Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (9)
Tangu uumbaji hadi leo, Mungu amestahimili maumivu mengi sana, na kupata mashambulizi mengi sana. Ilhali hata leo, bado mwanadamu hayalegezi matakwa yake kwa Mungu kwa urahisi, bado anamchunguza Mungu, bado hana uvumilivu Naye, na anachofanya ni kumpatia "ushauri," na "kumkosoa," na “kumfundisha nidhamu" kana kwamba Mungu atapotoka njia, kwamba Mungu duniani ni hayawani na Hana busara, au Atafanya fujo, au kwamba Hatafanya kitu chochote cha maana. Mwanadamu siku zote huwa na mtazamo wa aina hii kwa Mungu. Inawezekanaje isimhuzunishe Mungu? Kwa kuwa mwili, Mungu amevumilia maumivu na mateso mengi; ni vibaya kiasi gani, kumfanya Mungu akubali mafundisho ya mwanadamu? Kuwasili kwake miongoni mwa wanadamu kumemvua uhuru wote, kama vile Amefungwa Kuzimu, na Amekubali "uchunguzi" wa mwanadamu bila upinzani hata kidogo. Hii sio aibu? Katika kuja miongoni mwa familia ya wanadamu wa kawaida, Yesu amepitia uonevu mkubwa. Na kinachoumiza zaidi ni kwamba Amekuja katika ulimwengu huu wa vumbi na kujinyenyekeza Mwenyewe katika hadhi ya chini kabisa, na Amechukua mwili wa kawaida kabisa. Kwa binadamu kuwa mwembamba, je, Mungu Mwenyezi hapati shida? Je, na hii yote si kwa ajili ya binadamu? Kuna wakati wowote ambapo alikuwa Anajifikiria Mwenyewe? Baada ya kukataliwa na kuuawa na Wayahudi, na kukejeliwa na kudhihakiwa na watu, Hajawahi kulalamika mbinguni au kupinga duniani. Leo, janga hili lenye umri wa milenia limetokea tena miongoni mwa watu hawa wanaofanana na Wayahudi. Je, hawafanyi dhambi ile ile? Nini kinamfanya mwanadamu kuwa na sifa ya kupokea ahadi za Mungu? Je, hampingi Mungu na kisha kukubali baraka Zake? Kwa nini haifikii haki, au kutafuta ukweli? Kwa nini havutiwi na kile ambacho Mungu anafanya? Haki yake iko wapi? Usawa wake uko wapi? Je, ana ujasiri wa kumwakilisha Mungu? Ziko wapi fahamu zake za haki? Ni kiasi gani ambacho kile kinachopendwa na mwanadamu ndicho kile kinachopendwa na Mungu? Mwanadamu hawezi kutambua tofauti muhimu,[7] siku zote anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe, anakandamiza haki na ukweli, na anashikilia kutokuwa na haki wala usawa kwa kiwango kikubwa. Anafukuzia mbali mwanga na anarukaruka gizani. Wale wanaotafuta ukweli na haki badala yake wanafukuza mwanga, wale wanaomtafuta Mungu wanamkanyaga kwa miguu yao, na wanajipandisha angani. Mwanadamu hana tofauti na gaidi.[8] Sababu yake iko wapi? Nani anaweza kutofautisha kati ya jema na baya? Nani anaweza kushikilia haki? Nani yuko tayari kuteseka kwa ajili ya ukweli? Watu ni waovu na wana tabia za kishetani kabisa! Baada ya kumwangika Mungu msalabani wanapiga makofi na kufurahi, vilio vyao havikomi. Wako kama kuku na mbwa, wanashirikiana na kula njama, wameanzisha ufalme wao, udukuzi wao haujaachwa bila kusumbuliwa, wanafumba macho yao na kulia kwa maumivu makali zaidi na zaidi, wote wameungana pamoja, na hali ya kututumka imeenea kote, ni harakaharaka na hai, na wale ambao wanajishikamanisha kwa wengine kijinga wanazidi kuibuka, wote wakiwa wameshikilia majina "mashuhuri" ya mababu zao. Hawa mbwa na kuku wamemweka Mungu mbali na akili zao, na hawajawahi kuzingatia kabisa hali ya moyo wa Mungu. Si ajabu kwamba Mungu anasema mwanadamu ni kama mbwa au kuku, mbwa anayebweka anayewafanya mia wengine kutoa mlio mkali; kwa nia hii, kwa makelele mengi ameileta kazi ya Mungu katika siku ya leo, bila kujali kazi ya Mungu ni ya namna gani, bila kujali kuna haki, bila kujali Mungu ana nafasi Yake ya kuweka miguu Yake, bila kujali kesho itakuwaje, uduni wake, na hali yake ya kuwa mchafu. Mwanadamu hajawahi kufikiria juu ya mambo kiasi hicho, hajawahi kuhofia kesho, na amekusanya yale yote ambayo ni ya manufaa na ya thamani na kuyakumbatia, na bila kumwachia Mungu chochote isipokuwa mabaki na makombo.[9] Binadamu ni katili kiasi gani! Hana hisia hata kidogo kwa Mungu, na baada ya kuteketeza kila kitu cha Mungu, anamrusha Mungu nyuma yake na kuacha kujali kabisa kuhusu uwepo wake. Anamfurahia Mungu, halafu anampinga Mungu, na anamkanyagia chini ya miguu yake, wakati mdomoni mwake anamshukuru na kumsifu Mungu; anamwomba Mungu, na anamtegemea Mungu, wakati huo pia anamdanganya Mungu; "analiinua" jina la Mungu, na kuutazama uso wa Mungu, halafu pia bila haya na bila kuwa na aibu anakaa katika kiti cha enzi cha Mungu na "kuhukumu" "udhalimu" wa Mungu; kutoka katika kinywa chake yanatoka maneno haya "anapaswa kumshukuru Mungu," na anatazama katika maneno ya Mungu, halafu katika moyo wake anavurumisha shutuma kwa Mungu; ni "mvumilivu" kwa Mungu halafu anamkandamiza Mungu, na kinywa chake kinasema ni "kwa ajili ya Mungu"; mikononi mwake ameshikilia vitu vya Mungu, na kinywani mwake anatafuna chakula ambacho Mungu amempatia, bado macho yake yanamtazama Mungu yakiwa hayana hisia kabisa, kana kwamba anatamani kummeza; anautazama ukweli lakini anasisitiza kuwa ni hila za Shetani; anatazama haki lakini analazimisha iwe kujikana nafsi; anatazama matendo ya mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni kile Mungu alicho; anatazama karama za asili za mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni ukweli; anatazama matendo ya Mungu lakini anasisitiza kuwa ni kiburi na majivuno, majigambo na haki binafsi; mwanadamu anapomwangalia Mungu anasisitiza kumpachika uanadamu, na anajitahidi sana kumweka katika kiti cha kiumbe aliyeumbwa akishirikiana na Shetani; anajua kweli kabisa ni matamshi ya Mungu, bado atasema si kitu chochote zaidi ya maandiko ya mwanadamu; anajua kabisa kwamba Roho anatambulika katika mwili, Mungu anakuwa mwili, lakini anasema mwili huu ni uzao[10] wa Shetani; anajua kikamilifu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na hajionyeshi, lakini anasema kwamba Shetani ameaibishwa na Mungu ameshinda. Uzuri wa bure ulioje! Mwanadamu hata hafai kuwa mbwa mlinzi! Hawezi kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, na hata anachanganya kwa makusudi nyeusi ndani ya nyeupe. Je, nguvu za mwanadamu na husuru ya mwanadamu vinaweza kustahimili siku ya ukombozi wa Mungu? Baada ya kumpinga Mungu kwa kukusudia, mwanadamu hakuweza kujali sana, au hata kwenda mbali sana na kumuua, asimpatie Mungu nafasi ya kujionyesha Mwenyewe. Haki iko wapi? Upendo uko wapi? Anakaa kando ya Mungu na kumsukuma Mungu apige magoti ili Aombe msamaha, kutii mipango yake yote, kuridhia hila zake zote, na anamfanya Mungu kuchukua ishara Zake zote kutoka Kwake, la sivyo anaghadhibishwa[11] na kupandwa na hasira. Inawezekanaje Mungu asiwe na maumivu katika ushawishi huo wa giza, ambao unachanganya nyeusi kuwa nyeupe? Angewezaje kukosa kuwa na wasiwasi? Kwa nini inasemwa kwamba Mungu alipoanza kazi yake ya hivi karibuni kabisa, ilikuwa kama alfajiri ya mwanzo mpya? Matendo ya mwanadamu "yana utajiri," ni "chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima" bila kukoma "yanajaza tena" shamba la moyo wa mwanadamu, wakati "chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima" ya mwanadamu "inashindana" na Mungu bila haya[12]; wawili hawa hawapatani, na anawapa watu vitu kwa niaba ya Mungu bila kuacha chochote, wakati mwanadamu anashirikiana naye bila kujali hatari iliyopo. Na kwa athari gani? Anamtupilia mbali Mungu upande mmoja, na kumweka mbali sana, ambapo watu hawatamzingatia, akiogopa sana kwamba Atavuta usikivu wake, na anaogopa sana kwamba chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima ya Mungu itamteka mwanadamu, na kumpata mwanadamu. Hivyo, baada ya kupitia uzoefu wa miaka mingi wa masuala ya kidunia, anakula njama dhidi ya Mungu, na hata anamfanya Mungu kuwa mlengwa wa "adhabu." Ni kana kwamba Mungu amekuwa gogo machoni mwake, na anatamani kumnyakua Mungu na kumweka motoni ili Atakaswe na kusafishwa. Mwanadamu anapoona mahangaiko ya Mungu, anapiga kifua chake na kucheka, anacheza kwa furaha, na kusema kwamba Mungu pia Amewekwa motoni, na anasema kwamba atausafisha uchafu wa Mungu, kana kwamba hili ni la urazini na lina maana, kana kwamba hizi tu ndizo njia za haki na zenye mantiki za Mbinguni. Tabia hii ya fujo ya mwanadamu inaonekana kuwa ni ya makusudi na ya kutofahamu. Mwanadamu anafichua uso wake mbaya na roho yake mbaya, vilevile sura ya kusikitisha ya ombaomba; baada ya kufanya ghasia sana, anavaa sura ya kuhurumiwa na kuomba msamaha wa Mbingu, akifanana na udongo wa kufinyangwa. Mwanadamu siku zote hutenda kwa namna asiyotarajiwa, siku zote "anamwendesha duma kuwatisha wengine," anajiunga katika michezo vyovyote awezavyo, hajali hata kidogo moyo wa Mungu, wala halinganishi hadhi yake mwenyewe. Kimyakimya anampinga Mungu, kana kwamba Mungu amemkosea, na Hapaswi kumtendea hivyo, na kana kwamba Mbingu haina macho na inafanya kwa makusudi mambo kuwa magumu kwake. Hivyo mwanadamu anapanga njama za siri, na hajali matakwa ya Mungu hata kidogo, anatazama kwa macho ya mnyama mkali, anatazama kwa hasira kila kitu Anachokifanya Mungu, hafikirii kwamba yeye ni adui ya Mungu, na ana matumaini kwamba siku itakuja ambapo Mungu atautawanya umande na kuviweka vitu wazi, na kumwokoa kutoka katika "kinywa cha duma" na kulipiza kisasa kwa niaba yake. Hata leo, watu bado hawafikiri kwamba wanatekeleza jukumu la kumpinga Mungu, jukumu ambalo limefanywa kwa enzi nyingi sana, wangewezaje kujua kwamba, katika yote wanayofanya, wamepotoka tangu zamani sana, kwamba yote waliyoyaelewa yamemezwa na bahari zamani sana.
Ni nani amewahi kukubali ukweli? Ni nani amewahi kumkaribisha Mungu kwa mikono yote? Nani amewahi kutamani uwepo wa Mungu? Tabia ya mwanadamu imeoza tangu zamani sana, na unajisi wake umefanya hekalu la Mungu lisitambulike tangu zamani sana. Mwanadamu, wakati akiendelea kufanya kazi yake, amekuwa akimdharau Mungu. Ni kana kwamba upinzani wake kwa Mungu umeandikwa kwenye jiwe, na haubadiliki, na matokeo yake ni bora alaaniwe kuliko kuendelea kuteseka "kwa kufanyiwa vibaya" na maneno na matendo yake. Inakuwaje watu kama hawa wamjue Mungu? Wanawezaje kupata pumziko kwa Mungu? Na wanawezaje kufaa kuja mbele za Mungu? Bila shaka, hakuna chochote kibaya kujitoa kwa mpango wa usimamizi wa Mungu—lakini kwa nini watu daima huweka kazi ya Mungu na ukamilifu wa Mungu akilini mwao huku wakitoa kwa dhati damu na machozi yao wenyewe? Roho ya watu ya kujitokelea kwa dhati, bila shaka, ni ya thamani—lakini wangejuaje kwamba "hariri" wanayoisokota haiwezi kabisa kuwakilisha kile Mungu alicho? Nia nzuri za watu, bila shaka, ni za thamani na adimu—lakini wangewezaje kumeza "hazina ya thamani mno"?[13] Kila mmoja wenu anapaswa kufikiria juu ya maisha yenu ya zamani: Kwa nini hamjawahi kuwa mbali na kuadibu na laana ya kikatili? Kwa nini watu daima "huwa na uhusiano wa karibu" na maneno adhimu na hukumu yenye haki? Je, Mungu anawajaribu kwa kweli? Je, Mungu anawasafisha kwa makusudi? Na watu huingiaje katikati ya usafishaji? Je, wanajua kazi ya Mungu kweli? Ni mafunzo gani ambayo watu wamejifunza kutoka kwa kazi ya Mungu na kuingia kwao wenyewe? Watu wasisahau kusihi kwa Mungu, wawe na ufahamu katika kazi ya Mungu, waiamini kwa dhati, na kusimamia vizuri kuingia kwao wenyewe.
Tanbihi:
1. "Maangamizi" inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.
2. " Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng'ombe aliye radhi kufungwa" ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.
3. "Upendeleo" unahusu tabia ya watu ya ukaidi.
4. "Kuchukua mamlaka kamili" inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.
5. "Kibaraka" inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.
6. "Kuongezeka haraka" inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.
7. "Hawezi kutambua tofauti muhimu" inaonyesha wakati ambapo watu wanageuza mapenzi ya Mungu kuwa kitu cha kishetani, ikitaja kwa upana tabia ambayo kwayo watu humkataa Mungu.
8. "Gaidi" inatumiwa kuonyesha kwamba watu ni wapumbavu na hawana ufahamu.
9. "Mabaki na makombo" inatumiwa kuonyesha tabia ambazo kwazo watu humdhulumu Mungu.
10. "Uzao" inatumiwa kwa dhihaka.
11. "Anaghadhibishwa" inahusu uso mbaya wa mwanadamu aliye na hasira na aliyeudhika.
12. "Bila haya" inahusu wakati ambapo watu hawajali, na hawana uchaji kuhusiana na Mungu hata kidogo.
13. "Hazina ya thamani mno" inahusu ukamilifu wa Mungu.
a. Huu ni msemo wa Kichina.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni