8/15/2018

Upendo wa Mungu Unaenea Duniani Kote


Upendo wa Mungu Unaenea Duniani Kote

Mwenyezi Mungu, Wewe ni mwenye haki, Wewe ni mtakatifu.
Upendo Wako safi ni kama chembe ya theluji ikicheza hewani,
nyeupe, nzuri, inayonukia, ikiniangukia, ikiyeyuka katika upendo wangu mara moja.
Kupitia uboreshaji Wako upendo wangu Kwako umekuwa halisi kabisa.
Nikuache upange njia ya maisha yangu Wewe binafsi.
Wakati wowote moyo wangu unakutii Wewe na kukusifu, unajazwa na furaha tamu.
Aa … kukupenda kila wakati haitoshi.
Aa … kukupenda mchana na usiku, sitakuacha Wewe kamwe.
Nikifikiria upendo  Wako kwangu, moyo wangu una furaha;
Siwezi kukusahau Wewe kamwe.
Upepo unabusu milima ya kijani kibichi; mawingu yanaibusu bahari;
Watu wa Mungu wako pamoja na Mungu.
Chemichemi za milima zinatoa mawimbi, mawingu yanasonga;
yote yakiwa na harufu ya upendo kwa Mungu.
Mungu alitupangia sisi kabla ya enzi; hakuna anayeweza kututenganisha na Yeye.
Aa … kando ya kiti cha enzi tunamwabudu Yeye.
Aa… tazama! Nchi nzima imejawa na sifa kwa Mungu.
Upendo wa Mungu umekuwa ukiandamana nasi,
katika miaka ya giza kabla ya alfajiri kufika.
Mungu mwenye haki anamshinda Shetani kabisa, akitubadilisha kuwa mwanadamu mpya.
Ufalme wa Milenia umekuja duniani, Mungu ndiye Mfalme.
Tunaweza kuona upendo wa Mungu kila mahali …
Hakika, kwa kweli ukiipa joto mioyo ya wengi,
furaha isiyo na mwisho inaujaza moyo wangu.
Aa … watu wapya, nyimbo, ngoma, maisha mapya.
Aa … maisha yetu yamejaa nguvu.
Maisha yetu yamejaa nguvu.

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni