ili kuikamilisha kazi Yake na kuuokoa ubinadamu kutoka kwa taabu, Alilazimika kushutumiwa na binadamu, na kuvumilia dhambi za wanadamu wote. Kiwango cha mateso aliyopitia hakiwezi kwa kweli kueleweka au kutambulika na watu wa kawaida. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake. Je, hii inafichua chochote kuhusu kile Mungu anacho na alicho? Je, wanadamu wanastahili kuijua?
Katika enzi hiyo, japokuwa mwanadamu hakuuona utu wa Mungu, alipokea sadaka ya Mungu dhidi ya dhambi zake na akakombolewa kutoka kwenye msalaba na Mungu. Huenda mwanadamu awe amezoeana na kazi aliyofanya Mungu katika Enzi ya Neema, lakini yupo yeyote aliyezoeana na tabia na mapenzi yalionyeshwa na Mungu katika kipindi hiki? Binadamu anajua tu kuhusu maudhui ya kazi ya Mungu katika enzi tofauti katika vipindi mbalimbali, au anajua hadithi zinazohusiana na Mungu zilizofanyika kwa wakati mmoja na ule Mungu alikuwa akitekeleza kazi Yake. Maelezo haya na hadithi ni kwa ukweli zaidi taarifa fulani tu au hadithi za kumbukumbu kuhusu Mungu, na vyote hivi havina chochote kuhusiana na tabia na kiini cha Mungu. Hivyo haijalishi ni hadithi ngapi watu wanajua kuhusu Mungu, haimaanishi kwamba wanao uelewa wa kina na maarifa kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake. Kama hali ilivyokuwa katika Enzi ya Sheria, ingawaje watu kutoka Enzi ya Neema walikuwa wamepitia mtagusano wa karibu sana na wa kikweli na Mungu wa mwili, maarifa yao kuhusu Mungu na kiini cha Mungu kilikuwa karibu-mambo yasiyokuwepo.
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu akawa mwili tena, kwa njia sawa na ile Aliyotumia mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha kazi, Mungu angali anaonyesha bila kusita neno Lake, anafanya kazi anayofaa kufanya na kuonyesha kile Anacho na alicho. Wakati huohuo, Anaendelea kuvumilia na kustahili na kutotii na kutojua kwa binadamu. Je, Mungu hafichui kila wakati tabia Yake na kuonyesha mapenzi yake katika kipindi hiki cha kazi pia? Hivyo basi, kuanzia uumbaji wa binadamu hadi sasa, tabia ya Mungu, uwepo Wake na milika Yake, na mapenzi Yake, siku zote yamekuwa wazi kwa kila mmoja. Mungu hajawahi kuficha kimakusudi kiini Chake , tabia Yake au mapenzi Yake. Ni vile tu mwanadamu hajali kuhusu kile ambacho Mungu anafanya, mapenzi Yake ni yapi—ndio maana uelewa wa binadamu kumhusu Mungu ni finyu mno. Kwa maneno mengine, wakati Mungu anaficha ubinafsi Wake, Yeye pia Anasimama kando ya mwanadamu kila wakati, akionyesha waziwazi mapenzi Yake, tabia Yake na kiini chake halisi siku zote. Kimsingi, ubinafsi wa Mungu pia uko wazi kwa watu lakini kutokana na upofu na kutotii kwa binadamu, siku zote hawawezi kuuona kuonekana kwa Mungu. Hivyo kama hali iko hivyo, basi si kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe kunafaa kuwa rahisi mno kwa kila mmoja? Hili ni swali gumu sana kujibu, sivyo? Mnaweza kusema ni rahisi, lakini wakati watu wengine wanatafuta kumjua Mungu, hatimaye hawamjui Yeye au kupata uelewa wa wazi kumhusu Yeye—siku zote ni jambo lililojaa ukungu na lisiloeleweka. Lakini mkisema si rahisi, hilo si sahihi vilevile. Baada ya kuwa msomo wa kazi ya Mungu kwa muda mrefu, kila mmoja anafaa, kupitia uzoefu wake, kuwa amepitia kwa kweli mambo mbalimbali na Mungu. Anafaa kuwa amehisi Mungu angaa kwa kiwango fulani katika moyo wake au awali amegongana na Mungu katika kiwango cha kiroho, hivyo anafaa angaa kuwa na uelewa fulani wa kihisia kuhusu tabia ya Mungu au kupata uelewa fulani kumhusu Yeye. Kuanzia wakati binadamu alianza kumfuata Mungu hadi sasa, mwanadamu amepokea mengi mno, lakini kutokana na sababu za aina zote—uhodari wa kimasikini ya kibinadamu, kutojua, uasi, na nia mbalimbali—mwanadamu amepoteza mambo mengi mno. Je, Mungu hajampatia mwanadamu mali ya kutosha? Ingawaje Mungu huficha ubinafsi kutoka Wake kwa wanadamu, Anawatosheleza mahitaji yao na kile Anacho na alicho, na hata maisha Yake; maarifa ya ubinadamu wa Mungu hayafai kuwa vile yalivyo tu sasa. Ndiyo maana Nafikiri inahitajika kuwa na ushirika zaidi na nyinyi kuhusu mada ya kazi ya Mungu, kuhusu tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Kusudio ni ili miaka elfu ya utunzaji na fikira ambayo Mungu amemwagia binadamu isije ikaisha bure bilashi, na ili mwanadamu aweze kuelewa kwa dhati na kutambua mapenzi ya Mungu kwake. Ni ili watu waweze kusonga mbele kwenye hatua mpya ya maarifa yao kumhusu Mungu. Itaweza pia kumrudisha Mungu katika nafasi Yake inayofaa kwenye mioyo ya watu yaani kumfanyia Yeye haki.
Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Nilipata dondoo hizi mahususi kama nyenzo za marejeleo ili kuwasaidia kujua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Hapa Nitawagawiza ili muweze kuona ni aina gani ya tabia na kiini cha Mungu ambacho kimefichuliwa kupitia kwa kazi Yake ya kitambo lakini watu hawajui kukihusu. Sura hizi zinaweza kuwa nzee, lakini mada tunayowasiliana ni kitu kipya ambacho watu hawana na hawajawahi kusikia. Baadhi yenu huenda mkapata hazieleweki—je, kule kuwataja Adamu na Hawa na kurudi kwa Nuhu si kurudia hatua sawa tena? Haijalishi ni nini mnafikiria, sura hizi ni zenye manufaa kwa mawasiliano ya mada hii na zinaweza kutumika kama maandishi ya mafunzo au nyenzo za matumizi ya kwanza katika ushirika wa leo. Mtaelewa nia Zangu za kuchagua sehemu hizi kufikia wakati Nitakapoumaliza ushirika huu. Wale ambao wamesoma Biblia awali huenda wameona mistari hii michache lakini huenda hawajaelewa. Hebu tuangalie haraka kwanza kabla ya kupitia mistari hii mmoja baada ya mwingine kwa kina zaidi.
Adamu na Hawa ni mababu wa mwanadamu. Kama itabidi tutaje wahusika kutoka kwenye Biblia, basi lazima tuanzie kwa wawili hawa. Kisha Nuhu, mababu wa pili wa mwanadamu. Mnaona haya? Mhusika wa tatu ni nani? (Ibrahimu.) Je, nyote mnaijua hadithi ya Ibrahimu? Baadhi yenu mnaweza kuijua, lakini kwa baadhi yenu huenda isiwe wazi sana. Nani ndiye mhusika wa nne? Ni nani anayetajwa kwenye hadithi ya kuangamizwa kwa Sodoma? (Lutu.) Lakini Lutu hajarejelewa hapa. Ni nani anayerejelewa? (Ibrahimu.) Kitu kikuu kilichotajwa kwenye hadithi ya Ibrahimu ni kile Yehova Mungu alikuwa amesema. Je mnaona haya? Nani ndiye mhusika wa tano? (Ayubu.) Je, Mungu hataji mengi kwenye hadithi ya Ayubu wakati wa awamu hii ya kazi Yake? Basi mnajali sana kuhusu hadithi hii? Kama mnajali sana, je mmeisoma hadithi ya Ayubu kwenye Biblia kwa umakinifu? Je, mnajua ni mambo gani Ayubu alisema, ni mambo gani aliyofanya? Wale ambao wameisoma hadithi hiyo sana, ni mara ngapi mmeisoma? Je, mnaisoma mara kwa mara? Akina dada kutoka Hong Kong, tafadhali tuambieni. (Mimi niliisoma mara kadhaa hapo awali tulipokuwa katika Enzi ya Neema.) Hamjawahi soma tena tangu hapo? Kama ni hivyo, basi hiyo ni aibu kubwa. Wacha Niwaambie: Katika awamu hii ya kazi ya Mungu Alimtaja Ayubu mara nyingi, na hilo ni onyesho la nia Zake. Kwamba Alimtaja Ayubu mara nyingi lakini umakinifu wenu haukuzinduliwa ni thibitisho kwa ukweli kwamba: Hamna haja ya kuwa watu ambao ni wazuri na watu wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hii ni kwa sababu mnatosheka tu na kuwa na wazo la juujuu kuhusu hadithi ya Ayubu iliotajwa na Mungu. Mnatosheka na uelewa wa juujuu wa hadithi yenyewe, lakini hamjali kuhusu na hamtaki kufahamu maelezo ya Ayubu ni nani na kusudio linalomfanya Mungu kumrejelea Ayubu mara kadhaa. Kama hata hamjali mtu kama huyo ambaye Mungu amesifu, basi ni nini hasa mnayotilia maanani? Kama hamjali kuhusu na hamjaribu kuelewa mhusika muhimu sana kama huyu ambaye Mungu amemtaja, basi hiyo inasema nini kuhusu mwelekeo wenu katika neno la Mungu? Hilo si jambo baya? Je, hiyo haithibitishi kwamba wengi wenu hawajihusishi katika mambo ya kimatendo na nyinyi nyote hamfuatilii ukweli? Kama unatafuta ukweli, utatilia maanani kwa lazima watu ambao Mungu ameidhinisha na hadithi za wahusika ambazo Mungu amezungumzia. Haijalishi kama unaweza kuithamini au kuipata kuwa hadithi ya dhahiri shahiri, utaenda haraka na kuisoma, kujaribu kuifahamu, kupata njia za kufuata mfano wake, na kufanya kile unachoweza kwa uwezo wako bora zaidi. Hiyo ndiyo tabia ya mtu anayetamani ukweli. Lakini ukweli ni kwamba wengi wenu mlioketi hapa hamjawahi kuisoma hadithi ya Ayubu. Hii kwa kweli inaniambia kitu.
Hebu turudi katika mada niliyokuwa Nikizungumzia muda mfupi uliopita. Sehemu hii ya maandiko inayoshughulikia Enzi ya Sheria ya Agano la Kale ni haswa hadithi za wahusika Nilizokuwa nimedondoa. Hizi ni hadithi zilizozoeleweka kwa wingi wa watu ambao wamesoma Biblia. Wahusika hawa ni wawakilishi sana. Wale waliosoma hadithi hizi wataweza kuhisi kwamba kazi ambayo Mungu amewafanyia wao na maneno ambayo Mungu amewazungumzia yanashikika na yanafikika kwa watu wa leo. Unaposoma hadithi hizi na rekodi hizi kutoka kwenye Biblia, utaweza kuelewa namna ambavyo Mungu alivyofanya kazi Yake na namna alivyoshughulikia watu wakati huo. Lakini kusudio la Mimi kutafuta sura hizi leo si eti kwamba uweze kujaribu kung'amua hadithi hizi na wahusika ndani zao. Badala yake, ni ili uweze kupitia kwa hadithi zawahusika hawa , kuona vitendo vya Mungu na tabia Yake, na hivyo kurahisisha kujua na kuelewa Mungu, kuuona upande halisi Wake yeye, kusitisha kufikiria kwako, na kukomesha dhana zako kuhusu Yeye, na kusitisha imani yako na kuitoa katika hali ya kutokuwa na hakika. Kujaribu kuifahamu tabia ya Mungu na kuielewa na kupata kujua Mungu mwenyewe bila ya msingi, kunaweza mara nyingi kukufanya kuhisi kama mtu asiyeweza, asiye na nguvu, na asiye na hakika ni wapi wataanzia. Na ndiyo maana Nilifikiria ni wazo zuri kutumia mbinu kama hii na mtazamo ili kukufanya kuelewa kwa njia bora zaidi Mungu, na kwa uhalisia zaidi kutambua na kushukuru mapenzi ya Mungu na kupata kuijua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe na kukufanya kuhisi kwa dhati uwepo wa Mungu na kushukuru mapenzi Yake kwa wanadamu. Je, haya si ya manufaa kwenu? Sasa mnahisi vipi ndani ya mioyo yenu mnapoziangalia hadithi hizi na maandiko haya tena? Je, mnafikiria maandiko haya Niliyoyachukua yamezidi kuliko kawaida? Lazima Nitilie mkazo tena kile Nimetoka tu kuwaambia. Nia ya kuwaruhusu kusoma hadithi hizi za wahusika ni kuwasaidia kuelewa namna ambavyo Mungu anafanya kazi Yake kwa watu na mwelekeo Wake kwa wanadamu. Ni kupitia nini ndipo mtaweza kuelewa haya? Kupitia kwa kazi ambayo Mungu amefanya kitambo, na kuunganisha pamoja na kazi ambayo Mungu anafanya sasa hivi kuwakusaidia kuelewa mambo mbalimbali kuhusu Yeye. Mambo haya mbalimbali ni ya kweli, na lazima yajulikane na yatambulike na wale wanaotaka kumjua Mungu.
Tutaanza sasa na hadithi ya Adamu na Hawa. Kwanza, hebu tuyasome maandiko.
A. Adamu na Hawa
1. Amri ya Mungu kwa Adamu
(Mwa 2:15-17) BWANA Mungu akamchukua huyo mtu, na akamweka katika bustani ya Edeni ili ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwamuru huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula: Lakini ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usiyale: kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa.
Je, mlielewa chochote kutoka kwenye mistari hii? Je, ni vipi ambavyo sehemu hii ya maandiko inavyo wafanya kuhisi? Kwa nini “Amri ya Mungu kwa Adamu” ilidondolewa kutoka kwa maandiko? Je, kila mmoja wenu sasa anayo picha ya Mungu na Adamu katika akili yenu? Mnaweza kujaribu kufikiria: Kama ni nyinyi mliokuwa katika tukio hilo, je, Mungu katika moyo wenu angekuwa vipi? Ni hisia gani ambazo picha hii zinafanya mhisi? Hii ni picha ya kusisimua na ya kutuliza moyo. Ingawaje kunaye Mungu tu na binadamu ndani yake, ule ukaribu kati yao unastahili kuonewa wivu: Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu; Mungu anaonyesha hali ya kujali binadamu huku naye binadamu anaishi katika ulinzi na baraka za Mungu; kila kitu binadamu anachofanya na kusema kinaunganishwa kwa karibu na Mungu na hakiwezi kutofautishwa.
Mnaweza kusema kwamba hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu aliyoitoa kwa binadamu tangu kumuumba yeye. Je, amri hii ina nini? Amri hii inayo mapenzi ya Mungu, lakini pia inayo wasiwasi Wake kwa wanadamu. Hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu na pia ndio mara ya kwanza Mungu anakuwa na wasiwasi kuhusu binadamu. Hivi ni kusema, Mungu analo jukumu kwa binadamu tangu ule wakati alipomuumba yeye. Jukumu Lake ni lipi? Lazima amlinde binadamu, kumwangalia binadamu. Anatumai kwamba binadamu anaweza kuamini na kutii maneno Yake. Hili pia ndilo tarajio la kwanza la Mungu kwa binadamu. Na ni kwa tarajio hili kwamba Mungu anasema yafuatayo: “Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula: Lakini ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usiyale: kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo hakika utakufa.” Maneno haya rahisi yanawakilisha mapenzi ya Mungu. Yanafichua pia kwamba moyo wa Mungu tayari umeanza kuonyesha hali ya kujali binadamu. Miongoni mwa mambo yote, ni Adamu pekee aliyeumbwa kwa taswira ya Mungu; Adamu alikuwa kiumbe wa pekee aliye hai aliye na pumzi ya uhai ya Mungu; angeweza kutembea na Mungu, kuzungumza na Mungu. Na ndiyo maana Mungu alimpa amri kama hiyo. Mungu aliweka wazi katika amri hii kile binadamu anaweza kufanya, na vilevile akaweka wazi kile asichoweza kufanya.
Katika maneno haya machache rahisi, tunauona moyo wa Mungu. Lakini ni aina gani ya moyo tunaouona? Je, kunao upendo katika moyo wa Mungu? Je, upendo huo unao hali yoyote ya kujali ndani yake? Upendo wa Mungu na kujali kwake katika mistari hii hakuwezi kutambulika na kuthaminiwa tu na watu, lakini unaweza pia kuhisiwa vizuri na kwa kweli. Hayo ni kweli? Kwa vile nimesema tayari mambo haya, bado mnafikiria kwamba haya ni maneno machache tu rahisi? Si rahisi hivyo, kweli? Mngeweze kuona hivi awali? Kama Mungu mwenyewe angekuambia maneno hayo machache ungehisi vipi ndani yenu? Kama wewe si mtu mwenye utu, kama moyo wako ni baridi kama barafu, basi usingehisi chochote, usingethamani upendo wa Mungu, na usingejaribu kuuelewa moyo wa Mungu. Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha. Je, hayo ni kweli? Unapohisi mambo haya, utatenda vipi kwa Mungu? Utahisi ukiwa umeunganishwa kwa Mungu? Utampenda na kumheshimu Mungu kutoka kwenye sakafu ya moyo wako? Moyo wako utakuwa karibu zaidi na Mungu? Unaweza kuona kutoka kwa haya namna ambavyo upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa binadamu. Lakini kile kilicho muhimu zaidi ni kuthamini na kufahamu kwa binadamu upendo huu wa Mungu. Kwa hakika, Mungu hasemi mambo mengi yanayofanana kwenye awamu hii ya kazi Yake? Lakini je, watu wa leo wanauthamini moyo wa Mungu? Je, mnaweza kung'amua mapenzi ya Mungu Niliyoyazungumzia muda mfupi uliopita? Hamwezi hata kutambua mapenzi ya Mungu wakati yanaonekana waziwazi, yanaweza kushikika na ni ya kihalisia. Na ndiyo maana Nasema hamna maarifa na uelewa halisi wa Mungu. Je, haya si kweli? Hayo tu ndiyo yote tutakayowasiliana nanyi kwenye sehemu hii.
2. Mungu Amuumba Hawa
(Mwa 2:18-20) BWANA Mungu akasema, Si vizuri kwamba huyo mtu awe peke yake; Nitamfanyia msaidizi wa kupatana naye. Na kutoka katika ardhi BWANA Mungu akaumba kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani; akamletea Adamu ili aone atawaitaje: na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo. Adamu akawapa majina kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakupatikana wa kumsaidia Adamu aliyefanana.
(Mwa 2:22-23) Na ule ubavu, ambao BWANA Mungu aliuchukua kutoka kwa Adamu, yeye akaufanya mwanamke, na akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama zangu: basi ataitwa Mwanamke, kwa maana ametwaliwa kutoka kwa Mwanamume.
Kunazo kauli kuu chache kwenye sehemu hii ya maandiko. Tafadhali zichoree mstari chini: “na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo.” Kwa hivyo ni nani aliyepatia viumbe wote haya majina yao? Alikuwa Adamu, si Mungu. Kauli hii inamwambia mwanadamu ukweli: Mungu alimpa binadamu werevu alipomuumba Yeye. Hivi ni kusema kwamba, werevu wa binadamu ulitoka kwa Mungu. Hili ni kweli. Lakini kwa nini? Baada ya Mungu kumuumba Adamu, Adamu alienda shuleni? Je, alijua namna ya kusoma? Baada ya Mungu kuwaumba viumbe hai mbalimbali, je Adamu aliwatambua wanyama hawa wote? Je, Mungu alimwambia majina ya viumbe hao? Bila shaka, Mungu pia hakumfunza namna ya kutunga yale majina ya viumbe hawa. Huo ndio ukweli! Basi alijua vipi namna ya kupatia viumbe hawa hai majina yao na aina gani ya majina ya kuwapatia? Haya yote yanahusiana na swali kuhusu ni nini ambacho Mungu aliongezea kwa Adamu alipomuumba yeye. Ukweli unathibitisha kwamba wakati Mungu alipomuumba binadamu Alikuwa ameongezea werevukwake. Huu ni ukweli muhimu sana. Je, nyinyi nyote mmesikiliza kwa makini? Kunao ukweli mwingine muhimu ambao unafaa kuwa wazi kwenu? Baada ya Adamu kuwapatia viumbe hai majina yao, majina haya yalipangwa kwenye msamiati wa Mungu. Kwa nini Ninasema hivyo? Hii pia inahusisha tabia ya Mungu, na lazima Niielezee.
Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele. Kwa hivyo kauli hii “na kila ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, likawa ndilo jina lake kuanzia siku hiyo” inaonyesha nini? Inaopendekeza kwamba Mungu hakufanya marekebisho yoyote kwa majina ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema “Ndiyo” na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwengine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu. Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa. Hili ni jambo dogo tu, lakini kama huelewi kiini cha Mungu, kama moyo wako hautajaribu kujua namna ambavyo Mungu anatenda na mwelekeo wa Mungu ni ipi, basi hutajua tabia ya Mungu au kuyaona maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu. Je, hayo si kweli? Je, unakubali kile Nimetoka tu kukuelezea? Kwa kujibu matendo ya Adamu, Mungu hakutangaza kwa sauti kwamba, “Umefanya vyema. Umefanya sahihi Ninakubali.” Katika Moyo Wake, hata hivyo, Mungu aliidhinisha, akathamini, akashangilia kile Adamu alikuwa amefanya. Hili ndilo jambo la kwanza tangu uumbaji ambalo binadamu alikuwa amemfanyia Mungu akifuata maagizo Yake. Ni jambo ambalo binadamu alifanya badala ya Mungu na kwa niaba ya Mungu. Mbele ya macho yake, hili lilitokana na werevu Aliokuwa amempa binadamu. Mungu aliliona kama jambo zuri, kitu kizuri. Kile ambacho Adamu alifanya wakati huo kilikuwa maonyesho ya kwanza ya werevu wa Mungu kwa binadamu. Hili lilikuwa onyesho zuri kutoka kwa maoni ya Mungu. Kile Ninachotaka kukuambia nyinyi hapa ni kwamba nia ya Mungu katika kuongezea sehemu ya kile Anacho na alicho na werevu wake kwa binadamu ilikuwa ili mwanadamu aweze kuwa kiumbe hai anayemwonyesha Yeye. Kwa kiumbe hai kama huyo kufanya mambo hayo kwa niaba yake, ilikuwa ndicho hasa kile Mungu alikuwa akitamani kuona.
3. (Mwa 3:20-21) Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mama ya wote walio hai. Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.
Hebu tuangalie kifungu hiki ya tatu, kiachosema kwamba, kunayo maana katika jina Adamu alimpa Hawa, kweli? Hii inaonyesha kwamba baada ya kuumbwa, Adamu alikuwa na fikira zake na alielewa mambo mengi. Lakini kwa sasa, hatutasoma na kuchunguza kile alichoelewa au kwa kiwango kipi alielewa kwa sababu hiyo si hoja kuu Ninayotaka kuzungumzia kwenye kifungu hiki ya tatu. Hivyo hoja kuu katika kifungu cha tatu ni gani? Hebu na tuuangalie mstari huo, “Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.” Kama hatutakuwa na ushirika kuhusu mstari huu wa maandiko leo, huenda hamtawahi kutambua uzito ulio katika maneno haya. Kwanza, hebu niwape vidokezo fulani. Panua kufikiria kwenu na kuona picha ya bustani ya Edeni, huku Adamu na Hawa wakiishi ndani. Mungu anaenda kuwatembelea lakini wanajificha kwa sababu wako uchi. Mungu hawezi kuwaona, na baada ya kunawaita wao, wanasema, “Hatuwezi kudhubutu Kuwaona kwa sababu tuko uchi.” Hawathubutu kumwona Mungu kwa sababu wako uchi. Kwa hivyo Yehova Mungu anawafanya nini? Mandishi asilia yanasema: “Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha.” Sasa mnajua kile Mungu alitumia kutengeneza nguo zao? Mungu alitumia ngozi za wanyama kutengeneza nguo zao. Hivyo ni kusema, nguo ambazo Mungu alitengenezea binadamu zilikuwa za koti la manyoya. Hiki ndicho kilichokuwa kipande cha kwanza cha nguo ambacho Mungu alitengenezea binadamu. Koti la manyoya ni mavazi ya soko la vitu vya bei ghali kwa viwango vya leo, kitu ambacho si kila mtu anaweza kumudu kuvaa. Kama mtu atakuuliza: Kipande cha kwanza cha nguo kilichovaliwa na wazee wa wanadamu kilikuwa kipi? Unaweza kujibu: Kilikuwa ni koti la manyoya. Nani aliyekitengeneza hicho koti la manyoya? Unaweza kujibu zaidi: Mungu alikitengeneza! Hiyo ndiyo hoja kuu: Nguo hii ilitengenezwa na Mungu. Je, hilo ni jambo la kutilia maanani, sivyo? Kwa vile sasa nimetoka kukifafanua, picha imeibuka katika akili zenu ? Kunafaa kuwa angaa na mpangilio wa juu kukihusu. Hoja ya kuwaambia haya leo si kuwafahamisha kuhusu kipande cha kwanza cha nguo cha binadamu kilikuwa nini. Hivyo hoja ni gani? Hoja si lile koti la manyoya, lakini namna ya kujua tabia na uwepo na milika zilizofichuliwa na Mungu alipokuwa Akifanya hivi.
Katika picha hii ya “Pia BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi; na akawavisha,” ni wajibu gani ambao Mungu anatekeleza anapokuwa na Adamu na Hawa? Na ni katika aina gani ya uajibu ambao Mungu anajitokeza katika uliwengu akiwa tu na wanadamu wawili? Kutekeleza wajibu wa Mungu? Kaka na dada kutoka Hong Kong, tafadhali jibuni. (Kutekeleza wajibu wa mzazi.) Kaka na dada kutoka Korea Kusini, ni wajibu wa aina gani mnafikiria Mungu anatekeleza hapa? (Kiongozi wa familia.) Kaka na dada kutoka Taiwan, mnafikiria nini? (Wajibu wa mtu katika familia ya Adamu na Hawa, wajibu wa mwanafamilia.) Baadhi yenu mnafikiria kuwa Mungu anajitokeza kama mwanafamilia wa Adamu na Hawa, huku baadhi wakisema kwamba Mungu anajitokeza kama kiongozi wa familia na wengine wanasema kwamba Anajitokeza kama mzazi. Haya yote yanafaa sana. Lakini ni nini hasa Ninachotilia mkazo hapa? Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminfu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu. Hapa, ukweli na unyenyekevu wa Mungu unawezesha zaidi watu kuona namna ambavyo Anapendeka. Kwa kinyume cha mambo, yule Mungu mkubwa sana, Mungu anayependeka na yule Mwenyezi Mungu katika mioyo ya watu ni mdogo sana, asiyevutia, na asiyeweza kuhimiliwa hata mara moja. Unapouona mstari huu na kuisikia hadithi hii, unamkasirikia Mungu kwa sababu Alifanya kitu kama hiki? Baadhi ya watu wanaweza kufanya hivyo, lakini kwa wengine itakuwa ni tofauti kabisa. Watafikiri Mungu ni mkweli na anapendeka, na hasa ni ule ukweli na uzuri wa Mungu ndiyo unaowafurahisha. Kwa kadri wanavyoona ule upande wa kweli wa Mungu, ndipo wanapothamini uwepo wa kweli wa upendo wa Mungu, umuhimu wa Mungu katika mioyo yao, na namna anavyosimama kando yao kila muda.
Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahali, na enzi. Ukweli na uzuri wa Mungu unaweza kwa kweli kuonyeshwa kupitia kufanya jambo ambalo watu wanafikiria si la kipekee na ni dogo, jambo ambalo ni dogo sana kiasi cha kwamba watu hata hawafikirii angeweza kufanya. Mungu si mnafiki. Hakuna kupiga chuku, kufunika ukweli, majivuno au kiburi katika tabia na kiini Chake. Siku zote Hajigambi, lakini badala yake Anapenda, Anaonyesha hali ya kujali, Anaangalia, na kuwaongoza wanadamu Aliowaumba kwa uaminifu na dhati. Haijalishi ni kiwango kipi ambacho watu wanaweza kuthamini, kuhisi, au kuona, Mungu kwa hakika anafanya mambo haya. Je, kujua kwamba Mungu anacho kiini kama hicho kunaweza kuathiri upendo wa watu kwake Yeye? Kutaweza kushawishi namna wanavyomcha Mungu? Ninatumai utakapoelewa upande halisi wa Mungu utaweza kuwa hata karibu zaidi na Yeye na kuweza kuthamini hata zaidi na kwa kweli upendo Wake na utunzaji Wake kwa wanadamu, huku wakati huohuo pia kumpa moyo wako na kutowahi tena kuwa na shaka au wasiwasi wowote kwake Yeye. Mungu anafanya kimyakimya kila kitu Alicho nacho kwa ajili ya binadamu, akifanya kimyakimya kupitia ukweli, uaminifu, na upendo Wake. Lakini siku zote Hana hofu au majuto yoyote kwa yale yote Anayofanya, wala hahitaji mtu yeyote kumlipa Yeye kwa njia yoyote au kuwa na nia za kuwahi kupokea kitu kutoka kwa wanadamu. Kusudio tu la kila kitu Alichowahi kufanya ni ili Aweze kupokea imani na upendo wa kweli kutoka kwa wanadamu. Hebu tuhitimishe mada hii ya kwanza hapa.
Je, mazungumzo haya yamewasaidia? Yamewasaidia kwa kiasi kipi? (Uelewa na maarifa zaidi kuhusu upendo wa Mungu.) (Mbinu hii ya mawasiliano inaweza kutusaidia katika siku za mbele ili kuweza kuthamini zaidi neno la Mungu, kufahamu hisia alizokuwa nazo na maana ya mambo Aliyoyasema Alipoyasema, na kuhisi namna Alivyohisi wakati huo.) Je, yupo yeyote kati yenu anayehisi hata zaidi uwepo halisi wa Mungu baada ya kuyasoma maneno haya? Je, mnahisi uwepo wa Mungu si mtupu wala wa kutiliwa mashaka tena? Pindi mnapokuwa na hisia hii, mnahisi kwamba Mungu yupo tu kando yenu? Pengine hisia hiyo si ya dhahiri kwa sasa hivi au hamtaweza kuihisi sasa hivi bado. Lakini siku moja, mtakapokuwa na shukrani ya kina na ya kweli na maarifa halisi kuhusu tabia na kiini cha Mungu ndani ya moyo wako, utahisi kwamba Mungu yupo tu kando yako—ni vile tu kwamba haujawahi kumkubali kwa kweli Mungu ndani ya moyo wako. Haya ni halisi.
Mnafikiria vipi kuhusu mbinu hii ya mawasiliano? Mnaweza kuiendeleza? Mnafikiria aina hii ya ushirika kuhusu mada ya kazi ya Mungu na tabia ya Mungu ni nzito? Mnahisi vipi? (Vizuri sana, kuchangamka.) Ni nini kilichowafanya kuhisi vizuri? Kwa nini mlichangamka? (Ilikuwa sawa na kurudi kwenye Bustani ya Edeni, kurudi kuwa kando ya Mungu.) “Tabia ya Mungu” kwa kweli ni mada ambayo haijazoeleka sana na kila mmoja, kwa sababu kile ambacho unafikiria kwa kawaida, kile unachosoma kwenye vitabu au hapa kwenye ushirika, siku zote hukufanya kuhisi kama mtu asiyeona akimgusa ndovu—unahisi tu kila pahali kwa kutumia mikono yako, lakini kwa hakika huoni chochote kwa macho yako. Mguso wa mkono hauwezi tu kukupa mpangilio wa kimsingi wa maarifa ya Mungu, wacha hata dhana iliyo wazi. Kile ambacho mguso wa mkono unakupatia ni kufikiria zaidi, kiasi kwamba huwezi kufafanua kwa uhakika tabia ya Mungu na kiini halisi. Badala yake, masuala haya ya kutokuwa na uhakika yanayotokana na kufikiria kwako huwa siku zote yanaonekana kujaza moyo wako na shaka. Wakati ambapo huwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu na ilhali bado unajaribu kukielewa, ndani ya moyo wako bado siku zote kutaendelea kuwa na mambo yanayopingana na ukinzana, na wakati mwingine huenda hata yakabadilika na kuwa shida, na kukufanya kuhisi ni kana kwamba umepoteza kitu. Je, si jambo la kusikitisha sana unapotaka kumtafuta Mungu, kumjua Mungu, na kumwona Yeye waziwazi, lakini siku zote kutoweza kupata majibu? Bila shaka, maneno haya yanalengwa kwa wale wanaotamani kutafuta uwezo wa kumuheshimu sana Mungu na kuridhisha Mungu. Kwa wale watu ambao hawatilii maanani mambo kama haya, hili kwa hakika si muhimu kwa sababu wanatumaini kwamba ni bora zaidi kwamba uhalisi na uwepo wa Mungu uwe ni ngano ya kale au ndoto, ili waweze kufanya chochote wanachotaka, ili waweze kuwa wale wakubwa zaidi na wenye umuhimu zaidi, na kuweza kutenda vitendo vya maovu bila ya kujali athari zake, na hivyo basi kutoweza kukabiliana na adhabu au kulazimika kuwajibika , ili hata mambo ambayo Mungu anasema kuwahusu watendaji maovu hayataweza kuwahusu wao. Watu hawa hawako radhi kufahamu tabia ya Mungu, wamechoshwa na kujaribu kujua Mungu na kila kitu kuhusu Yeye. Wangependelea kwamba Mungu asiwepo. Watu hawa wanampinga Mungu na wao ndio watakaoondolewa.
Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.
Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. Mungu alimruhusu Nuhu kujenga safina ili kuokoa familia yake ya wanane, kuwaruhusu kuweza kuishi, ili kuwa babu wa kizazi kifuatacho cha wanadamu. Sasa hebu tuyasome maandiko.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni