5/17/2018

Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"



Ngoma ya Kikristo | Swahili Worship Song "Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu"

I
Mwenyezi Mungu mwenye mwili
Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,
kama tu vile jua la haki likichomoza;
mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.
Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma
Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,
Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.
Mwenyezi Mungu yuko uso kwa uso nasi.
Mungu uliyekuwa na kiu naye, Mungu niliyemngoja, leo anaonekana kwetu kwa utendaji.
Tuliutafuta ukweli, tulitamani sana haki;
ukweli na haki vimekuja miongoni mwa wanadamu.
Unampenda Mungu, nampenda Mungu;
mwanadamu amejaa sana matumaini mapya.
Watu wanatii, mataifa yanamwabudu
Mungu mwenye mwili wa utendaji.

II
Mwenyezi Mungu huonyesha ukweli na kuleta hukumu,
Akifichua tabia ya Mungu yenye haki.
Kwa hukumu, kuadibu na majaribu ya maneno,
Anashinda na kukamilisha kikundi cha washindi.
Maneno ya Mungu, ya gadhabu na uadhama,
yanahukumu na kuutakasa uovu wa mwanadamu,
yakiharibu kabisa enzi ya giza.
Ukweli na haki vinatawala duniani.
Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;
Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.
Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,
Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.
Dunia yote inashangilia, watu wote wanafurahia;
Tabenakulo ya Mungu inawasili miongoni mwa wanadamu.
Ulimwengu unatikisika na mataifa yanaabudu,
Mapenzi ya Mungu yanatekelezwa duniani.
Ufalme wa Kristo unapatikana miongoni mwa wanadamu.
Kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

    Umeme wa MasharikiKanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni