4/11/2018

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”


1. Tangu watu waanze kukanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu. Hili ni zaidi ya suala la hasara kwenu. Ni dosari kubwa iliyopo kwa wale walio katika ulimwengu wa dini. Hii ndiyo sababu kuu ya watu kutomjua Mungu, na hivyo dosari hii ni kasoro ya kawaida miongoni mwa wale wote wanaomtafuta. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kumjua Mungu, au amekwishawahi kuuona uso Wake halisi. Ni kwa sababu hii ndipo kazi ya Mungu inakuwa ngumu kama kazi ya kuhamisha mlima au kukausha bahari. Ni watu wangapi ambao wamejitoa sadaka maisha yao kwa ajili ya kazi ya Mungu; ni wangapi wametengwa kwa sababu ya kazi Yake; ni wangapi wameteswa hadi kufa kwa ajili ya kazi Yake; ni wangapi wamelia kwa ajili ya upendo wao kwa Mungu, wamekufa pasipo haki; ni wangapi wamekutana na mateso katili na ya kinyama...? Kwamba majanga haya yatapita–hii sio kwa sababu ya watu kutokuwa na maarifa juu ya Mungu? Inawezekanaje mtu ambaye hamjui Mungu awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Inawezekanaje mtu anayemwamini Mungu na bado anamtesa awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Haya si makosa kwa wale waliopo katika ulimwengu wa kidini pekee, bali ni makosa ya kawaida kwenu na kwao. Watu wanamwamini Mungu bila kumfahamu, ni kwa sababu hii watu hawamheshimu Mungu kutoka mioyoni mwao, na hawamchi Yeye mioyoni mwao. Hata kuna wale ambao, kwa majivuno makuu na hali, wanafanya kazi ambayo wanafikiria kichwani wenyewe katika mkondo huu, na wanaifanya kazi ya Mungu kulingana na matakwa yao wenyewe na tamaa zao za kibadhirifu. Watu wengi wanafanya ovyoovyo, hawamtukuzi Mungu bali wanafuata mapenzi yao wenyewe. Je, hii si mifano mizuri ya mioyo ya watu yenye ubinafsi? Je, haya hayaonyeshi dalili nyingi zaidi za udanganyifu walionao watu?
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
2. Watu wanaweza kuwa wenye akili sana, lakini inawezekanaje karama zao zichukue nafasi ya kazi ya Mungu? Watu wanaweza kujali mzigo wa Mungu, lakini hawawezi kufanya mambo kwa ubinafsi sana. Je, matendo ya watu ni ya kiungu kweli? Je, mtu yeyote anaweza kuhakikishwa kwa namna chanya? Kutoa ushuhuda kuhusu Mungu kurithi utukufu Wake—huyu ni Mungu Anayewatenga na kuwainua watu; kwa nafsi yao hawawezi kustahili. Kazi ya Mungu ndio kwanza imeanza, maneno Yake ndio kwanza yameanza kuzungumzwa. Katika hatua hii, watu wanajisikia vizuri kwa nafsi yao wenyewe; hii haiwezi kuwa ni kujitafutia fedheha? Wanaelewa kidogo sana. Hata mwanafalsafa mwenye karama ya juu sana, mzungumzaji mzuri kabisa, hawezi kuelezea yote kuhusu uteule wa Mungu—sembuse nyinyi? Ni vyema msijione wakubwa kabisa kupita viwango vya mbinguni, badala yake jioneni kuwa watu wa chini kabisa kuliko watu razini wengine wanaotafuta kumpenda Mungu. Hii ndiyo njia ambayo kwayo mnapaswa kuingia: kujiona wadogo kuliko wengine wote. Kwa nini mjiweke katika viwango vya juu? Kwa nini mjiweke katika heshima hiyo ya juu? Katika safari ndefu ya maisha, mmepiga hatua chache tu za kwanza. Mnachokiona ni mkono wa Mungu tu, si mwili mzima wa Mungu. Ni wajibu wenu kuiona kazi ya Mungu zaidi, kugundua zaidi juu ya kile mnachopaswa kuingia kwacho, kwa sababu mmebadilika kidogo sana.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
3. Kwa kweli, kati ya vitu vingi katika uumbaji wa Mungu, mwanadamu ni wa kiwango cha chini sana. Ingawa ni mtawala wa vitu vyote, mwanadamu ni kiumbe pekee ambaye yupo chini ya hila za Shetani, ni kiumbe pekee ambaye anashikwa kwa namna nyingi katika uharibifu wake. Mwanadamu hajawahi kuwa na ukuu juu yake mwenyewe. Watu wengi wanaishi katika uovu wa Shetani, na kuumizwa na dhihaka zake; anawaudhi kwa njia hii hata hapo watakapokuwa wamelemewa kabisa, wakistahimili kila badiliko, kila ugumu katika ulimwengu wa kibinadamu. Baada ya kuwachezea, Shetani anaweka mwisho wa hatima yao. Na hivyo watu wanapita katika maisha yao yote wakiwa na mkanganyiko, wala hawajawahi kufurahia hata siku moja vitu vizuri ambavyo Mungu Amewaandalia, badala yake wanajeruhiwa na Shetani na kuachwa wakiwa wameharibika kabisa. Leo wamekuwa wadhoofu na walegevu sana kiasi kwamba hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu. Ikiwa watu hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu, uzoefu wao utabakia kuwa vipandevipande na kutokamilika milele, na kuingia kwao kutabakia sehemu tupu milele.
kutoka "Kazi na Kuingia(1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
4. Katika Miaka elfu kadhaa tangu Mungu Alipokuja duniani, idadi yoyote ya watu wenye mawazo ya kiburi wamekuwa wakitumiwa na Mungu kufanya kazi Yake kwa miaka mingi; lakini wale wanaoijua kazi Yake ni wachache sana takribani hawapo kabisa. Kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu ambao hawajatajwa wanachukua jukumu la kumpinga Mungu na wakati huo huo wanafanya kazi Yake, kwa sababu, badala ya kufanya kazi Yake, kimsingi wanafanya kazi ya mwanadamu katika nafasi waliyopewa na Mungu. Je, hii inaweza kuitwa kazi? Wanawezaje kuingia? Mwanadamu amechukua neema ya Mungu na kuizika. Kwa sababu hii, kwa karne nyingi zilizopita wale wanaofanya kazi Yake wana kuingia kwa kiwango kidogo. Hawazungumzi juu ya kuijua kazi ya Mungu kwa sababu wana uelewa mdogo wa hekima ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, ingawa kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu, wameshindwa kuona jinsi Alivyoinuliwa, na hii ndiyo sababu watu wamejifanya wao ndio Mungu wa kuabudiwa na watu.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
5. Kwa miaka mingi sana Mungu Amebakia sirini katika uumbaji; Ameangalia katika misimu yote ya machipuko na kipupwe nyuma ya umande ufunikao; Ametazama chini kutoka katika mbingu ya tatu kwa siku nyingi sana; Ametembea miongoni mwa wanadamu kwa miezi na miaka mingi sana. Amekaa juu ya wanadamu wote Akisubiri kwa utulivu katika vipindi vingi vya baridi. Hajawahi kujionyesha wazi kwa mtu yeyote yule, wala kutoa sauti hata kidogo, Anaondoka bila ishara na kurudi kimyakimya. Nani anaweza kuujua uso wake halisi? Hajawahi kuzungumza na mwanadamu hata mara moja, Hajawahi kuonekana kwa mwanadamu hata mara moja. Ni rahisi kiasi gani kwa watu kufanya kazi ya Mungu? Wanatambua kidogo tu kwamba kumjua Yeye ni kitu kigumu sana kuliko vitu vyote. Leo Mungu Amezungumza na mwanadamu, lakini mwanadamu hajawahi kumfahamu, kwa sababu kuingia kwake katika maisha ni finyu sana na hakuna kina. Kwa mtazamo Wake, watu hawastahili kabisa kuonekana mbele za Mungu. Wana uelewa mdogo sana juu ya Mungu na wametanga mbali Naye sana. Aidha, mioyo inayomwamini Mungu ni tatanishi sana, na hawana taswira ya Mungu ndani ya mioyo yao. Na matokeo yake, juhudi za Mungu zenye kubeba maumivu, na kazi Yake, kama vipande vya dhahabu vilivyofunikwa mchangani, haviwezi kutoa mwanga. Kwa Mungu, tabia, nia, na mitazamo ya watu hawa ni machukizo sana. Ni dhaifu katika uwezo wao wa kupokea, hawana hisia kiasi cha kufa ganzi, wamejishusha thamani na kuharibika, wametumikishwa kupita kiasi, dhaifu wasiokuwa na dhamiri, ni lazima waongozwe kama ng'ombe na farasi wanavyoongozwa. Kama ilivyo kuingia kwao katika roho, au kuingia katika kazi ya Mungu, hawachukui tahadhari yoyote, hawajizatiti hata kidogo kuteseka kwa ajili ya ukweli. Kwa mtu kama huyu Mungu kumfanya awe mkamilifu haitakuwa rahisi. Hivyo ni muhimu kwamba mnapanga kuingia kwenu katika pembe hii - kwamba kupitia kazi yenu na kuingia kwenu ndipo mnakaribia kuijua kazi ya Mungu.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
6. Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya upande mmoja sana; kile ambacho Mungu Anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Kaka na dada wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu Anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu ya kuingia kwa mwanadamu kuwa kwa upande mmoja. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili kwamba muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia kwacho. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu walionao kwa Mungu na maarifa waliyonayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na kitu ambacho wanadamu wote wanapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuwa na uwezo wa kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia mwanadamu. Hii ndiyo kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho ambacho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
7. Kuna watu wengi ambao wanajikita tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, halafu hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuzia kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu anaona kufanya kazi na kuhubiri kuwa ndio kuingia, na hakuna anayechukulia uzoefu wake binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi kuridhika kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni ya kwao wenyewe.... Baada ya kuwa umehubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio mdogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unaamini kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako binafsi. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kuunufaisha zaidi uzoefu wako. Mwanadamu kudhani kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
8. Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia kazi Mungu, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi ya Mungu, mwanadamu anakuwa na fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zako katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaweza kupata kuingia kuzuri katika kazi yenu. Kama mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilichomo ndani ya mwanadamu, hakuna uwezekano wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisia, maana Roho Mtakatifu Huangazia katika njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili kwa mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwao. Hata hivyo, katika uhalisia, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa asili, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia uzoefu ambao mwanadamu anakabiliana na shida nyingi, kimo halisi cha mwanadamu unadhihirika katika mazingira kama hayo. Ni katika muda huo ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio mkubwa hivyo, na ubinafsi, kujitumainia nafsi, na tamaa za mwanadamu vyote vinaibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao watatambua kwamba haukuwa uhalisia wao hapo nyuma, bali ni nuru ya muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea mwangaza tu. Roho Mtakatifu Anapomwangazia mwanadamu ili kuuelewa ukweli, mara nyingi inakuwa katika namna ya wazi na tofauti, bila muktadha. Yaani, Hayajumuishi matatizo haya ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu....Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa kujikita zaidi katika kuingia kwenu, na wakati huo huo, kuona kipi ni kazi ya Roho Mtakatifu na kipi ni kuingia kwenu, vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa Naye vizuri na kuruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kuletwa pamoja ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusianao wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku kwa siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hii ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika kwamba kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mmepitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa heshima na ibada kwa Mungu.
kutoka "Kazi na Kuingia (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
9. Mungu Amemwaminia mwanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwa mwanadamu. Lakini kwa sababu tabia ya watu ni duni, maneno mengi juu ya Mungu ni shida sana kufuatwa. Kuna sababu mbalimbali za tabia yao duni, kama vile uharibifu wa itikadi na maadili ya binadamu, kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mtindo wa maisha uliopotoka unaopelekea maradhi mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanapata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni, hivyo, kimsingi watu hawajui Roho ni nini na Mungu ni nini, bali wana taswira hafifu ya Mungu na isiyoeleweka vizuri kama wanavyooneshwa na usihiri; mivuto yenye madhara iliyozama ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu iliyokuja baada ya maelfu ya miaka ya roho ya utaifa na fikra za utaifa vimewaacha watu wakiwa wamefungwa na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa, hawana ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana. Na kadhalika na kadhalika. Sababu hizi zimetengeneza taswira mbaya za itikadi, mawazo, maadili na tabia ya kibinadamu. Inaonekana wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora. Badala yake, wanakubali tu uchaguzi wao katika maisha na kutumia siku zao kukuza na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi, wakiwa na njozi ya kuwa na familia nzuri na yenye furaha, hisia za tendo la ndoa, adabu kwa mzazi kwa upande wa watoto, kuwa na maisha yenye furaha na kuishi kwa amani. ...Kwa miongo mingi, maelfu, makumi elfu ya miaka hadi leo, watu wamekuwa wakipoteza muda wao, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani aliyekuwa anatafuta mapenzi ya Mungu? Kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa anaitikia kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za ndani ya wanadamu zilizochukuliwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu toka zamani, hivyo ni vigumu sana kufanya kazi ya Mungu na hata agizo la Mungu halipewi uzito mkubwa leo. Ninaamini kwamba watu hawatanizingatia Ninapotamka maneno haya maana kile Ninachokisema ni historia ya maelfu ya miaka. Kuzungumza juu ya Historia kuna maana ya ukweli, aidha, ni kashfa zinazojulikana kwa wote, sasa kuna maana gani kuzungumza kitu ambacho ni kinyume na ukweli?
kutoka "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
10. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo, Mungu Anazichukia sana. Hata sasa, watu wengi bado hawawezi kuachana nazo na wanafikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na bado wanazo hadi leo hii, bado hawajaondokana nazo kabisa. Mambo kama sherehe za arusi au mahari, zawadi ya pesa na dhifa na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe, maneno ya zamani yamerithishwa, na shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi, yote haya yanachukiwa sana na Mungu; hata Jumapili (Sabato, kama ilivyoadhimishwa na Wayahudi) pia inachukiwa na Mungu, mahusiano ya kibinadamu na mawasiliano ya kidunia pia yanachukiwa sana na kukataliwa na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi ambazo zinajulikana kwa kila mtu hazikuamriwa na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo (keki ya Mwaka Mpya, mafataki, kandili, zawadi za Krismasi, sherehe za Krismasi na Ushirika Matakatifu) maana sikukuu hizi, je, sio sanamu katika mioyo ya watu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo na kitani nyembamba navyo ni sanamu. Siku mbalimbali za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizokuwa na maana kabisa katika ulimwengu wa kidini kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo, zote hazina ulinganifu na binadamu aliyeumbwa na Mungu. Ni uwezo mkubwa wa fikra za watu na "dhana bunifu" ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini yote hayo ni ukweli kwamba Shetani alifanya hila zake kwa wanadamu. Kadri Shetani anavyoishi katika eneo fulani ndivyo eneo hilo linarudi nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi za kishirikina zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha uhalisia mkubwa na zinaonekana kujenga daraja katika kazi ya Mungu, lakini ni vifungo visivyoshikika vya Shetani vikifungafunga maarifa ya watu juu ya Mungu, ni hila za Shetani. Kimsingi, hatua ya kazi ya Mungu ilipomalizika, Alikuwa Amekwishaharibu zana zake na mtindo wa wakati huo bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, "waumini wasalihina" bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika na kuacha kile Alicho nacho Mungu bila hata kukichunguza, wanaonekana wanampenda Mungu sana lakini uhalisia ni kwamba wamemtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Meza ya Bwana ya Mwisho, vyote hivi, watu wanavichukulia kama Mungu na wanaviabudu wakati wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia "Mungu Baba." Je, huu sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo iliyorithishwa kwa wanadamu, Mungu anaichukia, na inazuia kabisa njia ya kuelekea kwa Mungu na, aidha, inasababisha hasara kubwa katika kuingia kwa mwanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo, haya yote yameuteka moyo wa mwanadamu. Mungu hana namna ya kufanya kazi kwa wanadamu kwa sababu ndani yao kuna ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu na mifumo, na vitu hivi, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu yanazunguka, filamu ya kisasili katika rangi, ikiwa na watu wa ajabu wakiendesha mawingu, ya kubuni sana kiasi cha kusisimua na kustaajabisha.
kutoka "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
11. Njia nzuri ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaacha watu kuanza kubadilisha itikadi na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, tarehe, sikukuu, zote Mungu Anazichukia. Wanatakiwa kuwa huru kutoka katika vifungo hivi vya itikadi za kishirikina na kuondoa rangi za kishirikina zilizozama kabisa ndani. Haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu. Mnatakiwa kuelewa kwa nini Mungu Anawatoa watu kutoka katika ulimwengu usiokuwa na dini, kuwatoa katika kanuni. Hili ndilo lango la kuingia kwenu, ingawa halina uhusiano na uzoefu wenu wa kiroho, haya ni mambo makubwa yanayowazuia kuingia, yanayowazuia kumjua Mungu. Yanatengeza "mtego" unaowakamata watu. Watu wengi wanasoma Biblia sana na wanaweza kukariri mafungu mengi kutoka katika Biblia. Katika kuingia kwao leo, watu bila kujua wanaitumia Biblia kupima kazi ya Mungu kana kwamba msingi wa kazi ya Mungu ni Biblia, na chanzo chake ni Biblia. Kazi ya Mungu inapokuwa sambamba na Biblia, watu wanaunga mkono kazi ya Mungu kwa nguvu zote na kumwangalia Mungu kwa macho mapya; kazi ya Mungu inapokuwa haifanani na Biblia, watu wanakuwa na dukuduku sana kiasi cha kuhangaika na kutafuta msingi wa kazi ya Mungu; kama kazi ya Mungu haikutajwa katika Biblia, watu watampuuza Mungu. Inaweza kusemwa kwamba watu wengi wanakubali kwa hadhari sana, wanatii kwa kusita na wanatambua kwa kawaida uwepo wa kazi ya Mungu, na kuhusu mambo yaliyopita, wanashikilia nusu na kuacha nusu. Je, huku kunaweza kuitwa kuingia? Kushikilia vitabu vya wengine kama hazina, na kuvichukulia kama ufunguo wa dhahabu wa kufungua lango la ufalme, watu hawaonyeshi kuvutiwa na matakwa ya Mungu ya leo. Aidha, "wataalamu wengi wenye akili" katika mkono wao wa kushoto wanashikilia maneno ya Mungu, huku katika mkono wa kulia wanashikilia "kazi kuu" za wengine, kana kwamba wanataka kutafuta msingi wa maneno ya Mungu kutoka katika kazi kuu hizi ili kuthibitisha kabisa kwamba maneno ya Mungu ni sahihi, na hata wanatoa ufafanuzi kwa wengine kwa kuunganisha na kazi kuu, kana kwamba walikuwa wanafanya kazi. Kusema kweli, "watafiti wa kisayansi" wengi miongoni mwa wanadamu hawajawahi kufikiria juu ya mafanikio makubwa ya kisayansi leo, mafanikio ya kisayansi ambayo hayajawahi kufikiriwa (yaani, kazi ya Mungu, maneno ya Mungu na njia ya kuingia uzimani), hivyo watu "wanajitegemea," wakihubiri" wakitegemea sana ndimi zao, wakiringia "jina zuri la Mungu." Hata hivyo, kuingia kwao kupo hatarini na umbali wa matakwa ya Mungu unaonekana kuwa mbali sana kama kuanzia uumbaji hadi wakati huu. Ni rahisi kiasi gani kufanya kazi ya Mungu?
kutoka "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
12. Inaonekana watu wamekwishaamua kuacha nusu yao kwa mambo ya zamani na kuleta nusu yao kwa wakati wa leo, nusu kwa Shetani na nusu kwa Mungu, kana kwamba hii ndiyo njia ya kuwa na dhamiri iliyotulia na kuweza kuwa na hisia ya utulivu fulani. Mioyo ya watu inadhuru sana kwa siri, wanaogopa sio tu kupoteza kesho bali pia wanahofia kupoteza jana, wanaogopa sana kumkosea Shetani na kumkosea Mungu wa leo Anayeonekana kuwa ndiye na kuwa siye. Kwa sababu itikadi na maadili ya watu ni duni sana, uwezo wao wa kutambua vitu kwa kweli ni mbaya, na kimsingi hawajui kama kazi ya leo ni ile kazi ya Mungu au siyo. Pengine ni kwa sababu fikra za kishirikina za watu zimekita sana mizizi kiasi kwamba ushirikina na ukweli, Mungu na sanamu, vinawekwa katika kundi moja; wala hawajali kuweka tofauti baina ya vitu hivi. Inaonekana kama wametesa bongo zao lakini bado mambo hayo hayajawa wazi. Na hiyo ndio maana wanadamu wanasimama katika njia zao na hawawezi tena kusonga mbele. Haya yote yanatokea kwa sababu watu hawana elimu ya itikadi ambayo ni sahihi, kitu ambacho kinawafanya iwe vigumu katika kuingia kwao. Na matokeo yake, watu wanapoteza mvuto kabisa katika kazi ya Mungu wa kweli, bali wanaendelea kung'ang'ania katika kazi ya mwanadamu (kama vile watu wanaotazamwa kuwa ni watu wakubwa) kana kwamba imepigwa muhuri. Je, haya si masomo mapya kabisa kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu?
kutoka "Kazi na Kuingia (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
13. Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani. "Wanajificha wenyewe katika unyenyekevu." Ukweli ni kwamba, ni wachache miongoni mwenu mnaojua makusudi ya Mungu kuhusu siku za mwisho. Ni wachache sana miongoni mwenu wanaojua nyayo za Mungu, na wachache zaidi wanajua utimilifu wa mwisho wa Mungu utakavyokuwa. Halafu kila mtu, kwa utashi tupu, anakubali kufundishwa nidhamu na kushughulikiwa na wengine, kama vile anarekebisha na kusubiri siku ambayo hatimaye wamekwishaifanya na wanaweza kustarehe. Sitatoa maoni yoyote juu ya "maajabu" haya miongoni mwa watu, lakini kuna hoja moja ambayo wote mnapaswa kuielewa. Kwa sasa watu wengi wanaelekea katika hali isiyo ya kawaida, hatua zao za kuingia tayari zinaelekea katika mwisho wa mauti. Pengine watu wengi wanafikiri kwamba mwanadamu anatamani "Shangri-La" ('bonde la utulivu'), wakiamini kuwa ni "sehemu ya uhuru." Kimsingi, sivyo ilivyo. Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekwishapotoka tayari.
kutoka "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
14. Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake na kugeuza mitazamo yao ya zamani. Nakumbuka Mungu Alishawahi kusema, "Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.” Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, kuja Kwake duniani wakati huu kumeambatana na hatari nyingi zaidi. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu Alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya utakasaji, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu Amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Anajificha katika unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu msalabani, Yesu Alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Alikuwa hafanyi kazi ya utakasaji. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba Alianza kukusudia sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza Yeye binafsi, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kusaidia, Mungu Ameyavumilia maumivu makali ya kuja duniani kufanya kazi Yeye Mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu Alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema na kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililogeuka na kuwa rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu Hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje kila mtu avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani, Mungu Anakuwa kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu wala Hazingatii hayo moyoni Mwake hata kidogo, bali Anaendelea kufanya kazi Anayotaka kufanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu aliyetambua upendo wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alionao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba Aliyeko mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofia moyo Wake kuumia. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, utaona wawili Hawa wanatazamana wakati wote kutoka kwa mbali, sambamba na Roho. Ee binadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini tena Watengane, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba Anampenda Mwana Wake kama vile Mwana Anavyompenda Baba Yake. Kwa nini sasa asubiri kwa muda mrefu huku Akiwa na shauku hiyo? Ingawa Hawajatengana kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Hii yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba Anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu Anapokuja duniani, Anakabiliana na mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu kama mwanadamu. Mungu Mwenyewe hana hatia, sasa kwa nini Mungu Ateseke kwa maumivu kama mwanadamu? Pengine ndiyo maana Mungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuujua moyo wa Mungu? Mungu Anampatia mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; sasa Mungu Atawezaje kutokuwa na wasiwasi?
kutoka "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
15. Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimepoa sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu Anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya tabia ya wanyama ndani ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha kitu. Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama mbali na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kwamba siku moja ambapo Mungu Atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atakuwa ameuelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa ajili ya mema ya binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa sababu binadamu aweze kuishi vizuri. Ujio wa Mungu umeambatana na majaribu, na Mungu pia Anakuja katika adhama na ghadhabu Yangu. Muda ambapo Mungu Anamwacha mwanadamu, Atakuwa tayari Amepata utukufu, na Ataondoka Akiwa Amejawa na utukufu mwingi na furaha ya kurudi. Mungu Anayefanya kazi duniani Hazingatii mambo moyoni Mwake haijalishi watu wamemkataa kiasi gani. Yeye Anafanya tu kazi Yake.
kutoka "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
16. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu unaanzia mbali maelfu ya miaka huko nyuma, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunjavunja moyo wa Mungu tangu zamani sana. Wala Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka kikamilifu na shida za ulimwengu wa wanadamu. Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akarudisha kichwa Chake nyuma na kufumba macho Yake, Akisubiri Mwana Wake mpendwa kurudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu Amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu bado anajistarehesha, haiweki kabisa kazi ya Mungu moyoni mwake.
kutoka "Kazi na Kuingia (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili
17. Leo wote mnajua kwamba Mungu Anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuingia katika hatua nyingine kuingia katika enzi nyingine, huru kutoka katika enzi hii ya giza, ya kale, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, Akimruhusu kuishi katika ulimwengu wa uhuru. Kwa manufaa ya kesho ya kupendeza, ili kwamba watu wasibanwe katika hatua zao kesho, Roho wa Mungu Anapanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu, na ili kwamba mwanadamu aweze kuwa na furaha kubwa, Mungu Anajitolea jitihada Zake zote katika mwili Akiandaa njia mbele ya mwanadamu, ili kwamba siku ambayo mwanadamu anaitamani sana iweze kuja haraka. Nyote mnaweza kufurahia wakati huu mzuri, maana si rahisi kufanya mkutano na Mungu, na ingawa hamjawahi kumjua, mna muda mrefu tangu mmekutana Naye. Ikiwa tu kila mtu angeweza kukumbuka milele siku zote hizi nzuri lakini fupi, na kuzifanya kuwa mambo yao ya kuwafurahisha duniani.
kutoka "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili
18. Kwa maelfu ya miaka, Wachina wamekuwa wakiishi maisha ya utumwa na hii imebana mawazo yao, dhana, maisha, lugha, tabia na matendo kiasi kwamba wamebaki bila uhuru wowote. Maelfu kadhaa ya miaka ya historia imewabadilisha watu muhimu kutoka kutawaliwa na roho na kuwa kitu kinachofanana na maiti iliyoondokewa na roho. Wengi ni wale wanaoishi chini ya upanga wa Shetani, wengi wanaishi katika makazi yanayofanana na pango la mnyama, wengi wanakula chakula kama wanachokula ng'ombe au farasi, wengi wapo katika mchafuko huko ahera na hawana maana kabisa. Katika umbo, watu hawana tofauti na watu wa zamani, sehemu yao ya kupumzika ni kama kuzimu, na wote wanaowazunguka wanakuwa na mashetani na mapepo wachafu. Kwa umbo la nje, wanaonekana kuwa ni wanyama wenye mabadiliko ya hali ya juu; kimsingi wanaishi na kukaa na mashetani wachafu. Bila mtu yeyote kuwashughulikia, watu wanaishi katika mtego uliojificha wa Shetani, na wamenaswa kabisa kiasi kwamba hawawezi kutoroka. Hawakusanyiki na wapendwa wao katika makazi yao ya furaha, kuishi kwa furaha na kuyaishi maisha ya kuridhisha, bali wanaishi Kuzimu, wakishughulika na mapepo na kushirikiana na mashetani. Kimsingi, watu bado wamefungwa na Shetani, wanaishi mahali ambapo pepo wachafu wanakusanyika, wanatawaliwa na hawa mapepo wachafu, na ni kama vitanda vyao vipo mahali ambapo maiti zao zimelala, kana kwamba ni sehemu zao za kustarehe.
kutoka "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili
19. Mwanadamu anaishi bega kwa bega na wanyama, na wanatembea pamoja kwa amani bila ugomvi au vita vya maneno. Mwanadamu ni mgumu kuridhika vile anavyowajali na anavyohusika na wanyama, na wanyama wapo kwa ajili ya mwanadamu kuishi, ni kwa maslahi ya mwanadamu, bila wao kunufaika na chochote na kumtii mwanadamu kikamilifu. Kwa namna zote, uhusiano kati ya mwanadamu na mnyama ni wa karibu na wa amani–na pepo wachafu, inaweza kuonekana ni muungano kamilifu wa mwanadamu na mnyama. Hivyo, mwanadamu na pepo wachafu duniani wanafurahia ukaribu wao mkubwa, na hawawezi kuachana: Mwanadamu anaonekana kufarakana na pepo wachafu, lakini kimsingi ameunganika nao, wakati pepo wachafu hawamnyimi mwanadamu kitu chochote, na "wanajitoa" vyote walivyonavyo kwao. Kila siku, watu wanachacharika katika "kasri la mfalme wa kuzimu," wakichezacheza na "mfalme wa kuzimu" (babu yao), na kutawaliwa naye. Leo, watu wanapakwa masizi, na kuishi muda mrefu sana Kuzimuni, wana muda mrefu toka waache kutamani kurudi katika dunia ya viumbe hai. Hivyo, mara tu wanapoiona nuru, na kutazama matakwa ya Mungu, na tabia ya Mungu, na kazi ya Mungu, wanakuwa na wasiwasi na kuhisi kucheza dansi; bado wanatamani sana kurudi kuzimu na kuishi na mizimu. Wamemsahau Mungu zamani sana, na hivyo wamekuwa wakizungukazunguka katika makaburi.
kutoka "Kazi na Kuingia (5)" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Matamshi ya Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni