Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya Mungu, iwe ni kwa mwili au kwa Roho, yote inafanywa kulingana na mpango wa usimamizi. Kazi Yake haifanywi kulingana na kama ni ya umma au ya kibinafsi, au kulingana na mahitaji ya mwanadamu—inafanywa kikamilifu kulingana na mpango wa usimamizi. Hatua hii ya kazi haiwezi kufanywa kwa njia yoyote ya zamani: Inapaswa kukamilika juu ya msingi wa hatua mbili zilizopita za kazi. Hatua ya pili ya kazi iliyokamilishwa wakati wa Enzi ya Neema ilimpa mwanadamu ukombozi. Hii ilifanywa na Mungu mwenye mwili. Sio kwamba Roho hangeweza kufanya hatua ya sasa ya kazi, Roho pia alikuwa na uwezo, lakini hangekuwa mwenye kufaa sana, mwenye uwezo wa kumwokoa mwanadamu, kama vile kupata mwili.
Ni kwa kiwango gani hasa ndio watu wangeweza kuunda dhana kuhusu Roho na watu wangekuwa waasi jinsi gani kwa Roho? Baada ya yote, Roho hana uwezo wa kumshinda mwanadamu na kuwezesha ufahamu wa watu kumhusu Mungu kama kupata mwili. Ikiwa Roho ndiye Afanyaye kazi, Hawezi kuwa na watu daima; haiwezekani Roho kuongea moja kwa moja na watu na kuishi na kuzungumza nao uso kwa uso kama vile mwili unavyofanya sasa. Wakati mwingine Roho hawezi tu kufunua mambo ndani ya watu kama vile kupata mwili hufanya. Hatua hii ya kazi ambayo kupata mwili kunafanya inahusu hasa kumshinda na, kisha, kumkamilisha mwanadamu, kumruhusu mwanadamu kujua na kumwabudu Mungu. Hii ni kazi ya kumaliza enzi. Ikiwa hatua hii ya kazi haingehusu kumshinda binadamu, lakini kwa kumruhusu mwanadamu kujua kwamba Mungu yupo kweli, basi bila shaka Roho angeweza kufanya kazi hii. Ikiwa mnafikiri kwamba Roho anaweza kushikilia nafasi ya mwili wakati wa utekelezaji wa hatua hii ya kazi—angeweza kufanya kazi hii pia, kwa sababu Mungu ni mwenyezi—kama mnafikiri kuwa ikiwa ni mwili au Roho, Wote wawili wangeweza kutimiza matokeo sawa, basi mtakuwa mmekosea. Kazi Yake inafanywa kulingana na usimamizi Wake, kulingana na mpango na hatua ambazo Anamshughulikia mwanadamu. Sio kama unavyofikiri, kwa namna fulani, kwa sababu Roho, mwili na Mungu Mwenyewe ni wote wenye nguvu kabisa, kwamba Anaweza kufanya kazi kwa njia yoyote ya zamani Anayopenda. Kazi ya Mungu hufanywa kulingana na mpango wa usimamizi na utekelezaji wa kazi Yake, bila kujali ni hatua ipi, daima hufuata njia maalum ya hatua. Utekelezaji wa hatua hii na maelezo yote yamepangwa. Hatua ya kwanza ya kazi ilikamilishwa Uyahudi, hatua hii ya kazi inafanywa katika nchi ya joka kuu jekundu. Watu wengine huuliza: Haingetekelezwa katika nchi nyingine?" Kulingana na mpango wa usimamizi wa hatua hii ya kazi, hatua hii ni muhimu lazima itekelezwe katika nchi hii. Watu wa nchi hii ni wenye maendeleo kidogo mno na maisha yao yamepotoka, wako chini ya umiliki wa Shetani, na nchi yenyewe haina haki za binadamu na uhuru. Ikiwa ni kama mlivyosema, basi hakungekuwa na maana kwa kupata mwili kwa Mungu katika hatua hii. Ikiwa ingeweza kufanywa kwa njia yoyote ya zamani, maana ingekuwa nini? Haijalishi ni hatua gani Yeye anatekeleza, daima kuna umuhimu wa dhahiri—hatua inatekelezwa kwa namna fulani kwa sababu lazima ifanywe kwa njia hii. Hii ndiyo sababu kufanya mambo kwa njia hii ni kwa maana. Ingekuwa kama mlivyosema, kama ingeweza kufanywa kwa njia yoyote ya zamani, basi itakuwa haina maana. Chukua chakula, kwa mfano: Ikiwa mtu anahisi angeweza kula chakula au ashinde bila, basi chakula hicho hakina thamani kwa mtu huyo. Ikiwa yeye hasa ana njaa na chakula hicho kiwekwe mbele yake, basi kuna umuhimu mkubwa kwake kula hicho chakula kwa sababu ana njaa. Usielewe visivyo jambo hili. Kazi inayofanywa katika mwili ina uwezo wa kufanikisha matokeo fulani, kama vile kazi inayofanywa na Roho ina uwezo wa kufanikisha matokeo yake binafsi fulani. Anafanya uchaguzi Wake kati ya mwili na Roho kulingana na njia ipi au kipengele kipi kitafaa zaidi kwa kupata matokeo fulani. Kwa mfano, ikiwa kuna joto jingi nje, basi kuvaa jaketi yenye pedi ya pamba itakuwa isiostarehesha kabisa, lakini katika majira ya baridi itafaa kabisa. Njia ya manufaa zaidi ndiyo inayochaguliwa. Sio kama mlivyosema, kwamba njia yoyote pekee ya zamani ni nzuri—kwamba mwili unaweza kufanya kazi, kuonekana katika sura yoyote au kwamba Roho anaweza kufanya kazi hata kama Hakutani na watu na Watakuwa na uwezo wa kufikia matokeo fulani. Mungu ni mwenyezi. Mungu ana upande wa utendaji ambao watu hawauoni. Watu daima wanamfikiria kuwa Mungu sio mwenye busara, Hana uhalisi—wanafikiri kwamba Yeye hufanya kitu chochote cha zamani Anachofikiria bila maana yoyote maalum. Wanafikiri kwamba maana machoni pa Mungu ni vitu tu vilivyoundwa—kana kwamba Anasema tu chochote Anachotaka. Watu wanapaswa kujua kwamba ndani ya hili kuna ukweli. Namna ambayo Mungu anafanya kazi ni yenye maana, inazungukwa na umuhimu na inatimiza matokeo bora zaidi. Yote yanafanyika kuhusiana na kusudi fulani, maana na mpango. Wewe unafikiri kuwa kazi yote ya Mungu inafanywa tu bila utaratibu maalum? Ana kipengele chenye nguvu kabisa, lakini pia Ana kipengele cha vitendo. Ufahamu wako juu Yake ni wa upande mmoja tu, kuna matatizo mengine ya ufahamu wako juu ya kudura ya Mungu na hata zaidi kwa ufahamu wako juu ya kipengele chake cha vitendo—ufahamu wako wa kipengele Chake cha vitendo ni chenye matatizo hata zaidi. Roho alifanya hatua ya kwanza ya kazi na mwili ulifanya ya pili na ya tatu. Yote hii ilikuwa imezungukwa na umuhimu. Chukua[a] kusulubiwa kwa Yesu msalabani: Je, kungekuwa na maana yoyote ya kumsulubisha Roho msalabani? Roho hahisi maumivu yoyote, kwa hiyo hakungekuwa na maana. Kwa hatua hii ya kazi ya kumshinda mwanadamu, Roho hakuweza kushikilia nafasi ya mwili—Roho hawezi kufanya kazi ya mwili, kama vile mwili hauwezi kufanya kazi ya Roho. Katika hatua yoyote ya kazi, uteuzi wa mwili au Roho daima una umuhimu wa dhahiri katika kufikia matokeo bora zaidi na kufanikisha kusudi la mpango wa usimamizi wa Mungu. Mungu ana kipengele chenye nguvu na kipengele cha utendaji: Haijalishi ni hatua gani ya kazi Anayofanya, Yeye daima hufanya kazi kwa utendaji. Sio kama waaminivyo wengine, kwamba Mungu hafikiri au kusema na Hufanya chochote Anachohisi. Ana hekima na asili Yake, hii ni dutu Yake. Katika kufanya kazi Yake, Anahitaji dutu, hekima na ili tabia Yake yote ifunuliwe na itolewe ili mwanadamu apokee. Yeye hafanyi kazi bila mpango. Anazungumza kwa njia ya utendaji, Anafanya kazi Yake siku kwa siku, na Anapitia mateso siku kwa siku. Mateso Anayopitia pia ni machungu. Sio kana kwamba Mungu mwenye mwili Anapofanya kazi na Akizungumza Roho yupo pamoja naye na wakati Hafanyi kazi na kuzungumza Roho anatoweka. Ikiwa hali ingekuwa hivyo, Hangeteseka mateso yoyote na Hangeweza kuchukuliwa kuwa Mungu mwenye mwili. Watu hawaoni kipengele cha Mungu cha utendaji, hivyo watu hawawezi kamwe kumjua Mungu—hawamjui kabisa na kwa kweli. Watu wana ufahamu wa kijuu juu tu wa Mungu: Wao wanafikiri kwamba Mungu ni wa utendaji na wa kawaida au kufikiri kwamba Mungu ni mwenyezi na mwenye kudura. Mambo haya ambayo watu husema hutokana na yale waliyojifunza—hawana ufahamu wa kweli wa Mungu, hawana uzoefu Wake halisi. Kwa nini dutu ya kupata mwili imesisitizwa? Mbona Roho haongelelewi? Dutu ya mwili huupea mwili umaarufu. Ni mwili ndio hufanya kazi hasa; kazi ya Roho ni ya ziada, ni aina ya usaidizi. Hivi ndivyo mwili unapata matokeo kupitia kwa kazi Yake. Mtu anakuja kumjua Mungu katika hatua zinazofuatana. Ni vigumu kupenyeza na kujua hata zaidi. Kupitia kwa usemi wa Mungu mnapata kumjua Yeye hata zaidi, lakini bado hamjakuwa wazi kabisa, bado hamna ufahamu wa kiini cha vitu. Mnaamini kwamba kazi inaweza kufanywa katika mwili au kwa Roho—kwamba Roho anaweza kusimama katika nafasi ya mwili. Kwa hivyo, hamtawahi kuelewa umuhimu wa mwili na kazi katika mwili. Hutawahi kujua kamwe kupata mwili ni nini.
Tanbihi:
a. Nakala asili inaacha "kwa Yesu."
Tanbihi:
a. Nakala asili inaacha "kwa Yesu."
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni