6/13/2018

Ahadi ya Mungu kwa Waisraeli

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, injili
Katika mwaka wa Bwana wetu, mtoto wa kiume alizaliwa katika hori kwa nyumba ya wageni katika Bethlehemu ya Uyahudi. Wanaume watatu wenye busara kutoka mashariki, wakiongozwa na nyota ambayo haikuwahi kuonekana kabla, walifika mahali pa kuzaliwa kwa mtoto.Wakamsujudia kwa ibada. Mtoto huyu Ndiye aliyeahidiwa na Mungu, ambaye angewaongoza na kuwakomboa Waisraeli kutoka kwa sheria.
Soma Zaidi:Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
Mwenyezi Mungu alisema, Wakati Yesu Alikuja kufanya kazi yake, ilikuwa ni kwa uongozi wa Roho Mtakatifu; Yeye Alitenda yale ambayo Roho Mtakatifu Alitaka, na haikuwa kwa mujibu wa Enzi ya sheria ya Agano la Kale ama kwa mujibu wa kazi ya Yehova. Ingawa kazi ambayo Yesu Alikuja kufanya haikuambatana na sheria za Yehova ama amri za Yehova, chanzo chao kilikuwa sawa. Kazi ambayo Yesu Alifanya iliwakilisha jina la Yesu, na iliwakilisha Enzi ya Neema; kazi iliyofanywa na Yehova, iliwakilisha Yehova, na iliwakilisha Enzi ya Sheria. Kazi yao ilikuwa kazi ya Roho mmoja katika enzi tofauti. Kazi ambayo Yesu Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Neema, , na kazi ambayo Yehova Alifanya ingeweza tu kuwakilisha Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Yehova Aliwaongoza tu watu wa Israeli na Misri, na mataifa yote nje ya Israeli. Kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema ya Agano Jipya ilikuwa kazi ya Mungu katika jina la Yesu kwa kuwa Yesu ndiye Aliongoza enzi hii. Iwapo utasema kuwa kazi ya Yesu ilikuwa kwa msingi wa kazi ya Yehova, na kuwa hakufanya kazi yoyote mpya, na kuwa yote Aliyofanya ilikuwa kwa mujibu wa maneno ya Yehova, kulingana na kazi ya Yehova na unabii wa Isaya, basi Yesu hakuwa Mungu Aliyekuwa katika mwili. Kama Alitekeleza kazi yake kwa njia hii, basi Yeye Alikuwa mtume au mfanyikazi wa Enzi ya Sheria. Iwapo ni kama unavyosema, basi Yesu hangeweza kufungua enzi, wala hangeweza kufanya kazi nyingine. Kwa njia hiyo hiyo, Roho Mtakatifu ni sharti afanye kazi Yake hasa kupitia kwa Yehova, na isipokuwa kupitia kwa Yehova Roho Mtakatifu hangeweza kufanya kazi yoyote mpya. Mwanadamu amekosea kwa kuona kazi ya Yesu kwa njia hii. Kama mwanadamu anaamini kwamba kazi iliyofanywa na Yesu ilikuwa inaambatana na maneno ya Yehova na unabii wa Isaiah, basi, je, Yesu Alikuwa Mungu Aliyepata mwili, au Yeye Alikuwa nabii? Kwa mujibu wa mtazamo huu, hakukuwa na Enzi ya Neema, na Yesu hakuwa Mungu Aliyepata mwili, kwa kuwa kazi ambayo Alifanya haingeweza kuwakilisha Enzi ya Neema na ingewakilisha tu Enzi ya Sheria ya Agano la Kale. Kungekuwepo tu na enzi mpya wakati Yesu Alikuja kufanya kazi mpya, Alipozindua enzi mpya, na kupenya katika kazi iliyokuwa imefanyika hapo awali katika nchi ya Israeli, na hakufanya kazi yake kwa mujibu wa kazi iliyofanywa na Yehova huko Israeli, hakuzingatia sheria Yake ya zamani, na hakufuata kanuni zozote, na Alifanya kazi mpya ambayo Alitakiwa kufanya. Mungu mwenyewe huja kuanzisha enzi, na Mungu mwenyewe huja kuleta enzi kwenye kikomo. Mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha enzi na kuhitimisha enzi. Kama Yesu hakuleta kazi ya Yehova kwenye kikomo, basi hio inadhihirisha ya kwamba Yeye Alikuwa tu mwanadamu, na hakuwakilisha Mungu. Kwa usahihi kwa sababu Yesu Alikuja na kuhitimisha kazi ya Yehova, Akafuata kazi ya Yehova kwa kuanza kazi yake mwenyewe, kazi mpya, inathibitisha kuwa hii ilikuwa enzi mpya, na kwamba Yesu Alikuwa Mungu mwenyewe. Walifanya kazi katika awamu mbili zinazotofautiana. Awamu moja ilifanyika katika hekalu, na hiyo nyingine ilifanyika nje ya hekalu. Awamu moja ilikuwa ya kuongoza maisha ya mwanadamu kwa mujibu wa sheria, na awamu nyingine ilikuwa ya kutoa kafara ya dhambi. Awamu hizi mbili za kazi bila shaka zilikuwa tofauti; huu ni mgawanyiko wa enzi ya zamani na enzi mpya, na hakuna kosa kusema kuwa hizo ni enzi mbili! Maeneo ya kazi yao yalikuwa tofauti, na kiini cha kazi yao kilikuwa tofauti, na lengo la kazi yao lilikuwa tofauti. Kwa hivyo, enzi hizi zinaweza kugawanywa kwa awamu mbili: Agano la Kale na Jipya, ambayo ni kusema, enzi mpya na ya zamani. Yesu alipokuja hakuenda katika hekalu, ambayo inathibitisha kwamba enzi ya Yehova ilikuwa imeisha. Hakuingia hekaluni kwa sababu kazi ya Yehova katika hekalu ilikuwa imekamilika, na haikuhitajika kufanywa tena, na kwa hiyo kuifanya tena kungekuwa kuirudia. Kwa kuondoka tu hekaluni, kuanza kazi mpya na kufungua njia mpya nje ya hekalu, ndio Aliweza kuifikisha kazi ya Mungu kwa upeo wake. Kama Hangeenda nje ya hekalu kufanya kazi Yake, kazi ya Mungu haingeweza kamwe kuendelea mbele kupita hekalu, na hakungekuwa na mabadiliko yoyote mapya. Na kwa hiyo, Yesu Alipokuja Hakuingia hekaluni, na Hakufanya kazi Yake hekaluni. Alifanya kazi Yake nje ya hekalu, na Akafanya kazi Yake kwa uhuru Akiandamana na wanafunzi. Kuondoka kwa Mungu katika hekalu kufanya kazi Yake kulikuwa na maana kwamba Mungu alikuwa na mpango mpya. Kazi Yake ilikuwa ifanyike nje ya hekalu, na ilikuwa iwe kazi mpya ambayo haingezuiliwa kwa njia ya utekelezaji wake. Kuwasili kwa Yesu kulimaliza kazi ya Yehova ya wakati wa Agano la Kale. Ingawa ziliitwa kwa majina mawili tofauti, awamu zote mbili za kazi zilifanywa na Roho mmoja, na kazi ya pili ilikuwa mwendelezo wa kazi ya kwanza. Kwa kuwa jina lilikuwa tofauti, na kiini cha kazi kilikuwa tofauti, basi enzi ilikuwa tofauti. Wakati Yehova Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yehova, na wakati Yesu Alikuja, hiyo ilikuwa enzi ya Yesu. Na kwa hivyo, kila wakati Mungu Anapokuja, anaitwa kwa jina moja, Yeye anawakilisha enzi moja, na Yeye anafungua njia mpya; na kwa kila njia mpya, Yeye huchukua jina jipya, ambalo inaonyesha kuwa Mungu daima ni mpya na wala si wa zamani, na ya kwamba kazi yake daima inasonga mbele. Historia inasonga mbele daima, na kazi ya Mungu inasonga mbele daima. Ili mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita ufike upeo wake, lazima uendelee kusonga mbele. Kila siku ni sharti Yeye afanye kazi mpya, kila mwaka lazima Yeye afanye kazi mpya, ni sharti Yeye afungue njia mpya, sharti aanzishe enzi mpya, aanzishe kazi mpya na kubwa zaidi, na ni sharti alete majina mapya na kazi mpya. Roho wa Mungu daima hufanya kazi mpya, na kamwe Hashikilii njia za zamani na kanuni. Kazi Yake pia kamwe haikomi, na inatendeka wakati wote. Ukisema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni isiyobadilika, basi kwa nini Yehova aliwaruhusu makuhani kumhudumia Yeye hekaluni, lakini Yesu hakuingia hekaluni—hata ingawa Alipokuja, watu pia walisema kwamba Alikuwa kuhani mkuu , na kwamba Alikuwa wa nyumba ya Daudi na pia kuhani mkuu, na Mfalme mkuu? Na kwa nini Hakutoa dhabihu? Kuingia hekaluni au la—hii yote sio kazi ya Mungu Mwenyewe? Iwapo, kama mwanadamu anavyofikiria, Yesu Atakuja, akiwa anaitwa Yesu wakati wa siku za mwisho, na bado juu ya wingu jeupe, akishuka miongoni mwa wanadamu kwa mfano wa Yesu, je, hayo si marudio ya kazi yake? Je, si Roho Mtakatifu Atakuwa Ameshikamana na ya kale? Yote yale ambayo mwanadamu anaamini ni dhana, na yote ambayo mwanadamu anakubali ni kwa mujibu wa maana halisi, na ni kwa mujibu wa mawazo yale; na ni mbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na hayafuatani na nia ya Mungu. Mungu pia hawezi kufanya hivyo; Mungu si mpumbavu na mjinga kiasi hicho, na kazi Yake si rahisi kama unavyofikiria. Kwa mujibu wa mambo yote yanayofanyika na kufikiriwa na mwanadamu, Yesu Atarejea juu ya wingu na Atateremka kati yenu. Mtamwona, akipaa kwenye wingu, atawaambia yeye ni Yesu. Nanyi pia mtatazama alama za misumari katika mikono yake, na mtamjua Yeye ni Yesu. Naye ndiye Atakayewaokoa tena, na Atakuwa Mungu wenu Mwenye nguvu. Yeye ndiye Atakayewaokoa, na kuwakabidhi ninyi jina jipya, na kumpa kila mtu jiwe jeupe, ambapo baadaye mtakubaliwa kuingia katika ufalme wa mbinguni na kulakiwa kwenye paradiso. Je, imani kama hizo si dhana za mwanadamu? Je, Mungu hufanya kazi kulingana na dhana za mwanadamu, au, je, Yeye hufanya kazi kinyume cha dhana za mwanadamu? Je, si dhana zote za mwanadamu zatoka kwa Shetani? Je, mwanadamu hajapotoshwa na Shetani? Kama Mungu Alifanya kazi yake kulingana na dhana ya mwanadamu, je, si Mungu Angekuwa Shetani? Je, si Angekuwa sawa na viumbe? Kwa kuwa viumbe sasa vimepotoshwa na Shetani hadi mwanadamu amekuwa mfano halisi ya Shetani, kama Mungu Angefanya kazi kwa mujibu wa vitu vya Shetani, si angekuwa katika ligi ya Shetani. Mwanadamu anawezaje kupima kina cha kazi ya Mungu? Na kwa hivyo, Mungu hafanyi kazi kwa mujibu wa dhana ya mwanadamu, na hafanyi kazi kama wewe unavyofikiria. Kuna wale ambao husema kwamba Mungu mwenyewe Alisema kuwa Atawasili kwa wingu. Ni ukweli kuwa Mungu mwenyewe Alisema hivyo, lakini, je, wajua kuwa siri za Mungu haziwezi kueleweka na mwanadamu? Je, unajua kuwa maneno ya Mungu hayawezi kuelezwa na mwanadamu? Na wewe una hakika kuwa ulipewa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu? Je, Roho Mtakatifu Alikuonyesha moja kwa moja kwa namna hii? Je, haya ni maelekezo ya Roho Mtakatifu, au ni dhana zako? Walisema, “Haya yalisemwa na Mungu mwenyewe.” Lakini hatuwezi kutumia dhana zetu na akili zetu kupima maneno ya Mungu. Na kuhusu maneno ya Isaya, je, unaweza kueleza maneno yake kwa kujiamini kikamilifu? Je, wewe unathubutu kueleza maneno yake? Kwa sababu huthubutu kueleza maneno ya Isaya, mbona unathubutu kueleza maneno ya Yesu? Nani ameinuliwa kuliko mwingine, Yesu au Isaya? Kwa vile jibu ni Yesu, kwa nini unaeleza maneno yaliyosemwa na Yesu? Je, Mungu Angeweza kukwambia kuhusu kazi yake mapema? Hakuna kiumbe kinachoweza kufahamu, wala hata wajumbe walio mbinguni, wala hata Mwana wa Adamu, kwa hivyo wewe ungejuaje? Mwanadamu ana upungufu mkuu. Kilicho muhimu kwenu sasa ni kufahamu awamu tatu za kazi. Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu. Sasa, lazima uelewe kwamba kazi yote kutoka awamu ya kwanza hadi leo ni kazi ya Mungu mmoja, ni kazi ya Roho mmoja, ambapo hakuna shaka.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni