8/31/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?

Wale ambao wanashindwa ni foili[a], na ni baada tu ya kufanywa kamili ndiyo wao wanakuwa vielelezo na mifano ya kazi ya siku za mwisho. Kabla ya kufanywa kamili wao ni foili[a], vifaa, pamoja na vyombo vya huduma. Wale ambao wameshindwa kabisa na Mungu ni udhihirisho pamoja na vielelezo na mifano ya mpango Wake wa usimamizi. Majina haya tu machache duni kwa watu huonyesha hadithi nyingi za kuburudisha. Wale kati yenu ambao ni wa imani haba daima mtabishana juu ya jina lisilokuwa na maana mpaka nyuso zenu zinabadilika na kuwa nyekundu, na wakati mwingine hata mtaliruhusu kuathiri uhusiano wetu. Ingawa hili ni jina dogo tu, katika kufikiri kwenu, katika imani yenu, hili si jina dogo tu, bali ni jambo muhimu linalohusu majaliwa yenu. Basi, wale ambao hawana busara mara nyingi watapata hasara kubwa juu ya kitu kidogo kama hiki—huku ni kuwa mwangalifu katika mambo madogo lakini mfujaji wa makubwa, na mtatoroka na kamwe hamtarudi kwa sababu ya jina fulani dogo. Hii ni kwa sababu mnaona maisha kama hayana maana na mnaweka thamani kubwa sana kwa kile mnachoitwa. Hivyo katika maisha yenu ya kiroho, na hata katika maisha yenu ya vitendo, mara nyingi mtakuza hadithi nyingi zilizo ngumu kueleweka na ambazo ni za ajabu kwa sababu ya dhana zenu kuhusu hadhi. Labda hamtakubali jambo hili, lakini Nitawaambia kwamba watu hawa kweli wapo katika maisha yenu ya vitendo. Ni kwamba tu hamjafichuliwa mmoja mmoja. Mambo ya aina hii yamefanyika katika maisha ya kila mmoja wenu. Kama huamini hilo, angalia tu nakshi iliyo chini kutoka kwa maisha ya dada (au ya kaka). Inawezekana kwamba mtu huyo kwa kweli ni wewe, au labda ni mtu wa karibu nawe katika maisha yako. Kama Sikosei, nakshi hii ni uzoefu ambao umekuwa nao, na hakuna kitu kinachokosa katika maelezo, hakuna fikira au wazo hata moja limeachwa nje, lakini yamerekodiwa kikamilifu katika hadithi hii. Kama huamini jambo hilo, hebu tazama.
Huu ni uzoefu kidogo kutoka kwa "mtu wa kiroho" ambao umerekodiwa hapa. Alipoenda kanisani na kuona hali za ndugu zake, alihisi wasiwasi: "Mbona kamwe hamyaridhishi mapenzi ya Mungu? Viumbe wasiokuwa na busara! (Akiwakaripia ndugu zake.) Kweli, nyinyi mnapuuza dhamiri zenu ili kufanya mambo ya kinyama. ... Mimi kusema hili kwenu pia ni chuki yangu kwangu mwenyewe. Ninaona kwamba Mungu hawezi kuvumilia kabisa na ninahisi moto chini yangu. Kweli niko tayari kutekeleza kazi ya Mungu kwa ukamilifu na kweli ninataka muinuke kupitia huduma yangu. Ni kwamba tu uwezo wangu wa sasa ni mdhaifu sana. Mungu ametumia muda mwingi sana kwetu na Amenena maneno mengi sana, lakini bado sisi tuko hivi. Moyoni mwangu, daima nahisi kwamba nina deni kubwa sana kwa Mungu ...” (Akilia na kutoweza kuendelea kuzungumza.) Na kisha akaomba: “Ee Mungu! Nakuomba unipe nguvu na hata zaidi unisisimue, na Roho Wako aweze kufanya kazi ndani yangu. Niko tayari kushirikiana na Wewe. Mradi hatimaye Upate utukufu kwa sasa niko tayari kujitoa Kwako kabisa, hata kama inamaanisha ni lazima nife. Niko tayari[b] mradi tunaweza kutoa sifa kubwa, ndugu wanaweza kuimba na kucheza kwa furaha kulisifu jina Lako takatifu, kukutukuza, kukudhihirisha, na kuwa na uhakika na kazi Yako pamoja na kuwa tayari kuonyesha fikira kwa mzigo Wako....” Kwa ari aliomba kwa njia hii, na kweli Roho Mtakatifu alimsumbua. Kwa kipindi hiki alisumbuka sana, na akatumia siku nzima kusoma, kuandika, na kusikiliza. Alijishughulisha iwezekanavyo. Hali yake ya kiroho ilikuwa bora sana na daima moyoni alikuwa mwenye nguvu na wa kusumbuka. Mara kwa mara alikuwa dhaifu na kushindwa kuendelea, lakini kabla ya muda mrefu alipata tena hali yake ya kawaida. Baada ya kipindi cha muda kama huu, kuendelea kwake kulikuwa kwa kasi, aliweza kuelewa maneno mengi ya Mungu, naye pia alijifunza nyimbo kwa wepesi—kwa jumla, hali yake ya kiroho ilikuwa bora sana. Alipoona kwamba mambo mengi kanisani hayakukubaliana na mapenzi ya Mungu, alipata wasiwasi. Alipoona kwamba hakuna mtu aliathiriwa na kunakili tepu za kanda, alifadhaika: "Je, huu ni upendo kwa kazi ya Mungu? Je, huku ni kuridhisha mapenzi Yake? Hamuwezi kulipa gharama ndogo thabiti kama hii? Kama hamtaki kulifanya, nitafanya...."
Aliposumbuka, ndivyo Roho Mtakatifu alifanya kazi zaidi ndivyo alivyohisi vizuri zaidi. Mara kwa mara angekabiliwa na ubaya kiasi au matatizo kiasi, lakini aliweza kuyashinda. Yaani, alipopitia kazi ya Roho Mtakatifu, hata wakati hali zake zilikuwa nzuri sana hangeweza kuepuka matatizo fulani au udhaifu mdogo. Haya hayaepukiki, lakini kabla ya muda mrefu aliweza kutoka kwa hali hizo. Alipopitia udhaifu, mara tu alipoomba angehisi kwamba kimo chake mwenyewe kweli kilikuwa na upungufu lakini alikuwa tayari kushirikiana na Mungu. Haidhuru kile Mungu alichofanya, alikuwa tayari kuridhisha mapenzi Yake, na alikuwa tayari kutii mipango yote ya Mungu. Kulikuwa na baadhi ya watu ambao walikuwa na maoni fulani na chuki bila sababu kwake. Aliweza kujiweka kando na kwa vitendo kushiriki katika ushirika nao. Hizi zote zilikuwa hali katika kipindi cha kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Baada ya kipindi cha muda kazi ilianza kubadilika, na watu wote waliingia katika hatua nyingine ya kazi ambayo ilikuwa na mahitaji tofauti kwao. Hivyo kulikuwa na maneno mapya ambayo yalileta mahitaji kwa watu: "... Nina chuki tu kwenu, kamwe si baraka. Sijawahi kuwa na fikira ya kuwabariki kamwe, wala Sijawahi kuwa na fikira ya kuwafanya kamili. Yote Niliyo nayo kwenu ni chuki. Hii ni kwa sababu nyinyi ni waasi, kwa sababu nyinyi si waaminifu na ni wadanganyifu, na kwa sababu mnakosa ubora wa tabia na nyinyi ni wa hadhi ya chini. Hivyo kamwe hamjawahi kuwa karibu na macho Yangu au katika moyo Wangu. Kazi Yangu ni kwa kusudi la kuwahukumu tu; mkono Wangu kamwe haujawahi kuwa mbali nanyi, wala kuadibu Kwangu. Nimeendelea kuwahukumu na kuwalaani. Kwa kuwa hamna ufahamu Wangu. Hiyo ndiyo sababu ghadhabu Yangu daima imekuwa juu yenu. Ingawa daima Nimefanya kazi katikati yenu, mnapaswa kujua mtazamo Wangu kuwaelekea. Si chochote ila maudhi—hakuna mtazamo au maoni mengine. Ninataka tu mtende kama foili[a] kwa ajili ya hekima Yangu na uwezo Wangu mkubwa. Nyinyi si kitu zaidi ya foili[a] Wangu kwa sababu haki Yangu inafichuliwa kupitia uasi wenu. Ninawataka mtende kama foili[a] kwa ajili ya kazi Yangu, kuwa viambatisho vya kazi Yangu...." Mara tu alipoona maneno[c]"viambatisho" na “foili[a],” alianza kufikiri:" Jinsi gani hili lingenifanya kufuata? Baada ya kulipa gharama kama hii, mimi bado ni foili[a]. Je, foili[a] si mtendaji-huduma tu? Hapo zamani ilisemekana kwamba hatungekuwa watendaji-huduma, lakini tungekuwa watu wa Mungu, ilhali leo si bado tunatekeleza wajibu huo? Je, si watendaji-huduma wanakosa maisha? Hata kama ninateseka tena Mungu hatalisifu jambo hili! Baada ya mimi kumaliza kuwa foili[a] kwa ajili ya nguvu nyingi za Mungu, si litakuwa limekwisha? ... "Alipofikiri zaidi kuhusu jambo hilo ndivyo alivyokuwa mwenye huzuni zaidi. Alikuja kwa kanisa na kuona hali za ndugu zake na akahisi vibaya hata zaidi: "Nyinyi hamko sawa! Siko sawa! Mimi niko hasi. Wai! Ni kipi kinaweza kufanywa? Mungu bado hatutaki. Katika kufanya kazi ya aina hii, hakuna namna hatatufanya hasi. Sijui ni nini kibaya na mimi. Sitaki hata kuomba. Hata hivyo, siko sawa sasa hivi na siwezi kujitoa kutoka kwa jambo hili. Nimeomba mara nyingi lakini bado siwezi, na siko tayari kuendelea. Hivi ndivyo ninavyoona jambo hili. Mungu anasema kwamba sisi ni foili[a], hivyo je, si 'foili’[a] ni watendaji-huduma tu? Mungu anasema kwamba sisi ni foili[a], si wana, wala sisi si watu Wake. Sisi si wana Wake, sembuse wana Wake wazaliwa wa kwanza. Sisi si kitu chochote, bali foili[a] tu. Kwa jina la aina hiyo, labda tunaweza kuwa na matokeo yenye kufaa? Foili[a] hawana matumaini kwa sababu hawana maisha. Kama tungekuwa wana Wake, watu Wake, kungekuwa na matumaini katika jambo hilo, na tungefanywa kamili. Je, foili[a] wanaweza kuwa na uhai wa Mungu ndani yao? Je, Mungu anaweza kuweka uhai ndani ya wale ambao hufanya huduma kwa ajili Yake? Wale Anaowapenda ni wale ambao wana uhai Wake, na wale walio na uhai Wake ni wana Wake, watu Wake. Ingawa mimi ni hasi na dhaifu, natumaini kwamba nyinyi nyote si hasi. Ninajua kwamba kurudi nyuma na kuwa hasi hivi hakuwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu, lakini siko tayari kuwa foili[a]. Ninahofia kuwa foili[a]. Vyovyote vile, nina nguvu kiasi fulani tu, na siwezi kuendelea sasa. Ninatumaini kwamba nyinyi nyote hamtajifunza kutoka kwangu, lakini kwamba mnaweza kupata nuru kiasi kutoka kwangu. Ninafikiri afadhali nife! Nitawaacha na maneno fulani ya mwisho kabla sijafa—ninatumaini kwamba mnaweza kutenda kama foili[a] hadi mwisho; labda hatimaye Mungu atawasifu foili[a]....” Wakati ndugu walipoona hili, walishangaa:[d] Ni jinsi gani anaweza kuwa hasi hivyo? Je, hakuwa sawa kwa hizo siku chache? Mbona kwa ghafla yu katili sana? Je, mbona yeye hawi kawaida? Alisema: "Usiseme mimi siwi kawaida. Kwa kweli, nina uhakika na kila kitu moyoni mwangu. Ninajua kwamba sijaridhisha mapenzi ya Mungu—je, si ni kwa sababu tu siko tayari kutenda kama foili[a] Zake? Mimi sijafanya lolote lingine ambalo ni la maana mno. Labda siku moja Mungu atabadili jina la[e] foili[a] kuwa viumbe Wake ambao wanatumika naye kwa njia muhimu. Je, si kunayo matumaini kiasi katika jambo hili? Ninatumaini kwamba nyinyi si hasi au wenye huzuni, kwamba mnaweza kuendelea kumfuata Mungu na kuwa foili[a] bora. Kwa vyovyote, siwezi kuendelea. "Watu wengine walisikia hayo, na wakasema.[f] Ingawa huko sawa tutaendelea kufuata, na hatutabanwa kwa sababu wewe ni hasi.
Baada ya kupitia hili kwa kipindi cha muda yeye bado alikuwa hasi juu ya kuwa foili[a], hivyo Nilimwambia: "Wewe huna ufahamu wa kazi Yangu. Huna ufahamu wa ukweli wa ndani, asili, au matokeo yaliyokusudiwa ya maneno Yangu. Hujui malengo ya kazi Yangu, au hekima yake. Huna ufahamu wa mapenzi Yangu. Unajua tu kurudi nyuma kwa sababu wewe ni foili[a]—tamaa yako ya hadhi ni kubwa mno! Wewe ni mpumbavu! Hapo zamani Nimesema mengi sana kwako, na Nimesema Ningekufanya kamili. Je, umesahau? Kabla ya foili[a] kuzungumziwa, je, si kufanywa kamili kulikuwa kumezungumziwa?" "Acha, nitafikiri kuhusu jambo hilo! Kabla ya foili[a] kuzungumziwa, kweli Ulikuwa umesema hivyo; ilikuwa namna hiyo!" "Nilipozungumza kuhusu kukamilishwa, je, Sikusema kwamba ni baada tu ya watu kushindwa ndio wangefanywa kamili?" "Ndiyo!" "Je, maneno Yangu hayakuwa ya kweli? Je, hayakusemwa kwa nia njema?" "Ndiyo! Wewe ni Mungu ambaye hajawahi kusema kitu chochote cha udanganyifu na hakuna yeyote anayeweza kuthubutu kukana jambo hili. Lakini njia unazonena ni nyingi mno." "Je, si njia Zangu za kuzungumza hubadilika kulingana na hatua za kazi? Je, si kile Ninachosema kinafanywa na kusemwa kulingana na mahitaji yako?" "Wewe hufanya kazi kulingana na mahitaji ya watu na Wewe huwapa kile wanachohitaji. Jambo hili si la uwongo!" "Je, basi si matamshi Yangu, si kile Nimekwambia kimekuwa chenye manufaa? Je, si kuadibu Kwangu kumekuwa kwa ajili yako?" "Bado unasema kwamba ni kwa ajili yangu mwenyewe! Niko karibu kuadibiwa hadi kifo na Wewe na sitaki kuishi zaidi. Leo Unasema hili, kesho Unasema lile. Ninajua kwamba Wewe kunikamilisha ni kwa ajili yangu mwenyewe, lakini hujanikamilisha—Wewe unanifanya foili[a] na bado unaniadibu. Je, Hunichukii? Hakuna yeyote anayethubutu kuamini maneno Yako, na ni sasa tu Nimeona dhahiri kwamba ni kutatua tu chuki iliyo katika moyo Wako, si kuniokoa. Awali ulinificha jambo hili, Ulisema ungenikamilisha na kwamba kuadibu kulikuwa kwa ajili ya kunikamilisha. Hivyo daima nimetii kuadibu Kwako; sikuwahi kufikiri kwamba leo ningekuwa na jina la foili[a]. Mungu, je, haingekuwa bora zaidi kama Ungenitaka nitende kama kitu kingine chochote? Ni lazima unishurutishe kufanya wajibu wa foili[a]? Ingekuwa sawa kama ningekuwa bawabu mbinguni. Ninakimbia mbele na nyuma, sasa mikono yangu ni mitupu, na nimetoa kila kitu, ilhali hata sasa Unaniambia, Unanitaka nitende kama foili[a] Yako. Ninawezaje hata kuonyesha uso wangu?" "Nimefanya kazi nyingi sana za kuadibu zamani, na huna ufahamu? Je, huna ufahamu wako mwenyewe? Je, si kuadibu ni hukumu ya maneno? Je, si jina la “foili” pia ni hukumu ya maneno?" "Kuliweka jambo hilo namna hiyo, foili[a] unaozungumzia pia ni mbinu? Ni kunihukumu kupitia njia hii? Kama ni hivyo, nitafuata." "Basi ni jinsi gani ungenifuata sasa?" "Kukufuata—bado sijapanga jinsi ya kukufuata Wewe. Ninataka useme neno ambalo si mbinu. Je, mimi ni foili[a] au la? Je, foili[a] pia wanaweza kukamilishwa? Je, jina la 'foili[a]' linaweza kubadilishwa? Ninaweza kutoa ushuhuda mkubwa sana kupitia kuwa foili[a], na kisha kuwa mtu ambaye amekamilishwa, ambaye ni mfano wa kumpenda Mungu, na msiri wa Mungu? Ninaweza kufanywa kamili? Niambie ukweli!" "Je, hujui kwamba daima vitu vinageuka, daima vinabadilika? Mradi sasa hivi uko tayari kutii kuwa foili[a] utaweza kubadilika. Kama wewe ni foili[a] au la haina uhusiano wowote na kudura yako—cha muhimu ni kama unaweza kuwa mtu ambaye ana badiliko katika tabia ya maisha yake au la." "Niambie! Unaweza kunikamilisha au la?" "Mradi ufuate na kutii mpaka mwisho, Ninakuhakikishia kwamba Ninaweza kukufanya kamili." "Na itanibidi nipitie mateso ya aina gani?" "Shida pamoja na hukumu na kuadibu kwa maneno, hasa kuadibu kwa maneno—kuadibu sawa kama foili[a]!" "Kuadibu sawa na ya foili[a]pia? Lakini kama ninaweza kufanywa kamili na Wewe kwa kupitia shida, kama kuna matumaini hiyo ni sawa. Hata kama ni chembe ya matumaini tu, ni bora zaidi kuliko kuwa foili[a]. Jina hilo, ‘foili[a],' husikika kuwa baya sana. Siko tayari kuwa foili[a]!" "Ni nini kibaya na foili[a]? Si foili[a] pia ni wazuri kwa kiasi fulani? Je, foili[a]hawastahili kufurahia baraka? Nikisema kwamba foili[a] wanaweza kufurahia baraka utaweza kufurahia baraka. Je, si majina ya watu yanabadilika kwa sababu ya kazi Yangu? Ni jina tu linakusumbua kiasi hiki? Kuwa foili[a] wa aina hii kunastahili kabisa. Je, uko tayari kufuata au la?" "Hivyo unaweza kunifanya kamili au la?! Je, Unaweza kuniruhusu nifurahie baraka Zako?" "Je, uko tayari kufuata mpaka mwisho au la? Je, uko tayari kujitoa?" "Acha nilifikirie. Foili[a] pia anaweza kufurahia baraka Zako, na anaweza kufanywa kamili. Baada ya kukamilishwa nitakuwa msiri Wako na kufahamu mapenzi Yako yote, na nitamiliki Unachomiliki. Nitaweza kufurahia kile Unachofurahia, na nitajua kile Unachojua. ... Baada ya kupitia shida na kukamilishwa, ninaweza kufurahia baraka. Hivyo ni baraka zipi Nitafurahia kwa kweli?" "Usiwe na wasiwasi juu ya baraka utakazofurahia. Hata Ningekuambia, hungeweza kuzifikiria. Baada ya kuwa foili[a] mzuri, utashindwa, utakuwa foili[a]mwenye mafanikio. Huu ni mfano na kielelezo cha walioshindwa, lakini bila shaka unaweza tu kuwa hivyo baada ya kushindwa." "Mfano na kielelezo ni nini?" "Ni mfano na kielelezo kwa wote wasio Wayahudi, yaani, wale ambao hawajashindwa." "Ni watu wangapi?" "Ni watu wengi. Si tu watu elfu nne au tano kati yenu—wale ambao wanalikubali jina hili duniani kote lazima washindwe." "Hivyo si miji mitano au kumi tu!" "Usiwe na wasiwasi kuhusu hilo sasa—usijishughulishe mno. Lenga tu jinsi unapaswa kuingia ndani sasa hivi! Ninakuahidi kwamba unaweza kufanywa kamili." "Hadi kiwango kipi? Na ni baraka zipi ninazoweza kufurahia?" "Una wasiwasi sana kuhusu nini? Ninaahidi kwamba unaweza kufanywa kamili; je, umesahau kwamba Mimi ni mwaminifu?" "Ni kweli kwamba Wewe ni mwaminifu, lakini baadhi ya mbinu Zako za kuzungumza daima zinabadilika. Leo Unasema Unaahidi kwamba ninaweza kufanywa kamili, lakini kesho unaweza kusema hakuna uhakika. Na kwa watu wengine unasema 'Ninaahidi kwamba mtu kama wewe hawezi kufanywa kamili.' Sijui kile kinachoendelea na maneno Yako. Hasa sithubutu kuliamini kwa urahisi." "Hivyo unaweza kujitoa au la?" "Kutoa nini?" "Kutoa maisha yako ya baadaye, matumaini yako." "Wai! Hayo ninaweza kuyaachilia! Jambo kuu ni jina la 'foili[a]'—kwa kweli silitaki. Ukiondoa jina la 'foili[a]' kutoka kwangu nitakaribisha chochote, nitaweza kufanya chochote. Haya si mambo hafifu tu? Je, Unaweza kuondoa jina hilo?" "Je, hilo si rahisi tu sana? Kama Ninaweza kukupa jina hilo pia Ninaweza kuliondoa. Lakini sasa si wakati—lazima ukamilishe uzoefu wako wa hatua hii ya kazi, na ni hapo tu ndipo unaweza kupata jina jipya. Zaidi mtu alivyo kama wewe, ndivyo anahitaji zaidi kuwa foili[a]. Unavyoogopa zaidi juu ya kuwa foili[a], ndivyo Nitakavyokupachika jina hilo zaidi. Mtu kama wewe lazima apewe nidhamu kali na kushughulikiwa. Kadiri mtu alivyo muasi, ndivyo atakavyokuwa mtendaji-huduma zaidi, na mwishowe hatapata chochote." "Kwa aina hii ya kutafuta, kwa nini nisiweze kulitupilia mbali jina la 'foili[a]’? Tumekufuata hii miaka yote na kuteseka sana. Tumefanya hivi kwa ajili Yako na tumefanya hivyo kwa ajili Yako, tumekwenda nje kukiwa na upepo na mvua. Sote tuko kati ya miaka ishirini na sita hadi ishirini na tisa—tuko mwisho wa ujana wetu. Hatujaoa au kuanza familia, na wale kati yetu ambao wamefanya hivyo bado wamejitokeza wazi. Nilikuwa shuleni hadi shule ya upili; mara tu niliposikia kwamba ulikuwa Umekuja, niliacha nafasi yangu ya kwenda chuo kikuu. Na Unasema kwamba sisi ni foili[a]—tumepata hasara mno! Tunafanya mambo haya yote lakini inatokea kwamba sisi ni foili[a]Zako. Je, jambo hili linawafanyaje wafanyikazi wenzangu, wenzi wangu, na marika wangu kunifikiria mimi? Wanaponiona na kuuliza juu ya cheo changu na hadhi yangu, ninakosaje kuwa na aibu kuwaambia? Je, wangenifikiriaje? Mwanzoni, nililipa gharama yoyote kwa sababu ya imani yangu Kwako na wengine wote walinidhihaki kama mpumbavu. Lakini bado nilifuata, na nilikuwa na hamu ya wakati ambapo siku yangu ingekuja, na kuwaonyesha wale wote ambao hawakuamini. Lakini badala yake, leo Unaniambia kwamba mimi ni foili[a]. Kama Ungenipa jina la chini kabisa, kama Ungeniruhusu niwe mmoja wa watu wa ufalme, hilo lingekuwa sawa! Hata kama singekuwa mwanafunzi Wako au msiri Wako, ningekuwa sawa tu kuwa mfuasi Wako! Tumekufuata miaka hii yote, tumeziacha familia zetu, na imekuwa vigumu sana kuendelea kutafuta mpaka sasa, lakini tuna jina la 'foili[a]' tu! Nimeacha kila kitu kwa ajili Yako; Nimeacha utajiri wote wa dunia hii. Mwaka kabla ya mwaka jana mtu fulani alinitambulisha kwa mtu ambaye angeweza kuwa mwenzi. Kwa kweli alikuwa mwenye sura nzuri na alivalia vizuri, alikuwa mwana wa kada ya ngazi ya juu. Hakuwa na kazi nzuri, alikuwa dereva, lakini kweli alikuwa mwenye sura ya kupendeza, na wakati huo nilivutiwa naye. Lakini mara tu niliposikia kwamba Ulikuwa Utuongoze katika ufalme, kwamba Ungetukamilisha, na kwamba Ukatuuliza tuwe na uamuzi na kwa haraka tuache kila kitu nyuma, niliposikia hayo, niliona kwamba sikuwa na uamuzi wowote hata kidogo! Nilijikaza na kukataa jambo hilo. Alituma zawadi kwa familia yangu mara kadhaa, lakini hata sikuziangalia. Wakati huo, Ungesema kwamba nilikuwa nimefadhaika? Kitu kizuri kiasi hicho hakikufanikiwa. Ningekosaje kufadhaika? Nilifadhaika kukihusu kwa siku kadhaa hivi kwamba singeweza kulala usiku, lakini hatimaye bado nilikiacha. Kila wakati nilipoomba nilisisimuliwa na Roho Wako, ambaye Alisema: 'Je, uko tayari kutoa kila kitu kwa ajili Yangu? Je, uko tayari kujitumia kwa ajili Yangu?’ Kila Nilipofikiri juu ya maneno hayo Yako ningelia. Niliguswa na nikalia kwa huzuni mara nyingi zaidi ya ninavyojua. Baadaye, alikuja nyumbani kwangu mara chache lakini sikumuona hata mara moja. Sasa hata nimesahau vile anavyofanana; singeweza kumtambua. Mwaka mmoja baadaye nikasikia kwamba alikuwa ameoa. Ni wazi kwamba, nilikuwa mwenye taabu sana, lakini bado niliacha jambo hilo kwa ajili Yako. Niliacha ndoa hiyo—licha ya kuwa chakula changu na mavazi hayasaidii—nimeyaacha haya yote, kwa hivyo Hupaswi kunitaka nitende kama foili[a]! Wengine walisema kwamba baba yake ni kada, na ikiwa tungepata kuoana yeye angenipatia kazi. Nilijitesa juu ya jambo hili na kupambana nalo kwa nusu mwezi, lakini hatimaye niliibuka kutoka kwa jambo hilo. Niliiacha ndoa yangu kwa ajili ya kujidhabihu kwako, tukio la muhimu sana katika maisha yangu! Maisha yote ya mtu si kitu chochote zaidi ya kupata mwenzi mzuri na kuwa na familia yenye furaha. Niliacha jambo bora kabisa, na sasa mikono yangu ni mitupu na mimi niko pweke. Ni wapi Ungenitaka niende? Nimeteseka tangu nilipoanza kukufuata. Sijakuwa na maisha mazuri. Nimeiacha familia yangu na amali yangu pamoja na furaha za mwili, na gharama yote ambayo sote tumelipa bado haitoshi kufurahia baraka Zako? Hivyo sasa ni suala hili la 'foili[a]'. Mungu, kwa kweli Wewe umevuka mpaka! Tuangalie—hatuna kitu chochote cha kutegemea katika dunia hii. Wengine wetu tumewaacha watoto wetu, wengine tumeacha kazi zetu, wenzi wetu,[g] na kadhalika; tumeacha furaha zote za mwili. Tuna kipi kingine cha kutumainia? Tunawezaje kuendelea kuishi katika ulimwengu? Gharama hizi ambazo tumelipa hazina thamani ya peni moja? Huwezi kuona hilo kabisa? Hadhi yetu ni duni na ubora wetu wa tabia ni pungufu—tunatambua jambo hili, lakini wakati upi hatujawahi kutii kile Ulichotaka tufanye? Sasa unatuacha bila huruma na ‘tunzo' tu ya kuwa foili[a]? Gharama ambayo tumelipa imetuletea tu jina la[h] ‘foili[a]’? Hatimaye, watu wataniuliza ni nini nimepata kutokana na kumwamini Mungu. Je, ninaweza kuweka neno[i] ‘foili[a] ' mbele yao? Ninawezaje kufungua mdomo wangu kusema kwamba mimi ni foili[a]? Siwezi kujieleza kwa wazazi wangu, na siwezi kujieleza kwa yule angeweza kuwa mwenzi wangu wa zamani. Kwa sababu Yako, sina uhusiano wowote na wanafunzi wenza. Wamenitumia zawadi lakini nilizirudisha zote. Kuna baadhi yao ambao, kwa sababu walinitumia vitu mbalimbali na sikuvikubali, hawana nia tena ya kuwasiliana na mimi. Nimeacha vitu hivi na sishiriki tena katika shughuli za kidunia. Nimelipa gharama kubwa sana, na kile ninachopata kama malipo ni kuwa foili[a]! Aa! Nahisi vibaya sana!" (Akipiga mapaja yake na kuanza kulia.) "Ningesema kwamba sasa singekupa jina la[j] foili[a] lakini Ningekufanya mmoja wa watu Wangu na kukutaka uende ukaeneze injili, Ningekupa hadhi kukutaka uende ufanye kazi, je, ungeweza kuifanya? Kwa kweli ni kipi ambacho umepata kutokana na hatua baada ya hatua ya kazi hii? Na hata umesimulia hadithi yako—huna aibu! Unasema kwamba umelipa gharama lakini hujapata chochote. Inawezekana kwamba Sijakuambia masharti Yangu ni gani ya kumpata mtu? Kazi Yangu ni kwa ajili ya nani? Je, unajua? Unafungua majeraha ya zamani! Je, hata unahesabika kama mwanadamu tena? Je, kuteseka kokote hakukuwa kwa hiari yako mwenyewe? Na kuteseka kwako hakukuwa ili kupata baraka? Je, umetosheleza mahitaji Yangu? Yote unayotaka ni kupata baraka. Huna aibu! Ni lini mahitaji Yangu kwako yaliwahi kuwa ya lazima? Ikiwa uko tayari kunifuata ni lazima unitii katika mambo yote. Usinene kuhusu masharti. Hata hivyo, Nilikuambia awali kuwa njia hii ni njia ya kuteseka. Imejawa na uwezekano wa kutia hofu, na msaada kidogo. Je, umesahau? Nimesema jambo hili mara nyingi. Ikiwa uko tayari kuteseka basi Nifuate, na kama huko tayari kuteseka, acha. Sikulazimishi—uko huru kuja au kwenda! Hata hivyo, hivi ndivyo kazi Yangu inavyofanywa, na Siwezi kuchelewesha kazi Yangu yote kwa sababu ya uasi wako binafsi. Unaweza kuwa huko tayari kutii, lakini kunao wengine ambao wako tayari. Nyinyi nyote ni watu walio tayari kufanya lolote! Huogopi chochote! Unajadili masharti yako na Mimi—unataka kuendelea kuishi au la?! Unajipangia mwenyewe na kupigania umaarufu na faida yako mwenyewe. Je, si kazi Yangu yote ni kwa ajili yenu? Je, wewe ni kipofu? Kabla Nipate mwili hungeweza kuniona, na maneno hayo yangesameheka, lakini sasa Mimi Nimepata mwili na Ninafanya kazi kati yenu, lakini bado huwezi kuona? Ni nini huelewi? Unasema umepata hasara; hivyo Nimekuwa mwili ili kuwaokoa nyinyi watu wenye kukata tamaa na Nimefanya kazi kubwa sana, na mpaka sasa bado unalalamika—ungeweza kusema kwamba Nimeteseka? Je, si kile ambacho Nimefanya ni kwa ajili yenu? Nina jina hili kwa watu kulingana na kimo chao cha wakati uliopo. Nikikuita 'foili[a],' mara moja wewe ni foili[a]. Nikikuita 'watu wa Mungu,' mara moja wewe ni watu wa Mungu. Chochote Nikuitacho, wewe ni hicho. Je, yote si kama Ninavyosema tu? Na neno hili moja Langu linakughadhibisha sana? Sawa basi, Niwie radhi! Usipotii sasa, hatimaye utalaaniwa—utafurahi wakati huo? Huzingatii njia ya maisha lakini unalenga tu hadhi na jina lako; je, maisha yako yakoje? Sikani kwamba umelipa gharama kubwa, lakini angalia kimo na matendo yako mwenyewe, na hata sasa bado unajadili masharti yako. Je, hiki ni kimo ambacho umekipata kwa ajili ya uamuzi wako? Je, bado una uadilifu wowote? Je, una dhamiri? Je, ilikuwa Mimi ambaye Nimefanya kitu kibaya? Je, mahitaji Yangu kwako yalikuwa ya makosa? Ni nini? Ningetaka utende kama foili[a] kwa siku chache na huko tayari kufanya hivyo. Huo ni uamuzi wa aina gani? Nyinyi nyote ni wenye mioyo dhaifu, nyinyi ni waoga! Kuwaadhibu watu kama nyinyi ni jambo la linalotarajiwa!" Mara tu Niliposema jambo hili, hakusema neno lolote.
Kupitia kazi ya aina hii sasa, lazima muwe na ufahamu fulani kuhusu hatua za kazi na mbinu za kuwabadili watu. Hii ni njia pekee ya kutimiza matokeo katika mabadiliko. Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, tamaa ya[k] hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. Sababu ambayo vitu hivi vipo katika mioyo ya watu ni kwa sababu hasa sumu ya Shetani daima inaharibu fikira za watu, na watu daima hawawezi kuondoa majaribu haya kutoka kwa Shetani. Wanaishi katikati ya dhambi ilhali hawaiamini kuwa dhambi, na bado wanaamini: "Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima Atupe baraka na kupanga kila kitu kwa ajili yetu ipasavyo. Tunaamini katika Mungu, hivyo lazima tuwe wa cheo cha juu kuliko wengine, na lazima tuwe na hadhi zaidi na maisha zaidi ya baadaye kuliko mtu mwingine yeyote. Kwa kuwa tunaamini katika Mungu, lazima Atupe baraka bila kikomo. Vinginevyo, hakungeitwa kuamini katika Mungu." Kwa miaka mingi, mawazo ambayo watu wametegemea kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao yamekuwa yakiharibu mioyo yao hadi kiwango ambapo wamekuwa wadanganyifu, waoga, na wenye kustahili dharau. Hawakosi tu ushupavu na uamuzi, lakini pia wamekuwa walafi, wenye kiburi, na wa kudhamiria. Kabisa wanakosa uamuzi wowote upitao sana ubinafsi, na hata zaidi, hawana ujasiri hata kidogo wa kuondoa shutuma za ushawishi huu wa giza. Fikira na maisha ya watu ni mabovu, mitazamo yao juu ya kuamini katika Mungu bado ni mibaya kwa namna isiyovumilika, na hata watu wanaponena kuhusu mitazamo yao juu ya imani katika Mungu haivumiliki kabisa kusikia. Watu wote ni waoga, wasiojimudu, wenye kustahili dharau, na dhaifu vilevile. Hawahisi maudhi kwa nguvu za giza, na hawahisi upendo kwa nuru na ukweli; badala yake, wanafanya kila wanaloweza kuvifukuza. Je, si fikira na mitazamo yenu ya sasa iko hivi tu? "Kwa kuwa ninaamini katika Mungu ninapaswa tu kumiminiwa baraka na inapaswa kuhakikishwa kwamba hadhi yangu kamwe haitelezi na kwamba iko juu kuliko ile ya wasioamini." Hamjakuwa mkihodhi mtazamo wa aina hiyo ndani yenu kwa mwaka moja au miaka miwili tu; umekuwa hapo kwa miaka mingi. Mtazamo wenu wa shughuli umekua sana. Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. Watu hawajawahi kuweka kando tamaa yao ya starehe. Kwa sasa mnaadibiwa kwa njia hii, na hatimaye ni kiwango kipi cha uelewa mtakachokuwa nacho? Mtasema kwamba ingawa hadhi yenu haiko juu, mmefurahia kuinuliwa na Mungu. Hamna hadhi kwa sababu mlizaliwa katika hali ya chini, na kuwa na hadhi ni kwa sababu ya kuinuliwa na Mungu—ni kile ambacho Aliwapa. Leo mna uwezo wa kibinafsi wa kupokea mafunzo ya Mungu, kuadibu Kwake, na hukumu Yake. Huku ni kuinuliwa na Yeye hata zaidi. Mnaweza kupokea utakaso na kuchomwa Kwake binafsi. Huu ni upendo mkuu wa Mungu. Kupitia enzi hakujakuwa hata mtu mmoja ambaye amepokea utakaso na kuchomwa Kwake, na hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kupokea kukamilishwa kwa maneno Yake. Mungu sasa Ananena nanyi ana kwa ana, Akiwatakasa, Akifichua uasi wenu wa ndani—huu kweli ni kuinuliwa na Yeye Watu wanaweza kufanya nini? Kama wao ni wana wa Daudi au ni uzao wa Moabu, kwa jumla, watu ni viumbe ambao hawana chochote cha kujigamba kuhusu. Kwa kuwa nyinyi ni viumbe wa Mungu, lazima mtekeleze wajibu wa kiumbe. Hakuna mahitaji mengine kwenu. Na unaweza kuomba na kusema: "Ee Mungu! Kama nina hadhi au la, sasa ninajielewa mwenyewe. Hadhi yangu ikiwa juu ni kwa sababu ya kuinuliwa na Wewe, na ikiwa iko chini ni kwa sababu ya mpango Wako. Kila kitu ki mikononi Mwako. Sina chaguzi au malalamishi yoyote. Ulipanga kwamba ningezaliwa katika nchi hii na miongoni mwa watu hawa, na ninapaswa tu kuwa mtiifu kabisa chini ya utawala Wako kwa sababu kila kitu ki ndani ya yale Umepanga. Silengi hadhi; hata hivyo, mimi ni mmoja tu miongoni mwa uumbaji. Ungeniweka kuzimu, katika ziwa la moto wa jahanamu, mimi si chochote isipokuwa kiumbe. Ukinitumia, mimi ni kiumbe. Ukinikamilisha, mimi bado ni kiumbe. Usiponikamilisha, bado nitakupenda kwa sababu mimi si zaidi ya kiumbe. Mimi si chochote zaidi ya kiumbe mdogo sana aliyeumbwa na Bwana wa uumbaji, mmoja tu miongoni mwa wanadamu walioumbwa. Ni Wewe uliyeniumba, na sasa kwa mara nyingine tena Umeniweka katika mikono Yako ili niwe chini ya rehema Yako. Niko tayari kuwa chombo Chako na foili[a] Yako kwa sababu vyote ni vile Umepanga. Hakuna anayeweza kubadili jambo hilo. Vitu vyote na matukio yote yako katika mikono Yako." Wakati huo utakapofika, hutalenga tena hadhi, na utaondoa hiyo. Hapo tu ndipo utaweza kwa kujiamini, kutafuta kwa ujasiri, na ni hapo tu ndipo moyo wako unaweza kuwa huru dhidi ya vikwazo vyovyote. Mara tu watu watakuwa wamenasuliwa, wakati watakuwa wametoka katika jambo hili, hawana shaka tena. Ni nini kinawahangaisha wengi wenu sasa hivi? Daima mnazuiwa na hadhi na daima mnatafuta matarajio yenu wenyewe. Mnachukua vitabu na kuvipitia bila kuona kile kinachosemwa kuhusu hatima ya mwanadamu; mnadurusu kiasi zaidi lakini bado hamkipati. Mnafikiri:[l]"Inakuwaje kusiwepo na matarajio? Inawezekana kuwa Mungu ameondoa matarajio hayo? Haiwezekani! Basi kwa nini hakuna matarajio yoyote? Mungu hunena tu kuhusu foili[a], hivyo hakuna kitu kingine? "Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujitoa nje ya uhasi? Je, si daima ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo? Mara tu matamshi ya Mungu yanapotolewa nyinyi huharakisha kuona hadhi na utambulisho wenu kweli vikoje. Mnaweka hadhi na utambulisho kuwa msingi, na maono huja baadaye. La tatu ni kile mnapaswa kuingia ndani yake, na la nne ni mapenzi ya Mungu ya sasa. Nyinyi huangalia kwanza iwapo jina la Mungu kwenu kama "foili[a] " limebadilika au la. Mnasoma na kusoma, na mnapoona kwamba jina la "foili”[a] limeondolewa mnafurahi na kumshukuru Mungu siku zote, mnasifu nguvu Yake kuu. Lakini mara tu mnapoona kwamba nyinyi bado ni foili[a], mnafadhaika na mara moja hamna msukumo wowote katika mioyo yenu. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme? Ikiwa kusudi la kufuatilia kwako si kutafuta ukweli, basi afadhali utumie fursa hii na kurudi duniani ili kufanikiwa. Kupoteza muda wako hivi kwa kweli hakuna thamani—kwa nini ujitese? Hungefurahia mambo ya aina yote katika dunia nzuri? Pesa, wanawake warembo, hadhi, majivuno, familia, watoto, na kadhalika—si haya yote ni matokeo ya dunia mambo mazuri zaidi ambayo ungeweza kufurahia? Kuna faida gani kuzurura zurura hapa ukitafuta mahali ambapo unaweza kuwa na furaha? Mwana wa Adamu hana pahali pa kulaza kichwa Chake, hivyo ungekuwaje na pahali pa utulivu? Angewezaje kukuumbia pahali pazuri pa utulivu? Hilo lawezekana? Kando na hukumu Yangu, leo unaweza kupokea tu mafundisho ya ukweli. Huwezi kupata faraja kutoka Kwangu wala huwezi kupata mahali pa starehe unapopafikiria usiku na mchana. Sitakupa utajiri wa duniani. Ukifuatilia kwa kweli, Niko tayari kukupa njia ya uhai yote, kukutaka uwe kama samaki aliyerudi majini. Usipofuatilia kwa kweli, Nitayafuta yote. Siko tayari kutoa maneno kutoka kwa kinywa Changu kwa wale watu ambao ni wenye tamaa ya faraja nao ni kama nguruwe na mbwa tu!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha
b. Nakala ya asili inaacha "Niko tayari.
c. Nakala ya asili inaacha "maneno."
d. Nakala ya asili inaacha "walishangaa."
e. Nakala ya asili inaacha "jina la".
f. Nakala ya asili inaacha "na wakasema."
g. Nakala ya asili inasoma "wake."
h. Nakala ya asili inaacha "jina la".
i. Nakala ya asili inaacha "neno."
j. Nakala ya asili inaacha "jina la".
k. Nakala ya asili inaacha "tamaa ya."
l. Nakala ya asili inaacha "Mnafikiri."
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Sikiliza zaidi:Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni