5/28/2018

Enda Nje ya Biblia: Hudhuria Karamu ya Ufalme wa Mbinguni Pamoja na Bwana

Watu wengi ambao wana imani katika Bwana huhisi kwamba maneno na kazi ya Mungu vyote viko katika Biblia, kwamba wokovu wa Mungu kama ulivyoelezewa katika Biblia tayari umejaa, kwamba imani katika Mungu lazima iwe kwa msingi wa Biblia na kwamba kama imani yetu kwa Mungu ni kwa msingi wa Biblia, basi kwa hakika tutanyakuliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni. Dhana hizi za kidini hutenda kama kamba zisizoonekana ambazo huzifunga kwa uthabiti na kuzisonga fikira zetu kiasi kwamba hatuitafuti kazi ya Roho Mtakatifu na hutufanya tusiweze kuitii kazi ya sasa ya Mungu. Tunawezaje basi kuelewa uhusiano kati ya Biblia na Mungu na Biblia na kazi ya Mungu? Bwana Yesu alisema, “Na neno lake haliishi ndani yenu: kwani hammwamini yule aliyemtuma. Tafuta katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnadhani kuwa mna uzima wa milele: na hayo ndiyo yananishuhudia. Nanyi hamtakuja Kwangu, kwamba mpate uhai"(Yohana 5:38-40).Mwenyezi Mungu anasema, "Kristo wa siku za mwisho huleta uzima, na huleta kudumu kwa njia ya kweli na ya milele. Ukweli huu ni njia ambayo binadamu atapata uzima, na njia pekee ambayo mtu atajua Mungu na kuidhinishwa na Mungu" (Neno Laonekana katika Mwili). Ni kwa njia ya kuacha Biblia tu tunapoweza kuja mbele ya Mungu na kuukubali wokovu Wake na kuhudhuria karamu ya ufalme wa mbinguni pamoja na Yeye. 

Umeme wa MasharikiKanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.


Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni