5/16/2018

Umeme wa Mashariki | Nyongeza ya 1: Tamko la Kwanza

Umeme wa Mashariki | Nyongeza ya 1: Tamko la Kwanza

Mwenyezi Mungu alisema, Ninachotaka mfanye si nadharia isiyo dhahiri na tupu ambayo Naizungumzia, wala si ya kutofikirika kwa akili ya mwanadamu au ya kutotimizwa kwa mwili wa mwanadamu. Ni nani anaweza kuwa mwaminifu kabisa ndani ya nyumba Yangu? Na ni nani anaweza kutoa yake yote ndani ya ufalme Wangu? Kama si kwa ufunuo wa mapenzi Yangu, je, mngejitolea kuutimiza moyo Wangu? Hakuna ambaye amewahi kuufahamu moyo Wangu, na hakuna ambaye amewahi kutambua mapenzi Yangu. Ni nani amewahi kuuona uso Wangu au kuisikia sauti Yangu? Petro alifanya hivyo? Au Paulo? Au Yohana? Au Yakobo? Ni nani amewahi kuvishwa na Mimi, au kumilikiwa na Mimi, au kutumiwa na Mimi? Ijapokuwa mara ya kwanza Nilipopata mwili ilikuwa katika uungu, mwili ambao Nilijivika ndani haukujua mateso ya mwanadamu, kwa sababu Sikuwa mwili katika mfano, kwa hiyo haingeweza kusemekana kwamba mwili ulitekeleza mapenzi Yangu kwa ukamilifu. Ni wakati ambapo tu uungu Wangu unaweza kufanya vile Ningefanya na kunena vile Ningenena katika nafsi ya ubinadamu wa kawaida, bila kipingamizi au kuzuia, ndipo inaweza kusemekana kwamba mapenzi Yangu yametekelezwa katika mwili. Kwa kuwa ubinadamu wa kawaida unaweza kuukinga uungu, hivyo lengo Langu la kuwa mnyenyekevu na Aliyefichika linatimizwa. Wakati wa hatua ya kazi katika mwili, ingawa uungu unatenda moja kwa moja, vitendo kama hivyo si rahisi kwa watu kuviona, ambalo ni kwa sababu tu ya maisha na vitendo vya ubinadamu wa kawaida. Kupata mwili huku hakuwezi kufunga kwa siku 40 kama kupata mwili kwa mara ya kwanza, lakini Anafanya kazi na kunena kwa kawaida, na ingawa Anafichua siri, Yeye ni wa kawaida sana; sauti Yake si, jinsi wanavyodhani watu, kama radi, uso Wake haumemetuki kwa nuru, na mbingu hazitetemeki Anapotembea. Ingelikuwa hivyo, basi katika hili hakungekuwa na hekima Yangu yoyote, na haingeweza kumwaibisha na kumshinda Shetani.
Wakati ambapo Naonyesha uungu Wangu chini ya ulinzi wa ubinadamu wa kawaida, Natukuzwa kwa utele kabisa, kazi Yangu kuu inatimizwa, na hakuna chochote kinachodhihirisha matatizo yoyote. Hili ni kwa kuwa lengo la kupata mwili Kwangu hasa ni kuwaruhusu wale wote wanaoniamini waone matendo ya uungu Wangu katika mwili, na kumwona Mungu Mwenyewe wa vitendo, hivyo kuondoa ndani ya mioyo ya watu nafasi ya Mungu asiyeonekana na Asiyeshikika. Kwa kuwa Nala, Najivisha Nguo, Nalala, Naishi, na Natenda kama mtu wa kawaida, kwa kuwa Nazungumza na kucheka kama mtu wa kawaida, na Nina mahitaji ya mtu wa kawaida, na pia Nina dutu ya uungu kamili, Ninaitwa "Mungu wa vitendo." Hii si dhahania, na ni rahisi kuelewa; ndani yake inaweza kuonekana ni katika sehemu gani kiini cha Kazi Yangu kiko ndani, na lengo Langu liko katika awamu gani ya kazi. Kufichua uungu Wangu kupitia kwa ubinadamu wa kawaida ni lengo kuu la kupata mwili Kwangu. Si vigumu kuona kwamba kiini cha kazi Yangu kiko katika sehemu ya pili ya enzi ya hukumu.
Ndani Yangu, hakujawahi kuwa na maisha ya binadamu au ladha ya binadamu. Maisha ya binadamu hayajawahi kushikilia nafasi ndani Yangu, na hayajawahi kukomesha ufichuzi wa uungu Wangu. Hivyo, kadri Mtu anavyodhihirisha sauti Yangu mbinguni na mapenzi ya Roho Wangu, ndivyo Anavyoweza kumwaibisha Shetani zaidi, na ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kutekeleza mapenzi Yangu katika ubinadamu wa kawaida. Hili pekee limemshinda Shetani, na Shetani tayari ameaibishwa kabisa. Ingawa Nimefichika, hili halizuii matamshi na vitendo vya uungu Wangu—ambalo linatosha kuonyesha kwamba Nimekuwa mshindi, na Nimetukuzwa kabisa. Kwa kuwa kazi Yangu katika mwili haina kipingamizi, na kwa kuwa Mungu wa vitendo sasa Ana nafasi ndani ya mioyo ya watu na amekita mizizi ndani ya mioyo yao, imethibitishwa kwa ukamilifu kwamba Shetani ameshindwa na Mimi. Na kwa kuwa Shetani hawezi kufanya lolote zaidi miongoni mwa wanadamu, na ni vigumu kuingiza sifa ya Shetani ndani ya mwili wa mwanadamu, mapenzi Yangu yanaendelea bila kipingamizi. Maudhui ya kazi Yangu ni, hasa, kusababisha watu wote kutazama matendo Yangu ya ajabu na kuona uso Wangu halisi: Mimi si asiyeweza kufikika, Siendi juu sana katika anga, Mimi sikosi umbo wala kukosa sura maalum. Mimi si asiyeonekana kama hewa, wala Siko kama wingu linaloelea, rahisi kupeperushwa; badala yake, ingawa Naishi miongoni mwa wanadamu, na kupitia utamu, uchachu, uchungu, na ukali miongoni mwa wanadamu, mwili Wangu unatofautiana kimsingi na ule wa mwanadamu. Watu wengi sana huona vigumu kujishughulisha na Mimi, lakini wengi pia hutamani kujishughulisha na Mimi. Ni kana kwamba kuna siri kubwa, zisizoeleweka ndani ya Mungu aliyepata mwili. Kwa sababu ya ufichuzi wa wazi wa uungu, na kwa sababu ya ulinzi wa kuonekana kwa mwanadamu, watu hukaa mbali nami kwa heshima, wakiamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye huruma na upendo, lakini pia wanaogopa uadhama Wangu na ghadhabu. Hivyo, ndani ya mioyo yao, wanataka kuzungumza nami kwa dhati, lakini hawawezi kufanya watakavyo—kile ambacho mioyo yao inatamani, nguvu zao zinakosa. Hivyo ndivyo zilivyo hali za kila mtu katika hali hii—na kadri watu walivyo hivi, ndivyo thibitisho la ufunuo wa hali mbalimbali za tabia Yangu lilivyo kuu zaidi, hivyo kutimiza lengo la watu kujua kuhusu Mungu. Lakini hili ni la baadaye; kilicho muhimu ni kuwafanya watu wajue matendo Yangu ya ajabu kutokana na shughuli za mwili Wangu, kuwasababisha kujua dutu la Mungu: Mimi si, kama wanavyodhani watu, asiye wa kawaida na wa mwujiza; badala yake, Mimi ni Mungu wa vitendo aliye wa kawaida katika mambo yote. Nafasi "Yangu" katika dhana za watu imeondolewa, na wao huja kunijua kwa kweli. Ni wakati huo tu ndipo Mimi Huchukua nafasi Yangu ya kweli ndani ya akili zao.
Mbele ya watu wote, Sijawahi kufanya tu kitu chochote cha ajabu ambacho kimehifadhiwa kwa upendo mkubwa na watu, bali Mimi pia ni wa kawaida mno; Mimi kwa makusudi Siwaruhusu watu kuona chochote kilicho na ladha ya Mungu katika mwili Wangu. Lakini kwa sababu ya maneno Yangu, watu wanashindwa kabisa, na wanatii ushuhuda Wangu. Ni hivyo tu ndivyo watu huja kujua, bila wasiwasi, Mimi Niliye katika mwili juu ya msingi wa kuamini kwa ukamilifu kwamba Mungu Yupo kweli. Kwa njia hii, ufahamu wa watu kunihusu huwa halisi zaidi, dhahiri zaidi, na hautiwi doa hata kidogo kwa mwenendo wao mzuri; yote ni matokeo ya uungu Wangu kutenda moja kwa moja, ukiwapa watu ufahamu mkuu zaidi wa uungu Wangu, kwani uungu pekee ndiyo sura halisi ya Mungu na sifa ya asili ya Mungu—watu wanapaswa kuliona hili. Nitakacho ni maneno, vitendo, na matendo yaliyo katika uungu—Sijali kuhusu maneno na amali katika ubinadamu. Lengo Langu ni kuishi na kutenda katika uungu—Sitaki kukita mizizi na kuchipua katika ubinadamu, Sitaki kuishi katika ubinadamu. Je, mnaelewa Ninachosema? Ijapokuwa Mimi ni mgeni katika ubinadamu, Sitaki hili; Natenda katika uungu kamili, na ni kwa njia hii tu ndiyo watu wanaweza kuufahamu vizuri zaidi uso Wangu halisi.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni