6/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Niko Tayari Kukubali Usimamizi wa Wote

Xianshang     Mji wa Jinzhong, Mkoa wa Shanxi
Muda mfupi uliopita, kila wakati niliposikia kwamba wahubiri wa wilaya walikuwa wakija kwa kanisa letu, ningehisi kutaharaki kiasi. Sikufichua hisia zangu kwa nje, lakini moyo wangu ulijaa upinzani wa siri. Nilidhani: "Ingekuwa bora kama nyinyi nyote hamkuja. Mkija, angalau msifanye kazi kanisani nami. Vinginevyo, nitakuwa nimewekewa mipaka na kutoweza kuwasiliana kwa karibu." Baadaye, hali hiyo ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba kwa kweli nilichukia kuja kwao. Hata hivyo, sikufikiri kwamba kulikuwa na kitu kibaya nami na bila shaka sikujaribu kujijua katika mazingira ya hali hii.
Hadi siku moja, nikasoma kifungu kifuatacho cha neno la Mungu: “Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. … Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii…. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, na kumtukana na kumwangamiza, na kujaribu kuchana na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu 'akiingilia' kazi yake miongoni mwa wanadamu wa duniani? Anawezaje kumruhusu Mungu kufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? … Mapepo na roho wa Shetani … wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha!” (“Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilifikiria maana ya kifungu hiki nikitafakari juu ya hali yangu ya karibuni: Ni kwa nini nilichukia sana wafanyakazi wa wilaya kuja kwa kanisa letu? Kwa nini sikuwa tayari kuwaacha wafanye kazi pamoja nami kanisani? Si ilikuwa ni kwa sababu nilikuwa na wasiwasi kwamba kama wangekuja kanisani, wangetambua kwamba sikuwa nikifanya kazi kulingana na kanuni au mapenzi ya Mungu na wangenishughulikia kuhusu suala hili? Aidha, si nilikuwa na hofu kwamba kuja kwao kungezuia mafanikio ya mipango yangu ya kazi? Si nilikuwa na hofu kwamba wangewasiliana kwa karibu vyema kuniliko na kunisababisha kupoteza hadhi yangu ya heshima katika mioyo ya ndugu zangu wa kiume na wa kike? Kama hawangekuja, ningeendelea na mipango yangu ya kazi kama nilivyotaka. Hata kama mbinu zangu hazikukubaliana na kanuni au mapenzi ya Mungu, hakuna mtu angejua na bila shaka hakuna mtu angenishughulikia au kunikosoa. Kwa njia hii, cheo changu katika mioyo ya ndugu zangu wa kiume na wa kike kingekuwa kikubwa zaidi, cha heshima zaidi na imara zaidi. Ndugu wote wa kiume na wa kike wa kanisa wangeniheshimu sana, kunipenda na kutii amri zangu. Kanisa lote liliniangalia. Si hili ndilo lililokuwa kusudi langu la kweli? Si nilikuwa nikipanga kumfukuza Mungu kutoka mioyoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike ili niweze kupata hadhi katika mioyo yao? Si nilikuwa mfano halisi wa hizo sumu za joka kubwa jekundu, "Mbingu iko juu na mfalme yuko mbali na upeo wa macho," "Hakuna mfalme ila mimi"? Ili kudhibiti na kudai mamlaka juu ya wanadamu, joka kubwa jekundu lilipigana na ujio wa Mungu kwa nguvu zote, bila kumruhusu Mungu kuhusika katika masuala ya wanadamu, ili kufichua uso wake katili, kuharibu mipango yake au kutawala katika utawala wake. Kwa hiyo, lilipinga ovyo ovyo, kuvuruga, kuharibu na kuangamiza kazi ya Mungu. Liliota ya kwamba, siku moja, lingeweza kumpokonya Mungu kutoka mioyoni mwa wanadamu na kutimiza lengo lake lenye kustahili dharau la kuwa mpatanishi wa milele wa mwanadamu na kuwalazimisha wanadamu kumwabudu. Kulikuwa na tofauti gani kati ya mawazo yangu mwenyewe na matendo ya joka kubwa jekundu? Kwa sababu nilitaka kudumisha hadhi yangu mwenyewe na kuhakikisha kuwa niliweza kwenda njia yangu mwenyewe na nisizuiliwe katika kazi yangu, sikutaka kuwaruhusu viongozi wengine au wafanya kazi kuisimamia au kuikagua kazi yangu. Sikutaka mtu mwingine yeyote aingilie kazi ya kanisa langu au kuwanyunyizia ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kwa nini sikutaka hili? Si ni kwa sababu tu nilitaka kudhibiti na kudai mamlaka juu ya wengine? Si lengo langu la mwisho lilikuwa ni kujitangaza mfalme na mtawala wa kidunia juu ya ndugu zangu wa kiume na wa kike? Niliona kwamba sumu ya joka kubwa jekundu—kile kiburi kisichozuiliwa na cha kupenda makuu—ilikuwa tayari imepenya kwa kiini cha uhai wangu. Ushawishi wa joka kubwa jekundu kwa muda mrefu umekita mizizi ndani yangu: Nilikuwa nimekwisha kuwa pepo mbaya kama joka lenyewe. Kwa juujuu, nilikuwa ninafanya kazi ili kutimiza wajibu wangu, lakini moyo wangu ulishikilia nia zilizofichika. Kwa kweli, nilitaka kuvunja kiti cha enzi, kuweka machafuko kwa watu waliohudumu na kuunda ufalme wangu mwenyewe katika upinzani kwa Mungu na katika kuzuia utekelezaji wa mapenzi ya Mungu. Asili yangu ilikuwa uovu halisi na ya kutisha sana! Kama sio kwa ajili ya ufunuo na hukumu kali ya neno la Mungu, singeweza kamwe kujua ni kwa kiwango gani nilikuwa nimepotoshwa na Shetani na nilivyompinga Mungu. Singeweza kamwe kutambua kwamba, ndani kabisa ya nafsi yangu, njama ya katili ilikuwa imebuniwa na kwamba asili yangu ya kweli ilikuwa imeumizwa kwa kina sana na uovu.
Asante Mungu kwa ufunuo Wako na kunipa nuru, ambazo zimenikubali kutambua asili yangu ya kishetani ya kiburi na upotovu. Ninaona kwamba mimi, kwa kweli, ni mtoto wa joka kubwa jekundu na wa malaika mkuu. Mungu, ninaahidi kutafuta ukweli kwa bidii na kuja kwa ufahamu wa kina wa jinsi sumu ya joka kubwa jekundu huiumiza asili yangu. Ninaapa, zaidi ya hayo, kukubali ukaguzi na usimamizi wa wafanyakazi wengine na viongozi. Nitakubali kushughulikiwa na kupogolewa kwa wote. Nitajiweka chini ya ukaguzi wa mkusanyiko wote wa waumini ili nipate kutekeleza majukumu yangu kwa uangalifu sana ili kuufariji moyo Wako.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo Juzuu ya 1

Sikiliza zaidi:Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni