4/27/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | 9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Zhang Min, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mvua ilianza kunyesha sana asubuhi. Kufikia wakati wa adhuhuri wakati nilipaswa kwenda kwa mkutano, niliona mvua ilikuwa nzito sana kiasi kwamba sikutaka kwenda. Lakini ulikuwa mara moja tu kwa wiki, kama singeenda singekuwa na njia yoyote ya kufanya kazi yangu ya kanisa. Chochote kilichokuwako kikiendelea nje, bado ilinipasa nishiriki nao. Nilipofikiria hayo, niliharakisha kwenda kwa mkutano. Baada ya saa kumi alasiri hiyo, yule ndugu wa kiume wa mahali pa kukutana alikimbia akarudi nyumbani akisema: "Bado mnafanya mkutano, endeni nyumbani, kuna maji mengi yanayoteremka pale." Nilikwenda na kuangalia na kulikuwa na maji mengi sana yaliyokuwa yakiteremka, mto huo ulikuwa umefurika na ukipanda juu sana. Sikuwa nimewahi kuona maji mengi hivyo, sikuwa na namna ya kwenda nyumbani. (Hadi kwangu ilikuwa ni mita 300 nje ya kijiji hiki.) Nilikuwa na wasiwasi sana. Hakukuwa na chochote ambacho ningeweza kufanya, ilinibidi nirudi mahali pa mkutano, kwa sababu mahali hapo palikuwa juu, na salama. Baada ya muda mfupi nikasikia sauti za makelele zikitoka nje. Nilikwenda kutazama, na ilikuwa ni watu wazima na watoto wa kijiji changu wakija kwa kutumia kamba na fito. Nikakimbia kuuliza jinsi nyumba yangu ilivyokuwa, na mtu fulani aliniambia kuwa ilikuwa imesongwa na maji, lakini maji yalikuwa kimo cha juu nje ya ukuta wa uga. Nikafikiria mwenyewe: Vitu vyote viko mikononi mwa Mungu. Hata kama nyumba hiyo imesongwa na maji, kuna kusudi jema la Mungu ndani yake.
Alfajiri ya siku ya pili, nilirudi nyumbani pamoja na wale watu wengine wa kijiji. Tukiingia ndani ya kijiji sisi sote tulikodoa macho, tukipigwa na bumbuazi. Maji ya mvua yalikuwa yameacha mkuza wa machafuko pande zote za kijiji, hatungeweza kabisa kuyaamini macho yetu. Lakini jambo lililonishangaza sana lilikuwa hili. Kulikuwa na nyumba kumi na nane tu katika kijiji chetu, ni nyumba nne tu zilizokuwa upande wa chini sana, na yangu ndiyo iliyokuwa hatari zaidi. Kama maji katika mitaro yangetiririka chini yote yangekusanyika nyuma ya nyumba yangu, na yangesomba nyumba yangu wakati wowote. Sijawahi kamwe kufikiria kwamba maji ya mafuriko yangepitia kabisa kando ya nyumba yangu, na nilishangaa hata zaidi nilipoingia ndani ya uga. Mchanga na matope yaliyoteremka kutoka kwa uga wa nyumba iliyokuwa juu yalilitoka kwa mtata fulani nje ya ukuta wa uga hadi kwa nyumba mbele ya yangu, hivyo nyumba yangu ilikuwa salama salimini. Ingawa kulikuwa na ukuta mdogo wa bwawa uliodhibitiwa nyuma ya nyumba yangu, miamba ilikuwa midogo sana, lakini haikuwa imesombwa na mafuriko. Tofauti na hiyo, nyumba ambazo watu kwa kawaida wangedhani zilikuwa imara na salama, kuta za nyua zao zilisombwa na maji, au zilikuwa zimegubikwa na mchanga, na baadhi yazo zilijaa maji. Kati ya kaya kumi na nane ni tano tu ambazo hazikupatwa na maafa, zingine zote zilikumbwa na uharibifu. Nilipoona tukio hili, moyo wangu ulikimbia. Sikujua jinsi ya kuonyesha hisia zangu. Lakini baada ya msisimko wangu, nilianza kuchukia jinsi nilivyoujeruhi moyo wa Mungu daima kabla, kumuasi na kumpinga Mungu sana. Kwa kweli sikustahili wema huu, ulinzi huu, ambao Mungu alinipa.
Ni wakati tu nilipopitia mafuriko haya ya kuogofya nilipohisi kikamilifu maana ya maneno ya Mungu: “kwamba bila huduma, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi juhudi au mapambano yake” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). “mtu anaweza kufanya mipango elfu moja, au mipango elfu kumi, lakini hatimaye hawezi kutoroka kutoka kwa kiganja cha mkono Wangu. Vitu vyote na matukio huendeshwa katika mikono Yangu” (Matendo na Ushuhuda wa Kristo Hapo Mwanzo). Kwamba neno la Mungu huahidi watu kwamba Mungu hutunza na hulinda, kwamba Mungu hutawala vyote, kamwe halitakuwa tena fungu la maneno tu kwangu. Katikati ya maafa haya nilipata nuru kwa wingi. Nilipata uzoefu kwamba tukiweka mustakabali na jaala zetu mikononi mwa Mungu, sio kuandaa mbadala na mipango kwa ajili yetu wenyewe, lakini kutafuta ukweli na kumridhisha Mungu kikamilifu, basi bila kujali ni hali ipi Mungu atatufadhili, kutulinda, na kutusaidia wakati wa matatizo yoyote. Kwa sababu Mungu ni mwenye haki kwa kila mtu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi MunguUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni